Juliana Shonza, Mtela Mwampamba wahamia CCM...

Juliana Shonza, Mtela Mwampamba wahamia CCM...

DAMU CHANGA YA MOTO YAKINUKISHA DODOMA....

JULIANA SHONZA NA MWAMPAMBA WARUDISHA KADI ZA CHADEMA NA KUCHUKUA ZA CCM....... WANAWAPA VIONGOZI WA CHADEMA ZA USO BILA KUTAFUNA MANENO, MORE TO COME



................Tanuru la fikra
Mkuu unashau huyu mamluki alianza kutukana wakubwa zake akiwa ndani ya CDM hivyo hatushangai akipewa mshiko wake kwa nini asilipe fadhira???

 
Maskini Juliana mdogo wangu, anaonekana kwenye hiyo picha ana msongo wa mawazo. Mungu amsaidie huko aendako ili ndoto zake kwenye eneo la siasa zisipotee.

Pia namshauri akiweza atafute shule tena nje ya nchi akasome kama Masters Degree hivi au something else. When she comes back atakuwa amesettle kiakili.

Mungu akubariki mdogo wangu. Politics are not easy game (both to CCM and CDM).

Bless you Juliana

Queen Esther
Ester,mdogo wako inawezekana hakupata muda wa kukaa na wewe hata akapata hekima uliyonayo wewe mbele ya jamii hilo ni la msingi sana.katika siasa angalia sana unachosema na unachokifanya vinginevyo sasa hivi boya litageuka mifano ni mingi,ila itatosha kusema tu kwamba pengine azingatie ushauri wa kwenda kusoma japo hata akirudi na Uprofesa maadamu yuko CCM yaani unakuwa kama umelogwa vile,CCM hao wako wengi sana na hawana impact yoyote kwa taifa kwa kuwa hao ndio wezi wa mali za umma,mafisadi wala rushwa n.k.CDM bado ni chama imara na ndio tegemeo la wanyonge,wapo watu wanaomba na kufunga kwa ajili ya CDM na hakuna maombi yanayokwenda patupu ili tu andiko litimie,KILA PANDO ASILOPANDA MUNGU LAZIMA LING'OLEWE,ameanza huyo wengine wanafuata.
 
Siyo Rahisi kufanikisha mkakati wa kuisambaratisha CHADEMA, CHADEMA ni mpango wa Mungu kuwakomboa watanzania kutoka mikono dhalimu ya CCM! Shonza hiyo ndo safari yako ya mwisho kisiasa! RIP Juliana Shonza
Utabiri wa mzee wa Gombe kuwa Chadema kitasambaratika ndani ya mwaka mmoja unazidi kufifia, waliowategemea kufanya kazi hiyo wameanza kusalimu amri mmoja baada ya mwingine na waliomo wamedhibitiwa vibaya sana na makamanda, chezea Chadema.
 
Hii ni safi sana ,Shonza naomba uelewe kuwa CHADEMA sio chama cha matumbo ni chama cha MASIKINI JEURI umeshindwa ulichotumwa sasa umerudi kwenu SISIEMU, tuachie kazi ya kuikomboa nchi yetu kutoka kwenye makucha ya MAFISADI, ACHA TUPAMBANE , SHONZA KUMBUKA KUWA HERI MASIKINI WA MALI KULIKO UFUKARA WA AKILI NA MAWAZO
 
Duh! kweli JK hana kazi. President anao muda hata wa kuwapokea hawa wakinyiha wa Itaka, badala ya kushughulikia mambo nyeti ya chama na nchi kwa ujumla.
Nilitegemea katika masaa 24 kuanzia saa 4 asubuhi jana angelikuwa ameongelea suala la Buselesele, Gaita. Au ameshafanya hivyo ila mimi ndiye niko nyuma ya pazia!?
Kwa jinsi suala la vijana hawa lilivyo, hata Nape kuwapokea isingekuwa busara labda katibu wa wilaya wa chama!
 
Hekaheka zooote zile mwisho wake ulikuwa ni huo.
Sasa amehamia vipi huko wakati yeye ni Makamu Mwenyekiti wa Bavicha na ana mpango wa kugombea uenyekiti wa Bavicha uchaguzi ujao?
wewe vipi?si umuache agombee?kwani inakuuma nini?
 
".....waliondoka kwetu ili wadhihirishwe hawakuwa wa kwetu kama wangekuwa wa kwetu wangekaa nasi..." ameenda kuungana na wa kwao.
 
CHAMA MAKINI NI CHADEMA PEKEE!!! Uozo wa Chadema unaenda CCM!
 
Hili bomu bora likalipukie huko huko kwa maccm.kicheche wa siasa na mzandiki mkubwa!
 
Watanzania wana uana Geita kwa propaganda zilizo asisiwa na ccm ili kuendelea kutawala. Badala ya Rais wa nchi kutoa tamko yeye anapoteza muda kuwa rubuni vijana wenzetu wasomi uchwara,wapiga dili na wachumia tumbo.
 
Hahaha ccm kushiney, wanashangilia kulamba magalasa!? Kwakuwa imekosa mvuto kwa vijana si vibaya ikajipongeza kwa kuwapata hao maPM7.
Sasa nimefahamu kwanini muda wote walikuwa wanapiga piga makelele kwamba bado wao ni wanaChadema kumbe ilikuwa mbinu ya kuwafanya ccm iwathaminishe zaidi.
 
Hekaheka zooote zile mwisho wake ulikuwa ni huo.
Sasa amehamia vipi huko wakati yeye ni Makamu Mwenyekiti wa Bavicha na ana mpango wa kugombea uenyekiti wa Bavicha uchaguzi ujao?

huko ndiko kunako mstahili huyo gamba.
 
Kichwa cha habari kisomeke CCM yawapokea wanachama wake walioshindwa kazi MAALUM waliyotumwa CHADEMA.

Hapo namsikitikia sana Mtela Mwampamba kwa kuwa yeye ndio kapoteza, hana fedha za kushinda kura za maoni na kugombea ubunge kupitia CCM. Labda kama watampa kazi nyingine inayolipa, na hakuna kazi kama hizo CCM zaidi ya kuiba kodi zetu. Wenzake waliokimbilia NCCR wameangalia mbali kwa kuwa watapitishwa kirahisi kugombea ubunge 2015 lakini kwa CCM 2010 MTAJI wa kugombea ubunge ilikuwa ni Milioni 60 so 2015 inaweza kuzidi milioni mia. Kwa kijana kama Mtela ambaye hata kazi yenye mshahara hana itakuwa ngumu sana kupambana na watu kama akina Zambi kule mbozi ambao watakuwa na boom la kiinua mgongo cha ubunge.

They are too small fishes in a big and corrupt pond called CCM. Its an end of their political era. Kila la heri katika ajira mtakazopewa na CCM kwa miaka hii miwili iliyobaki, obvious zitakuwa low profile employments kwa kuwa hakuna mkuu wa wilaya atakayekufa hivi karibuni
 
Back
Top Bottom