Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Mkuu nchi inaongozwa kwa katiba na sheria.
Siamini kama Tanzania inaendeshwa na Katiba na Sheria ,naona ni vurugu mechi tu ,maana haiwezekani sheria iwe inahusu upande mmoja tu ,waislamu wanapotoa madai inabidi iangaliwe sheria,wanachama wapinzani wanapojiandikisha inabidi wafuate sheria,vyama vya upinzani vinapofanya mikutano inabidi viangalie sheria ,mgombea waupinzani anaposhindwa inabidi ifuatwe sheria ,tume ya uchaguzi inapotangaza matokeo ya ushindi wa wizi inabidi ifuatwe sheria ,mapapa na manyangumi wanapoiibia serikali inabidi ifuatwe sheria na kama haitoshi iundwe tume na kamati kuchunguza wizi huo ,ila wahujumu uchumi wengine wao wanatakiwa wafuate sheria ya papo kwa papo.
Hivi ni sheria gani na katiba gani unayoizungumzia wewe ,vipimo vingi hivyo hapo juu inaonywesha sheria haifuatwi ila kwa wachache ?
 
uitishwa mjadala wa kitaifa ....pia gharama zao na mipaka na haki na wajibu wa serikali na mahakama zake ziwe wazi na watendaji wajue wazi kuwa kesi hii inaanagukia wapi....pia makahama za rufaa yaani vurugu tupu...sijui ila linajadilika....

It is illogical kuwa na mjadala wa kitaifa kuhusu dini moja. Kwa nini wasiongelee huko misikitini na kumalizana wenyewe wenye dini? Hiyo ibada ya kiislamu inawahusuje wengine?
 
Nimerudia tena kusoma post ya kwanza hapa ambayo niliandika 2006 na makala nyingine nilizofafanua hili. Inashangaza imechukua serikali miaka mitatu kufikia hitimisho hilo hilo ambalo halikutahitaji utaalamu wa Fizikia ya Anga kulifikia! Nina uhakika wametumia fedha nyingi tu kuweza kujadiliana na hatimaye kufikia msimamo ambao ni wabure!
 
Katika hili nadhani Pinda ameonesha ujasiri mkubwa!

Kwa mtizamo wangu, jambo hili lilitakiwa litolewe ufafanuzi na mwenyekiti wa sisiemu taifa. Anatakiwa awaeleze waislamu ni kwa nini serikali ya chama chake haipo tayari kutekeleza moja ya ahadi zake ilizozitoa katika kampeni zao na katika ilani ya uchaguzi.

Kama walichemka kuweka mahakama ya kadhi kwenye ilani ya uchaguzi basi waseme na wawaombe radhi waislamu waliopigia kura sisiemu kwa kudhani kuwa watapata mahakama ya kadhi itakayohudumiwa na serikali.
 
Katika maamuzi ya busara ambayo serikali hii imefanya (kama yapo!), hili ni moja wapo - kuitenga serikali mbali na masuala ya ibada ya dini fulani. Acha wafuasi wa dini wajiendeshee wenyewe masuala ya ibada zao bila kuingiliwa na serikali. Kwa hili NAWAPA FIVE!
 
Kwa nin watu hawaangalii hii ishu kwa mapana na marefu? Suala sio kukataa au serikali kugharamia. Nafikiri Waislam watakuwa na uwezo wa kuendesha hii mahakama.

Suala liko kwenye sheria nzima za nchi, na sijui tuanzie wapi. Kwa sasa, nafikiri mahakama ya nchi ina uwezo wa kurudisha baadhi ya kesi za ki-familia au jamii kwa wazee wa koo kwa usuluhisho wa hizo kesi. Kumbuka kesi kama hizi zinaanzia polisi (chombo halali cha dola)

Kuja kwenye mahakama ya kadhi, nani atakayekuwa anakamata wanaovunja sheria? Mimi nisipovaa HIJABU, ni askari yupi ataniuliza mbona sijavaa hijabu? Atajuaje mimi ni Muislamu au sio? Kama mimi ni Muislam na sikubaliani na baadhi ya sheria zake, rufaa yangu itasikilizwa wapi kama Mtanzania na raia wa kawaida? Serikali ina nafasi gani ya kuwalinda watu kama mimi? Sheria gani itabidi itungwe kutulinda? Kama mahakama ya kawaida itatumika kusikiliza rufaa yangu, je kutakuwa na ushahidi wowote? Je kutakuwa na POLISI WA KIISLAMU (Mzee Kifimbo-Cheza) kama Saudia?

