Joseph Mbilinyi 'Sugu' amlipua Zitto Kabwe

Joseph Mbilinyi 'Sugu' amlipua Zitto Kabwe

Acha ubabaishaji; hoja ni jinsi huyo Zitto alivyoihujumu nchi kwa kujihusisha katika kashfa hiyo. Suala hapa si uchadema au u-CCM bali ni uchungu kwa taifa na dhulma ya fedha za walalahoi.

Maelezo ya zitto yako very clear...fungua macho achana na siasa taka na uuone ukweli. Pesa zimelipwa kihalali na zimefanya kazi halali!! Sugu kakurupuka na wivu tuu wala si kitu kingine!!
 
Duh yaani siamnini kabisa ZITTO amekuwa jambazi la kutupwa kiasi hiki! kweli lisemwalo lipo kama halipo lajongea.
 
Kwa bahati mbaya hili suala la zitto litawaumbua watu wengi sana ndani siasa hasa chadma zitto hajawahi kushindwa kwenye harakati zake,
Kama watakuwa wamempakazia walahi nawaambia sugu na chama chake atafute pakujificha moto atakaowasha zitto utakuwa mkubwa sana.

ndivyo anavyowadangganya lumumba?
 
Nimesoma baadhi ya maelezo na michango ya wachangiaji wa hii mada ya zzk ila nimesikitika sana. Kilicho nisikitisha ni jamii forum kubadilika kutoka kuwa kisima cha great thinkers na kuwa jalala la waropokaji watoa matusi nk. Nilitarajia wanasheria waliomo humu kutueleze kama maelezo ya sugu kuhusu zzk kama ni ya kweli basi kuna sheria na taratibu fulani zimekiukwa. Au sheria zilizoelezwa na "sugu" ni kweli zimevunjwa .

Tusisahau kuwa wanasiasa nao ni binadamu kama sisi na wanaweza ingiwa tamaa na kufanya ndivyo sivyo. Sakata la kupeleka risiti fake za malipo kwenye bunge la uingereza liliwagusa wabunge wote wa labour, conservatives na liberal party. Hivyo linapokuja suala la maslahi kwa umma halina chama wandugu.

Naomba kujulishwa kama sheria zetu zina ruhusu mbunge a, ana miliki kampuni yake ambayo inapata tenda kwenye makampuni ambayo mbunge huyo huyo anazisimamia. Wachangiaji wengi wanamtetea zzk na wanaweza kuwa sawa. Je aliye kuwa mkurugenzi wa tanesco bwana mhando kashitakiwa kwa makosa yapi?
 
Hivi kodi ya mapato ililipwa kutokana na hayo mapato?
Hivi tenda ilitangazwa ?
Mbona pesa ilikuwa in atolewe fasta na cash kama ilivyokuwa kwa Deep green na EPA ?
Hivi alitangazaa umilikaji wa kampuni hizi wakati anatangaza mali zake kama kiongozi wa umma ?
 
Wewe Bibie toka mgombani Mamndenyi siku hizi TANAPA imeacha jukumu lake la uhifadhi wa mbuga za wanyama na kujipachika jukumu lingine la kukopesha fedha kama CRDB na NMB ha ha ha ha ha ha unamahaba na wanasiasa uchwara.
Sugu ameona hilo tu?Bunge limekuwa kijiwe cha majungu;Na atakapojua kuwa ulikuwa mkopo halalihuyo sugu atajibu nini?
 
Last edited by a moderator:
Nimeushughulisha ndiyo maana nimesema kama kuna ukweli,kwa maana kwamba sina uhakika aliyoyasema sugu.Na pili kwa Mhasinu hata Tzs.20,000 isipoonekana lazima ujue imekwenda wapi.Kwa taaluma yangu hizo milioni ulizazitaja zikikosekana au zisipokuwa na maelezo ya kutosha lazima nita-qualify report.

Angalizo,kila mtu namna anavyoiona hiyo milioni unayoiona siyo kitu.Na ndiyo maana kwa kudharau vitu vidogo uchumi wetu upo hapa ulipo.Pole kama nimekukwaza.


