MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ney wa Mitego amezidi kujipatia umaarufu huku akiendelea kushika chati miongoni mwa wasanii wanaongoza kuimba nyimbo zinazoibua ukweli kwa baadhi ya mambo yanayotendeka kwa jamii. Katika mashahiri yake, rapa huyo anahoji uhalali wa kazi zinazofanywa na mawaziri vizuri, pamoja na uhalali wa kuwepo wabunge wa viti maalumu bungeni. Msanii huyo ambaye leo anaachia ngoma mpya inayojulikana kwa jina la 'Salaam zao', ameandika mashahiri ya kumpa salaam Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kuachana na masuala ya muziki wa bongo fleva na ajikite zaidi kwenye siasa. Mashahiri hayo yametokana na kile kinachodaiwa kuwa mbunge huyo kuanzisha kundi la Kigoma All Stars na kulitelekeza. Rapa huyo amemtumia salamu, mbunge huyo kuwa ni vyema aachane na bongo fleva na kujikita zaidi kwenye siasa, kwani huko ndiko kunakomfaa zaidi.