Hakuna kitu kinachoudhi kama ubabe wa serikali. Inasikitisha kuona kuwa katika Tanzania tunatikiwa kuinama na kupigwa bong'oa kwa vile serikali imesema jambo fulani. Katika suala hili la wanafunzi wa vyuo vikuu kufukuzwa na serikali kushikilia msimamo wake wa kuwataka walipe fedha za chuo kikuu, wakati umefika kuwaonesha serikali kuwa "nguvu iko kwa watu"!!
Nyinyi wanafunzi wa vyuo vikuu ambao mmekubali kuburuzwa na serikali na utawala wa vyuo kwa vile mnaona hamna njia nyingine nawasihi mtulizane na kutafakari upya. Mtaendelea kusukumwa sukumwa kwani baadaye wakiwaambia "tumeona mnaweza kulipa asilimia 40, sasa itabidi mlipie asilimia 60" mtakataa!! Ni lazima mchore mstari ardhini na kuiambia serikali kuwa hakisomeki kitu hadi suala hili la malipo linatafutiwa ufumbuzi once and for all!!
It is about time to put your feet on the ground and don't you dare move! Viongozi wa Daruso na wengine wenye maslahi nawashaurini mfanye kile ambacho hufanywa mara nyingi kwenye nchi za kidemokrasia, siyo maandamano na mabango bali kukaa chini (Sit Ins)
a. Wanafunzi wote rudini vyuoni kwenu kwa makundi (siyo mtu mmoja mmoja) Mkishikilia mabango yasemayo yenye kuhamasisha serikali kuwaruhusu wote kurudi shuleni na kukabili tatizo zima la kulipia elimu ya juu. Mmekubali kugawanywa, hamuwezi kufika mbali! La maana wale walioruhusiwa kurudi wagome kurudi hadi wenzao wote nao wamerudi!
b. Jifungeni vitambaa midomoni (ishara ya kunyamazishwa!). Na mnaweza kuvaa nguo nyeusi kuonesha msiba mkubwa wa elimu ya juu Tanzania.
c. Nendeni na kukaa kwenye maeneo ya vyuo (hasa kwenye milango ya madarasa) na msiondoke hadi muondolewe kwa nguvu huku kamera zinaroll na picha zinapigwa ili kuionesha serikali mbele ya umma!
Mbinu hii ya kukaa chini, imetumiwa tangu wakati wa Mahtma Gandhi, na wakati wa kutafuta haki za raia kule Marekani. NI mbinu ambayo haina uchokozaji kwa serikali. Lengo kubwa la kutumia mbinu ni hii ni kulazimisha hoja ya watu isikilizwe na kuonesha hadhara kubwa kuwa kutotumia nguvu kwaweza kujibiwa kwa matumizi ya nguvu. Nina uhakika mkiamua kukaa chini kwenye milango na viwanja vya vyuo vyetu, watawaleta polisi na kuwasomea "Riot Act".. msibabaike, wala msikimbie, kaeni chini kama watawabeba na kuwapeleka kwenye makarandinga wawabebeni... mtazijaza mahakama, na jela, lakini wakati wa kuchukua msimamo umefika... woga wenu ndio umewaponza hadi hivi sasa!!
Wanafunzi wenzenu kwenye vyuo vikuu vingi duniani ndio wamekuwa chachu ya mabadiliko.. katika kupiga vita Ubaguzi wa Rangi Afrika ya Kusini, Sera ya Utenganisho wa Rangi huko Marekani, Vita vya Vietnam, kule Ujerumani mwaka 1968 n.k
There comes a point in a relationship between the State and the People when the people have to take a stand. Hili suala la kulipia asilimia 40 ni wakati kama huo, na watanzania tuwaunge mkono kuhakikisha kuwa vijana wetu wanarudi shuleni bila kubaguliwa kwa sababu ya uwezo wao wa kifedha!! Lengo la "kukaa chini" ni kuhakikisha Msolla anaondolewa na bodi ya Mikopo inavunjwa ili apatikane Waziri mpya na Bodi mpya yenye uwezo wa kukabiliana na matatizo ya elimu ya juu na kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu!
let there be a showdown.. yes, this looming showdown between the state and unarmed, peaceful body of students!! Let the Kikwete's government take a stand and make a choice!!