Maswali li mengi sana. People need to analyze this issue as well as the government. It is not an overnight thing.

Goodluck!

Hakuna cha kuumiza kichwa hapa! Nilidhani zitahusu mambo ya ndoa, mirathi na talaka kama wanavyodai waislamu kumbe kuna zaidi ya hapo? Polisi kwa mambo ya ndoa, mirathi na talaka? Na kama mtu hajavaa hijab ndio akamatwe na polisi yupi? Nilisema mahakama za kadhi ni daraja la kutaka kuisilimisha nchi! Tukatae kwa nguvu zote mahakama hizi kuingizwa kwenye kuhudumiwa na dola!
 
Hapo ndo penyewe palepale pa Maimuna kubadilika ghafla akawa Mariatereza! lol!
 
Hapa hapahitajiki ushabiki wa kidini, hili jambo kama hatutakuwa makini halijadiliki hata kidogo, maana hili ni suala ambalo linahusu taifa kwa ujumla, amani ikitoweka hapatakuwepo cha mwisalam au mkiristo, so let us be careful kipindi tunajadili hii maada tamu,ila pinda ame make it very clear, hizo mahakama hazitahudumiwa na serikali,sass je hao mahakimu wataajiliwa na nani na watalipwa na nani, hilo ndo suala lilobaki la kujadiliwa japo kuajili siyo issue, je hizo mahakama zitaendelea kupokea misaada kwa ajili ya kuwalipa watumishi wake au la!, serikali inatakiwa kuwa makini, ikisema hakuna mahakama hiyo Tanzania, lazima iwe straight forward, na ikisema ndiyo, iwajibike kuwalipa mishara wanafanyakazi wote wa mahakama hizo.Je wakirsto watajisikiaje kama serikali ikiamua kuchukua hilo jukumu la kuwalipa mishara, hapo ndipo patakuwa patamu sana.kama wataka kura za hao ndugu zetu, wafanye mambo kwa kukurupuka, yatawatokea puani.
 
Mimi bado sioni kama ni sahihi. hivi wahehe wakidai mfumo wa sheria ulikuwepo kwenye jamii yao kabla ya kuvurugwa kwa wakoloni itakuwaje. wanyanyembe watabora nao wakidai mfumo wao wa sheria, hivyo hivyo wale wa msovero na kwingineko si tutaligawanya taifa.

Kwa nini huu utamaduni wa kikoloni uonekane ni bora kuliko utamaduni wetu halisi. nasema utamaduni wa kikoloni sababu dini kuu mbili ( wakiristu na waislamu) ni dini zakikoloni. dini hizi hazikuwa sehemu ya utamaduni wetu . zililetwa zikapandikizwa na hii leo sisi tulioletewa ndio tunajifanaya kuzijua zaidi hata ya wale waanzilishi. Tumefikia hata kukana tamaduni zetu.

Kwa kukuza umoja wa kitaifa serikali wala haitakiwi kuongelea suala la mahakama ya kadhi. serikali iongelee mfumo wa mahakama za kijadi na kimila uliovurugwa na wakoloni amabao lo hii unesaidia matatizo ya mauaji ya albino na matatizo kama ya kule rorya na tarime.
 
