Joseph Mbilinyi 'Sugu' amlipua Zitto Kabwe

Joseph Mbilinyi 'Sugu' amlipua Zitto Kabwe

Katika wanasiasa niliokuwa nawakubali basi ni Zitto...Ata wakati wanaanza kumuanika nikajua ni siasa chafu wanamuonea......Nilikuja kuchoka nilipokaa na kina Linex wanamuziki members wa Leka Tugite waliponiambia namna alivyokuwa anawatumia wasanii kupiga pesa.....Yani jamaa walikuwa wanaongea kwa uchungu uwezi kuamini ni Zitto uyu uyu ... rip leka tugigite

acha uongo kabsa,tena hujui chochote,na huyo linex ulikua umelala naye.
 
Last edited by a moderator:
Mi nina mashaka nahisi ni mambo binafsi, na sisi wengi wetu tunapenda kushabikia mambo ya watu tusiowakubali hata km ni ya uzushi but wakifanya tunaowakubali tutapinga na kudai uzushi hata kama ni kweli...Tusiongozwe kwa ushabiki tutaendelea kuwa nyuma mpk lini mwisho tutapigana wenyewe wao wataenda uhamishoni
 
Ni katika Hotuba yake ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ya Wizara ya Habari,Utamaduni na Michezo aliyoiwasilisha Bungeni leo hii muda mfupi uliopita. Waziri Kivuli Joseph Osmundi Mbilinyi aka Sugu amemtaja Zitto Z. Kabwe kama Mmiliki wa Kampuni ya Leka Dutigite aliyofanya biashara isivyo halali na Mashirika ya Umma ya NSSF na TANAPA.

Mapambano ya Kambi Rasmi ya Upinzani yanaendelea.Hayachagua mtu,taasisi au kundi la watu au taasisi
Mkuu Petro, asante kwa uzi huu, nimeutumia kwenye thread yangu fulani.
Thanks.

Pasco
 
yaani mhangaika na m 12 kupoteza muda wooote huo kusoma hotuba?
 
hapo ndio utashangaa

Jamani tuwe tunakaa chini na kufikiri kabla ya kuandika. Mbunge Sugu yuko bungeni anazungumzia mambo ya serikali na maslahi ya umma/taifa. Mambo ya chama yana mahala pake. Vile vile anaetajwa ni mbunge. Sasa suala la vyama linaingiaje? Tujifunze kutofautisha mambo. Tunawesema wabunge wetu vilaza kumbe sisi ndio vilaza na washabiki tu tusiojua kuchanganua hoja mbalimbali.
 
Sifa za kijinga.....heri kuwa mtumwa wa Calpeters kuliko kuwa mtumwa wa Tumbo (C.H.A.D.E.M.A)....sugu jitathmini sana uwezo wako wa kufikili kwani 2015 sio mbali sana.
Na ndo maana mimi siku zote huwa nina wasiwasi na uwezo wa kufikili wa huyu mwana Ubongo wa Fleva
Wanasema 'akili za kuambiwa changanya na za kwako.' Yupi wa kuonewa huruma kati ya anayependa sifa za kijinga na mtu anayefahamishwa kuwa fedha zake (huko NSSF, TANAPA,nk ) zinafisadiwa lakini yeye anatetea? Hapa nakuongelea wewe unayekilimbilia kumlaumu Sugu kwa kufichua ufisadi eti ni 'mtumwa wa tumbo- CHADEMA.'

Mara nyingi tunawalaumu watawala wetu mafisadi lakini tatizo kubwa na la msingi ni baadhi ya wenzetu ambao wameupa likizo ubongo wao, na kamwe hawasikii maumivu wanapofisadiwa. Ifike mahala tuweka masuala ya itikadi pembeni-kama alivyofanya Sugu- na kutambua kuwa wrong is wrong hata ikifanywa na swahiba wako.
 
Kweli aise,maana kina Ali kiba walikuwa wanalazimishwa tu kujiunga na leka dugitike ila jamaa aliwang'ang'ania hasa
zzk hana tofaut na ridhiwan
 
mnaanza kuhangaika na tumbili manyani yamewashinda
 
uwe na akili kidogo unapotetea wezi analakujibu hata Kikwete atamsemea tumezoea CAG afanye kazi yake
Una uhakika gani kama aliiba?
Magazeti ya leo Zitto amesema kuwa CAG akague na kama ni kweli atawajibika.
NSSF wamesema kuwa walitumia hizo hela kuwalipa kurecord wimbo wa NSSF na pia kuwadhamini na walipowadhamini NSSF waliweza kupata wanachama wapya 30000 kutoka katika sekta isiyo Rasmi.
TANAPA wao waliwalipa LEKADUTIGITE ili wawatangazie mbuga yao.
 
