Juliana Shonza, Mtela Mwampamba wahamia CCM...

Juliana Shonza, Mtela Mwampamba wahamia CCM...

Duh! kweli JK hana kazi. President anao muda hata wa kuwapokea hawa wakinyiha wa Itaka, badala ya kushughulikia mambo nyeti ya chama na nchi kwa ujumla.
 
Hii ni haki yake kikatiba,lakini sasa tunawaelewa waliokuwa wakimtumia kwa kuleta mambo ya UWT ndani ya peoples power,
Huyu ni mwananchi wa kawaida kabisa na aende salama kabisa,huku CDM hatuna mabomu ya kuficha bali huko magamba.
Kansa ikikipata kidole tiba yake huwa ni kukikata.
 
Ni vyema ukatenda haki kwa kufanya nukuu nzuri ya maneno ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere; '... BILA CCM IMARA, NCHI HII ITAYUMBA..' hebu tujiulize kwa sasa CCM ni imara?, na je! nchi yetu iko salama ama imeshaanza kuyumba.
 
ona sura ilivyompalama, kama jiwe la kiama,nliwahi kusema humu ndani huyo mtoto kama ningewahi kukutana nae ningempa hata vibao viwili,maana alipokuwa anaelekea ni kutufanya wana jf ni wajinga kama yeye,bora hata hvyo umejipambanua mwenyewe nadhani sasa wale waliokuwa wanakusapoti watakuwa washajua wewe ulikuwa mtu wa type gani,MSALIMIE SANA MZEE WA TEMBO, MWAMBIE ULIPOTOKA NGOMA NI NGUMU,
 
Hizi siasa za hawa maCCM SIJUI ataziweza kama mwanamke?

Bhanji+1.jpg
 
Mhhhhh!Kwani mtoto kurudi kwa baba au mama yake kuna tatizo?Amerudi kwa wazazi wake,ila asitukane maana kuna methali inasema hivi"Usitukane wakunga na Uzazi.................
 
Apumnzike kwa amani na mwanga wa milele amwangazie
 
Ameamua kuondoka kwa sababu hahusishwi kwenye mgao wa fedha za mabwana wa Ujerumani. Anakula Dr Slaa, Mzee Mbowe, Zitto, Ndesamburo na Mtei. Wengine wanahusishwa kupiga kelele za M4C tu. Watahama wengi we subiri.
Utasubiri saana maana mnajidanganya, watatolewa mmoja mmoja hadi mkubwa wao jibu unalo mwenyewe!!!

 
Mwanaukweli

I am not sure about her political future.

I am afraid that she has been used by CCM, and now she has reached the end of the road.

Anyway, best wishes to you Juliana Shonza
 
Last edited by a moderator:
Haa imekula kwao yani unadhani magamba waliwapenda kivile hao labda wagombee uenyekiti wa mtaa
 
wanachadema msiwe na wasiwasi na huyo binti na huyo jamaa yake,hawana jipya watalosema ambalo hawajasema before...........waende salama ssisi hadi kieleweke
 
I told you alitumwa na CCM watu wakabisha sasa yako wapi amezuga wee lakini wapi ukweli umejulikana kuwa alikuwa anatumwa. Mkumbusheni basi kasahau kuresign cheo chake BAVICHA.
 
Staili aliyohamia huko inataka kufanana kidoogo na ile ya Nakaaya Sumari.
Wanadhani kupokelewa na JK ndo umemaliza kila kitu.
 
Kwa maneno ya ndugu zetu wa upande wa pili wangesema "wamechagua tawi lililo jeme" na kuchagua tawi hilo inamaanisha na kusadifu kuwa ni tawi walililo kuwa wanaliona na sasa wameamua kulishikilia ili wasianguke huku wakiwa hawana pa kushika.

Ki mantiki na kidemokrasia wameshibisha mitima na matumbo yao yaliyo kuwa na njaa ya kisiasa.kinacho nishangaza sio shonza na Mwampamba kuhamia CCM, bali maneno, kauli na matendo yao kabla ya kuhamia.

Lakini kubwa kuliko ni hadhi ya mwenyekiti wa chama chao kipya kuwapokea wanachama hao wapya. nabaki mdomo wa wazi!kwa leo nina kila sababu ya kumheshimu sana Heche kuliko Jk aliyetumia mkutano mkubwa wa chama kuwapokea MASALIA
 
Back
Top Bottom