Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Uanzishwaji wa mahakama ya kadhi una uhalali wowote kua na usimamizi wa serikali wakati huo huo serikali haina dini? Mi sijaelewa hapa uhalali wake mwenye kujua zaidi afunguke basi nimuelewe vizuri

Mbona imeanzishwa mahakama ya Ardhi na mahakama ya Biashara. Sasa kwanini isiwe hii ya kadhi?

Na mbona hata Mabenk yenu wameanzisha utaratibu wa Bank kufuata utaratibu wa kuhifadhi pesa wa Kiislam ( Islamic banking) na sasa zina wateja wengi sana na wanazidi siku hadi siku. Lazima Serikali yenu iwe flexible kukubali changes.

Jiulizeni watakao pata huduma hapo watakuwa sio wa TZ. Je Serikali itaweza lipia watu wake watakao peleka masuala yao pale na kuhudumiwa? Lazima mjua kila mtanzania ana haki sawa na hakuna first citizen na second citizen. Wote mpo daraja moja nawashangaa wanaopinga?

Kuna namna hapo.
 
Hawa waislam sijui vp,wenzao wanawaza kuanzisha na kuendeleza shule,vyuo na hospitals wao wanang'ang'ania mahakama isiyokuwa na umuhimu kwa maendeleo ya taifa!
 
Hili ndio tatizo kubwa, wanadhani taratibu za ibada za kiislamu zi aweza kuwa sawa na za kwao. Kwanza kwa wakristo sheria si muhimu! Munadai mutaokolewa kwa neema au mtu fulani kutundikwa msalabani! No wonder wakristo hawana sheria madhubuti za kuzifuata. Kwa waislamu kuhukumiwa nje mwa sheria za Muumba ni kufur, na kunamtoa mtu kwenye uisilamu wake. Hivyo kama katiba inatoa uhuru wa kuabudu..kwa waislamu uhuru huo ni mpana zaidi ya kupiga gitaa! Hili siamini kama mnaweza kulielewa!.

Kuanzishwa mahakama y kadhi ndani ya dola n i muhimu ili ruling zake ziwe binding! Hata mabaraza ya usuluhishi ya kata yameanzishwa ndani ya dola!

Kama vipi tufuate ile sera ya CHADEMA, tugawane majimbo, wengine waanzishe hizo mahakama wengine wasianzishe kama ilivyo NIGERIA..
Hii nchi yetu wote na hatuwezi kulazimishwa kufuata mila za kiyahudi!
.

sasa wewe ndo inawezekana umesha aply kazi kwenye hiyo mahakama
 
Mbona imeanzishwa mahakama ya Ardhi na mahakama ya Biashara. Sasa kwanini isiwe hii ya kadhi?

Jiulizeni watakao pata huduma hapo watakuwa sio wa TZ. Je Serikali itaweza lipia watu wake watakao peleka masuala yao pale na kuhudumiwa? Lazima mjua kila mtanzania ana haki sawa na hakuna first citizen na second citizen. Wote mpo daraja moja nawashangaa wanaopinga?

Kuna namna hapo.

sasa wewe hujui hata maana ya hiyo mahakama ninini. unataka kufananisha mahakama ya kadhi na mahakama ya ardhi, kwani mahakama ya ardhi ni ya dini? we kweli hazikutoshi
 
Na wakiristu nao waanzishe mahakama ya Kikristu na yasimamiwe na Serikali au sio bana sasa sijui mahakama za serikali zitabaki kutoa huduma za wapagani au,uhuru ukizidi mpaka mwishowe ni machafuko,kwenye katiba kwa makusudi makubwa haikusema Tanzania ni nchi itakayoendeshwa kidini na hatta katiba itakayotungwa itakuwa vivyo hivyo kuwa TZ haina dini,kama mahakama ya kadhi basi ni hukoo Zanzibar ambako 99.999% ni waislamu (na inaendeshwa kama nchi ya kiislamu) na kama kuna kesi basi nendeni Zanzibar,mazingira ya Tanzania bara nitofauti na Zanzibar,lakini maandamano ni haki ya rai andamaneni tu wee wakati wenzenu wanaingiza njuruku mifukoni mwao,wenzenu wako madarasani wakibukua nyie endeleeni kuandamana,na mkishachoka kuandamana mtakuta wenzenu waliokuwa shule wako silabasi nyingine,nakuendelea,pia waambieni wanafunzi kama wa shule zenu wawaunge mkono kuandamana,gepu lilizidi kuwa kubwa,mmeshakuwa Chadema wa pili kila kitu kulalamika na kila siku kulalamika badala ya kutafakali hilo la mahakama mnalijua fika kuwa haliwezekaniki lakini baado ,mumeambiwa muanzishe wenyewe hamtaki mnataka eti serikali isimamie,loh hata kwenye mabenki mnapata faida kwa kuto kutoa riba kwa hela yangu ninayotoa riba ni kama unakataa kupokea mkono wa kulia na unapokea mkono wa kushoto
 
jamani waislamu wenzangu muwe waelewa serikali ya jamuhuri wa muungano haina dini na katiba ya jamuuri wa muungano ipo wazi kwa hili ndio maana kikwete kawapa ukweli,someni katiba ya nchi
 
Mbona imeanzishwa mahakama ya Ardhi na mahakama ya Biashara. Sasa kwanini isiwe hii ya kadhi?

Jiulizeni watakao pata huduma hapo watakuwa sio wa TZ. Je Serikali itaweza lipia watu wake watakao peleka masuala yao pale na kuhudumiwa? Lazima mjua kila mtanzania ana haki sawa na hakuna first citizen na second citizen. Wote mpo daraja moja nawashangaa wanaopinga?

Kuna namna hapo.

Nanyi muanzishe mahakama yenu ..... !

na wachawi nao waanzishe mahakama yao ..... !

narrow thinking
 
Mbona imeanzishwa mahakama ya Ardhi na mahakama ya Biashara. Sasa kwanini isiwe hii ya kadhi?

Na mbona hata Mabenk yenu wameanzisha utaratibu wa Bank kufuata utaratibu wa kuhifadhi pesa wa Kiislam ( Islamic banking) na sasa zina wateja wengi sana na wanazidi siku hadi siku. Lazima Serikali yenu iwe flexible kukubali changes.

Jiulizeni watakao pata huduma hapo watakuwa sio wa TZ. Je Serikali itaweza lipia watu wake watakao peleka masuala yao pale na kuhudumiwa? Lazima mjua kila mtanzania ana haki sawa na hakuna first citizen na second citizen. Wote mpo daraja moja nawashangaa wanaopinga?

Kuna namna hapo.

As far as JF iko na idadi ya kutosha ya Wislam tutegemee vituko kila post,hakuna anaepinga uanzishwaji ya mahakama ya kadhi,issue ni kwmba ianzishwe na waislam,iendeshwe na waislam uhudumie waislam,waislam hawataki waanzishe,wanataka waanzishiwe !!! Waendeshewe !!! iwahudumie wao.
 
sasa wewe hujui hata maana ya hiyo mahakama ninini. unataka kufananisha mahakama ya kadhi na mahakama ya ardhi, kwani mahakama ya ardhi ni ya dini? we kweli hazikutoshi

Ingawa waswahili husema ASIYEJUA MAANA USIMFUNZE MAANA lakini mimi nitavunja mwiko huo kwa kukujuza.

Mahakama ya Ardhi inashughulikia masuala yanayohusiana na mambo ya ardhi tu na si vinginevyo.
Mahakama ya kadhi itashughulikia masuala ya waislam hususan mirathi, talaka n.k na si vinginevyo.
Mahakama ya Biashara halikadhalika inashughulikia masuala yanayokhusu biashara tu.

Sasa kama una hoja , karibu.
 
  • Kuandamana usiku na mchana kushinikiza Mahakama ya Kadhi
JUMUIYA ya Taasisi za Kisilamu, imesema utatumia maandamano ya usiku na mchana, kushinikiza kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi na kwamba hatua hiyo inakuja baada ya kushindikana kwa njia ya kidiplomasia, kuhusu kuanzishwa kwa mahakama hiyo.

Hayo yalibainishwa jana na Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Shehe Issa Ponda, alipokuwa akisoma tamko la msimamo wa Taasisi za Kisilamu kufuatia kauli ya Rais Kikwete katika Baraza la Idd el Fitri, lililofanyika Septembe mosi mwaka huu mjini Dodoma, kuhusu kuanzishwa kwa mahakama hiyo.

Shehe Ponda alizitaja taasisi zilizokutana na kuazimia kutoa tamko hilo kuwa ni pamoja na Baraza Kuu, Jopo la Mashehe, Baraza la Vijana wa Kiislamu na Basuta.

Soma zaidi hapa Waislamu sasa kuandamana kushinikiza Mahakama ya Kadhi
Mungu naomba utende miujiza ili waislam wawe kama wakristo, na ukomeshe vitendo vyote vya kujitoa muhanga na umwagaji damu kwa visingizio vya kupigania maslahi ya dini, nani asiyejua nchi hii haiana dini? nani asiyejua kodi hulipwa mpaka na watu wasio na dini yeyote? iweje pesa zao zitumike kwa mambo ya kidini? Mahakama ya kadhi iwe chini ya wizara gani? na waziri wake awe dini gani? huu ni upuuuzi tu, mimi naamini kwamba watu kama Osama Bin Laden ni wahuni tu wasiotaka amani itamalaki duniani. Amen
 
As far as JF iko na idadi ya kutosha ya Wislam tutegemee vituko kila post,hakuna anaepinga uanzishwaji ya mahakama ya kadhi,issue ni kwmba ianzishwe na waislam,iendeshwe na waislam uhudumie waislam,waislam hawataki waanzishe,wanataka waanzishiwe !!! Waendeshewe !!! iwahudumie wao.MAZUZU KWELI KWELI

Nafikiri wewe umejichanganya. Kwa masingi wowote ule lazima serikali yenu angalie na kukubali maamuzi yake.

katika mfumo wa Mahakama ya kadhi, Mwenye mamlaka ya mwisho katika hukumu ni Chief Kadhi na hukumu yake haitenguki hata ukukata rufaa kwenye mahakama ya rufaa TZ.

Lakini vle vile watakaokwenda kushughulikiwa masuala yao ni wa TZ kama walivyo wa Tz wengine regardless dini yao ya Uislam. Je Serikali ya JMT itaweza kuwalipia hao raia wake walioamua kutumia makhakama hizi kutafuta haki zao?

Hapo ndio naona kuna kitu kimejificha. Chukulia mfano Kenya zipo na afisi zao zinakuwa kwenye mahakama zao za kawaida kwani wanaopata huduma ni wananchi kama wengine nao wana haki sawa na wengine.

Fungukeni jamani sio kupinga. Mbona hamuulizi JMT inapotoa Ruzuku kwenye mashirika ya dini kama hospitali kama Bugando, KCMC n.k.

Kwa waislam inakuwa Nongwa. Au ndio yale yale kunya anye kuku, akinya bata ......
 
Ingawa waswahili husema ASIYEJUA MAANA USIMFUNZE MAANA lakini mimi nitavunja mwiko huo kwa kukujuza.

Mahakama ya Ardhi inashughulikia masuala yanayohusiana na mambo ya ardhi tu na si vinginevyo.
Mahakama ya kadhi itashughulikia masuala ya waislam hususan mirathi, talaka n.k na si vinginevyo.
Mahakama ya Biashara halikadhalika inashughulikia masuala yanayokhusu biashara tu.

Sasa kama una hoja , karibu.

Kuna wakati unafikiri vema,wakati mwingine sijui nini? Mahakma ya ardhi. ni mahakama ya dini gani ?,Mahakama ya biashara.Na mahakama ya dini gani ?

Toka ndani ya box linakusbabishia upungufu katika uwezo wako wa kufikiri.
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Nafikiri wewe umejichanganya. Kwa masingi wowote ule lazima serikali yenu angalie na kukubali maamuzi yake.

katika mfumo wa Mahakama ya kadhi, Mwenye mamlaka ya mwisho katika hukumu ni Chief Kadhi na hukumu yake haitenguki hata ukukata rufaa kwenye mahakama ya rufaa TZ.

Lakini vle vile watakaokwenda kushughulikiwa masuala yao ni wa TZ kama walivyo wa Tz wengine regardless dini yao ya Uislam. Je Serikali ya JMT itaweza kuwalipia hao raia wake walioamua kutumia makhakama hizi kutafuta haki zao?

Hapo ndio naona kuna kitu kimejificha. Chukulia mfano Kenya zipo na afisi zao zinakuwa kwenye mahakama zao za kawaida kwani wanaopata huduma ni wananchi kama wengine nao wana haki sawa na wengine.

Fungukeni jamani sio kupinga. Mbona hamuulizi JMT inapotoa Ruzuku kwenye mashirika ya dini kama hospitali kama Bugando, KCMC n.k.

Kwa waislam inakuwa Nongwa. Au ndio yale yale kunya anye kuku, akinya bata ......

