mungu wetu atuepushie balaa ya mambo haya ya OIC na mahakama ya kadhi. nafikiri mambo haya wala hayakupaswa kuzungumziwa katika nchi hii! Tuna mambo mengi ya msingi ya kushughulikia katika kuondokana na umaskini wetu na haya hayaingii kwenye equation.
Ukiondoa faida yake kijamii/kidini kwa waislamu,kiuchumi suala la mahakama ya kadhi halina tija na wakati huu si muafaka kutumia rasilimali muda na fedha kulizungumzia.
Matatizo mengine tunayatafuta wenyewe kama taifa wala hayakupaswa kuwepo kwenye nchi isiyo na dini (secular state) kama Tanzania.
Namuomba mungu wa ibrahimu,isaka na yakobo atuepushie mbali mambo haya ya udini kuingia katika uendeshwaji wa nchi yetu.
Mungu ibariki Tanzania yangu isiyoegemea upande wowote wa dini,Mungu ibariki Afrika
kazi kwelikweli mapovu yatawakauka, na keyboard zitachunika! naona baada ya OIC na kadhi patakuwa hamna tena cha kujadili
Hii ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Usitufananishe na hao wa Somalia na Nigeria. Wewe huoni kuwa unadekshia na uhuru wako wa kutoa maoni - huria!!!!!!!!That wont be the end but the beginning of an end! Tukishamaliza hayo tutaomba Mahakama za Wakristo, wasukuma, wachaga, etc. Watu wakianza kupigwa mawe, kukatwa mikono, etc na wafuasi wa Shetani Muhammad patakalika kweli hapo? Usifikiri wafuasi wa Muhammad wakipata hivyo ndio watatulia, look at Somalia, juzi Wakristo saba wamekatwa vichwa kwa sababu tu ya kuwa wakristo! Tazama Nigeria hapakaliki mpaka sasa! Open thy eyes!
sawa.Hiyo ni negative propaganda. Wewe nenda kaishi kule Zanzibar angalau kwa miezi mitatu -uone yanafanyika hayo? Mtoto wa Kikiristo (miaka 18) amempenda mtoto wa Kiislamu. Si kapenda? kwa kwetu kule ndoa haifungikiki mpaka Mkiristo akubali kuwa Muislamu. Anyway ni mambo ya ustawi wa jamii hayo. Lakni kuwa makini na Negative propaganda.
[ame=http://www.youtube.com/watch?v=ZWr1qHDSznA]YouTube - Persecution and Revival of the Church in Islamic Zanzibar[/ame]sawa.Hiyo ni negative propaganda. Wewe nenda kaishi kule Zanzibar angalau kwa miezi mitatu -uone yanafanyika hayo? Mtoto wa Kikiristo (miaka 18) amempenda mtoto wa Kiislamu. Si kapenda? kwa kwetu kule ndoa haifungikiki mpaka Mkiristo akubali kuwa Muislamu. Anyway ni mambo ya ustawi wa jamii hayo. Lakni kuwa makini na Negative propaganda.
Hii ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Usitufananishe na hao wa Somalia na Nigeria. Wewe huoni kuwa unadekshia na uhuru wako wa kutoa maoni - huria!!!!!!!!
Kuleta muswada wa kuzuia mjadala wowote wa dini kutazua maswali mengi kuliko majibu. Kwanza mjadala upi wa dini na upi si wa dini? Wapi una draw the line? Je wabunge wataruhusiwa ku nukuu vitabu vya dini? Je miswada ya serikali inayohusu dini (kodi za taasisi za kidini, structures za vyombo vya kidini) itaruhusiwa.
Kinachohitajika si kuzuia mijadala hii, bali ni kuongelea mambo kwa upana zaidi ili tuone ubaya/uzuri wake.
Hizi orwellian constructs za kuzuia watu kuongea zilitakiwa kufa na ukomunisti.
Nyalandu amekuwa so clear kwaba Serikaloi isijihusishe na kusaidia wala nini kuunda chombo cha dini .Full stop na kama watafanya mambo yao huko misitini ni sawa again Pinda anatakiwa sasa kusema waislam wafanye wenyewe mambo yao na serikali haiko na haitaisaidia katika mmchakato wowote .
Nyalandu amekuwa so clear kwaba Serikaloi isijihusishe na kusaidia wala nini kuunda chombo cha dini .Full stop na kama watafanya mambo yao huko misitini ni sawa again Pinda anatakiwa sasa kusema waislam wafanye wenyewe mambo yao na serikali haiko na haitaisaidia katika mmchakato wowote .Wo wao kama wao waendelee wasitake msaada wa serikali wakisha fanya hilo then maneno ya OIC na Kadhi yaondoke Bungeni mle ndani yawe misikitini .Nyalandu ana maana hii .Namuunga mkono huyu rafiki yangu siku zote napingana naye kwa mengi na hata majuzi tukiwa Munich na baadaye Arusha nilimweleza msimamo wangu na Chama chake ila kwa hili niko naye
Kama mbunge hawezi kuongelea jambo bungeni, uhuru wa kuongea uko wapi Tanzania?
Kama hoja haina msingi, izimwe kwa nguvu ya hoja nyingine, si kwa hoja ya nguvu kama hii inayotaka kuletwa na Nyarandu.
Naunga mkono kuwa habari hizi ni muhimu zisizungumzwe bungeni, lakini tukianza na hili leo bungeni, kesho tutasema EPA na Meremeta zisiongewe, tutasema Muungano usijadiliwe, mwishoe tutasema bajeti ipitishwe tu isijadiliwe.
This is an important precedent ambayo hatutakiwi kuifanya.Tayari tusha cross Rubicon na Meremeta, sasa tukiwa tunaongeza issues kwenye list hii tutliondoa bunge letu kutoka bunge butu kuja kuwa bunge bubu.
Kwenye bunge wabunge wapewe kinga ya kuongea hata visivyoongeleka, hatutaki wafungwe midomo.
Kuna issues zitasemwa lakini si hii ya upande mmoja kila mara Uislam , Waislam, OIC , Kadhi , kuonewa waislam nk now way .Ndiyo maana Makinda alikanyaga mafuta leo na kumwacha Mdhihiri analia lia .Hii ni ishara kwamba watu wamechoka kupindishiwa hoja .Kesho kadhi watasema mtoto wa Mdhihiri kaiba akatwe mkono yeye atakubali ?Wakubaliane pembeni huko na si kutuhusisha sisi .