Just in: UDSM wafukuzwa

Just in: UDSM wafukuzwa

Mwanakijiji

Uongozi, ujasiri na kutokuwa mwoga hakuanzii ukiwa chuo kikuu; hayo ni malezi ambayo tunakuwa nayo...jamaii inabidi ibadilike from top to bottom.

Watawala wetu ni reflection ya wananchi; na ili mabadiliko yaje ni lazima iwe process kama hii ya kuelimisha jamii. Wengine watabadilika haraka wengine itawachukua karne....Kizazi Kijacho; watoto watakao lelewa na wakina mwanasiasa na mkjj hao ndio wataleta mabadiliko katika jamii. Hawa ambao tayari wapo chuo kikuu it's very too late. Maana hao pengine ni kama mimi niliyewahi kuambiwa na Mama yangu "usiende shule na kiatu cha gharama kuliko anachovaa mwalimu wako". 18 years later ndio naelewa alikuwa anamaanisha nini.

Very true Yeboyebo. Tumekuzwa katika mfumo wa kuwambiwa kuwa kumhoji mkubwa ni ukosefu wa adabu. hata majumbani, baba akikosea unatakiwa unyamaze au umsingizie mwingine. Ndio maana hata humu kwenye forum JK akikosea tunawanyoshea vidole washauri badala ya JK mwenyewe. Hili ni tatizo zito la jamii yetu, bahati mbaya mfumo wetu wa elimu pia unafundisha watu ukondoo. But slowly, things are changing. At least we are now getting some daring guys ambao ndio hao wanaonekana wasaliti. Tutafika lakini!
 
Ama kweli serikali ameamua kuwanya wanafunzi wa elimu ya juu wafunge midomo yao, hizi fomu haziwatendei haki wanafunzi
 
This is illegal!!! ni kinyume na sheria na utaratibu wa kibaguzi. Kama kuna wanafunzi wametia sahihi fomu hizo basi wajue wamekwisha!! Chuo Kikuu na HESLB wangefikishwa mahakamani kwa kutunga taratibu ambazo ni kinyume na katiba, ni adhabu inayo dhalilisha na kuteza watu.
 
Mzee Mwanakijiji,
Utanisamehe ustadhi lakini mimi nasimama nje kidogo ya lingo hili na kulitazama swala hili kama ni swala la kitaifa!
Sidhani kama ni hatua nzuri kuwashauri wanafunzi jinsi ya kupambana na serikali hali swala hili haliwahusu wao pekee ila kizazi kizima cha Watanzania. Utaratibu wa elimu nchini ni mbovu! mbegu mbaya ktk maendeleo ya taifa na utaathiri elimu nchi nzima na sio hawa wanafunzi waliopo vyuoni leo hii...
Kwa nini sisi wananchi (tena wasomi) leo tunajitenga nao kama sio nasi tumevutwa ktk mkumbo wa Ubinafsi?
Na kwa nini pia vyama vya upinzani wasijihusishe bega kwa bega na wanafunzi hawa hata kuwakilisha Upinzani mkubwa ktk chama tawala. Je, kweli hili ni swala lao kama inavyo aminika katika kufuta Umaskini....

Vyama vya upinzani vimesimama wapi ktk swala hili zaidi ya ahadi zao ktk sera. Ikiwa hawawezi kusimamia sera zao leo hii itakuwaje rahisi kwao kutekeleza sera hizi hali kitendo kidogo sana cha kuungana na wanafunzi kudai haki yao ya msingi..Na vipi nyie wasomi kusimama na kutoa makosa yote ya serikali hali wenyewe mmekaa kijiweni na kunyoosha vidole.. Lini tutakuwa kitu kimoja kupambana na utawala mbaya!.. jamani leo hii ni miaka 22 ndani ya soko huria, nchi yetu inategemea zaidi misaada ya hali mali na hata elimu toka nje kuliko wakati wowote!..
Come to think of it, nadhani hata sisi tumekumbwa na fikra za kibinafsi kwa kunyoosha vidole vyetu kuonyesha kwamba hili tatizo ni la wanafunzi WALIOPO vyuo vikuu. Jamani mapinduzi ya kifikra India na China hayakuanza hivyo!.. hayakutegemea wanafunzi wa vyuo vikuu kusimama na magongo yao hali wao ndio vilema.
Kama nilivyokwisha sema toka huko nyuma kwamba Ubinafsi ndio ustaarabu MPYA wa Mwafrika...
Hulka hii inabidi tujifunze na kuiondoa kabisa kwani leo hii tatizo la elimu limekuwa ni tatizo la baadhi ya watu! yaani kundi fulani. Wale wote wasiokuwepo vyuoni sii tatizo lao tena, hii ni kukosa UMOJA na msimamo. Hii inawapa nguvu sana viongozi wa kiafrika inapofikia swala gumu nazito la kitaifa kuwekwa ktk mafungu mafungu.
Nilipokuwa Dar-es- Salaam ktk viwanja vyangu nimegundua kwamba wanafunzi wetu, watoto wetu wanapata taabu kubwa sana kuitafuta ELIMU. Leo hii watoto wa kike wanauza miili yao kuitafuta elimu. Ni jambo la kawaida kuwakuta akaina dada wa vyuoni ktk mabaa wakisaka wanaume ili wapate kulipia ada za shule. Tembelea mabaa ya Sinza hasa pale mitaa ya Ambianse wamejaa watoto wa vyuoni wakiuza miili yao kila siku. Rais wetu na viongozi wetu wanatakiwa kupewa wazi ukweli huu kuhusu taifa tunalolijenga leo.
Hao wa kiume sifahamu hata wanachokifanya lakini tatizo la Ujambazi na biashara za Unga zinaweza kuwa ni moja ya matokeo ya kuifanya elimu nchini kuwa ni biashara.

