Just in: UDSM wafukuzwa

Just in: UDSM wafukuzwa

Mniwie radhi, najaribu kuamua kama niweke sasa hivi, mida ya usiku au mapema kesho kwani tukio na kile ambacho nataka niwaambie kitatokea Alhamisi... Nafikiri itakuwa ni too early to break the news kwani nikiweka sasa hivi, serikali will act tomorrow na kuvuruga mipango ya Alhamisi...

.....halafu msosi wenyewe alhamisi.....huku si ni kushindishana njaa!
 
Huenda habari yenyewe ndiyo hii? http://www.mwananchi.co.tz/habari/habari1.asp

Chuo Kikuu waanza kuwashughulikia waliosimamishwa

UONGOZI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), umeanza kushughulikia suala la wanafunzi 56 waliosimamishwa masomo kwa tuhuma za kuchochea mgomo kwa kuwataka kufika chuoni hapo kuchukua barua zao na kuzijibu leo.
 
mtu mzima hatishiwi nyau.mzee wa shamba watu walisema wew ukijua huu wenzako wanajua kule.
 
kakalende.. jaribu zuri lakini siyo hizo... ila zinahusiana....lakini ni kubwa zaidi kuliko unavyoweza kufikiri....
 
Dar si Lamu,

Eeeeh mwenzetu wee ni mwanamama?... maanake majibu yako kidogo yameniacha nje kuwa wajua kwa nini wanafunzi wa vyuo vyetu wanajiuza.
Ama ndio Dar sii Lamu kweli?..

Sikiliza ndugu yangu kutembea na wanaume wengi kama starehe ni umalaya ambao unatokana na hulka ya mtu lakini mwanamke wa chuoni anapo UZA mwili wake kama biashara ya kusukuma maisha hili ni swala zito zaidi ya unavyofikiria wewe....Unless una hoja nyingineyo zaidi ya kuwashusha dada zetu kwa mtazamo wako.
Ni kweli Umalaya ulikuwepo toka zamani lakini umalaya huo haukuwa kwa wanafunzi kujiuza miili yao ila moja ya starehe zao...Walikuwa wakitoka majumbani mwao kwenda sehemu za starehe tena wengine watoto wa hawa vigogo lakini kutembea na mtu ilikuwa ni ktk starehe yao..Haikuwa na malipo zaidi ya chicken n Chips pale Mermaid!
Pili, sitegemei kabisa kwamba wewe mwanaume unaweza kunipa sababu zinahusu hisia za kike ktk swala hili. Na iweje leo iwe umalaya huu kwa wasichana wanaosoma vyuo vikuu wakati sikumbuki kuwepo kwa hulka kama hii miaka ya zamani.
Nitafurahi zaidi ikiwa kuna mwanamke humu ambaye anaweza kunambia kuhusu wimbi hili la wasichana kuuza miili yao kwa madai ya kutafuta Ada ya chuo anachosoma.
Pili, ndugu Dar hata huku nje UGENINI, wasichana wetu wengi wanajisomesha na kuna kila haja ya wao kupenda anasa zaidi ya huko nyumbani maanake vishawishi ni vingi zaidi, kila kitu kipo madukani kwa daraja tofauti.
Lakini hata hivyo wengi wao wameweza kutafuta njia nyingine nje ya kuuza miili yao, wakifanya kazi mbuzi kabisa ambazo wewe hapo Bongo huwezi kuzifanya wala kumshauri mtu kufanya. Na wameweza kulipa ada ya shule.. Wanaofanya umalaya kwa starehe wanafahamika na haihusiani kabisa na utafutaji wa karo ya shule...
 
Mniwie radhi, najaribu kuamua kama niweke sasa hivi, mida ya usiku au mapema kesho kwani tukio na kile ambacho nataka niwaambie kitatokea Alhamisi... Nafikiri itakuwa ni too early to break the news kwani nikiweka sasa hivi, serikali will act tomorrow na kuvuruga mipango ya Alhamisi...

why did yoy tell us in the first place? watu presha hiyo!
 
Dar si Lamu,

Eeeeh mwenzetu wee ni mwanamama?... maanake majibu yako kidogo yameniacha nje kuwa wajua kwa nini wanafunzi wa vyuo vyetu wanajiuza.
Ama ndio Dar sii Lamu kweli?..