1.Kama watu wanajua historia ya nchi hii ni kwamba hii mahakama ilikuwepo tangu kipindi cha ukoloni.
2.Kuhusu alichosema Pinda,angetakiwa kujiuliza awali hii mahakama ilikuwa inahudumiwa na nani?Lakini pia,angestahili kuchukua baadhi ya nchi ambako mahakama kama hii iko na inafanya kazi kama vile UK,Uganda nakadhalika halafu ndiyo atupatie jibu nani anastahili kuihudumia hii mahakama.Kwasababu kwa hii habari iliyoripotiwa hapa bado haina jibu la nani atakae hudumia!
Hata hivyo hizo mahakama nyingine zinahudumiwa na nani?Kama maamuzi yatabakia kama Pinda alivyosema basi ni full ubaguzi na siyo vinginevyo.
Hii ni sawa na mvulana kuingia choo cha kike and vice-versa is true.

Sasa wakati wa ukoloni na kabla ya ukoloni nani alikuwa akiihudumia hii mahakama? Sababu hatukuwa na serikali...! Huyo aliyekuwa akihudumia wakati huo ndio anapaswa kuhudumia sasa.
 
Sasa wakati wa ukoloni na kabla ya ukoloni nani alikuwa akiihudumia hii mahakama? Sababu hatukuwa na serikali...! Huyo aliyekuwa akihudumia wakati huo ndio anapaswa kuhudumia sasa.

Peasant na wenzako!

Hivi hiyo ujinga mliokuwa nao wa elimu ya kupepea utawatoka lini!! Nilikwisha sema Pinda hajui wala haisomi Katiba just in the same way as JMK. Zanzibar kuna Kadhi; Uganda kuna kadhi hawa wapumbavu na wachovu waTZ Hawajui watakalo mahakama ya kadhi haiwezi kuwepo becuase ni kinyume cha katiba period.

Narudia kama Waislamu wanao msuli wanaowatishia CCM nyau wakomae tubadili katiba waruhusiwe kuwa na Sharia Law! Why go for a fake au fotokopi wakati original ipo?

These people kweli shule ni taabu since sharia law is inhuman na nyie mwategemea tende na nyama ya kondoo kutoka Suadia hamtaweza kuitimiza sharia katika karne hii ya 21. Just go to Nigeria sharia law iko kule kaskazini but they have failed kumkata mikono hata mtu mmoja for the past 10years!!! Sasa kwa nini mwataka hii mahakama uchwara ya KADHI hilo haliwezekani kwani watu wasiokuwa waislamu watasigana na nyie kinoma labda muanzishe JAMHURIYA YENU!!! tena hewani!!! Kalakabaho!!!!
 
Katika hili nadhani Pinda ameonesha ujasiri mkubwa!

Kwa mtizamo wangu, jambo hili lilitakiwa litolewe ufafanuzi na mwenyekiti wa sisiemu taifa. Anatakiwa awaeleze waislamu ni kwa nini serikali ya chama chake haipo tayari kutekeleza moja ya ahadi zake ilizozitoa katika kampeni zao na katika ilani ya uchaguzi.

Kama walichemka kuweka mahakama ya kadhi kwenye ilani ya uchaguzi basi waseme na wawaombe radhi waislamu waliopigia kura sisiemu kwa kudhani kuwa watapata mahakama ya kadhi itakayohudumiwa na serikali.

Suala sio kuweka mambo ya kadhi kwenye ilani. Suala ni kwamba kuhusu mahakama ya kadhi ilani ilikuwa inasemaje, na sio kukurupuka. Ilani ilisema kwamba serikali ingeangalia uwezekano wa kutatua suala la mahakama ya kadhi. Je, huko unakosema kugharamiwa na serikali kwa mahakama za kadhi kuliandikwa kwenye ilani? Kama hakujaandikwa kuna umuhimu wa kuomba msamaha? Kwani waislamu kugharamia mahakama za kadhi, ambayo ni ibada yao ya kidini, SIO KUTATUA SUALA LA MAHAKAMA ZA KADHI? Acheni kutubabaisha hapa!!
 
Peasant na wenzako!

Hivi hiyo ujinga mliokuwa nao wa elimu ya kupepea utawatoka lini!! Nilikwisha sema Pinda hajui wala haisomi Katiba just in the same way as JMK. Zanzibar kuna Kadhi; Uganda kuna kadhi hawa wapumbavu na wachovu waTZ Hawajui watakalo mahakama ya kadhi haiwezi kuwepo becuase ni kinyume cha katiba period.

