Just in: UDSM wafukuzwa

Na Hassan Abbas

UONGOZI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) leo huenda ukajitia kitanzi utakapotoa hatma ya viongozi wa Serikali ya Wanafunzi (DARUSO) ambao ni miongoni mwa 56 waliokuwa wamesimamishwa awali.

Wakati 'vinara' hao wa mgomo wakianza kuhojiwa asubuhi hii, hali ya mambo katika chuo hicho inaonesha dhahiri kuwa wanafunzi wamejipanga kupinga uamuzi wowote wenye madhara kwa wenzao, uongozi wa chuo utakapotoa uamuzi wake leo mchana.

Jana wakati wanafunzi waliosimamishwa wakiendelea kukamilisha taratibu za utetezi wao, ziliibuka fununu chuoni hapo kuwa huenda baadhi yao wakasamehewa na wengine kukumbwa na 'fagio la chuma.'

"Hizo taarifa zimeenea hapa chuoni, lakini hakuna mwenye uhakika nazo," alisema mmoja wa wabunge wa chuo hicho na kuongeza:

"Sisi tunasubiri hatma itakayotangazwa na mara tu tutakapopata taarifa rasmi, Bunge letu litakaa kujadili kitakachokuwa kimeamuliwa."

Jana mamia ya wanafunzi wa kampasi ya Mlimani wakiwa na baadhi ya viongozi wao wa DARUSO waliosimamishwa walikusanyika kwenye uwanja maarufu chuoni hapo wa Rodney Revolution Square, ambapo lilipitishwa azimio la kukutana tena kesho, mara baada ya hatma ya wenzao kutangazwa.

Akizungumza na Majira, Makamu wa Rais wa DARUSO, Bi. Renedata Rushau, alisema wanafunzi wote ndio watakaokutana hapo Rodney Square kesho saa tisa alasiri na kuamua wafanye nini iwapo kutakuwa na uamuzi unaowaumiza wenzao.

"Azimio lililofikiwa leo ni wanafunzi wote kesho kukusanyika, ili watoe maoni yao na kisha Bunge la Wanafunzi litakaa kutangaza kile kitakachopaswa," alisema.

Juzi akizungumza na gazeti hili, Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandala, alisema chuo kinatarajia kulimaliza suala hilo katika namna ambayo itarejesha amani na utulivu.

Wakati huo huo, Agness Mayagila, anaripoti kutoka Arusha, kwamba
Kurugenzi ya Vijana Taifa ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) imepongeza uamuzi wa uongozi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam kuwarejesha wanafunzi wote waliokuwa wamesimamishwa masomo yao kutokana na mgomo wakiishinikiza Serikali kuwakopesha asilimia 100 ya ada na mahitaji mengine.

Taarifa ya Uongozi wa Chuo Kikuu hicho, ilisema kuwa idadi ya waliotimiza masharti ya kurejea chuoni ni asilimia 41 jambo linaloonesha kuwa Watanzania wengi hawana uwezo wa kujilipia gharama za masomo.

Aidha, taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Mkurugenzi wa Vijana wa CHADEMA, Bw. John Mnyika, ilisema waliotimiza masharti walifanya hivyo kwa kujibana sana, ikiwa ni pamoja na kuuza mali, vifaa vya ndani, kwa lengo la kuhakikisha wanarejea chuoni.

Iliiomba Serikali kutotumia asilimia 41 ya waliolipa kama kiwango cha Watanzania wanaoweza kujilipia, kwani wengi wamelipa kwa shinikizo na hofu ya kupoteza masomo na wamelipia kwa matarajio ya kupatikana ufumbuzi baadaye.

Ilieleza kuwa kwa upande wa pili, wananalaani uamuzi wa Chuo Kikuu kusimamisha wanafunzi 56 wakiwamo viongozi wa DARUSO kwa madai kuwa walitumia nguvu ikiwa ni pamoja na viboko kuwashinikiza wanafunzi wengine wagome.