Sikiliza ndugu yangu kutembea na wanaume wengi kama starehe ni umalaya ambao unatokana na hulka ya mtu lakini mwanamke wa chuoni anapo UZA mwili wake kama biashara ya kusukuma maisha hili ni swala zito zaidi ya unavyofikiria wewe....Unless una hoja nyingineyo zaidi ya kuwashusha dada zetu kwa mtazamo wako.
Ni kweli Umalaya ulikuwepo toka zamani lakini umalaya huo haukuwa kwa wanafunzi kujiuza miili yao ila moja ya starehe zao...Walikuwa wakitoka majumbani mwao kwenda sehemu za starehe tena wengine watoto wa hawa vigogo lakini kutembea na mtu ilikuwa ni ktk starehe yao..Haikuwa na malipo zaidi ya chicken n Chips pale Mermaid!
Pili, sitegemei kabisa kwamba wewe mwanaume unaweza kunipa sababu zinahusu hisia za kike ktk swala hili. Na iweje leo iwe umalaya huu kwa wasichana wanaosoma vyuo vikuu wakati sikumbuki kuwepo kwa hulka kama hii miaka ya zamani.
Nitafurahi zaidi ikiwa kuna mwanamke humu ambaye anaweza kunambia kuhusu wimbi hili la wasichana kuuza miili yao kwa madai ya kutafuta Ada ya chuo anachosoma.
Pili, ndugu Dar hata huku nje UGENINI, wasichana wetu wengi wanajisomesha na kuna kila haja ya wao kupenda anasa zaidi ya huko nyumbani maanake vishawishi ni vingi zaidi, kila kitu kipo madukani kwa daraja tofauti.
Lakini hata hivyo wengi wao wameweza kutafuta njia nyingine nje ya kuuza miili yao, wakifanya kazi mbuzi kabisa ambazo wewe hapo Bongo huwezi kuzifanya wala kumshauri mtu kufanya. Na wameweza kulipa ada ya shule.. Wanaofanya umalaya kwa starehe wanafahamika na haihusiani kabisa na utafutaji wa karo ya shule...

.....posting yangu,haizungumzii wao kufanya umalaya wa starehe[ambao maana yake ni mhusika kufanya ngono na watu wengi kwa lengo la kuburudika!].....bali,hufanya hivyo kwa sababu tafauti na kutafuta karo, sababu ambazo zimejikita zaidi kwenye kuendekeza maisha ya anasa na kutaka kuishi maisha wasiyoyaweza au ya kuiga!.

hao wa nje kujiuza kwa ajili ya karo[sana sana hela ya matumizi ya kila siku]...hilo linafahamika....miaka ya nyuma india ilikuwa inasifika kwa hilo!

hizo kazi nyingine...huko majuu zinafahamika!....huku huwezi kuzifanya kwa kuwa ni nyumbani na mtu anaweza kula bure[kwa kuhemea kwa rafiki,ndugu na wengineo],kitu ambacho huko hakiwezekani.

mi ni bibie....endelea kujaribu!...hivi kujua mtu anaumwa malaria ni lazima kabisa umpime na uwe daktari sio!.....au mwenzetu we ndiye,ndo maana unanishangaa mi kufahamu?...au hukuelewa vya kutosha nilichokisema?
 
why did yoy tell us in the first place? watu presha hiyo!

mwanasiasa... I was too excited... then I thought suala la time difference na advantage ambayo serikali itakuwa nayo... so.. I'm holding back for few hours, kwani for now I'm the only one who could break that news...!!! Unless serikali wa ni preempty... otherwise...
 
.....tutasubiri tuone kama mahubiri yatatimia!
 
Dar si Lamu,
mengine wayaongeza mwenyewe maanake umesema unafahamu kwa uhakika kwa nini wanawake wanauza miili yao. Hili ni swala la maamuzi ya mtu na hata kisayansi sio rahisi kwa mwanamke kufahamu kwa nini mwanamme ni malaya! Hakuna hakika zaidi toka nje unless wewe ni mmoja wao. Huo ndio ukweli na yatubidi kuukubali....hatuzungumzii imani za dini hapa.
Sasa ikiwa hao wanawake wanafanya Umalaya kwa sababu kuendekeza maisha ya anasa na kutaka kuishi maisha wasiyoyaweza au ya kuiga!. Ni maisha gani hayo?.. bia wanapewa bure, kwenda club wanaume wanatoa offer na wengine wapo radhi kununua magari ikiwa mtoto wa kike ataweza kujiheshimu. Na wengi wamefanikisha maisha hayo nje ya vyuo... tatizo langu kubwa ni hili wimbi la wasichana wa shule kuweka NIPE - NIKUPE mbele ya starehe hizo hizo unazozizungumzia. Na ukitazama maisha yao hawana starehe hata kidogo labda ungepata muda ukakaa nao na kuwahoji kuhusu swala hili.
Dar si lamu,
Nimefanya hivyo, nimekaa na baadhi ya wasichana na kuwauliza kwa undani zaidi kuhusu maisha yao vyuoni na niamini naposema hawafanyi haya kwa kupenda anasa. Hii ni hukumu ya kiume mbele ya wanawake....
Sikujaribu.. hajaribiwi mtu hapa isipokuwa hoja kujibiwa kwa hoja! Kilichotangulia ni lugha ya Dar ama Lamu ambayo kama unavyosema wewe sii tusi wala kumjaribu mtu. Nipe source ya madai yako utakuwa umerahisisha zaidi....
 