Nawaombeni nyote ndugu zangu tuwakilishe mawazo yetu kama wahusika na waathirika wa mipango mibaya kama hii.
 
Mkandara, mgomo huu ulichukua hatua mbaya pale wapinzani walipoingilia kati na hivyo kuwa chanzo cha kuwagawa wanafunzi na hatimaye kuwepo wale wa TAHLISO na wale wa DARUSO. Wakati Daruso haijali kupokea mawazo na ushirikiano wa wapinzani, TAHLISO wanadai wanataka wawe neutral. Ni kutokana na mgawanyo huu wa mwanzo ndio maana mgomo huu umeshindwa. Binafsi, wapinzani wasiliteke nyara suala hili kwa mtazamo wa kisiasa. Katiba inasema wazi kuwa ni jukumu la serikali kuhakikisha kuwa mtanzania yeyote anapata nafasi ya kusoma hadi kiwango chochote!

Kama kweli wapinzani wanataka kuwasaidia wanafunzi hawa ni kufanya hivyo kwa vile wao ni Watanzania wanoajali maslahi ya elimu ya juu na siyo kwa vile wao ni wapinzani. Kwenye masuala ya kitaifa kama hilo mgawanyo wa wapinzani, chama tawala n.k hauna maana yoyote zaidi ya kudumaza mawazo na kulegeza uthabiti wa hoja.

Wako wapi Haki Elimu? wako wapi TAMWA, FEMACT n.k wako wapi watetezi wa haki za msingi za binadamu? Hiyo fomu hapo juu kama siyo kamba ya kujinyongea ni nini hiyo? Hili ni suala la Taifa na watanzania wasikubali watu wachache wawaamulie mambo muhimu kama hayo.

Nimefafanua kwa kina hoja yangu hii hapa: KLH News International
 
Mzee Mwankijiji,
Ni jukumu letu kuzama zaidi ya mgogoro wa TAHLISO na DARUSO. Nimekwisha sema kwamba vyuo vyetu vinapokea wanafunzi wa aina mbili...Wale wanaosoma bure na wengine KULIPA.. Hii ni mbinu mbaya sana ktk maendeleo ya elimu nchini, ni mbinu ya kuwatenga wanafunzi kimawazo. Rahisi kuelewa mwanachama wa Daruso na yule wa Tahliso kwa sababu chuo kimoja kina wanafunzi wa aina mbili...Elimu ni haki ya kila Mtanzania.

We have to set standard! na sio fedha kuweka standard!..
 
Uongozi UDSM wapewa saa 48 kuwarejesha waliosimamishwa

Habari Zinazoshabihiana
• SUA yasogeza tarehe ya wanafunzi kurejea chuoni 07.05.2007 [Soma]
• UDASA yapinga UDSM kuwa na makamu watatu 14.04.2006 [Soma]
• UDASA yapinga UDSM kuwa na makamu watatu 14.04.2006 [Soma]

*Ni uamuzi wa Bunge la dharura la Wanafunzi
*Ladai hawakuongoza mgomo, walitekeleza maamuzi
*Pia waazimia kukiburuza chuo mahakamani

Na Hassan Abbas
HALI ya mambo bado si shwari katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) baada ya wanafunzi waliorejeshwa jana kuibua hoja nzito wakiutaka uongozi wa chuo hicho kuwarejesha wenzao 56 waliosimamishwa, bila masharti hadi kufikia kesho saa 4 asubuhi, vinginevyo mgomo mkubwa utatangazwa.

Maamuzi hayo yalifikiwa kwenye kikao cha dharura cha Bunge la Wanafunzi wa Kampasi ya Mlimani (USRC) kilichofanyika jana jioni kwenye ukumbi wa Art Theatre B (ATB).

