Taswira
JF-Expert Member
- Sep 23, 2012
- 1,198
- 452
Taarifa zilizopatikana muda huu ni kwamba Juliana Shonza na Aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la mbozi mashariki(Mteka Allam Mwampamba) wamehamia CCM na kupokelewa na Mwenyekiti wa CCM TAIFA Rais Kikwete
Tukio la kuwapokea vijana hao limefanyika Dodoma mbele ya Rais wa nchi (MWENYEKITI WA CCM TAIFA) Mh. Jakaya Mrisho Kikwete.
Vijana hao ambao wameteka mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kwa muda mrefu sasa, Wamepewa nafasi ya kutoa ushuhuda wa kile kinachofanyika ndani ya CHADEMA. Kila mmoja ametoa ushuhuda wake kadri alivyotendewa na yanayotendeka ndani ya CHADEMA.
Mapokezi yao yamekuwa makubwa sana kutokana na kuunganishwa na shughuli zingine za kichama zinazomalizika muda si mrefu.
Taarifa zaidi itakujia nikifanikiwa kupata VIDEO nitaiweka, Dr J.Kikwete awapokea rasmi muda huu,,!!

Juliana Shonza akijitambulisha kwa wana CCM leo tarehe 12/2/2013, katika Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma
Mtela Mwampamba akijitambulisha kwa wana CCM, wakati wa sherehe za utambulisho wa wajumbe wa kamati kuu ya CCM.
Mwenyekiti wa CCM-Taifa, Rais Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na wanachama wapya wa CCM, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba, kushoto kwenye picha ni Makamu Mwenyekiti CCM-Bara ,Ndugu Philip Mangula na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahaman Kinana.

Happiness Mtweve, Dodoma
ALIYEKUWA Makamu Mwenyekiti Baraza la Vijana la CHADEMA Juliana Shonza pamoja na aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Mbozi Mashariki mwaka 2010, Mtera Mwampamba, wamejiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM). Shonsa ambaye hivi karibuni alitimuliwa ndani ya Umoja wa Vijana wa CHADEMA (BAVICHA), alikabidhiwa kadi yake ya CCM na Mwenyekiti wa CCM, taifa, Rais Jakaya Kikwete mjini Dodoma.
Akizungumza mjimi hapa mbele ya Kikwete, Shonza alidai amefanya uamuzi huo kutokana na CHADEMA kukosa demokrasia. Aliilalamikia CHADEMA kuwa imekithiri kwa ufisadi, lakini imekuwa mstari wa mbele kuzungumzia ufisadi wa CCM. Aidha alisema ndani ya CHADEMA kuna mfumo dume na kwamba hakuna mwingine anayetoa kauli zaidi ya viongozi wa juu wa chama hicho.
Shonza alitumia fursa hiyo kumtumia salamu Mbunge wa Ubungo John Mnyika (CHADEMA) na kumtaka ajiandae kwa mapambano katika uchaguzi wa mwaka 2015. Kwa upande wake Mwampamba alisema amejiunga na chama hicho kwa hiari yake mwenyewe bila kushinikizwa na mtu yeyote. Rais Kikwete ambaye ndiye aliyetoa kadi za CCM kwa vijana hao, aliwapongeza kwa kuamua kujiunga na chama hicho tawala.
source: tanzania daima 13/02/2013