Lunyungu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 8,873
- 1,925
Muda sasa umefika wa kila mtu kubeba msalaba wake .Wakati wanalia na kuitukana Chadema kwa jina la wakabila na chama kama NGO hawakujua kwamba yale yaliyo mkumba Mtikila Tarime na yaliyo wakumba KAFU na muafaka yatawafika .Najua sasa wataanza kupita na kuzua hoja oh wapi msimamo wa Upinzani juu ya swala la Kadhi na OIC.Nasema Chadema ni chama makini endeleeni kuwapa watu Elimu na kuibana Serikali juu ya ufisadi acheni hoja ya hii ya Udini ni CCM na uroho wao .Achana wapambane maana Chadema naamini ni Chama cha wote bila ya kujali dini zao na hata kipato chao .Nina furaha kwamba hadi sasa si Chadema Bungeni wala Chadema nje jukwaani imerukia swala hili kama Mrema na TLP na KAFU na sasa CCM. Waacheni wasulibishane lakini Chama makini simamieni issues msiwe derailed .Mnanisoma hapa akina Mtei , Slaa na Mbowe , Zitto , Mrema na wengine wote wana Chadema chonde , matumaini yetu yako kwenu .Endeleeni nakumwaga Elimu na kuwafungua Watanzania masikio , kimbieni kule vijijini mkajipange huko nasi tunakuja kuwapa support .Huu ni mwiba mkali CCM inamchoma tuone atafika wapi .