Dar si Lamu,
mengine wayaongeza mwenyewe maanake umesema unafahamu kwa uhakika kwa nini wanawake wanauza miili yao. Hili ni swala la maamuzi ya mtu na hata kisayansi sio rahisi kwa mwanamke kufahamu kwa nini mwanamme ni malaya! Hakuna hakika zaidi toka nje unless wewe ni mmoja wao. Huo ndio ukweli na yatubidi kuukubali....hatuzungumzii imani za dini hapa.
Sasa ikiwa hao wanawake wanafanya Umalaya kwa sababu kuendekeza maisha ya anasa na kutaka kuishi maisha wasiyoyaweza au ya kuiga!. Ni maisha gani hayo?.. bia wanapewa bure, kwenda club wanaume wanatoa offer na wengine wapo radhi kununua magari ikiwa mtoto wa kike ataweza kujiheshimu. Na wengi wamefanikisha maisha hayo nje ya vyuo... tatizo langu kubwa ni hili wimbi la wasichana wa shule kuweka NIPE - NIKUPE mbele ya starehe hizo hizo unazozizungumzia. Na ukitazama maisha yao hawana starehe hata kidogo labda ungepata muda ukakaa nao na kuwahoji kuhusu swala hili.
Dar si lamu,
Nimefanya hivyo, nimekaa na baadhi ya wasichana na kuwauliza kwa undani zaidi kuhusu maisha yao vyuoni na niamini naposema hawafanyi haya kwa kupenda anasa. Hii ni hukumu ya kiume mbele ya wanawake na wala sikujaribu.. hajaribiwi mtu isipokuwa hoja kujibiwa kwa hoja! Kilichotangulia ni lugha ya Dar ama Lamu ambayo kama unavyosema wewe sii tusi wala kumjaribu mtu. Nipe source ya madai yako utakuwa umerahisisha zaidi....

......hiyo research yako pesa unakula mwenyewe!

sina madai mzee wangu....huo ni ufahamu wangu wa uhakika....kama mambo sio hivyo tena[na siamini,labda sababu ziongezeke]haya!

hivi wajua kuwa....wanashindana toka kwenye mavazi hadi vifaa vya vyumbani walivyonavyo vyumbani mwao.....aidha, nani bwana wake ana gari zuri na la bei mbaya zaidi[kama movie vile]......anywayz,tuyaache haya!

hiyo research inabidi utoe hela watu wakusaidie data[source],sio ule peke yako......just joking!
 
Dar sio Lamu,
Ndugu yangu usifanye mzaha hawa wasichana wanakaa ktk mabweni hivyo vifaaa vya nini hali kula yao wenyewe wanategemea msosi wa chuo. Nguo zao wenyewe mitumba kama walivyo wengi - Kwa gharama gani hasa wakafikie kuuza mili yao hali kuna designer feki kibao zinauzwa kwa bei posho ya mzazi.
Kushindana mavazi inatokea kote hata wake zetu mama zetu wanshindana kwa pair za kanga lakini harakati zao hazifikii kufanya ufuska wa kuufanya mwili wao for rent!..
Utafiti wangu nimeufanya kwa mapenzi yangu na ukereketwaji wangu ktk maswala tofauti ya kiuchumi na maisha ya Wadanganyika na sintapenda kuyaweka mengi mezani. Kumbuka nilikuwa nikijaribu kutafuta ufumbuzi wa Mada nzito niliyoiacha ikiwa haikutimia...Na ndio maana nimekuja na sura mpya nikisisitiza kuwa UBINAFSI ndio adui yetu mkubwa aliyetangulia vitu vyote!...
 
Kwa Msolla kila kitu kinawezekana,

Huyu jamaa ni mkorofi by nature. Ni mmoja wa wachache ambao hawaoni tabu kusema yaliyo moyoni hata kama yataumiza roho ya mtu. ninavyomjua mimi ni kuwa kwake yeye jinsi gani watu watakavyomuuna sio issue endapo anaamua lake.

Lakini ndugu zangu kuna yule mama deputy wake. With all due respect, mama ni mtupu na confidence zero!!!!!!!! Anyway huwa sipendelei kuongelea watu hivyo naomba ninyamzie hapa. Labda pale itakapolazimu kabisa

Tanzanianjema
 
ndugu yangu mwanakijiji?

Usiwe na mori sana kaka. Hizo technique zako sio ngeni kufikiriwa lakini kamwe huwa haziwezekani katika mazingira ya mlimani. watu wamejaribu sana lakini tatizo inapofika wakati wa mgomo wanafunzi wanajawa na emotions hivyo ukiwapa taktic hizo wanaona unawaletea usiku.

