Guyz kama title unavyo eleza napanda ndege kwa mara ya kwanza maishani ..Naomba Abc za kuzingatia
1. Fika mapema – masaa 2 safari kabla zingatia sana wengi tumezoa kama tunaenda kupanda Kimbinyiko
2. Check-in – online au airport counter, pokea boarding pass, kabidhi mizigo ikiwa inawekwa label maalum ya utambuzi mizigo yako utaonana nayo baada ya kufika safari yako sehemu maalum ya kupokea mizigo hiyo.
3. Security – toa belts, saa, vitu vya metal, zipitie scanning, Laptop/ Ipad iwe peke yake haitakiwi kuchanganywa na mizigo mingine mfano kwenye bag.
4. Immigration – onyesha pasipoti wagonge exit ambayo itagongwa pia kule unakoelekea kama entiry pia onesha na boarding pass maana hy ndio inaonesha unaenda wapi na kumpa mtu wa immigration confidence ya kuwa unatoka nje ya nchi (kwa kimataifa) local flight hazina issue ya immigration
5. Nenda gate – angalia gate, fika mapema kabla ya kufungwa. Dakika 40 local, dakika 60 International. Manukato yenye zaidi ya 100Ml hayataruhusiwa kwenye mizigo ya cabin kama wataka weka kwenye mizigo unayokabidhi wakati wa check in.
6. Boarding yaani kuingia kwenye ndege – hufanyika kwa makundi: viti maalum, business/first, economy angalia nafasi status ya kwako uwe kwenye hilo kundi kwa kawaida hutangaza.
7. Kiti na usalama – tafuta kiti kama kilivyooneshwa kwenye tiket yako, 20A, 20B,20C 20D, 20E etc. Weka mzigo wako wa cabin juu ya carry-on.
Kaa funga mkanda wa usalama kama inavyoonesha kwenye display ya juu mara nyingi huonesha katazo la uvutaji sigara, na kufunga mkanda. Mahali hapo pata kuongoza ni wapi unaweza fungua mkanda kwa mlio na alama kuoneshwa kila mara hasa wakati wa kuruka take off na kutua yaani landing.
8. Ndege ikishafika – subiri isimame na kuzimwa engine kbs, kwa kawaida huwa wanataangaza kuwa sasa unaweza kushuka. Chukua mizigo wako wa cabin, pitia customs (kimataifa), pita immigration gonga entry kwenye passport (nchi destination) nenda kasubiri mzigo wako mkubwa uliokabidhi wakati wa ku-check in mizigo huwa kwenye Baggage Carousel/Baggage Claim Conveyor Belt. Angalia mzigo wako kwa makini inakuwa inazunguka so ukiuona wako uchukue nenda exit door.
Mara nyingi hz ndege za local zikiwa zinatoa tairi kwa ajili ya kutua yaani landing gear wakati inakaribia kutua huweza kutoa sauti ya kushtua. Weka kichwani usishtuke sana na kuleta hofu!!
Nakutakia safari njema mpwa.