CHADEMA wanatapatapa! Kumuengua Zitto Kabwe ni kosa kubwa sana lililowahi kutokea katika historia ya Chadema! Ni ukweli usiopingika, ZITTO KABWE ndiye alikuwa anaibeba Chadema...na ndio usemi wa Zitto ni Chadema na Chadema ni Zitto!

Hizi siasa za majitaka, u------- unaofanywa na freeman Mbowe na kundi lake ni vichekesho na ni dalili la kufilisika kisiasa! Lengo la upinzani ni kuchukua madaraka ya nchi, na siyo kudhoofisha upinzani!! Kwa mtaji huu wa kibwege Chadema wanafikiria nini?

SHAME ON YOU SUGU, umesahau ulishalialia kwenye lile sakata lako la dili za pesa za Malaria...wewe vs Clouds FM?? Sugu ni mufilisi wa siasa, huna jipya, badala ya kuwatetea wasanii na kazi zao, badala ya kuwasaidia kupata dili unaendelkeza siasa uchwara....siasa Mufilisi!!

AIBU KWENU CHADEMA

Ndio maana hata ile

Ni katika Hotuba yake ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ya Wizara ya Habari,Utamaduni na Michezo aliyoiwasilisha Bungeni leo hii muda mfupi uliopita. Waziri Kivuli Joseph Osmundi Mbilinyi aka Sugu amemtaja Zitto Z. Kabwe kama Mmiliki wa Kampuni ya Leka Dutigite aliyofanya biashara isivyo halali na Mashirika ya Umma ya NSSF na TANAPA.

Sehemu husika ya Hotuba hiyo ni hii:

Mheshimiwa Spika, Tarehe 13 Agosti, 2012, Msajili Msaidizi wa Makampuni katika Wakala wa Usajili wa Makampuni na Leseni (BRELA) alitoa Hati ya Usajili (Certificate iof Incorporation) kwa kampuni inayoitwa Leka Dutigite Limited. Kwa mujibu wa nyaraka za BRELA, Leka Dutigite Ltd. ina ofisi zake katika ghorofa ya kwanza ya jengo la City House lililoko katika Mtaa wa Mkwepu, Dar es SalaaM. Mheshimiwa Spika,

Katiba, yaani Memorandum and Articles of Association, ya kampuni ya Leka Dutigite Ltd. iliyosajiliwa BRELA tarehe 13 Agosti, 2012 inaonyesha kwamba mwenye hisa nyingi katika kampuni hiyo ni kampuni nyingine inayoitwa Gombe Advisors Ltd. ya Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa za kibenki ambazo Kambi Rasmi ya Upinzani ya Bunge lako tukufu imezipata, mnamo tarehe 10 Desemba, 2012, Hifadhi ya Taifa ya Saadani ilihamisha jumla ya shilingi 12,200,000 kwenda kwenye akaunti na. 0150357447800 iliyoko CRDB Bank tawi la Pugu Road, Dar es Salaam, inayomilikiwa na Leka Dutigite Ltd. Hifadhi ya Taifa ya Saadani inamilikiwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), ambayo ni shirika la umma. Siku moja baadae, fedha hizo zilitolewa kwa pesa taslimu kutoka kwenye akaunti hiyo.

Baada ya hapo, kati ya tarehe 14 Januari na 7 Februari, 2013, akaunti ya Leka Dutigite Ltd. iliingiziwa jumla ya shilingi 28,600,000. Fedha hizi zote ziliingizwa kama fedha taslimu na mtu aitwaye Mchange (shilingi 3,600,000 tarehe 14 Januari, 2013) na Leka Dutigite (shilingi 25,000,000 tarehe 23 Januari na 7 Februari, 2013). Kufikia tarehe 7 Februari, 2013, fedha hizo zote zilikwishatolewa benki.

Mheshimiwa Spika,
Tarehe 28 Februari, 2013, akaunti ya Leka Dutigite Ltd. iliingiziwa shilingi 32,367,000 na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Kwa mujibu wa taarifa za kibenki, siku hiyo hiyo, fedha hizo zilitolewa kwenye akaunti hiyo. Siku nne baadae, yaani tarehe 4 Machi, 2013, NSSF ilifanya malipo mengine kwenye akaunti ya Leka Dutigite Ltd., kwa mikupuo miwili, ya jumla ya shilingi 46,663,000. Siku hiyo hiyo, fedha hizo nazo zilitolewa kutoka kwenye akaunti hiyo kwa mikupuo miwili. Kwa hiyo, katika kipindi cha miezi mitatu katika ya tarehe 10 Desemba, 2012 na 4 Machi, 2013, Leka Dutigite Ltd. ililipwa shilingi 119,930,000 kwa utaratibu huo huo wa ingiza na toa fasta. Kati ya fedha hizo, shilingi 12,200,000 zililipwa na TANAPA na shilingi 79,027,000 zililipwa na NSSF.

