Ama kweli ujinga ni kwenda........kurudi ndio werevu....huyu si alitamka haya majuma kadhaa tu yaliyopita?
MWISHO:
Ndugu waandishi wa habari,Nipo kwenye mchakato na wanasheria wangu kushughurikia swala la kumpeleka mahakani Bwana John heche na gazeti la Tanzania daima toleo namba 2958 kwa kuniita msaliti wa chadema, natumiwa na CCM na kuwa nina mahusiano (natumiwa)na Wassira tena bila kunihoji mimi Juliana Shonza. Kwa maana hiyo wamenichafua na kunidhalilisha mbele ya umma wa watanzania.
Pili naomba kuweka wazi kwamba natarajia kuomba ufafanuzi wa kikatiba juu ya shutuma zilizotolewa kwenye vyombo vya habari dhidi yangu na bwana Wegesa Suguta (John heche) ili aseme ni aminisho lipi la kuthaminisha na kusakidikisha mtazamo wa maono yake ili bongo za watanzania zijue ukweli.
Mimi Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA natangaza rasmi Mtela Mwampamba na Habib Mchange ni wanachama hai na halali wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Hivyo nawaomba waendelee na kazi zao za ujenzi wa chama kwenye majimbo yao na taifa kwa ujumla. Nawaomba wananchi na wanachama wote wa chadema waendelee kuwa na imani dhidi ya vijana hawa. Kama mlivyomwamini Mwampamba na kumpa kura 32000 na kama mlivyo mwamini Mchange na kumpa kura 10400 kwenye uchaguzi wa Ubunge mwaka 2010. Vivyo hivyo naowaomba muendelee kushirikiana nao kuhakikisha wanatimiza adhima ya ukombozi mwaka 2015.
Wenu katika ujenzi wa demokrasia makini
Juliana Daniel Shonz
Hii ni habari mbaya kwa wanaharakati wa ukweli ndani ya CCM; ni upuuzi mwingine kuwapokea kundini waapuuzi kutoka Chadema; hakika Shonza hutadumu kwenye chama cha wanyonge kwa umalaya wako wa kisiasa; Shonza rudi kwenu Cdm ukaendeleze upuuzi na utoto, Wanaharakati wa ukweli ndani ya CCM hatukutaki hata kama umepokelewa na Mwenyekiti wa Chama
Mimi naona kama amechelewa vile. Kuvuja kwa pakacha nafuu ya mchukuzi.
hayo yote hayaondoi uhalali wake wa kuhamia chama kingine.
Huyu ana hadhi ya kupokelewa na mwenyekiti taifa? Kikwete unaidhalilisha hadhi yako.
Haaaaa Mkuu Chakaza bwana umenifanya nicheke, hizo ndio kazi za Mwigulu msemo wa bi mkubwa shuka kwa shuka!!!!Mwigulu meli hiyooo! Pakua sasa kwa raha zako. Zamani ulikuwa unapakuwa kwa kificho sasa ruksa si kesha kuwa kada! Na nyie kupakuwa kada si ruksa bwana!
Ahasante Mkuu Mwana ukweli M4C Mbele kwa mbele kina Shonza na masalia wengine kazi kwenu kusuka au kunyoa!!!!Watameza nyembe mwaka huu!!!Amejua wametoswa na Masalia imekufa kifo cha mende.