Kuhusu kutimuliwa/kufungwa chuo naona ndugu yangu Rwekaza mwana wa Mukandala ameamua kutumia mazoea badala ya creativity kushughulikia suala hilo. Nilidhani angetumia ujuzi wake wa hali ya juu katika kuwa na mikakti endelevu lakini bahati mbaya ndugu yangu huyu ameshindwa kusoma dalili za nyakati.

Hii ni clearcut case of Malicious Prosecution na bahati mbaya wapo wengi tayari kuisimamia. Tatizo watanzania tunapenda njia za mkato kudeal na yale tunayoyaona ni matatizo. Matokeo yake yanatugharimu zaidi ya Richmond, IPTL, Manjis Godowns, Mashangingi na mengineyo mengi.

Tanzanianjema
 
Kaka mukandala,

Embu waache hao mabinti wa watu. Wao ni matokeo ya mfumo tuliujenga, kuuneemesha na kuulinda kwa gharama kubwa tu. Yote wanayoyafanya yanafanyika kuanzia majumbani kwao, makazini, mitaani na hat kwenye nyumba za ibada.

Vilevile kwanini huwaongelei hao wanaowahonga na pesa zao wanazotuibia kila kukicha. Ina maana huwajui wahongaji wakubwa wanaoneemesha hilo tatizo ni kina nani? Waseme na wao pia.

Kaka mukandara hayo ndio matunda ya kufakamia soko huria, tunabinafsisha kila kitu hadi miili na akili zetu. Sisi kwa staili moja na wao kwa stail nyingine.

Tanzaninjema
 
Tanzanianjema... subiri utaona..kile ambacho hakijawahi kuwezekana kitawezekana...! Viongozi huwa hawafuati...
 
Kaka una maana ile shughuli ya yule Prof wangu mstaafu wa sheria.......ndio maana nikakwambia mkandala ameshindwa kusoma alama za nyakati...

tanzanianjema
 
Tanzanianjema,

Haya ndio maneno nayoyazungumza humu wala usije fikiria nawalaumu hawa dada zetu ila system nzima. Tumelivaa soko huria kama vile soko la Kariakoo ambalo halina viwango ktk kila kinachopokelewa maadam somo linasema huu ni wakati wa biashara.
Hao wanaohusika na madangulo haya ni mafisi ambao kamwe hatuwezi kuwazungumzia ikiwa sisi wenyewe tumesababisha kuwepo kwa mizoga!...hakuna mizoga fisi hawana nafasi ila huko mwituni -Joly club!
Kinachosikitisha zaidi ni pale serikali inapohesabu ukubwa wa jeshi kama la Saadam ktk Elimu kutangaza mafanikio hali jeshi dogo kama la Israel (Botswana) linatutoa kapa.... Hii ni dalili mbaya sana ya viongozi wetu kutofahamu umuhimu wa elimu bora ktk nchi maskini. Asilimia kubwa ya wanafunzi nchini inatoka ktk familia ambazo pato lake kwa siku ni chini ya dollar moja!..Na maisha ya wenzetu hasa nchi za magharibi hayawezi kuigwa wala kufananishwa na sisi hata kidogo kwa sababu wana uwezo wa kujisomesha. Maskini tuna malengo yetu na hao Matajiri wana malengo yao na wala hoja hii haiondoi hoja ya kuwepo kwa shule za private!.

Tunakokwenda sisi ndiko wao walikotoka na kamwe haitatokea tairi la gari la nyuma kulikamata la mbele...labda tu gari hili limeharibika!..Siku Tanzania itakapo weza tengeneza hata baiskeli yake basi jua magari yatakuwa yakiruka hewani huko Ulaya..

Nitaiomba serikali yetu ijaribu kufikiria upya elimu nchini na hasa sehemu muhimu kama vyuo vyetu ambako ndiko tunakotegemea zaidi ktk ufanisi wa kila hatua ya maendeleo yetu. Kilio cha wanafunzi hakikutoka bure na hakikuanza jana. Tena basi moja ya mikakati ya serikali ni kufuta umaskini jambo ambalo huwezi kulimaliza kirahisi ikiwa fedha itakuwa msingi wa kumaliza umaskini huo!..
Maskini husaidiwa kupunguza uzito wa mzigo na sio kuongezewa mzigo.
 
Mzee inaonekana unai-miss Jolly? Lol
 
Leo ni mwanzo tu.. Msolla atang'oka kwa kuvuruga elimu ya juu na kushindwa kabisa kuonesha uongozi wakati ulipohitajika!! Profesa Mkandara naye asipotatua tatizo hili la wanafunzi leo, na yeye tutamuumbua!!! Wakati wa wana jambo kupiga soga tu na kutotenda umepita... ni lazima tushiriki kikamilifu katika kuleta mabadiliko tunayoyataka...
 
Back
Top Bottom