Juliana Shonza, Mtela Mwampamba wahamia CCM...

Juliana Shonza, Mtela Mwampamba wahamia CCM...

CDM wamebweteka na kujiona ni miungu wadogo. Tutawafanyia finishing in 2015......
 
Habari ambazo bado sijazipatia evidance ni kwamba Huko mikoani hali si shwari ndani ya ccm hususani katika jumuiya yake ya UVccm kutokana na hatua ya uongozi wa ccm taifa kuwakumbatia wanachama wapya wa kutoka upinzani.Leo nikiwa stand ya Moshi-KCMC nilikuta mazungumzo yakiwa hivi"Hawa wazee wasitufanye mazuzu,sisi tunahainga wao wanatafuta watu wapya na kuwakumbatia,kwanza fikiria wazee wanajuaje kama ndiyo mbinu ya Magwanda kuingiza mamluki ndani ya ccm?kubwa ilikuwa ni hii"kwanza mimi mwenyewe sijawahi hata kukutana m-sure halafu wageni faster tu,halafu huyu Nape huyu ngoja,mwisho wa kunukuu".Mbeya nako hali si shwari,kwa mujibu wa taarifa nilizopewa kutoka Mbozi.KAMA KUNA ALIYE NA TAARIFA ZAIDI JUU BUNDI ANAYEWIKA NDANI YA NYUMBA YA CCM ATUPIE HAPA.ALAMSIKI
 
Happiness Mtweve, Dodoma

ALIYEKUWA Makamu Mwenyekiti Baraza la Vijana la CHADEMA Juliana Shonza pamoja na aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Mbozi Mashariki mwaka 2010, Mtera Mwampamba, wamejiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM). Shonsa ambaye hivi karibuni alitimuliwa ndani ya Umoja wa Vijana wa CHADEMA (BAVICHA), alikabidhiwa kadi yake ya CCM na Mwenyekiti wa CCM, taifa, Rais Jakaya Kikwete mjini Dodoma.

Akizungumza mjimi hapa mbele ya Kikwete, Shonza alidai amefanya uamuzi huo kutokana na CHADEMA kukosa demokrasia. Aliilalamikia CHADEMA kuwa imekithiri kwa ufisadi, lakini imekuwa mstari wa mbele kuzungumzia ufisadi wa CCM. Aidha alisema ndani ya CHADEMA kuna mfumo dume na kwamba hakuna mwingine anayetoa kauli zaidi ya viongozi wa juu wa chama hicho.

Shonza alitumia fursa hiyo kumtumia salamu Mbunge wa Ubungo John Mnyika (CHADEMA) na kumtaka ajiandae kwa mapambano katika uchaguzi wa mwaka 2015. Kwa upande wake Mwampamba alisema amejiunga na chama hicho kwa hiari yake mwenyewe bila kushinikizwa na mtu yeyote. Rais Kikwete ambaye ndiye aliyetoa kadi za CCM kwa vijana hao, aliwapongeza kwa kuamua kujiunga na chama hicho tawala.



source: tanzania daima 13/02/2013
 
Jamani huyu si alikata rufaa kwa katibu mkuu kwamba hakuondolewa kihalali? mbona anaondoka mapema kabla kamati kuu haijakaa.AU alifikiri ataendelea kuwatumikia mabwana wawili mpaka lini.
 
Jamani huyu si alikata rufaa kwa katibu mkuu kwamba hakuondolewa kihalali? mbona anaondoka mapema kabla kamati kuu haijakaa.AU alifikiri ataendelea kuwatumikia mabwana wawili mpaka lini.

chadema walikataa kuisikiliza rufaa yake. Kiujumla ubabe umetumika kuwafukuza bila kufuata katiba...
 
Back
Top Bottom