Taaluma yako huitumii vizuri, huwezi kusikia tu jambo akatoa hukumu, km msomi ungefanya utafiti japo kidogo. Kundi hilo la wasanii wako zaidi ya 10, na wamesajiri kampuni yao ili kutafuta mkate, ukichukua gharama za kurekodi mziki na faida wanayopata wasanii ni kidogo sana, kwa taarifa yako Zito ndiye aliwakutanisha hao wasanii na kuwashauri kutunga wimbo leka tutigite, hata editing ya wimba zito alikuwa mshauri wao, kwa kuwa ni kundi ni vigumu kugawana mapato wanayoayata bila kuwa na kampuni, wimbo wa leka tutigite uliredodiwa katika hifadhi ya wanyama maarufu kwa sokwe mtu iliyoko Kigoma (GOMBE) kupitia wimbo ule walitangaza utalii wa nchi yetu, sasa kuna ubaya gani wakipewa mkataba kutangaza zaidi utalii wetu? wewe km mhasibu km ulivyotaja, huwezi ku-qualify Audit bila kufanya Audit program lazima report yako itakuwa na makosa, kwa kifupi labda utafanya investigation na siyo Audit.
 
zitto ameshatoa taarifa kuwa kampuni ile imesajiliwa kama kampuni isiyo ya kibiashara. Hilo linatosha kumaliza mjadala wa mgongano wa maslahi. Maswali mengine aliyoibua sugu yanapaswa kujibiwa na NSSF na TANAPA sio zitto wala kampuni zake.

Watu wengine hizi ID zenu mlishazijengea heshima kwenye hoja zingine nyingi tu..........usijiingize kwenye hizi siasa kichwakichwa ukaishia kuvua thamani yako..........Kampuni imesajiliwa kuwa si ya kibiashara sasa ilichofanya na NSSF na TANAPA ni nini kombolela?

Walilipa kodi? unadhani kampuni isiyo ya kibiashara ni tiketi ya kutolipa kodi? Zitto ni mwenyekiti wa PAC unafikiri hao wasanii ndio walienda kuomba hiyo kazi huko NSSF na TANAPA bila influence ya Zitto ? wewe binafsi umewahi kusikia hayo matangazo ya NSSF na TANAPA? kama hujawahi kuyasikia kuna Value for money hapo? Unajua hao wasanii wanasema nini baada ya haya yote?

Ukiamua kuwa mkweli simamia ukweli maana Uongo unatabia ya kujikataa wenyewe hata ukilazimisha vipi..........kuna wakongwe humu wameshaamua kupotezea hizi issue maana zinakatisha tamaa...........
 
Hivi kwa michango hii ya vivuli kweli kuna haja ya kuendelea kuwa na hotuba za vivuli, manake kila kivuli kikipanda hakina jipya ngonjera zilezile. Nani anayewaandikia hawa vivuli vitu vya kusema, mbona hakuna kivuli afadhali ya kingine mtindo wao ni huo huo tu.

Ni Bunge la bajeti, yaani mapato na matumizi sasa badala ya kujadili mapato na matumizi wao wanaajenda zao za siasa ukiwazuia hapo watasusa na kutoka nje.
 
Ni katika Hotuba yake ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ya Wizara ya Habari,Utamaduni na Michezo aliyoiwasilisha Bungeni leo hii muda mfupi uliopita. Waziri Kivuli Joseph Osmundi Mbilinyi aka Sugu amemtaja Zitto Z. Kabwe kama Mmiliki wa Kampuni ya Leka Dutigite aliyofanya biashara isivyo halali na Mashirika ya Umma ya NSSF na TANAPA.

Sehemu husika ya Hotuba hiyo ni hii:

Mheshimiwa Spika, Tarehe 13 Agosti, 2012, Msajili Msaidizi wa Makampuni katika Wakala wa Usajili wa Makampuni na Leseni (BRELA) alitoa Hati ya Usajili (Certificate iof Incorporation) kwa kampuni inayoitwa Leka Dutigite Limited. Kwa mujibu wa nyaraka za BRELA, Leka Dutigite Ltd. ina ofisi zake katika ghorofa ya kwanza ya jengo la City House lililoko katika Mtaa wa Mkwepu, Dar es SalaaM. Mheshimiwa Spika,

Katiba, yaani Memorandum and Articles of Association, ya kampuni ya Leka Dutigite Ltd. iliyosajiliwa BRELA tarehe 13 Agosti, 2012 inaonyesha kwamba mwenye hisa nyingi katika kampuni hiyo ni kampuni nyingine inayoitwa Gombe Advisors Ltd. ya Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa za kibenki ambazo Kambi Rasmi ya Upinzani ya Bunge lako tukufu imezipata, mnamo tarehe 10 Desemba, 2012, Hifadhi ya Taifa ya Saadani ilihamisha jumla ya shilingi 12,200,000 kwenda kwenye akaunti na. 0150357447800 iliyoko CRDB Bank tawi la Pugu Road, Dar es Salaam, inayomilikiwa na Leka Dutigite Ltd. Hifadhi ya Taifa ya Saadani inamilikiwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), ambayo ni shirika la umma. Siku moja baadae, fedha hizo zilitolewa kwa pesa taslimu kutoka kwenye akaunti hiyo.

