Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Mimi ni mkristo na niko bega kwa bega na waislamu wanaotaka mahakama yao, ila hiyo mahakama isigaramiwe chochote na serikali wala kingizwa kwenye katiba ya nchi na isivunje sheria za nchi kama ni hivyo ianzishwe haraka. Na iwe mahakama inayotatua matatizo yanayohusiana na Dini tu bila kupingana na sheria zilizopo za nchi.

Mimi ninavyoona hiyo mahakama itakuwa ya kusuluisha ndoa zilizofungwa kiislamu tu pamoja na ugomvi wa kwenye misikiti kama uliotokea Morogoro wa kugombea kumiliki msikiti wa Kilakala Bong'ola kati ya waislamu wenye msimamo mkali na waislamu wa kawaida.

Lakini ukianza kusema wanawake wasivae suruali na vimini na kuifanya ni sheria, au mwizi akatwe mkono au aliyezaa bila ndoa apigwe mawe hadi kufa hapo patakuwa hapatoshi. Mwanamke ndio anapigwa mawe mwanaume wala!!!
 
Suala siyo kuanzisha suala ni nani anayetaka kugharamia mahakama hizo kama siyo waislamu wao mwenyewe
 
Kufuta kauli ni kukiuka katiba kwani Waziri wa Sheria alitamka kama Katiba ambayo ni sheria mama ya nchi inavyoelekeza.Hii si nchi ya kidini na Serikali kugharamia mambo ya dini moja ni kinyume na sheria za nchi yetu.Pinda usichanganywe na shinikizo la mahakama ya kadhi ukakiuka katiba.
 
Mimi ni mkristo na niko bega kwa bega na waislamu wanaotaka mahakama yao, ila hiyo mahakama isigaramiwe chochote na serikali wala kingizwa kwenye katiba ya nchi na isivunje sheria za nchi kama ni hivyo ianzishwe haraka. Na iwe mahakama inayotatua matatizo yanayohusiana na Dini tu bila kupingana na sheria zilizopo za nchi.

Mimi ninavyoona hiyo mahakama itakuwa ya kusuluisha ndoa zilizofungwa kiislamu tu pamoja na ugomvi wa kwenye misikiti kama uliotokea Morogoro wa kugombea kumiliki msikiti wa Kilakala Bong'ola kati ya waislamu wenye msimamo mkali na waislamu wa kawaida.

Lakini ukianza kusema wanawake wasivae suruali na vimini na kuifanya ni sheria, au mwizi akatwe mkono au aliyezaa bila ndoa apigwe mawe hadi kufa hapo patakuwa hapatoshi. Mwanamke ndio anapigwa mawe mwanaume wala!!!

Mkuu sijui kama unaelewa undani wa suala hilo. Hiyo ni hatua ya kwanza tu na hatua ya kwanza ikipigwa basi ujue kutakuwa na hatua ya pili ya tatu na ya nne. Usijeukaamini kuwa itakuwa ni mahakama kwa ajili ya waislamu tu, na haitagharamiwa na waislamu tu. Inaweza ikachukua pesa kutoka sehemu nyingine zikapelekwa huko.
Hata sisi wapagani kama tukioa waislamu basi hiyo sheria itatuhusu kwa namna moja au nyingine, au kama sisi wapagani tuna mabucha ya nguruwe basi mahakama hiyo inaweza kutaka ivunjwe. Itakuwa na mambo zaidi ya unayosema, na kuna siku utakuja sikia wengine wanataka kesi zao zishughulikiwe kwenye mahakama za kiraia, na utakuwa ni mkoroganyo, mvurugano tu.
Kama uamuzi huu ukipita basi itakuwa ni failure nyingine ya serikali ya JK. Itakuwa ni big step backward. Itakuwa inafuta misingi ya umoja wa kitaifa, tutyaanza kuwa na makundi ya vijitaifa ndani ya taifa.Wakristo nao wakianzisha ya kwao, sijui sisi wapagani itakuwaje.
 
media za kiislamu zipo,jaribu kufanya utafiti ndg mbogela

Inawezekana media zipo, lakini hawajainvest kiasi cha kutosha, unaona tunaangalia vipindi vingapi vya mahubiri kutoka kwa viongozi wa dini wa kikristo kwenye TV? Kuna makala ngapi kwenye magazeti? Kuna vipindi vingapi kwenye Redio? Living alone I-net, ukigonga saa hizi hayo majina yaliyopendekezwa hapo kwenye Google you will hardly find habari zao. Gonga Kakobe au any from wakristo side. Kwa hiyo nachosema hawajawekeza kiasi cha kuwasaidia kufanya lobbying kirahisi.
 
media za kiislamu zipo,jaribu kufanya utafiti ndg mbogela

Katika population ya WaTZ, 1/3 ni wakrsito, 1/3 ni wakristo. 1/3 hawafungamani na dini yoyote ya kigeni (wanawaita wapagani). lakini Ukiangalia ugawanyo wa media utaonaje? sijaona scientifica document nitatafuta. Nikiangalia ratio ya mgawanyo wa media kwa Serikali😛rivate:wakristo:waislam:Others nadhani hapo utaona kabisa kuwa Jamii ya kiislam ina sehemu ndogo. Lobbyong inahitaji sana eneo la media sana hasa zama hizi. watu hawategemei kupata ujumbe kwenye misikiti au makanisani, people shold get a mesege where there are.
 
Ina maana hiyo mahakama itaendeshwa kwa jasho la mpagani na madhehebu mengine au ni sadaka zao.
 
Ina maana hiyo mahakama itaendeshwa kwa jasho la mpagani na madhehebu mengine au ni sadaka zao.

Serikali inatoa ruzuku kwenye hospitali na mashule ya kikristo why not mahakama ya kadhi????
 
Ingefaa zaidi ungeweka na CV zao hasa kwa upande wa elimu dunia maana hiyo nayo ina determine uelewa wa mtu.
 
Swali lako sawasawa na kumwita Kabwe "mpinzani" wakati anatoa hoja ya Richmond, madini, BOT, n.k. halafu CCM "inapinga hoja hizo". Hapo nani mpinzani Bungeni??

Mada ni MAHAKAMA YA WAISLAMU - full stop!

Malizia: 'ambayo itaendeshwa na kugharamiwa na inayowahusu-WAISLAMU'.
 
Kuna umuhimu Mashekh nao kuinvest kwenye media kama wenzao Maaskofu, hapo nimesoma orodha sijamfahamu hata mmoja, ...
Haa haa haaa !! Watafahamika tu, wee ngoja kila mmoja katika hao awe kadhi, utajuuuta kumfahamu! Investment katika kitu ni priority tu Mkuu, Wakristu wameweka priority ya investment katika Elimu, afya, media etc, na waislamu wameamua priority yao ya investment iwe katika Mahakama. Mambo ya Elimu na Afya na vitu kama media kwao (Waislamu) labda vitafuata baadaye (wakiwa wamepata mahakama).
 
No more argument, ,,,, kwa msisitizo PRIORITY!!!!
 
nani asiemjua Sheikh kundecha ni msomi aliemaliza Chuo Kikuu. nani asiemfahamau Kilemile na nani asiemfahamu bAWAZIRI. wengi mnawatizama akina Kakobe na vichekesho vyao waslam hawapendi Kujinadi kwenye Media. Ibada kwenye media kila wakati ni sawa na kujionyesha
 
Mkuu labda huwa unachagua media za kusikiliza na kutizama ndio huwaoni waislamu! mbona wana redio kama vile radio Imani kule morogoro, redio Q'uran, wan gazeti hutoka kila Ijumaa! ukitaka kujua habari zao utazipata tu!
 
nani asiemjua Sheikh kundecha ni msomi aliemaliza Chuo Kikuu. nani asiemfahamau Kilemile na nani asiemfahamu bAWAZIRI. wengi mnawatizama akina Kakobe na vichekesho vyao waslam hawapendi Kujinadi kwenye Media. Ibada kwenye media kila wakati ni sawa na kujionyesha

Mzee wa hoja nimekupata, Lakini hakuna msomi atakaye kataa kuwa media ina impact siku hizi??? sizungumzi ibada hapa nazungumzia kupashana habari na lobyying, ukitaka kufanikiwa kuwaleta watu upande wako wafikishie Ujumbe waupate, sasa kuweza kufanikiwa hili tunahitaji watunga sheria (waiislam na wasio) walipitishe, je wote watajua faida za mahakama Msikitini?????
 
Last edited:
Hiyo mahakama itaendeshwa kwa kodi ya watanzania wote au sadaka za waaminio
 
Back
Top Bottom