NB:

Napenda kuwatangazia mapema kuwa endapo uongozi utawapa viongozi wa DARUSO masharti ya kujinyonga ili warudi chuoni, msiwe na shaka HAWATATUABISHA!
 
Tanzanianjema,
Unafikiri hivyo?..
Labda hunifahamu vizuri ndugu yangu lakini mtu kama mimi siwezi kupendekezwa wala kupewa nafasi ktk kundi la washindi kwa sababu nitakuwa mzigo mkubwa sana.. eeeeh bwana wee mimi baba ubishi sii rahisi kubebeka hata kidogo. Tatizo kubwa ni kwamba nina Imani ya dini namuogopa Mungu na pia imani ya nchi kuiogopa sheria.
Kujiunga na hao jamaa inawezekana kabisa ikiwa watanipa nafasi kwa sababu haikatazwi kuingia msikitini/kanisani kuomba dua.
Na pengine JK anahitaji vichwa kama vyetu kuupata ushindi kwa njia halali na hilo fagio la chuma kuwa kwa viongozi wabaya!..
Nyerere kawahi kusafisha baraza zima la mawaziri!...nasikia kutokana na kichwa kimoja tu kilichomshauri!...
 
This has made my day, nauona moto wa activism kwa hawa vijana. Hapa walipofikia ningewaomba ndugu zangu wa vyama vya siasa wakae kimya, wasitie neno-wanaweza kuchafua hewa. Huyu dada Bernadetta ni kiongozi shupavu mpaka hapo!
 
FFU watanda Chuo Kikuu kusubiri amri

2007-05-17

Na Jackson Joseph


Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), jana waliwekwa tayari kukabiliana na vurugu zozote ambazo zingetokea, kufuatia kuwepo kwa taarifa kwamba, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani, walipanga kukutana kujadili hatma ya wenzao 56 ambao bado wamesimamishwa masomo.

Magari aina ya Landrover Pick-up 110 ambayo mara nyingi hutumiwa na kikosi hicho, yalionekana yakiranda randa maeneo ya Chuo na yanayokizunguka.

Magari hayo yalipitapita huku na kule kwa mwendo wa taratibu yakiwa na askari waliokuwa wakionyesha dhahiri wanasubiri tu amri ya kuanza "kuwashughulikia" wanaofanya fujo.

Mbalia na Land Roer hizo, pia kulikuwa na magari makubwa ya maji na jingine ambalo inadhaniwa kuwa ni la kumwaga upupu.

Hata hivyo, askari hao hakuwataka kuongea na waandishi wetu kuzungumzia sababu ya kuyazunguka mara kwa mara maeneo ya chuo kikuu.

Wanafunzi walipanga kukutana jana saa 4:00 asubuhi eneo la Revolution Square, ambalo hutumiwa kwa ajili ya mikutano ya dharura, mara nyingi ikiitishwa na wanafunzi wenyewe, badala ya Serikali yao (DARUSO) ili kutoa madai kwa uongozi wa chuo.

Hata hivyo, uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, uliwasihi viongozi wa DARUSO kuwashawishi wanafunzi hao kuahirisha mkutano huo hadi jana saa 7:00 mchana, jambo ambalo walikubali.

Lakini baadaye, Makamu wa Rais wa DARUSO, Bi. Benedetta Rushahu aliwaeleza waandishi wa habari kuwa, Uongozi wa Chuo ulishauri mkutano huo wa wanafunzi, uahirishwe hadi leo saa 11.00 jioni.

Alisema Uongozi wa Chuo umeomba muda huo kwa kuwa kamati ya nidhamu inaanza kikao leo saa 2:00 asubuhi kuwajadili wanafunzi hao waliofukuzwa.

Alisema hivyo uliona kuwa ni busara wanafunzi hao kukutana baada ya maamuzi ya kikao cha nidhamu kutolewa leo.

"Ndiyo sasa tunabandika tangazo la kuwajulisha wanafunzi kuwa mkutano wa Revolution Square, utafanyika kesho saa 11:00 jioni na umepewa baraka zote na uongozi wa chuo," alisema.

