Jumatatu napanda ndege kwa mara ya kwanza

Jumatatu napanda ndege kwa mara ya kwanza

Kila siku tunajifunza kiongozi sio mimi nais pia kuna washamba kama mimi humu hivo elimu itasaidia wengi
Hii si elimu chochote bali mashauzi tujue umepanda ndege tena kwa kuchelewa mwanangu. Anyway, i respect your choice and views altogether. Enjoy
 
1. Fika mapema – masaa 2 safari kabla zingatia sana wengi tumezoa kama tunaenda kupanda Kimbinyiko

2. Check-in – online au airport counter, pokea boarding pass, kabidhi mizigo ikiwa inawekwa label maalum ya utambuzi.

3. Security – toa belts, saa, vitu vya metal, zipitie scanning, Laptop/ Ipad iwe peke yake haitakiwi kuchanganywa na mizigo mingine mfano kwenye bag.

4. Immigration – onyesha pasipoti waginge exit ambayo itagingwa pia kule unakoelekea kama entice pia onesha na boarding pass (kwa kimataifa) local flight hazina issue ya immigration

5. Nenda gate – angalia gate, fika mapema kabla ya kufungwa. Dakika 40 local, dakika 60 International. Manukato yenye zaidi ya 100Ml hayataruhusiwa kwenye mizigo ya cabin kama wataka weka kwenye mizigo unayokabidhi wakati wa check in.

6. Boarding yaani kuingia kwenye ndege – hufanyika kwa makundi: viti maalum, business/first, economy angalia nafasi status ya kwako uwe kwenye hilo kundi kwa kawaida hutangaza.

7. Kiti na usalama – tafuta kiti kama kilivyooneshwa kwenye tiket yako, 20A, 20B,20C 20D, 20E etc. Weka mzigo wako wa cabin juu ya carry-on.
Kaa funga mkanda wa usalama kama inavyoonesha kwenye display ya juu mara nyingi huonesha katazo la uvutaji sigara, na kufunga mkanda. Mahali hapo pata kuongoza ni wapi unaweza fubgua mkanda kwa mlio na alama kuoneshwa kila mara hasa wakati wa kuruka take off na kutua yaabi landing.

8. Ndege ikishafika – subiri isimame, chukua mizigo wako wa cabin, pitia customs (kimataifa), pita immigration ginga entry kwenye passport nenda kasubiri mzigo wako mkubwa uliokabidhi wakati wa ku-check in kwenye Baggage Carousel/Baggage Claim Conveyor Belt Angalia mzigo wako kwa makini inakuwa inazunguka so ukiuona wako uchukue nenda exit door.

Mara nyingi hz ndege za local zikiwa zinatoa landing gear wakati inakaribia kutua huweza kutoa sauti ya kushtua. Weka kichwani usishtuke sana na kuleta hofu!!
Nakutakia safari njema mpwa.
Asante kwa dondoo hizi nilikuwa sijui chochote Vipi kuhusu cash utaakiwa kuwa na tsh ngapi mfukoni je viburungutu vinaruhusiwa?
 
Guyz kama title unavyo eleza napanda ndege kwa mara ya kwanza maishani ..Naomba Abc za kuzingatia
Ndege sii daladala wala boda boda,kuachwa nje nje na hamna kudai nauli!
 
Kawaida sana hata hakuna la ajabu we kufuata tu maelekezo basi kuwa busy na simu yako
 
Lingine, ukiwa ardhini mawingu unayaona juu ila ukiwa kwenye ndege mawingu utayaona kwa chini. Usishangae
 
Back
Top Bottom