Mheshimiwa Spika,
Katika mazingira ya kawaida, sio kitu cha ajabu kwa mashirika ya umma kama NSSF na TANAPA kufanya biashara na watu au taasisi mbali mbali kama makampuni binafsi. Ukweli ni kwamba, kwa upande wa malipo yaliyofanywa na TANAPA, Kambi Rasmi ya Upinzani ya Bunge lako tukufu imeweza kupata nakala ya mkataba unaohusu Maandalizi ya Filamu (Documentary) kwa Ajili ya Kuhamasisha Shughuli za Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Saadani kwa Kutumia Wasanii Kutoka Kigoma. Mkataba huo umesainiwa tarehe 5 Desemba, 2012, kati ya Hifadhi ya Taifa ya Saadani na Leka Dutigite Ltd. na una thamani ya shilingi 12,200,000, kiasi kile kile kilicholipwa na Hifadhi hiyo.

Hata hivyo, Mheshimiwa Spika, mazingira ya malipo haya sio ya kawaida. Hii ni kwa sababu ya uwepo wa kampuni ya Gombe Advisors Ltd. Kwa mujibu wa nyaraka za BRELA, kampuni hii ilisajiliwa tarehe 24 Novemba, 2011. Kwa mujibu wa nyaraka hizo, ofisi za Gombe Advisors Ltd. ziko kwenye jengo la City House, Mtaa wa Mkwepu, Dar es Salaam, ziliko ofisi za Leka Dutigite Ltd. Kwa mujibu wa nyaraka hizo, wakurugenzi wa Gombe Advisors Ltd. ni Zitto Zuberi Kabwe ambaye kazi yake inatajwa kuwa ‘mchumi’, na Raphael Ongangi ambaye anatajwa kuwa ‘mchambuzi wa fedha na vitega uchumi’ (Financial and Investment Analyst). Bwana Ongangi aliwahi kutajwa na gazeti la kila wiki la ----- la tarehe 26 Desemba 2013 kuwa ni mmoja wa washauri wa Zitto Zuberi Kabwe na anasemekana kuwa msaidizi wake.

Mheshimiwa Spika,
Zitto Zuberi Kabwe sio ‘mchumi’ anayetajwa katika nyaraka za BRELA zinazoihusu kampuni ya Gombe Advisors Ltd. pekee, bali pia ni Mbunge, tangu mwaka 2005, wa Bunge lako tukufu. Kama Mbunge, Mheshimiwa Zitto Kabwe ni ‘kiongozi wa umma’ kwa mujibu Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, 1995. Sheria hii inawalazimu viongozi wa umma, wanapokuwa madarakani, kuwa “waadilifu, wenye huruma, utulivu, umakini na watakaoendeleza viwango vya juu vya maadili ili kujenga na kuendeleza imani ya umma kwa uadilifu wa Serikali.”

Aidha, viongozi wa umma “... watawajibika kutekeleza wajibu wao kwa umma na kuendesha shughuli zao binafsi kwa namna ambayo itaonekana na kuthibitika kuwa ni wazi kwa umma na haitatosheleza kwao kutekeleza wajibu wao kwa kufuata sheria tu.” Vile vile, kuhusiana na maslahi binafsi, Sheria hii inaelekeza kwamba “... viongozi wa umma hawatakuwa na maslahi binafsi ambayo yanaweza kuathiriwa na maamuzi ya serikali wanayoshiriki katika kuyafanya.”

Mwisho, kuhusiana na maslahi ya umma, viongozi wa umma wanatakiwa, pale wanapochaguliwa au kuteuliwa, kupanga masuala yao “kwa namna itakayozuia migongano ya maslahi ya wazi, iliyojificha au inayoonekana kuwepo na pale ambapo migongano hiyo inatokea kati ya maslahi binafsi na maslahi ya umma basi itatatuliwa kwa kuangalia zaidi maslahi ya umma.” Kwa kadri ya ufahamu wa Kambi Rasmi ya Upinzani ya Bunge lako tukufu, Mheshimiwa Zitto Kabwe hajawahi kutangaza maslahi aliyonayo kwenye mikataba ya Gombe Advisors Ltd. na Leka Dutigite Ltd. na NSSF na TANAPA.

Mheshimiwa Spika,
Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe sio tu ni Mbunge anayebanwa na masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, bali pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Fedha za Serikali (PAC). Kwa mujibu wa kipengele cha 12 cha Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge lako tukufu, mojawapo ya majukumu ya PAC ni kushughulikia maeneo yenye matatizo sugu ya matumizi mabaya ya fedha za umma katika Wizara na Mashirika ya Umma yaliyoainishwa katika taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. NSSF na TANAPA ni baadhi tu ya Mashirika ya Umma yaliyo chini ya usimamizi wa kibunge wa PAC.