Habari za kuaminika kutoka ndani ya kikao hicho, zinaeleza kuwa awali Bunge hilo lilikumbwa na mgawanyiko katika suala la kugoma kabla ya kufikia muafaka.

"Kikao kimepitia tathmini ya mgomo na kuona kuwa viongozi waliozuiwa kuanza masomo wamesimamishwa kimakosa kwa sababu wao si chanzo cha mgomo, bali walisimamia maamuzi halali yaliyopitishwa na Bunge la Wanafunzi ambalo linatambuliwa katika kanuni na sheria za chuo,"kilisema chanzo chetu.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, Bunge hilo pia lilikubaliana katika kipindi cha kusubiri kama uongozi wa chuo utatekeleza ombi lao hadi kesho, kuwasiliana na wataalamu wa masuala ya sheria ili pia kuangalia uwezekano wa kuchukua mkondo huo katika kuhakikisha wenzao wanarejea masomoni na kufanya mitihani inayoanza wiki ijayo.

Uamuzi huo wa Bunge umetokana na ukweli kwamba karibu viongozi wote wa Serikali za Wanafunzi kwenye Kampasi za Mlimani, Chuo Kikuu cha Ardhi na Usanifu wa Majengo (UCLAS), Chuo Kishiriki cha Elimu Chan'gombe (DUCE), Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa (Iringa) na Taasisi ya Habari na Mawasiliano (IJMC), wamezuiwa kwa muda usiojulikana kuanza masomo yanayoanza leo.

Mbali ya kukosa masomo, wanafunzi wengi walioripoti jana wamekuwa wakiamini kuwa viongozi hao wametolewa kafara baada ya kusimamia hoja za msingi kwa niaba ya wanafunzi wenzao.

Wanafunzi kadhaa waliozungumza na Majira kwenye Kampasi ya Mlimani mapema jana, walikiri kuwa baada ya kurejeshwa masomoni, wengi wao wanaangalia mbele hasa wakijiandaa na mitihani inayoanza wiki ijayo lakini suala la wenzao 56 bado linawachanganya.

"Hakuna kiongozi aliyeanzisha mgomo. Mgomo ulikuwa wa wanafunzi wote walioamini kuwa walikuwa na hoja ya kutaka majibu kutoka serikalini," alisema mmoja wa wanafunzi wa shahada ya uchumi kwa sharti la kutotaja jina na kuongeza:

"Hivi sasa kama unavyoona wanafunzi wengi wanahangaika kujaza fomu ili kesho (leo) waanze masomo lakini hakuna mwenye furaha anapoona viongozi ambao hawakuwa na makosa wanatolewa kafara.
"Watu wanataka kujua hatma yao ila tatizo umoja haupo kwa sababu hakuna wa kuwaongoza wafanye nini."

Katika Kampasi za Mlimani na UCLAS, gazeti hili lilishuhudia wanafunzi wakijaza fomu za aina mbili; Fomu 'A' ambayo ni ya kukubali kutii kanuni na sheria za chuo, ambayo inawabana wote walioshiriki katika mgomo kutojiingiza tena katika suala kama hilo.

Pia wanafunzi hao walikuwa wakijaza Fomu'B' ambayo ni maalumu kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza walioshindwa kulipa asilimia 40, ambayo baadaye itafanyiwa tathmini na Bodi ya Mikopo ili kuona namna ya kuwasaidia.

Wakati wanafunzi hao wakiendelea kujaza fomu hizo imebainika pia kuwa uongozi wa chuo ulikuwa umeshatoa ratiba ya mitihani katika vitivo mbalimbali ambayo imepangwa kuanza Jumatatu ijayo.

Uongozi wa chuo hicho hadi jana haukuwa umetoa tamko lolote jipya kuhusu hatma ya waliosimamishwa, hali inayoashiria kuwa msimamo unaobaki ule wa mwishoni mwa wiki wa Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandala, aliyeahidi kuwa mchakato wa kuwahoji upya wanafunzi hao 56 ungefanyika na usingechukua muda mrefu.

Alipoulizwa jana jioni kwa njia ya simu kuhusu maamuzi hayo ya Bunge la Wanafunzi, Prof. Mukandala alisema hakuwa na taarifa za kikao hicho na kuahidi kuzifanyia kazi na kutoa taarifa.

"Ndio kwanza unaniarifu kuhusu uamuzi huo, sikuwa na taarifa. Tutaliangalia hilo katika taratibu zetu na kulitolea ufafanuzi," alisema.
 
mimi nawaunga mkono kama wataonyesha mshikamano kwa kizazi kijacho.matokeo na mafanikio ya mgomo wao ndio ufumbuzi wa watoto wetu ambao wapo shule za msingi.
hapa ndipo kaka na dada watakapoonyesha njia kwa wadogo zao..
wito kwa watanzania wote muda wa kulala umekwisha tuwaunge mkono vijana wetu,viongozi na serikali yetu wanakula na kuvimbiwa hivyo hawamjui mwenye shida.
 
