Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Mimi ni mkristo na niko bega kwa bega na waislamu wanaotaka mahakama yao, ila hiyo mahakama isigaramiwe chochote na serikali wala kingizwa kwenye katiba ya nchi na isivunje sheria za nchi kama ni hivyo ianzishwe haraka. Na iwe mahakama inayotatua matatizo yanayohusiana na Dini tu bila kupingana na sheria zilizopo za nchi.

Mimi ninavyoona hiyo mahakama itakuwa ya kusuluisha ndoa zilizofungwa kiislamu tu pamoja na ugomvi wa kwenye misikiti kama uliotokea Morogoro wa kugombea kumiliki msikiti wa Kilakala Bong'ola kati ya waislamu wenye msimamo mkali na waislamu wa kawaida.

Lakini ukianza kusema wanawake wasivae suruali na vimini na kuifanya ni sheria, au mwizi akatwe mkono au aliyezaa bila ndoa apigwe mawe hadi kufa hapo patakuwa hapatoshi. Mwanamke ndio anapigwa mawe mwanaume wala!!!

Kama wanataka mahakama ya kidini basi wafanye kwelikweli kama Mahakama za Nigeria hapo ndiyo nitaona waislamu wote wanaounga mkono wako serious. Kwa nini wachague kesi fulani fulani tu. Kama ni sharia na iwe sharia ila isituguse sisi tusio na dini halafu tuone kama watu hawatabadili majina.
 
Mie naona nimeachwa nyuma kidogo. Can someone educate me on this so-called Mahakama ya Kadhi? What is it all about?
 
Mie naona nimeachwa nyuma kidogo. Can someone educate me on this so-called Mahakama ya Kadhi? What is it all about?

MzeePunch, hivi kweli ni wewe? au si yule MzeePunch tunayemjua miaka yote? anyway soma toka mwanzo wa thread.
 
Serikali inatoa ruzuku kwenye hospitali na mashule ya kikristo why not mahakama ya kadhi????

Kwa sababu huduma zile ni kwa wote..mahakama ya kadhi ni kwa wasilamu peke yao..Sasa unaweza kuona mfano wako ulivyo mfu..tayari?
 
Utakufa kwa chuki ndugu...punguza kidogo walau uwe Mtanzania too much (hate) is coming kwenye hilo koo lako. Lipumzishe hilo koo lako na hatred utapata amani ya bwana!! wacha nasi tufarahi na mahakama zetu
Unaona shida gani jirani yako (muislamu) akifurahia mahakama ya kadhi Tanzania after all this long struglle (20 years)

Chuki unazo wewe ila kama wahenga huwa hawakosei walisema ' Nyani haoni makalio yake' ..Sasa tupe break kidogo na Upupu wako mazee ..Mahakama ya Kadhi ni ya Wasilamu..kama wanataka kuianzisha waianzishe, wasiihusishe serikali yetu tukufu maana sisi wengine hatutakubali..hiyo ndio bottom line.
 
Mahakama ya kadhi gharama si issue sana kwangu mie. Serikali itoe hela basi ya kuianzisha. Shida yangu siku zote ni ule utendaji kazi utakaoingiliana na shughuli za serikali. Hii baadaye itakuwa chanzo cha nongwa. Ni afadhali waislam waseme bajeti yao ni shiling ngapi halafu basi serikali iwape hela waiendeshe wenyewe.

Nakuambia haya mambo yakiingia serikalini baadaye serikali itakuwa haiwezi kuongozeka. Ukitaka kujua balaa lake we angalia BAKWATA. Labda waislam waseme wanataka kutap management na organizational skills kutoka kwa wakristo walio serikalini. Nawashauri kama hilo ndo wanalotaka waombe washauri (maconsultants) wawasaidie kuiendesha badala ya kuing'ang'aniza iingie serikalini.

Waislam wanajua fika humo serikalini watendaji si wote waislam. Maanake ni kuwa religious profiling itaanza kuwa kitu cha kawaida ndani ya serikalini. Kuna maamuzi hutayafanya juu ya mtu mpaka ujue dini yake. Hii itakuwa kitu kisichofaa kwa serikali inayosema haina dini.