Uislam hauwezi kujitosheleza wenyewe mambo yake hadi msaada wa serikali,kwani mashule na mahospital yana hudumia kwa misingi ya dini ? Funguka ndugu yangu,mahakama ya kadhi na mahakama kwa ajili ya mashauri ya waislam peke yao,snzisheni ziendesheni mufaidi matunda yake,mkiingiliwa na yeyote lalamikeni,uhuru wa kuabudu ni pamoja na uhuru wa kuchagua mahakama ya kukuhukumu kidini,naamini ukuiamua kuwa muislam utakuwa automatically umekubali kuhukumiwa na mahakama ya kadhi katika mashauri ya kidini,lakini ukiukana uislam hufungwi na sharia za mahakama ya kadhi, wapi na kwanini mwataka serikali iwe na mkono kwenye hiyo mahakama kwanini hamjiamini ? nani amesema kwamba hukumu yenu itapelekwa JMT courty of appeal ? iende kufanya nini wakati mahakama yenu itakuwa imejitoshereza na waislam watakuwa wanajua muundo wake na utendaji wate ? una matatizo gani kuelewa hilo ndugu yangu
 
walisema huyo muislamu mwenzetu atatusaidia sasa kawachinjia baharini...............................
 
Mbona imeanzishwa mahakama ya Ardhi na mahakama ya Biashara. Sasa kwanini isiwe hii ya kadhi?

Na mbona hata Mabenk yenu wameanzisha utaratibu wa Bank kufuata utaratibu wa kuhifadhi pesa wa Kiislam ( Islamic banking) na sasa zina wateja wengi sana na wanazidi siku hadi siku. Lazima Serikali yenu iwe flexible kukubali changes.

Jiulizeni watakao pata huduma hapo watakuwa sio wa TZ. Je Serikali itaweza lipia watu wake watakao peleka masuala yao pale na kuhudumiwa? Lazima mjua kila mtanzania ana haki sawa na hakuna first citizen na second citizen. Wote mpo daraja moja nawashangaa wanaopinga?

Kuna namna hapo.

jamaa yangu fikiria kwanza.mahakama ya ardhi inamhudumia kila mtanzania kama ilivyo mahakama ya biashara na ndio maana mahakama hizi zinaendeshwa kwa kodi za watanzania.lakini mahakama ya kadhi itahudumia waislamu pekeyao kwanini iendeshwe kwa kodi za watanzania?kumbuka unapotamka neno 'mtanzania' unakua umejumuisha waislamu na wakristo lakini ukishasema muislamu tayari umebagua huwezi tena kuleta utanzania ktk huo ubaguzi.hamjakatazwa kuanzisha!!!nyie anzisheni lakini tumieni hela zenu.msitake kutumia mpaka michango yetu ya kodi kujinufaisha pekeyenu.hii idea ni ya kibinafsi zaidi na waislam ndio wanakua wabinafsi kwa kutaka kutumia tunachochangia wote kujinufaisha wao peke yao!!
 
Uislam hauwezi kujitosheleza wenyewe mambo yake hadi msaada wa serikali,kwani mashule na mahospital yana hudumia kwa misingi ya dini ? Funguka ndugu yangu,mahakama ya kadhi na mahakama kwa ajili ya mashauri ya waislam peke yao,snzisheni ziendesheni mufaidi matunda yake,mkiingiliwa na yeyote lalamikeni,uhuru wa kuabudu ni pamoja na uhuru wa kuchagua mahakama ya kukuhukumu kidini,naamini ukuiamua kuwa muislam utakuwa automatically umekubali kuhukumiwa na mahakama ya kadhi katika mashauri ya kidini,lakini ukiukana uislam hufungwi na sharia za mahakama ya kadhi, wapi na kwanini mwataka serikali iwe na mkono kwenye hiyo mahakama kwanini hamjiamini ? nani amesema kwamba hukumu yenu itapelekwa JMT courty of appeal ? iende kufanya nini wakati mahakama yenu itakuwa imejitoshereza na waislam watakuwa wanajua muundo wake na utendaji wate ? una matatizo gani kuelewa hilo ndugu yangu

Kinachobainishwa hapo ni kuingiza mfumo wa mahakama ya kadhi ndani ya mfumo wenu wa Mahakama ili kusilete mgongano wa maamuzi yake na mahakama za kawaidia kama walivyoweka hata wenzenu Kenya.

Nitakupa mfano mdogo sana wa mabaraza ya ardhi ya kata na mahakama za mwanzo. haya hayaingiliani katika mamuzi sababu yamewekwa pale kisharia. Sasa kwanini unakwepa mahakama ya kadhi.