Dakika chache zijazo nitawaletea "Breaking News" kuhusu suala ambalo linazidi kushangaza.. itawashtua na kuimbua serikali yenu, na itasababisha hatimaye kujiuzulu kwa Prof. Msolla!!!
 
You must be kidding!

This' Tz bwana... Hajiuzulu mtu hata kwa ndumba. Nyie mlie tu. Sasa kwa taarifa yako atakingiwa kifua. Hebu hiyo habari inayovunjika tuisome fasta maana wengine tuna hamu ya kuweza kujua kama INAWEZEKANA kwa jamaa huyu kujitoa kafara kama unavyodai.

Binafsi siamini katika serikali ya Tz wenye 'ulaji mkubwa' wako tayari kuuachia. Hata Dito sasa hivi ukimwuliza naamini atakwambia anatamani angekuwa mkuu wa mkoa bado!

That's Bongo bwana
 
Mbona wanitisha mkjj,lakini mtu mzima hatishiwi nyau.Nasubiri kwa hamu hizo habari
 
_41662286_breaking_news_203.jpg


Prof Msolla ajiuzulu? Hebu Mwanakijiji wacha kuchelewesha. Can you tell us what's going on? Unavuta attentions zetu kwanza sio?
 
MKJJ

Ahadi ni deni....au amemtuma mtu aende Bagamoyo kuroga...wewe umejuaje kama Msolla atajiuzulu kutokana na hiyo habari utakayoivunja?
 
_41662286_breaking_news_203.jpg


Prof Msolla ajiuzulu? Hebu Mwanakijiji wacha kuchelewesha. Can you tell us what's going on? Unavuta attentions zetu kwanza sio?


wOrM

Umenistua....lol..mimi nilijua tayari imeshavunjika hiyo habari...!!
 
Kwa upande mwingine, wanafunzi wanavuna walichopanda. Wamekuwa hawamwangalii JK kwa akili. Amewadanganya mengi, nao wakawa wanamshangilia tu kama vile mtu anavyoshangilia mpira.

.......kama hili ni kosa la jk...sidhani,kwani jk ameyakuta haya tayari. anachoweza kufanya ni kuyarekebisha....hebu ngoja tuone atafanya nini juu ya hili.

for sure ku-act ata-act....tusubiri!
 
mambo yote yako tayari yamesetiwa... na serikali ya JK iko tayari kuumbuliwa kwenye jamii ya Kimataifa.. ENOUGH IS ENOUGH!!! .. in 20 Minutes.. I'll break the news...!!
 
Nilipokuwa Dar-es- Salaam ktk viwanja vyangu nimegundua kwamba wanafunzi wetu, watoto wetu wanapata taabu kubwa sana kuitafuta ELIMU. Leo hii watoto wa kike wanauza miili yao kuitafuta elimu. Ni jambo la kawaida kuwakuta akaina dada wa vyuoni ktk mabaa wakisaka wanaume ili wapate kulipia ada za shule. Tembelea mabaa ya Sinza hasa pale mitaa ya Ambianse wamejaa watoto wa vyuoni wakiuza miili yao kila siku. Rais wetu na viongozi wetu wanatakiwa kupewa wazi ukweli huu kuhusu taifa tunalolijenga leo.
Hao wa kiume sifahamu hata wanachokifanya lakini tatizo la Ujambazi na biashara za Unga zinaweza kuwa ni moja ya matokeo ya kuifanya elimu nchini kuwa ni biashara.

.......mzee wangu,sidhani kama ada ndio inawafanya hao dada zetu[wodogo na watoto zetu pia]wauze miili yao but rather ukweli wa maisha ya mlimani[tamaa za maisha mazuri,kushindana hali ya maisha,na upenzi wa kujirusha na kudoweya vya bure].....nayasema haya kwa ufahamu halisi!

halafu tukumbuke kuwa maadili ya bongo yalimomonyoka zamani hasa. hawa toka wakiwa o'level walikuwa wakiliwa uroda,tena na mijibaba mijitu mizima kama siye...isiyo na aibu na kupenda vichanga.

wa kiume sijui!....sijasikia kama kuna mashoga hapo mlimani!
 
Mniwie radhi, najaribu kuamua kama niweke sasa hivi, mida ya usiku au mapema kesho kwani tukio na kile ambacho nataka niwaambie kitatokea Alhamisi... Nafikiri itakuwa ni too early to break the news kwani nikiweka sasa hivi, serikali will act tomorrow na kuvuruga mipango ya Alhamisi...
 
Ish!

Huyu kishaogopa sasa... Nipe mimi nikuvunjie hizo habari basi. Anyway; mi nalala kwanza
 
Back
Top Bottom