Kwa hiyo nashauri; waislam ombeni msaada wa bajeti ya kuendesha mahakama hiyo hata wasio waislam watachangia. Mimi mwenyewe binafsi niko tayari kuwachangia ndugu zangu waislam ili wapate mahakama yao. Mimi si mwislam ila uislam ni sehemu ya maisha yangu na siwezi kujitenga nao kwani nina marafiki, ndugu, n.k. na watu ambao siwezi kuwakana hata iweje ambao ni waislam. Serikali itoe hela, ila waislam wenyewe waamue nani wa kuwa kadhi na atateuliwa mwingine vipi. Waislam waamue wenyewe na waiendeshe wenyewe bila kuingiliwa na serikali. Serikali kujiingiza hapa itakuwa ni kuingiza petroli kwenye moto. Viongozi wasio waislam itakuwa balaa kwao. Bajeti si ishu. Ishu ni kuwa kadhi ikiwa ishu ya kiibada haitakiwi kuingiliana na shughuli za serikali ambayo si ya kiislam!! Incompatible!
 
Wewe ndugu ni mwislamu halisi? maana kwa mwislamu mwenye akili timamu anajua kuwa mahakama ya kadhi itasababisha waislamu wengi kuhamia ukristo!

.
teh teh teh

SAHAU! Takwimu zinaonye
Sha wakristo wengi wanarudi ktk dini yao ya asili UISLAMU
 
... Ili waweze kupata kazi. Ndio maana nikauliza, wanadai Mahakama ya Kadhi au Mahakama ya Kazi?
...
MKITAKA MSITAKE MAHAKAMA ya KADHI itaundwa kama humjuwi kiswahili tutawafundisha.

.
 
.
teh teh teh

SAHAU! Takwimu zinaonye
Sha wakristo wengi wanarudi ktk dini yao ya asili UISLAMU

wakristo na waislam wa Tanzania hawatenganishiki. Haya ya kuenda na kurudi ni mambo ya kila siku. Mkristo akitaka kuhalalisha ndoa ya pili anabadili dini na kuwa mwislam. Mwislam akitaka uhuru wa kula nyama ya nguruwe n.k. anabadili anakuwa mkristo.

Kuna wakristo wanaishi kama waislam; bado anasali kanisani ila mambo mengine hana tofauti na waislam (angalau maisha ya nje). Kuna waislam ambao kwa kweli maisha yao ni ya kikristo; hawawezi kuoa mke zaidi ya mmoja, wanakula nguruwe na kunywa pombe, n.k.

Mi wakati nakua, kwetu tulikuwa hatuchinji kuku. Hata kama tunakula wenyewe, ilikuwa lazima tumwalke jirani yetu mwislam aje kuchinja. Kwa nini? Kwa sababu wakati wowote tungepata mgeni mwislam na kuchangia naye chakula. Na hilo halikuwa tatizo wala si tatizo hadi leo huko vijijini. Siku hizi kuku ananunuliwa mlimani city ameshachinjwa kwa hiyo ndugu yangu mwislam haniulizi tena kama nyama imechinjwa kihalali au la.

Wakristo na waislam hawawezi kushindwa hili la kadhi. Tatizo tu itakuwa pale siasa zinapoingilia, ndo maana nashauri mahakama itengwe na serikali hata kama serikali atatoa hela; uendeshaji wake uwe solely controlled na waislam. This will be great and Tanzania will continue to be great country.
 
He has no choice lazima akubali hata kama maaskofu hawataki...sasa ndio tutajua kama Pinda anaongoza au (ni proxy) on behalf of church???
 
Chuki unazo wewe ila kama wahenga huwa hawakosei walisema ' Nyani haoni makalio yake' ..Sasa tupe break kidogo na Upupu wako mazee ..Mahakama ya Kadhi ni ya Wasilamu..kama wanataka kuianzisha waianzishe, wasiihusishe serikali yetu tukufu maana sisi wengine hatutakubali..hiyo ndio bottom line.
.
Khah! .mtafanyaje??? tutaona hilo mtalofanya
 
wakristo na waislam wa Tanzania hawatenganishiki. Haya ya kuenda na kurudi ni mambo ya kila siku. Mkristo akitaka kuhalalisha ndoa ya pili anabadili dini na kuwa mwislam. Mwislam akitaka uhuru wa kula nyama ya nguruwe n.k. anabadili anakuwa mkristo.

Kuna wakristo wanaishi kama waislam; bado anasali kanisani ila mambo mengine hana tofauti na waislam (angalau maisha ya nje). Kuna waislam ambao kwa kweli maisha yao ni ya kikristo; hawawezi kuoa mke zaidi ya mmoja, wanakula nguruwe na kunywa pombe, n.k.

Mi wakati nakua, kwetu tulikuwa hatuchinji kuku. Hata kama tunakula wenyewe, ilikuwa lazima tumwalke jirani yetu mwislam aje kuchinja. Kwa nini? Kwa sababu wakati wowote tungepata mgeni mwislam na kuchangia naye chakula. Na hilo halikuwa tatizo wala si tatizo hadi leo huko vijijini. Siku hizi kuku ananunuliwa mlimani city ameshachinjwa kwa hiyo ndugu yangu mwislam haniulizi tena kama nyama imechinjwa kihalali au la.

