J'tatu hiyooo, Lema njeeee....

J'tatu hiyooo, Lema njeeee....

Well said. If everyone of us are exposed JF will cease to exist , if others think a publicity of who are they or where are they working from can scare some members to dare speaking openly!, I have some news for tell them, some of us are working from hell!.

Yeah mkuu ndio hivyo,maana humu tunajuana kwa keyboard so tukitaka kusema kila kitu hapa hapatatosha na ni uswahili vile vile, ila watu kama hao ukija kuangalia hamna mpya
 
Wanajamvi: Hivi inakuwaje pale Polisi wasipoingilia maandamano/mikutano ya CDM huwa hakuna uvunjifu wa amani na hakuna anayepoteza maisha au kuumia?

Mara mbili hilo limetokea hapo Arusha – kwanza ni mapema mwaka huu siku ile ya kuiaga miili ya marehemu wanaChadema waliokufa kutokana na risasi za polisi. Hafla yote ile kubwa haikuingiliwa na polisi hata mmoja na hakuna hata mtu aliyechubuka.

Pili ni tukio la leo pale Mh Lema aliposhindikizwa kwa maandamano makubwa kutoka mahakamani baada ya kupewa dhamana. Polisi hawakuingilia na hakuna aliyechubuka. Halafu hapa hapa kuna swali, je maandamano yale ya kumshindikiza Mh Lema leo yalikuwa na ‘kibali' cha polisi? Nauliza tu.

Kwa hivyo conclusion ni kwamba polisi ndiyo huanzisha vurugu – kuzuia mikutano/maandamano bila ya sababu ya msingi, kwani sababu hiyo wanayoiimba kila siku ya eti kuzuia uvunjifu wa amani huwa ni uwongo mtupu. Wakubali kwamba wanatumika tu kisiasa – kuwapaka matope wapinzani kuwa daima ni watu wa vurugu, kitu ambacho siyo kweli kabisa.


Kitu kingine: Leo hii IGP Mwema kazungumza lakini alionekana kubadilisha hoja ya kwa nini hasa polisi huzuia maandamano/mikutano kwa sababu eti hii huwanyima watu wengine kufanya kazi zao za kila siku za kujitafutia riziki.

Hii inawezekana ni kweli kwa asilimia flani, lakini siyo suala la polisi kamwe. Mimi nikiamua kwenda kwenye maandamano haiwi shauri la polisi kutaka kujua kwa nini nilitelekeza kazi yangu inayonipatia riziki. Mie najua mwenyewe ninachokifanya.

Inawezekana kuna wengine ambao hawataki maandamano lakini yakitokea inabidi wasimamishe biashara zao kwanza. Hii sababu pia haina mashiko sana kwa sababu kama ni hivyo, basi maandamano yote yapigwe marufuku kwa sababu inawanyima haki wengine kufanya kazi zao.

Ningependa kujadili suala hili.

Nimeyaona hayo maandamano ya Lema leo na pia nimemskia IGP Mwema. Mie nadhani sababu kubwa ya polisi kuzuia maandamano ya CDM ni kuwaokoa CCM ambao hawawezi tena kupata halaiki kubwa katika maandamano yao hata wafanyeje.

Na kuhusu Mwema nimeshangaa kumsikia leo akitoa hiyo hoja ya eti maandamano yanawafanya wasishughulikie kazi zao za kujipatia riziki.

Kha! Imekuwa hivyo tena? Maelfu ya vijana hawana kazi, kwa hiyo wakao tu vijiweni kupanga uhalifu? Si bora waandamane kudai haki kwa niaba ya wengine woty\e?
 
Jamani hivi hawa polisi -- yaani baadhi yao ambao wanasapoti harakati za ukombozi, si bora wakatuambia hao wakubwa wao huwa wanapata wapi amri/maelekezo ya kuyazuia maandamano ya upinzani?

Hebu tuvujieni siri hiyo kama mnayo.
 
Polisi ni wahalifu wenye sare. Si mnajua waliiba hata stika za nenda kwa usalama Traffic HQ? Hawana maana wala amana.
 
Yani nawaambia ya kwmb hawa polisisisiem wasingeingilia maandamano ya hapa A town yani hata inzi hafi.
 
Nauliza wana jukwaa, leo ndo jumatatu mpaka saa hizi sijasikia chochote kuhusu dhamana ya mh, goddy lema. Mwenye neno atujuze!
 
Nauliza wana jukwaa, leo ndo jumatatu mpaka saa hizi sijasikia chochote kuhusu dhamana ya mh, goddy lema. Mwenye neno atujuze!
Uko Tanzania ya wapi hata runinga huangilii hata humu leo watu wamejadiliana au uko Kenya?
 
Mkuu kabla ujaandika thread jenga kautamaduni kakupitia kwanza thread humu jukwaa la siasa..
 
Wanajamvi:.

Kitu kingine: Leo hii IGP Mwema kazungumza lakini alionekana kubadilisha hoja ya kwa nini hasa polisi huzuia maandamano/mikutano kwa sababu eti hii huwanyima watu kufanya kazi zao za kila siku za kujitafutia riziki.

Hii inawezekana ni kweli kwa asilimia flani, lakini siyo suala la polisi kamwe. Mimi nikiamua kwenda kwenye maandamano haiwi shauri la polisi kutaka kujua kwa nini nilitelekeza kazi yangu inayonipatia riziki. Mie najua mwenyewe ninachokifanya.

Unafiki ni zaidi ya wazimu!
 
Mkuu kabla ujaandika thread jenga kautamaduni kakupitia kwanza thread humu jukwaa la siasa..

Kwa Mara ya kwanza nimeona umeongea pwenti! Yaani umemwelekeza mtu na kumfundisha
 
Wewe ni mwisilamu halafu unakwenda kinyume na BAKWATA?

who told you?, do you know who am I?, dini yangu mimi haikuhusu, BAKWATA is a religious wing of CCM, I am not one of them. I am a free person.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom