Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,192
- 1,976
Kuhusu Zanzibar kuwa na Mahakama za Kadhi, sheria zao zinaruhusu, za Bara haziruhusu kuchanganya siasa na dini. Pia fungua macho vizuri kama Zenj hakuna mushkeli. Juzi kuna kanisa limechomwa moto na sheha alionyesha kutokukerwa na suala hilo. Kadhi Mkuu wa Zenj anateuliwa na Rais wa Zanzibar. Inategemea sheria zao na lifestyle yao. Pia wazenj hawavunji katiba ya jamhuri ya muungano kwa kuwa suala la mahakama ya kadhi sio la muungano. Waislamu kama wanataka kuishi kwa amani waunde Mahakama na kuigharamia wenyewe kama wanavyoigharamia BAKWATA. Nani amewauliza chochote juu ya kujiendesha na kujigharamia wenyewe? Pinda kama anataka kusilimu afanye mwenyewe, hakuna anayemzuia!