Baada ya hapo, kati ya tarehe 14 Januari na 7 Februari, 2013, akaunti ya Leka Dutigite Ltd. iliingiziwa jumla ya shilingi 28,600,000. Fedha hizi zote ziliingizwa kama fedha taslimu na mtu aitwaye Mchange (shilingi 3,600,000 tarehe 14 Januari, 2013) na Leka Dutigite (shilingi 25,000,000 tarehe 23 Januari na 7 Februari, 2013). Kufikia tarehe 7 Februari, 2013, fedha hizo zote zilikwishatolewa benki.

Mheshimiwa Spika,
Tarehe 28 Februari, 2013, akaunti ya Leka Dutigite Ltd. iliingiziwa shilingi 32,367,000 na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Kwa mujibu wa taarifa za kibenki, siku hiyo hiyo, fedha hizo zilitolewa kwenye akaunti hiyo. Siku nne baadae, yaani tarehe 4 Machi, 2013, NSSF ilifanya malipo mengine kwenye akaunti ya Leka Dutigite Ltd., kwa mikupuo miwili, ya jumla ya shilingi 46,663,000. Siku hiyo hiyo, fedha hizo nazo zilitolewa kutoka kwenye akaunti hiyo kwa mikupuo miwili. Kwa hiyo, katika kipindi cha miezi mitatu katika ya tarehe 10 Desemba, 2012 na 4 Machi, 2013, Leka Dutigite Ltd. ililipwa shilingi 119,930,000 kwa utaratibu huo huo wa ingiza na toa fasta. Kati ya fedha hizo, shilingi 12,200,000 zililipwa na TANAPA na shilingi 79,027,000 zililipwa na NSSF.

Mheshimiwa Spika,
Katika mazingira ya kawaida, sio kitu cha ajabu kwa mashirika ya umma kama NSSF na TANAPA kufanya biashara na watu au taasisi mbali mbali kama makampuni binafsi. Ukweli ni kwamba, kwa upande wa malipo yaliyofanywa na TANAPA, Kambi Rasmi ya Upinzani ya Bunge lako tukufu imeweza kupata nakala ya mkataba unaohusu Maandalizi ya Filamu (Documentary) kwa Ajili ya Kuhamasisha Shughuli za Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Saadani kwa Kutumia Wasanii Kutoka Kigoma. Mkataba huo umesainiwa tarehe 5 Desemba, 2012, kati ya Hifadhi ya Taifa ya Saadani na Leka Dutigite Ltd. na una thamani ya shilingi 12,200,000, kiasi kile kile kilicholipwa na Hifadhi hiyo.

Hata hivyo, Mheshimiwa Spika, mazingira ya malipo haya sio ya kawaida. Hii ni kwa sababu ya uwepo wa kampuni ya Gombe Advisors Ltd. Kwa mujibu wa nyaraka za BRELA, kampuni hii ilisajiliwa tarehe 24 Novemba, 2011. Kwa mujibu wa nyaraka hizo, ofisi za Gombe Advisors Ltd. ziko kwenye jengo la City House, Mtaa wa Mkwepu, Dar es Salaam, ziliko ofisi za Leka Dutigite Ltd. Kwa mujibu wa nyaraka hizo, wakurugenzi wa Gombe Advisors Ltd. ni Zitto Zuberi Kabwe ambaye kazi yake inatajwa kuwa ‘mchumi’, na Raphael Ongangi ambaye anatajwa kuwa ‘mchambuzi wa fedha na vitega uchumi’ (Financial and Investment Analyst). Bwana Ongangi aliwahi kutajwa na gazeti la kila wiki la ----- la tarehe 26 Desemba 2013 kuwa ni mmoja wa washauri wa Zitto Zuberi Kabwe na anasemekana kuwa msaidizi wake.

