Just in: UDSM wafukuzwa

Just in: UDSM wafukuzwa

wanafunzi warejeshwa chuo.

41.2 watimiza masharti. Wengine watakiwa kulipa kabla ya mwaka wa masomo kuanza.

vinara 56 watajwa na kutakiwa kutoa maelezo ya ziada juu ya mgomo
Ni vizuri kama wamekubali kuwarudisha wote.natumai sasa watasoma na watatumia njia nyingine kuendelea kudai kile wanachoona kitawapa unafuu.
 
Uongozi wa chuo kikuu cha Dar es salaam umetangaza kufungua chuo kuanzia tarehe 14 mwezi huu. Wakati huo huo, wanafunzi 56 wamesimamishwa chuo, wengi wao wakiwa ni viongozi wa serikali za wanafunzi toka UDSM, MZUMBE, na UCLAS.

Asilimia 41.2 waliweza kutimiza masharti yote tisa, wakati wanafunzi wengine walishidwa kukamilisha kipengele cha fedha. Hata hivyo chuo kimerudisha wanafunzi wote na kuwataka watimize masharti makuu mawili.

Wanafunzi wote watahitaji kufanya means test, itakayo baini uwezo wa wanafunzi kifedha. Form hizo zinatakiwa kujazwa na kurudishwa kwa bodi ya mikopo kabla ya tarehe 30, June, kwa ajili ya uchambuzi. Watakao hawana uwezo wa kulipa, bodi ya mikopo bodi ya mikopo iwakopeshe. Walionauwezo watadaiwa na kuombwa kulipwa kufuatia utaratibu wa chuo.

Mwaka wa pili wanatakiwa kulipa kabla ya kuingia mwaka wao watatu wa masomo. Mwaka wa tatu wanatakiwa kulipa kabla hawajachukua vyeti vyao.

Mitihani imepangwa kuanza me1 21.
 
Sasa ndio tuwaone wanafunzi hapa kama walijiandaa kisawasawa kugoma. Kama walikuwa serious hawatakubali kurudi huku wenzao wakibaki. Otherwise, walikuwa walikuwa hawana sababu ya kugoma in the first place!
 
Mwanasiasa, you divide and rule.....

Swala la kujipanga tena na kugoma bila uongozi si lelemama unahitaji watu shupavu, makini na wendawazimu.

Chuo kilitambua uwezekano wa kuwepo mgomo iwapo wanafunzi watarudi na viongozi wao.

Just out of context, and i am not yet sure, but i was informed the university was under security watch due to the boam threated announced with vc on thursday...

My assumption is to legitimize the presence of security when they student return. My other guess the security is to monitor and control students until they finish their exams. I could be wrong...
 
Hapa pana utata yaani viongozi ndiyo wamekuwa wahanga pamoja na kusimama kidete kuwatetea asilimia hamsini na zaidi ambayo imeonekana haina uwezo hata wa kufurukuta kutimiza sharti la kulipa.Tusubiri tuone kama umoja ulikuwepo au ilikuwa tumsukume mlevi.
 
Mwanasiasa, you divide and rule.....


My assumption is to legitimize the presence of security when they student return. My other guess the security is to monitor and control students until they finish their exams. I could be wrong...


If this happens/is happening, then our universities are in mess. You do not expect intellectualism to flourish under such situation! God bless!

I hope safari hii angalau hawatachangamkia magwanda na kadi za CCM na kukubali kusombwa kama mizoga kwenda Diamond Jubilee! A lesson must have been learnt!
 
Rotten system.

Afadhali tuenze upya - kama mwaka 1961
 
If this happens/is happening, then our universities are in mess. You do not expect intellectualism to flourish under such situation! God bless!

I hope safari hii angalau hawatachangamkia magwanda na kadi za CCM na kukubali kusombwa kama mizoga kwenda Diamond Jubilee! A lesson must have been learnt!


Duh...ama kweli inaogopesha.
 
Uongozi wa chuo ume-decapitate student body wakijua kabisa kuwa haitaweza kufanya lolote bila kuwa na kichwa. Bila uongozi ni vigumu kwa wanafunzi wale kugoma tena; sijui wataanzaje.