Narudia kama Waislamu wanao msuli wanaowatishia CCM nyau wakomae tubadili katiba waruhusiwe kuwa na Sharia Law! Why go for a fake au fotokopi wakati original ipo?

These people kweli shule ni taabu since sharia law is inhuman na nyie mwategemea tende na nyama ya kondoo kutoka Suadia hamtaweza kuitimiza sharia katika karne hii ya 21. Just go to Nigeria sharia law iko kule kaskazini but they have failed kumkata mikono hata mtu mmoja for the past 10years!!! Sasa kwa nini mwataka hii mahakama uchwara ya KADHI hilo haliwezekani kwani watu wasiokuwa waislamu watasigana na nyie kinoma labda muanzishe JAMHURIYA YENU!!! tena hewani!!! Kalakabaho!!!!

Mbona povu lakutoka?! Kuita watu wajinga si ujanja! Angalia tena post yangu utajua nauliza nini, maana ninaamini serikali ya Tanzania/Tanganyika haijawahi kuhudumia hii mahakama hivyo sioni sababu kwa nini ianze sasa..!
BTW, grow up and try to find life!
 
It is logic, hakuna mtu anayepinga mahakama ya kadhi kuundwa Tanzania,tatizo kubwa ni kuhudumiwa na serikali, that is totally deplorable due to the fact that Tanzania is a secular state, how comes walazimishe serikali kuihudumia hizo mahakama?? serikali ikiamua kufanya hivyo itakuwa imekika katiba ya nchi.Hiyo mahakama iundwe na ihudumiwe na waislam wenyewe.Siyo kila kitu kinapendeza pale ambapo watu fulani kwa manufaa yao wanalazimisha kifanyike.
hivi CCM walipoweka hii kitu kwenye ilani yao hawakujua hilo..mi naona wanaweweseka tu
 
Kuna wakati niliweka mada hii kuhusu Mfumo wa Mahakama za Kadhi Zanzibar, kulingana na The Kadhis' Courts Act, 1985, No. 3 of 1985, sikuona kama kulikuwa na wachangiaji wengi. Naleta hapa mada na mnaweza kuona kwamba lengo la waislamu ni kuifanya nchi kuwa ya kiislamu, it is a long term process! Hii mahakama ya Kadhi ni daraja tu. Tunaweza kujifunza kulingana na Sheria hii ambapo mambo ya kiserikali yamejichanganya na mambo ya dini ambapo unaweza kusema kwa haraka haraka kuwa Zanzibar ni nchi (kama ni nchi anyway) ya kiislamu:
1. Kifungu cha 3 (1) cha Sheria hiyo kimeunda Mahakama za Kadhi kulingana na Ibara ya 99 (1) ya Katiba ya Zanzibar, 1984.
2. Kifungu cha 3 (1), Kutakuwa na Mahakama ya Kadhi Mkuu wa Zanzibar na Mahakama za Kadhi kwa kila Wilaya.
3. Kifungu cha 4 (1) na (2), Kutakuwa na Kadhi Mkuu (Chief Kadhi) ambaye atateuliwa na kuapishwa na Rais wa Zanzibar.
4. Sifa za kuwa Kadhi Mkuu [Kifungu cha 4 (3)]: Kuwa na kufuata dini ya Kiislamu, kuwa na taaluma ya Sheria za Kiislamu ambapo kwa maoni ya Rais anafaa kuteuliwa kushika nafasi hiyo (ya Ukadhi Mkuu).
5. Kifungu cha 5 (1): Kutakuwa na idadi ya makadhi, ambao hawatapungua kumi na hawatazidi kumi na watano ambao watateuliwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama (the Judicial Service Commission) kwa kushirikiana na Rais na Kadhi Mkuu.