Mheshimiwa Spika,
Zitto Zuberi Kabwe sio ‘mchumi’ anayetajwa katika nyaraka za BRELA zinazoihusu kampuni ya Gombe Advisors Ltd. pekee, bali pia ni Mbunge, tangu mwaka 2005, wa Bunge lako tukufu. Kama Mbunge, Mheshimiwa Zitto Kabwe ni ‘kiongozi wa umma’ kwa mujibu Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, 1995. Sheria hii inawalazimu viongozi wa umma, wanapokuwa madarakani, kuwa “waadilifu, wenye huruma, utulivu, umakini na watakaoendeleza viwango vya juu vya maadili ili kujenga na kuendeleza imani ya umma kwa uadilifu wa Serikali.”

Aidha, viongozi wa umma “... watawajibika kutekeleza wajibu wao kwa umma na kuendesha shughuli zao binafsi kwa namna ambayo itaonekana na kuthibitika kuwa ni wazi kwa umma na haitatosheleza kwao kutekeleza wajibu wao kwa kufuata sheria tu.” Vile vile, kuhusiana na maslahi binafsi, Sheria hii inaelekeza kwamba “... viongozi wa umma hawatakuwa na maslahi binafsi ambayo yanaweza kuathiriwa na maamuzi ya serikali wanayoshiriki katika kuyafanya.”

Mwisho, kuhusiana na maslahi ya umma, viongozi wa umma wanatakiwa, pale wanapochaguliwa au kuteuliwa, kupanga masuala yao “kwa namna itakayozuia migongano ya maslahi ya wazi, iliyojificha au inayoonekana kuwepo na pale ambapo migongano hiyo inatokea kati ya maslahi binafsi na maslahi ya umma basi itatatuliwa kwa kuangalia zaidi maslahi ya umma.” Kwa kadri ya ufahamu wa Kambi Rasmi ya Upinzani ya Bunge lako tukufu, Mheshimiwa Zitto Kabwe hajawahi kutangaza maslahi aliyonayo kwenye mikataba ya Gombe Advisors Ltd. na Leka Dutigite Ltd. na NSSF na TANAPA.

Mheshimiwa Spika,
Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe sio tu ni Mbunge anayebanwa na masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, bali pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Fedha za Serikali (PAC). Kwa mujibu wa kipengele cha 12 cha Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge lako tukufu, mojawapo ya majukumu ya PAC ni kushughulikia maeneo yenye matatizo sugu ya matumizi mabaya ya fedha za umma katika Wizara na Mashirika ya Umma yaliyoainishwa katika taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. NSSF na TANAPA ni baadhi tu ya Mashirika ya Umma yaliyo chini ya usimamizi wa kibunge wa PAC.

Kwa maana hiyo, Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Zitto Kabwe, kwa kutumia makampuni yake ya Leka Dutigite Ltd. na Gombe Advisors Ltd., amefanya biashara na TANAPA, shirika la umma analolisimamia kama Mbunge na Mwenyekiti wa PAC. Mheshimiwa Zitto Kabwe na wanamuziki washirika wake, kwa kutumia makampuni ya Gombe Advisors Ltd. na Leka Dutigite Ltd., wamelipwa fedha za umma za TANAPA na NSSF.

Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kutoa maelezo juu ya madai ya ukiukwaji wa Sheria uliofanywa na viongozi wa umma na mashirika ya umma katika kashfa hii. Pamoja na maelezo yatayotolewa , Kambi Rasmi ya Upinzani inataka Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi maalum juu ya matumizi ya fedha zilizotolewa na TANAPA na NSSF; msukumo uliofanya fedha hizo zitolewe na matumizi ya fedha hizo kwa kuzingatia masharti yanayosimamia fedha za umma na utawala bora katika usimamizi wa fedha za umma. Aidha, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ifanye uchunguzi juu ya malipo na matumizi husika kwa kurejea masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Sheria nyingine zinazohusika. Kwa upande mwingine, kwa kuwa suala hili linahusu mbunge na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge inayohusika na usimamizi wa fedha za umma, Kamati ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge nayo ifanye uchunguzi wake juu ya madai ya masharti ya Katiba ya Nchi, Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge na Kanuni za Bunge juu ya maadili ya kiongozi wa umma ikiwemo yahusuyo utangazaji wa maslahi.