Miaka ya themanini migomo mingi ilikuwa haiendeshwi na viongozi wa wanafunzi ila walikuwa wakishinikizwa kuiunga mkono. Kwa mfano kuna wakati mgomo uliendeshwa na jamaa mmoja mwanafunzi wa mwaka wa nne Civil Engineering ambaye hakuwa hata class representative; 'mahogi' wote ikabidi wamsikilize. Miaka miwili baadaye kukatokea mgomo ulioendeshwa jamaa mmoja wa Law ambaye naye hakuwa na cheo chochote pale chuoni; jina lake lilikuwa kama Phillemon au Sarungi vile nafahamu alikuwa aki-share jina moja na Phillemon Sarungi; nasikia baadaye alifariki kwa sickle cell anemia. Hapa ndipo nakumbuka "hogi' mmoja mwoga (sasa hivi mhadhiri pale Faculty of Education) aliposaliti wanafunzi na kujivua uongozi hadharani.

Sijui kama watu wenye kuweza kumobilize wanafunzi wenzao bila wao wenyewe kuwa viongozi bado wapo tena pale mlimani.
 
fist_of_glory_icon.JPG

Hakuna kitu kinachoudhi kama ubabe wa serikali. Inasikitisha kuona kuwa katika Tanzania tunatikiwa kuinama na kupigwa bong'oa kwa vile serikali imesema jambo fulani. Katika suala hili la wanafunzi wa vyuo vikuu kufukuzwa na serikali kushikilia msimamo wake wa kuwataka walipe fedha za chuo kikuu, wakati umefika kuwaonesha serikali kuwa "nguvu iko kwa watu"!!

Nyinyi wanafunzi wa vyuo vikuu ambao mmekubali kuburuzwa na serikali na utawala wa vyuo kwa vile mnaona hamna njia nyingine nawasihi mtulizane na kutafakari upya. Mtaendelea kusukumwa sukumwa kwani baadaye wakiwaambia "tumeona mnaweza kulipa asilimia 40, sasa itabidi mlipie asilimia 60" mtakataa!! Ni lazima mchore mstari ardhini na kuiambia serikali kuwa hakisomeki kitu hadi suala hili la malipo linatafutiwa ufumbuzi once and for all!!

It is about time to put your feet on the ground and don't you dare move! Viongozi wa Daruso na wengine wenye maslahi nawashaurini mfanye kile ambacho hufanywa mara nyingi kwenye nchi za kidemokrasia, siyo maandamano na mabango bali kukaa chini (Sit Ins)

a. Wanafunzi wote rudini vyuoni kwenu kwa makundi (siyo mtu mmoja mmoja) Mkishikilia mabango yasemayo yenye kuhamasisha serikali kuwaruhusu wote kurudi shuleni na kukabili tatizo zima la kulipia elimu ya juu. Mmekubali kugawanywa, hamuwezi kufika mbali! La maana wale walioruhusiwa kurudi wagome kurudi hadi wenzao wote nao wamerudi!

b. Jifungeni vitambaa midomoni (ishara ya kunyamazishwa!). Na mnaweza kuvaa nguo nyeusi kuonesha msiba mkubwa wa elimu ya juu Tanzania.

c. Nendeni na kukaa kwenye maeneo ya vyuo (hasa kwenye milango ya madarasa) na msiondoke hadi muondolewe kwa nguvu huku kamera zinaroll na picha zinapigwa ili kuionesha serikali mbele ya umma!


Mbinu hii ya kukaa chini, imetumiwa tangu wakati wa Mahtma Gandhi, na wakati wa kutafuta haki za raia kule Marekani. NI mbinu ambayo haina uchokozaji kwa serikali. Lengo kubwa la kutumia mbinu ni hii ni kulazimisha hoja ya watu isikilizwe na kuonesha hadhara kubwa kuwa kutotumia nguvu kwaweza kujibiwa kwa matumizi ya nguvu. Nina uhakika mkiamua kukaa chini kwenye milango na viwanja vya vyuo vyetu, watawaleta polisi na kuwasomea "Riot Act".. msibabaike, wala msikimbie, kaeni chini kama watawabeba na kuwapeleka kwenye makarandinga wawabebeni... mtazijaza mahakama, na jela, lakini wakati wa kuchukua msimamo umefika... woga wenu ndio umewaponza hadi hivi sasa!!