Wakristo na waislam hawawezi kushindwa hili la kadhi. Tatizo tu itakuwa pale siasa zinapoingilia, ndo maana nashauri mahakama itengwe na serikali hata kama serikali atatoa hela; uendeshaji wake uwe solely controlled na waislam. This will be great and Tanzania will continue to be great country.
I Salute you as a Patriotic Tanzanian.
 
kazi kwelikweli hamlali kwa mahakama ya kadhi, hamuachi? yenu mangapi mnafanya basi hili la waislam ndio mada, mnabadilisha title tu za thread content ile ile, ebu tuacheni tupumue,

kama mnataka nanyie anzeni kudai ya kwenu, mna haki ya kufanya hivyo kama mnaona waislam watafaidi, kwani itakuja kuwahukumu nyie, hata kama watadhulumiana waislam ni awo na sheria zao, kila mtu anauwezo wa kufuata akitakacho, muislam atakayeona mahakama ya kadhi haimfanyii wema ataenda atakako,

sasa sababu imekuwa oh kodi zetu zitaendesha hata kabla ya kujua nini kitaiendesha mliishaanza kelele, unadhani waislam wangekuwa wanauhuru wa kuanzisha hiyo bila ya go ahead ya serikali wangekuwa wanabembeleza siku zote,
 
Kwa watanzania, waliozaliwa tanzania na nje ya mipaka ya Tanzania wenye jina, , hali na damu ya kitanzania Asalaamu Aleikum!


Kwa mimi niliyekulia katika nchi ambayo tofauti ya mwislamu na mkristo unaona katika majina tu nachanganyikiwa! Nimekua na waislamu, ngali mimi mkristo, marafiki zangu waislamu , shemeji na hata baadhi ya wadogo zangu waislamu! Sijakweleza habari ya rafiki yangu mwislamu ambaye ameoa mkristo, alikuwa anamfuata mpaka kanisani, na sasa wamewekeana zamu wiki hii msikitini, wiki ijayo kanisani. Nakueleza ili uijue Tanzania iliyoibiwa leo, , Nyerere na ukatoliki wake hakuweka mbele dini wala kabila, matokeo yake ni historia nzuri ya taifa letu, wakati waarabu wanaeneza dini na kuchukua babu zetu, wakristo wao walieneza dini , kujenga shule na kuchukua madini!

Nimekula futari ya waislamu, nimekaribisha waislamu kwenye x-mass na pasaka achilia mbali sherehe za ubatizo na kipaimara.Hivi sijakueleza habari ya yule kaka yangu ana wake wawili wa kwanza mkristo wa pili mwislamu.Kabla ya hapo acha nikueleze mama yangu alikuwa hachinji kuku yeye anaita mwislamu ili kuku aelekezwe kibra, maana muda wowote anaweza akaja mgeni mwislamu kula chakula! Wale wenzangu na mie wasiofunga siku za ramadhani tulikuwa tunawekeana siri na kufichiana chakula.Achilia mbali siku ya kitimoto hata kama nitajificha watoto wakijua watanitafuta tu, naweka mfukoni nawapa, si wameomba!


Hii ndio Tanzania tuliyokuwa nayo na amani hii ni uthibitisho ieleweke kuwa

  • Dini Tanzania ni mfumo wa maisha ambao watu wengi wamerithi toka kwa mababu zao na ni wachache wenye ufahamu mzuri wa dini hizi, si waislamu,wakatoliki, wakristo wengineo n.k
  • Kuwa dini hizi kwa sababu ni za kurithi na maisha ya watanzania bado tunalelewa na wazazi , basi wengi huenda misikitini na makanisani kujionyesha tu na kufurahisha wazazi
  • Ya kuwa hizi dini ni hiari ya mtu, mtu ana uhuru wa kwenda imani yeyote ile saa yoyote ile pale atakapokosa amani na faraja ndani ya moyo wake.
Ieleweke pia kuwa

  • Mpaka sasa uthibitisho wa kuwa wafuata dini watanzania wengi ni wanafiki ndio maana uzinzi, umasikini, ufisadi uko kila mahali na kamwe dini hizi hazijaweza kukomesha hayo
  • Ya kuwa Tanzania ni nchi maskini sana, iko kumi bora hivyo basi elimu , umoja , upendo na kuchapa kazi pekee ndio vitatufanya tuwe na maisha bora
  • Dini hazijengi barabara wala si vitabu vyenu hivyo ndio vinaleta maji safi
  • Ya kuwa dini ni sehemu pekee ya kujengeka kuwa na adabu na kuheshimu mamlaka pamoja na katiba ambayo ndio dira ya taifa!
  • Badala ya kupoteza muda kuandika nayaraka za kikatoliki au mahakama ya kadhi ni vizuri tuangalie tumeweza kufanya nini mpaka sana na tumeathirika kiasi gani kwa kukosa yale tunayoyadai, mathalani mtu akisema leo mnapata mahakama ya kadhi au mahakama ya kikatoliki je shule zenu zinatoa wanafunzi wangapi ili wajenge taifa ili changa?