Mheshimiwa Spika;
Mwisho, Kambi Rasmi ya Upinzani ya Bunge lako tukufu inatoa rai kwa wanamuziki na wasanii wengine wote nchini kuwa waangalifu na watu wanaotaka kutumia umaarufu wao kama wanamuziki na wasanii kwa lengo la kufanikisha dili za kifisadi. Bila kuchukua tahadhari ya kutosha, wasanii hao wanaweza kujikuta wakipoteza sifa na umaarufu wao ambao wameujenga kwa jitihada zao wenyewe.

************************************************************************************************

Mapambano ya Kambi Rasmi ya Upinzani yanaendelea.Hayachagua mtu,taasisi au kundi la watu au taasisi

Duuu, mi naswali dogo tu..
Kwa nn sehemu ya hutuba hii umekua rahisi sana kupatikana kuliko hutuba nyingine kutoka kambi ya upinzani?!!
Au ndo uongo hupaa kwa ndege au mmlizamiria kwa nia zenu zote kusambaza illiiiiii
 
Taaluma yako huitumii vizuri, huwezi kusikia tu jambo akatoa hukumu, km msomi ungefanya utafiti japo kidogo. Kundi hilo la wasanii wako zaidi ya 10, na wamesajiri kampuni yao ili kutafuta mkate, ukichukua gharama za kurekodi mziki na faida wanayopata wasanii ni kidogo sana, kwa taarifa yako Zito ndiye aliwakutanisha hao wasanii na kuwashauri kutunga wimbo leka tutigite, hata editing ya wimba zito alikuwa mshauri wao, kwa kuwa ni kundi ni vigumu kugawana mapato wanayoayata bila kuwa na kampuni, wimbo wa leka tutigite uliredodiwa katika hifadhi ya wanyama maarufu kwa sokwe mtu iliyoko Kigoma (GOMBE) kupitia wimbo ule walitangaza utalii wa nchi yetu, sasa kuna ubaya gani wakipewa mkataba kutangaza zaidi utalii wetu? wewe km mhasibu km ulivyotaja, huwezi ku-qualify Audit bila kufanya Audit program lazima report yako itakuwa na makosa, kwa kifupi labda utafanya investigation na siyo Audit.

Nimejibu hoja ya wamba pesa zilizotumika ni ndogo na hazihitaji kuhojiwa,kwa mantiki hiyo ndilo nililojibu.Sijahoji kuhusu wasanii,nimehoji kuhusu Mwenyekiti wa Kamati ya PAC,kwanini alikubali kupokea jukumu hilo wakati yeye ni mhusika mkuu na mtu anayetakiwa kufuatilia matumizi ya sekta hiyo (Mashirika ya Umma).

Kwa hiyo majibu yangu yanaendana na aliyeleta hoja kuwa pesa hizo Mil.119,ni ndogo na hazihitaji kuhojiwa,ndiyo maana nikajibu kama auditor nikikuta upotevu wa pesa hizo na hazina maelezo,lazima nitaqualify report,sina ulazima wa kufanya investigation,pesa hazijulikani matumizi yake leo unaniambiaje?Muulize auditor yoyote atakacho fanya kama kuna matumizi ya pesa yasiyonamaelezo ya kutosha huwa wanafanyaje kabla ya kufanya investigation?

Na kwa sababu kuu moja kuwa mwanahisa kunamfanya asiwe na moral authority ya kuhoji matumizi ya pesa ya taasisi hizo.Ndiyo maana nikasema
 
Wewe Bibie toka mgombani Mamndenyi siku hizi TANAPA imeacha jukumu lake la uhifadhi wa mbuga za wanyama na kujipachika jukumu lingine la kukopesha fedha kama CRDB na NMB ha ha ha ha ha ha unamahaba na wanasiasa uchwara.

Mkuu kwani kuna sehemu Imeandikwa hizo fedha zimekopeshwa?
 
Last edited by a moderator:
Mamndenyi jitafakari....hizo ni pesa za kisanii,uliwahi ona wapi TANAPA kuwa shirika la ukopeshaji?
 
Sugu toka amekuwa mbunge hakuna alichowasaidia wasanii Wa Tanzania...Zaidi ya kuwatumia vijana Wa watu Na kuwaacha kwenye mataa. Kawapiganisha wenzake alipopewa hela nyuma ya pazia kawaaacha wenzake wote wanagongea chipsi mayai.
 
Maneno ya Linex hayo hayo chini.... Sugu akawaombe Radhi Antivirus kawagombanisha Na watu.. Yeye kapewa hela akaamua kunyamaza kawaacha wenzake kwenye mataa.
 
Back
Top Bottom