Mimi naamini wazi watakao pata hudima kwenye mahakama hizi ni raia wa Tanzania kama walivyo raia wengine wa Tz na hivyo kupunguza msongamano wa kesi nyyingi sana za madai kama talaka na miradhi katika mahakama zenu.

Suala langu hapa. Je Serikali ya JMTz ipo tayari kuwalipia wa TZ kama raia wake watakaoamua kutumia mahakama hizi kutafuta haki zao?

Fungukeni kiakili na mjitoe katika mental slavery.
 
Kuna wakati unafikiri vema,wakati mwingine sijui ni hayo majini yanakupumbaza ? Mahakma ya ardhi. ni mahakama ya dini gani ?,Mahakama ya biashara.Na mahakama ya dini gani ?

Toka ndani ya box la uislam linakusbabishia upungufu katika uwezo wako wa kufikiri.

Kwanini unafikiria katika upande wa DINI. sasa naomba ufunguke zaidi na kuangalie mbaaaaaaaaali zaidi ya dini kuna URAIA.

Je watakao hudumiwa na mahakama za Kadhi watakuwa sio raia wa Tanzania. Au huko kwenu waislam hawachukuliwi kama Raia na hawalipi kodi?
 
Waweza tukana unavyotaka hiyo haibadilishi ukweli! Akili zako zinakutuma uone kitimoto na mbege ni bora kuliko kahawa na mbuzi!
Unaweza kuabudu chochote unachotaka hakuna anayekuzuia...ila usilazmishe wengine wafanye unavyotaka wewe..
Kama wewe unaona bora kumwabudu mwanadamu mwenzako aliyekula na kunya...poa..
Au kama unaona kuwa na board ya miungu in trinity ni akili endelea nazo tutajua mbele ya safari.......
 
Mimi kwa mtazamo wangu hawa waislamu wanapaswa kuelemishwa. Wameshaambiwa waanzishe mahakama. Hawakatazwi, lakini mahakama hiyo iwe nje ya mfumo wa serikali. Wakatoliki wana mahakama yao. Tena Hakimu alikuwa wakati huo paroko wa kipawa, Padre Kimario ambaye sasa ni Askofu wa Same. Anglikana wanayo mahakama na waruteli wanayo. Sina uhakika makanisa ya kakobe na mwingira. Sasa ili mahakama ya kadhi iwekwe kwenye katiba basi, ziwekwe zote. Mie nawashauri waanzishe kwanza ili yale mapungufu ya kutokuwemo kwenye katiba yaonekane.
Tatizo linalowasumbua waislamu ni elimu ndogo za maimamu wao hawa-judge mambo critically wanachukulia kirahisi tu na mara nyingi kwa jaziba.
 
jamaa yangu fikiria kwanza.mahakama ya ardhi inamhudumia kila mtanzania kama ilivyo mahakama ya biashara na ndio maana mahakama hizi zinaendeshwa kwa kodi za watanzania.lakini mahakama ya kadhi itahudumia waislamu pekeyao kwanini iendeshwe kwa kodi za watanzania?kumbuka unapotamka neno 'mtanzania' unakua umejumuisha waislamu na wakristo lakini ukishasema muislamu tayari umebagua huwezi tena kuleta utanzania ktk huo ubaguzi.hamjakatazwa kuanzisha!!!nyie anzisheni lakini tumieni hela zenu.msitake kutumia mpaka michango yetu ya kodi kujinufaisha pekeyenu.hii idea ni ya kibinafsi zaidi na waislam ndio wanakua wabinafsi kwa kutaka kutumia tunachochangia wote kujinufaisha wao peke yao!!

Labda nikuulize kwani mkristo akienda kudai haki yake kwa kutumia mahakama ya kadhi atakataliwa? Mbona Islamic banking huko Tz nasikia kuna wakristo wengi sana wanajiunga.

Mbona aulalamiki ruzuku kubwa sana kutoka Serikalini zinazopewa shule na hata vyuo na mahospitali ya taasisi za kidini kama KCMC na Bugando?

Au ni kama ulivyobainisha kuwa waislam sio sehemu ya walipa kodi na hivyo hawastahikhi hata kidogo kula matunda ya kodi hizo.

Ama kweli Tanganyika na UDINI na kama pete na chanda. Muungano unaficha mengi.

Kila la kheir
 
Back
Top Bottom