Wanajamvi: Hivi inakuwaje pale Polisi wasipoingilia maandamano/mikutano ya CDM huwa hakuna uvunjifu wa amani na hakuna anayepoteza maisha au kuumia?
Mara mbili hilo limetokea hapo Arusha – kwanza ni mapema mwaka huu siku ile ya kuiaga miili ya marehemu wanaChadema waliokufa kutokana na risasi za polisi. Hafla yote ile kubwa haikuingiliwa na polisi hata mmoja na hakuna hata mtu aliyechubuka.
Pili ni tukio la leo pale Mh Lema aliposhindikizwa kwa maandamano makubwa kutoka mahakamani baada ya kupewa dhamana. Polisi hawakuingilia na hakuna aliyechubuka. Halafu hapa hapa kuna swali, je maandamano yale ya kumshindikiza Mh Lema leo yalikuwa na ‘kibali' cha polisi? Nauliza tu.
Kwa hivyo conclusion ni kwamba polisi ndiyo huanzisha vurugu – kuzuia mikutano/maandamano bila ya sababu ya msingi, kwani sababu hiyo wanayoiimba kila siku ya eti kuzuia uvunjifu wa amani huwa ni uwongo mtupu. Wakubali kwamba wanatumika tu kisiasa – kuwapaka matope wapinzani kuwa daima ni watu wa vurugu, kitu ambacho siyo kweli kabisa.
Kitu kingine: Leo hii IGP Mwema kazungumza lakini alionekana kubadilisha hoja ya kwa nini hasa polisi huzuia maandamano/mikutano kwa sababu eti hii huwanyima watu kufanya kazi zao za kila siku za kujitafutia riziki.
Hii inawezekana ni kweli kwa asilimia flani, lakini siyo suala la polisi kamwe. Mimi nikiamua kwenda kwenye maandamano haiwi shauri la polisi kutaka kujua kwa nini nilitelekeza kazi yangu inayonipatia riziki. Mie najua mwenyewe ninachokifanya.
Inawezekana kuna wengine ambao hawataki maandamano lakini yakitokea inabidi wasimamishe biashara zao kwanza. Hii sababu pia haina mashiko sana kwa sababu kama ni hivyo, basi maandamano yote yapigwe marufuku kwa sababu inawanyima haki wengine kufanya kazi zao.
Ningependa kujadili suala hili.