Hayo ni machache kati ya mengi kuhusu Mahakama ya Kadhi, Zanzibar. Je, kukiwa na Rais Mkristo au wa dini nyingine atamteua Kadhi Mkuu kwa Zanzibar? Au haiaminiki kwamba Rais asiye mwislamu hawezi kuchukua madaraka Zanzibar?
 
Pinda amewapindisha hasa waislamu wasioelewa..kama mwataka mahakama ya kadhi nendeni mkawaombe hao waarabu wawapeni pesa za kuendesha mahakama zenu.
kabla ya kukimbilia misaada ya OIC
tuone jinsi gani waarabu watakavyotoa hela za kuendesha mahakama ya kadhi
 
Kuna wakati niliweka mada hii kuhusu Mfumo wa Mahakama za Kadhi Zanzibar, kulingana na The Kadhis' Courts Act, 1985, No. 3 of 1985, sikuona kama kulikuwa na wachangiaji wengi. Naleta hapa mada na mnaweza kuona kwamba lengo la waislamu ni kuifanya nchi kuwa ya kiislamu, it is a long term process! Hii mahakama ya Kadhi ni daraja tu. Tunaweza kujifunza kulingana na Sheria hii ambapo mambo ya kiserikali yamejichanganya na mambo ya dini ambapo unaweza kusema kwa haraka haraka kuwa Zanzibar ni nchi (kama ni nchi anyway) ya kiislamu:
1. Kifungu cha 3 (1) cha Sheria hiyo kimeunda Mahakama za Kadhi kulingana na Ibara ya 99 (1) ya Katiba ya Zanzibar, 1984.
2. Kifungu cha 3 (1), Kutakuwa na Mahakama ya Kadhi Mkuu wa Zanzibar na Mahakama za Kadhi kwa kila Wilaya.
3. Kifungu cha 4 (1) na (2), Kutakuwa na Kadhi Mkuu (Chief Kadhi) ambaye atateuliwa na kuapishwa na Rais wa Zanzibar.
4. Sifa za kuwa Kadhi Mkuu [Kifungu cha 4 (3)]: Kuwa na kufuata dini ya Kiislamu, kuwa na taaluma ya Sheria za Kiislamu ambapo kwa maoni ya Rais anafaa kuteuliwa kushika nafasi hiyo (ya Ukadhi Mkuu).
5. Kifungu cha 5 (1): Kutakuwa na idadi ya makadhi, ambao hawatapungua kumi na hawatazidi kumi na watano ambao watateuliwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama (the Judicial Service Commission) kwa kushirikiana na Rais na Kadhi Mkuu.

Hayo ni machache kati ya mengi kuhusu Mahakama ya Kadhi, Zanzibar. Je, kukiwa na Rais Mkristo au wa dini nyingine atamteua Kadhi Mkuu kwa Zanzibar? Au haiaminiki kwamba Rais asiye mwislamu hawezi kuchukua madaraka Zanzibar?
tafadhali ndugu yangu katika mada hii achana na Zanzibar. Usihangaike na mfano wa huko. Zanzibar karibu asilimia 98 ya watu wake ni Waislamu. Serikali inahudumia watu sasa wengi wao wakiwa ni haon (Waislamu) kwa nini isiyakumbatie mambo yao. Usitudahil Bwana Kule kuna Makadhi na wanaheshimika wakiwa na hadhi kamili. Mazonge ya talaka na mirathi tunayapeleka Mahkama ya kadhi na yanatatuliwa kwa mujibu wa dini yetu. Kwa hilo tuache -please. Usitutolee mfano katika malumbano yenu.
 
Hivi Wkuu, kwanini Waislamu wanadai Mahakama ya Kadhi na Wakiristu hawadai yao? sikuwa ilioko hayendi sambamba na dini yao, na kwa wakrisu inakwenda na sambamba!

Pili, ikiwa Waislamu wajigharimiye mahakama ya Kadhi kwa kuwa pesa za walipa kodi wa dini zote, sasa pale wasio waislamu watapokuwa wanahudumiwa na mahakama zilizopo, hao hawatakuwa wanatumia pesa za walipa Wakiislamu?
 
Back
Top Bottom