Wanafunzi wenzenu kwenye vyuo vikuu vingi duniani ndio wamekuwa chachu ya mabadiliko.. katika kupiga vita Ubaguzi wa Rangi Afrika ya Kusini, Sera ya Utenganisho wa Rangi huko Marekani, Vita vya Vietnam, kule Ujerumani mwaka 1968 n.k

There comes a point in a relationship between the State and the People when the people have to take a stand. Hili suala la kulipia asilimia 40 ni wakati kama huo, na watanzania tuwaunge mkono kuhakikisha kuwa vijana wetu wanarudi shuleni bila kubaguliwa kwa sababu ya uwezo wao wa kifedha!! Lengo la "kukaa chini" ni kuhakikisha Msolla anaondolewa na bodi ya Mikopo inavunjwa ili apatikane Waziri mpya na Bodi mpya yenye uwezo wa kukabiliana na matatizo ya elimu ya juu na kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu!

let there be a showdown.. yes, this looming showdown between the state and unarmed, peaceful body of students!! Let the Kikwete's government take a stand and make a choice!!
 
That is a very good strategy MKJJ. I hope watasikia. Lakini wasiwasi wangu ni ubinafsi, wewe subiri kesho watakavyokuwa wanakimbilia madarasani na kuacha wenzao wakikaangwa. I may be wrong, lets wait and see!

PS> Kusema kweli kama wanafunzi hawa wataamua kurudi madarasani na kuacha wenzao wakisota "rumande" ni wazi kuwa watakuwa ni wasaliti wakubwa na hawakuwa na sababu ya kugoma in the first place.
 
kuna msemo uanao sema mguu niponye,sasa hawa baada ya kurudishwa chuoni ndio imesha toka hiyo,kila mtu anaangalia alikotoka alifika pale peke yake na begi lake.leo sio raihisi hawa watu wakawa kitu kimoja.kunawalio toka mikoani na kwenye familia duni na wazazi wao wamesha sema ukifukuzwa tena utafute kwa kwenda.
Amani tuliyonayo hapa bongo ni ya watu wamezidiwa na matatizo ya kimaisha na kukosa muda wa kufikiri mambo mengine.
 
kuna msemo uanao sema mguu niponye,sasa hawa baada ya kurudishwa chuoni ndio imesha toka hiyo,kila mtu anaangalia alikotoka alifika pale peke yake na begi lake.leo sio raihisi hawa watu wakawa kitu kimoja.kunawalio toka mikoani na kwenye familia duni na wazazi wao wamesha sema ukifukuzwa tena utafute kwa kwenda.
Amani tuliyonayo hapa bongo ni ya watu wamezidiwa na matatizo ya kimaisha na kukosa muda wa kufikiri mambo mengine.


Sasa walipaswa kulijua hili mapema na wasingegoma, maana hamna walichopata zaidi ya kupoteza!
 
..........ushasahau jamii unayoi-address ni ya kitanzania....isiyo mshikamano,iliyo na woga,yenye ubinafsi moyo,na isiyounganishwa kwa lolote bali pesa,njaa,hofu,na huzuni!

tatizo hapo wengine wamekuja darsilamu,wengine mlimani....wengine hawana pa kukimbilia,wengine hizo siku walizofukuzwa walishukuru mungu wamepata off ya kusimamia biashara na miradi yao...wengine kujirusha...si unajua bongo wakati mwingine watu wanaenda mlimani ili nao wawe na digirii...na si wapate degree!

jamii zinazoweza hayo ziko asia na kwingineko ambako watu wa tabaka moja[almost]uhudhuria vyuo vyao...na tabaka jingine vyao....halafu wana tamaduni ya mass protest...ambayo hapa kwetu hamna!
 
Hivi pamoja na 58% kushindwa kulipia BADO WANAONA VIJANA HAWAKUWA NA HAKI YA KUSEMA HAWAKUWA NA UWEZO WA KULIPA.Kuna sababu gani ya msingi ya kutowarudisha viongozi ambao walikuwa wanawakilisha waliorudishwa,Hawa waliorudishwa lazima wawasimamie wenzao Kama wao walivyokubali kubeba jukumu la kusimama nao ktk kuhakikisha wasio na uwezo hawalipi.Umoja ni Nguvu!
 
yaani kama wanafunzi wetu wa vyuo vikuu ni waoga na wasio na msimamo isipokuwa kufuata mkumbo basi inaelezea ni kwanini tuna viongozi tulio nao!! Suala la intellectual honest halipo tena.
 
Back
Top Bottom