JK keshasema waislam mnaweza kuanzisha mahakama ya kadhi kwa utaratibu wenu ndani ya dini yenu, kwa gharama zenu na kuzisimamia nyie wenyewe na sio serikali. Kwa kuwa mahakama hiyo ni ya kidini na itatatua mambo yenu ndani ya dini yenu (Ndoa, Talaka, Wakfu, Mirathi, Urithi) na serikali ya Tanzania haina dini. Hii ni kutokana na utafiti & ushauri ambao serikali imeupata kutoka kwa wataalam wa kisheria (za kawaida& kiislam). Sasa hili la hawa waislam kutaka serikali ndio iwaanzishie, izisimamie & inziendeshe mahakama za kadhi, linaleta utata mkubwa, nina uhakika kuna jambo lilikuwa limejificha nyuma ya mpango wa kudai mahakama ya kadhi.
Nina hamu kubwa kumsikia Shekh mkuu Mufti Simba akitoa kauli ya kupinga au kuunga mkono mpango huu, kwa kuwa mara nyingi amekuwa akiwabeza wapinzani wanaoandamana dhidi ya utawala wa JK, akidai kuwa JK anaandamwa kwa kuwa tu ni muislam na huku akiwahamasisha waislam wamuunge mkono JK kwa kuwa ni muislam mwenzao!!