Kama wewe ni mfuatiliaji wa hali ya sasa kuna Jambo litatokea mahakama ya kadhi ikianzishwa, soma kwa makini;

  • Dini hii yarafiki yangu ina kitu kinaitwa ‘makafiri' ni wale wasioamini uislamu! Nashangaa kwa mwislamu safi kama rafiki yangu aliyeoa mkristo kujichanganya kiasi hiki, MAHAKAMA YA KADHI KUPITIA SERIKALINI MAANA YAKE WALE WAKRISTO WATAKAOKUWA WANAIDHINISHA PESA ZA KUZIENDESHA HIZI MAHAKAMA YA KADHI SI MAKAFIRI? KWA NINI DINI ICHANGAMANE NA HAYA? KWANI WAO HAWAJUI? WANAJUA FIKA
Kitakachotokea; Ikiishaanzishwa makahama ya kadhi then wakristo wote walio kwenye pipeline(watakaokuwa wakihusika na mahakama ya kadhi) ndani ya serikali itabidi waondoke, kwa maana nyingine, siku zijazo waislamu watadai sehemu ya serikali iwe ya kiislamu!

A. Sijui zitakuwaje lakini kama ni zile mahakama za kadhi kama za iran, iraq (kwa wenyewe), basi natabiri kuwa waislamu wengi wataacha uislamu na kuwa wapagani, wakristo, HII ITASABABISHA HASIRA KWA BAADHI YWA WAISLAMU NA KUONA KUWA WANAIBIWA WAUMINI, HASIRA HIZI ZITAPELEKEA MAKANISA KUCHOMWA MOTO, KULIPULIWA, KUCHOMWA NA MAJAMBIA n.k MAMBO YA JIHAD! na hii watapata support kutoka huko mashariki..

B. Kumbukeni uislam pia una madhehebu sasa sijui ni wote wanataka au ni wachache tu na tukiwapa hamtapigana kama ilivyo desturi, shule zenu ndio zinaongoza kufanya vibaya nchi hii na afrika kwa ujumla mnajua hilo?, KWA KIASI GANI MMEJITAYARISHA?


Kwa nini tuwaze dini? Je ni janja ya CCM kutusahaulisha maumivu ya ufisadi? Kama ni hivyo basi wamewapata waislamu, je wakristo watakaa kimya? Kwa nini maada hii haikuzuiwa tangu mwanzo? Ona sasa ! Je kwa akina sie tuliokuwa katikati ya waislamu-wakristo hivi nyie mnaodai mahakama ya kadhi mmetuuliza?Je kitu gani kinamfanya mtanzania aliyeishi nchi hii ya amani kuwaza dini? Je kesho akija rais mkristo basi waanzishe mahakama ya kikristo, wakija wahindu nao pia n.k

Sijasema katiba hapa, nikiingia huko hakuna wa kupona si mkristo wala muislamu, hakuna nafasi ya dini kwenye serikali ya watanzania.

Je mimi mlokole mkinipa urais sitaanzisha mahakama maana hakuna matatizo ya kudai mahakama kwenye ulokole, ila nitakachofanya ni kuhakikisha wote mnamjua Yesu , sijajua ni kwa kiasi gani mko tayari!

Kaeni chini fikirini tena, Tanzania tamu hivi tulivyo, amani ikipotea tutaenda wapi, Rwanda?

Hii kitu CCM zimeni kisiongelewe kabisa kinatia kichefuchefu!

waberoya
 
Halafu wanataka iingizwe kwenye katiba!
Yaani katiba ijenge matabaka ya kidini? Kwamba mwizi muislamu ahumukiwe kwa sheria za kadhi na mwizi huyohuyo mkiristu ahukumiwe kwa mahakama za serikali?
Waislamu tusidanganyane kewa mahakama ya kadhi itaishia kwenye ndoa na mirathi tu. Hiyo ni janja tunavunga kuanza na vitu vidogovidogo ili baadae tudai makubwa kama ya kutumia islamic sharia.
 
Back
Top Bottom