Kwa maana hiyo, Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Zitto Kabwe, kwa kutumia makampuni yake ya Leka Dutigite Ltd. na Gombe Advisors Ltd., amefanya biashara na TANAPA, shirika la umma analolisimamia kama Mbunge na Mwenyekiti wa PAC. Mheshimiwa Zitto Kabwe na wanamuziki washirika wake, kwa kutumia makampuni ya Gombe Advisors Ltd. na Leka Dutigite Ltd., wamelipwa fedha za umma za TANAPA na NSSF.

Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kutoa maelezo juu ya madai ya ukiukwaji wa Sheria uliofanywa na viongozi wa umma na mashirika ya umma katika kashfa hii. Pamoja na maelezo yatayotolewa , Kambi Rasmi ya Upinzani inataka Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi maalum juu ya matumizi ya fedha zilizotolewa na TANAPA na NSSF; msukumo uliofanya fedha hizo zitolewe na matumizi ya fedha hizo kwa kuzingatia masharti yanayosimamia fedha za umma na utawala bora katika usimamizi wa fedha za umma. Aidha, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ifanye uchunguzi juu ya malipo na matumizi husika kwa kurejea masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Sheria nyingine zinazohusika. Kwa upande mwingine, kwa kuwa suala hili linahusu mbunge na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge inayohusika na usimamizi wa fedha za umma, Kamati ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge nayo ifanye uchunguzi wake juu ya madai ya masharti ya Katiba ya Nchi, Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge na Kanuni za Bunge juu ya maadili ya kiongozi wa umma ikiwemo yahusuyo utangazaji wa maslahi.

Mheshimiwa Spika;
Mwisho, Kambi Rasmi ya Upinzani ya Bunge lako tukufu inatoa rai kwa wanamuziki na wasanii wengine wote nchini kuwa waangalifu na watu wanaotaka kutumia umaarufu wao kama wanamuziki na wasanii kwa lengo la kufanikisha dili za kifisadi. Bila kuchukua tahadhari ya kutosha, wasanii hao wanaweza kujikuta wakipoteza sifa na umaarufu wao ambao wameujenga kwa jitihada zao wenyewe.

************************************************************************************************

Mapambano ya Kambi Rasmi ya Upinzani yanaendelea.Hayachagua mtu,taasisi au kundi la watu au taasisi
 
Last edited by a moderator:
huo ndo upinzan so kwa ccm 2 hapo zitabanwa tanapa na nssf
 
Sio chuki bali CDM haiwezi kufumbia macho ubadhirifu kwa rasilimali za nchi hii, mchezo huo wakudekeza watu kutokana na majina yao mmeozoea huko kwenu ccm.
CHADEMA waache chuki binafsi za kumshambulia mtu kisa tu hataki kufuata mkumbo wao.
 
Wewe ukiona mtu ametimuliwa CHADEMA sio bure CHADEMA ni chama makini sana,,, Haya sasa Zitto na kashfa ya wizi wa fedha za umma sijui safari hii atatokea wapi??
 
CHADEMA wanatapatapa! Kumuengua Zitto Kabwe ni kosa kubwa sana lililowahi kutokea katika historia ya Chadema! Ni ukweli usiopingika, ZITTO KABWE ndiye alikuwa anaibeba Chadema...na ndio usemi wa Zitto ni Chadema na Chadema ni Zitto!

Hizi siasa za majitaka, u------- unaofanywa na freeman Mbowe na kundi lake ni vichekesho na ni dalili la kufilisika kisiasa! Lengo la upinzani ni kuchukua madaraka ya nchi, na siyo kudhoofisha upinzani!! Kwa mtaji huu wa kibwege Chadema wanafikiria nini?

SHAME ON YOU SUGU, umesahau ulishalialia kwenye lile sakata lako la dili za pesa za Malaria...wewe vs Clouds FM?? Sugu ni mufilisi wa siasa, huna jipya, badala ya kuwatetea wasanii na kazi zao, badala ya kuwasaidia kupata dili unaendelkeza siasa uchwara....siasa Mufilisi!!

AIBU KWENU CHADEMA

Ndio maana hata ile
Kweli wewe ----- -----
 
Fungua LINK Hii http://ubuntuone.com/3Yvcq8P9kqiHBUtIcCzFB5 MSIGWA, LISSU NA LEMA ;- WAHONGWA NA PROF. MUHONGO na MASWI kumchafua ZITTO KABWE na WABUNGE WENGINE WOTE WAZALENDO. wamdhurumu SUGU, nayeye akataa kusoma mashtaka ya LISSU dhidi ya ZITTO KABWE kwenye Hotuba yake.
 
Back
Top Bottom