Wakati tangazo hilo linabandikwa saa 6:50 mchana, baadhi ya wanafunzi walikuwa tayari wamekusanyika katika eneo hilo huku mvua ikionyesha tayari kwa mkutano huo, lakini walitawanyika baada ya kusoma tangazo hilo.

Baadhi ya wanafunzi walisema matangazo ya mkutano wao uliotakiwa kufanyika jana saa 4:00 asubuhi, yaling?olewa na askari waliokuwepo chuoni hapo.

"Tunashangaa matangazo yote tuliyoweka kuwajulisha mkutano wa saa nne yameng?olewa na polisi na kisha Uongozi wa Chuo ukabandika ya kwao ya vitisho," alisema.

Tangazo lililotolewa jana na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Taaluma, Ushauri na Utafiti), Profesa Makenya Maboko katika mbao za matangazo, liliwaonya wanafunzi kuepuka mikusanyiko isiyoruhusiwa chuoni hapo kwani ni kinyume na taratibu za sheria ndogo za chuo.

Sambamba na tangazo hilo, pia kulikuwa na minong`ono kuwa kulikuwa na idadi kubwa ya watu wa usalama wa taifa wakifuatilia hali ya usalama chuoni hapo.

Bi. Benedetta alisema hatma ya wenzao 56 ambao wamekwishapewa barua za kutakiwa kufika kesho kujieleza itajulikana leo saa 9.00.

Alisema chochote kitakachojitokeza baada ya kikao hicho, Daruso watafahamishwa na taarifa zitatolewa kwa wanafunzi kupitia mbao za matangazo.

"Baada ya kamati ya nidhamu kukaa na kuwahoji wanafunzi hao 56 mmoja mmoja, ndipo uamuzi utatolewa, na saa 11:00 jioni tutakutana Revolution square wanafunzi wote," alisema.

Hata hivyo, alisema kama wenzao hawatarudishwa chuoni hapo, uongozi mzima wa Daruso na bunge lote litalazimika kujiuzulu.

Alisema watalazimika kufanya hivyo ili kuuachia uongozi wa chuo madaraka yote kwa kuwa hawaoni umuhimu wa wao kuwepo wakati wenzao hawapo.

"Tutakuwa tumewasiliti wenzetu ikiwa tutaendelea na masomo wakati wote tulikuwa pamoja kudai haki zetu," alisema.

Hata hivyo, alisema wana imani kuwa baada ya kikao hicho wenzao watarudishwa na kuendelea na masomo.

Katika barua walioandikiwa wanafunzi waliosimamishwa ambayo Nipashe ina nakala yake, wanatakiwa kujieleza kwa maandishi namna walivyoshiriki kwenye mgomo huo. Barua hizo waliziwasilisha jana.


SOURCE: Nipashe

Serikali inatumia sana vyombo vya dola kunyanyasa wananchi wake?
 
Mwanasiasa hapa leo naona nikupinge unaposema wanasiasa wakae pembeni ni kosa kwani bila prtesha za wanasiasa chuo kisingelifunguliwa na hapo keshokutwa jumamosi watakuwa na mkutano mwingine kule tanga kuwaamsha watanzania ili kujua maana ya asilimia 40. kumbuka kule morogoro walifanikiwa kuamsha hisia za watanzania nami nawapa go ahead kuwani huwa hii serikali ya jk kazi yake ni kusikilizia tuu wakiona watu wnaelewa ukweli wanatafuta pa kutokea. kumbuka ishu za richmond hadi wanawatuma pcb,ishu nza malima vs mengi, nssf ona limekufa kwani hakuna wanasiasa waliolivalia njuga.
Wanasiasa tieni timu nchi imeuzwa hii.
 
Kama kawaida ya serikali ya CCM-kutoa majibu rahisi kwa maswail magumu, dakika chache zilizopita, vijana wetu wa mlimani wameambiwa wafungaishe vilivyo vyao warudi nyumbani.

Haya Kikwete huyu aliyeahidi kuwa yeye asingefunga vyuo vikuu kwa sababu ya migomo imekuwaje tena?!
Prof unakumbuka hapa?
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom