Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 141,511
- 283,970
Zitto ni mwanasiasa makini,hawezi kuchafuliwa kwa propaganda za kijinga.
dogo kama huna unalolijua si ukae kimya tu !
Zitto ni mwanasiasa makini,hawezi kuchafuliwa kwa propaganda za kijinga.
wakati mbowe anakopa hakuwa mbunge mwaka 92mkopo aliokopa mbowe na dr.slaa wamesharudisha?
Sasa mbona anawatoa CHADEMA jasho namna hii?
uongo mtupu
Tuwekeni siasa kando na tufanye kazi. Tumesikia upande mmoja wa shilingi tusubiri Zitto nae aseme upande wake ili tulinganishe na tutoe hukumu kwani Chadema kwa chuki yao juu ya Zitto wanaweza ongea lolote lile.
Afu pia wao kina Sugu walipata wapi hizo documents kama wao nao sio wadau?
Haya, mjibie Zitto sasaKweli sugu hana sera. Nimemuona akishangilia wakai Juma Nkamia akijibu hoja kwa ufasaha na weledi mkubwa
Ccm wanamuharibia Zito. Why kila Zito akishutumiwa au kutuhumiwa,watu wa ccm ndio huwa fasta kumtetea. Mfano Lizaboni na Msalani humu jf. Why?
Nadhani mbilinyi amenunuliwa ili kuweka chunvi ktk kidonda. Kwani kwa kauli hiyo mbilinyi hajengi bali anabomoa. Anaonyesha wazi kwamba hata upinzani nao kumbe wanapiga dili. Hivyo kelele zao ni sababu hawajahusishwa. Na wakihusishwa ni washiki wazuri. Haya yetu macho
Ngoja muone zitto atavyo wamaliza hawa chadema. uzuri ni mtu makini na wataumbuka.
Umeshasikia kutoka upande wa pili kwa Mh.Zitto? au umeimeza nzima nzima.
Kafulila, Juliana Shonza, Mtela Mwampamba, Chacha Wangwe ni waislam wa Msikiti upi we ukoko?
Hayo malipo ni kwa kazi ipi?!??
Hotuba Hii haijazungumzia mipango name maendeleo ya wizara husika Bali vijembe kwa MTU mmoja je tutafika?
ww unafikir Zuber kabwe anataka nin? tena fedha anayo tena mingi!!umaarufu wa kutosha.wewe piga ZOGO mtandaoni.kesho utamkuta MJOMBA SUGU yuko ndan ya ACT lissu na mnyika hawa watarudi lumumba2
Mkuu.
MSALANI na Lizaboni ni wapuuzi wachimia tumbo wasiojitambua.
Pamoja nao kuna ifweero Ruttashobolwa utaifakwanza na Simiyu Yetu.
Hawa tulishawapuuza kitambo sana hapa jukwaani.
Uongo Wa mchana kweupe
Mh Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe kwenye picha na Mh Mbunge wa Mbeya Mjini ambaye ni moja kati ya wasanii wenye mchango mkubwa kwenye muziki wa kizazi kipya,Sugu(Joseph Mbilinyi).
PENDEKEZO BINAFSI LA MBUNGE KUHUSU KUZUIA UNYONYAJI DHIDI YA WASANII WA TANZANIA KATIKA BIASHARA YA MIITO (RING BACK TONES)
Kwenda kwa: DR ABDALLAH KIGODA, Waziri wa Viwanda na Biashara
Kuhusu: BIASHARA YA MIITO YA SIMU (RINGBACK TONES)
Kumekuwa na malalamiko makubwa sana kuhusu biashara ya mauzo ya nyimbo kama miito kwenye simu. Malalamiko haya yalianzia kwa wasanii wenyewe na baadaye mimi binafsi niliwasilisha hoja zao Bungeni mwaka 2012. Hata hivyo, hadi sasa malalamiko haya bado hayajapatiwa ufumbuzi na hivyo wasanii kuendelea kunyonywa. Tatizo kubwa katika biashara hii ni USIRI na UNYONYAJI kwa wasanii wa Tanzania. Suala la USIRI lipo Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia. Suala la Unyonyaji lipo Wizara ya Viwanda na Biashara.
USIRI
Biashara hii ya Ring Back Tones (RBT) hufanywa na Kampuni za simu (Network providers) kwa kununua maudhui kutoka wachuuzi (Content Providers) ambao nao huingia mikataba na Wasanii (Content Creators).
Hakuna sheria yoyote au Kanuni hapa nchini inayoongoza biashara hii na hivyo Network providers na Content Providers kuwa watu pekee wenye taarifa zote za biashara hii. Kampuni za simu hujumuisha mapato ya biashara hii na mapato yake mengine (Not Ringfenced), hawatoi taarifa za manunuzi ya nyimbo (au content nyingine yeyote) kwa wadau na hasa wasanii. Wachuuzi (Content Providers) nao hawatoi taarifa za mauzo kwa wasanii na wanatumia uelewa mdogo wa wasanii kuwasainisha mikataba inayowanyonya. Matokeo yake ni kwamba msanii hupata kiasi cha asilimia mbili tu (2.5%) ya mapato ghafi ya kazi yake. Hivi sasa biashara hii inathamani (turnover) ya takribani shilingi 44 bilioni kwa mwaka.
Suluhisho:
Serikali kupitia Wizara ya Mawasiliano iandike kanuni (regulations) zitakazolazimisha makampuni ya simu kuweka wazi mapato yatokanayo na biashara ya RBT (Miito ya simu) kila baada ya miezi 4 (disclosure rules). Kanuni hizi zielekeze makampuni kutoa taarifa za mauzo kwa kila kazi (nyimbo/vichekesho etc.)
UNYONYAJI
Kutokana na usiri ulioelezwa hapo juu, wasanii wamekuwa wakinyonywa kimapato. Kwa mfano Msanii hulipwa mapato yatokanayo na ununuzi wa awali wa kazi yake (wimbo) katika mwezi (downloads).
Lakini mapato yatokanayo na subscriptions ambapo mlaji hukatwa shilingi 30 kila siku msanii hapati chochote. Hivyo katika mapato ya sh. 1,300 kila mwezi kwa kila mteja kwa kila wimbo, msanii hupata mgawo wake kutoka shilingi 400 tu za downloads na ndio maana wasanii wote nchini hupata 2.5% ya shilingi 44 bilioni zinazokusanywa na Kampuni za Simu.
Nchini Marekani biashara ya miito ya simu (RBT) imetafsiriwa kama maonyesho (Public Performances) na hivyo copyright Association ya Marekani imeweka kiwango cha chini cha mrahaba (royalty) ambacho msanii hulipwa. Marekani msanii hulipwa asilimia 10 ya patoghafi linalozalishwa na kazi yake kama muito wa simu.
SULUHISHO
Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara iandike kanuni kwamba mauzo ya kazi za wasanii kama miito ya simu inachukuliwa kama performance na kwamba Kampuni za simu zitalipa sio chini ya asilimia 12 (12%) ya mapato ghafi, ambapo asimilia 10% itakwenda kwa msanii na asilimia 2% COSOTA kwa ajili ya usimamizi na Ulinzi wa kazi za Wasanii.
HITIMISHO
Kanuni za Uwazi (disclosure rules) katika biashara hii ya Ring Back Tones na mgawo wa haki wa mapato (fair and just revenue share) ndio suluhisho endelevu na litakaloleta tija kwa wasanii wa Tanzania na hata Serikali kukusanya mapato stahili. Kanuni (Regulations) zinazopendekezwa zianze kutumika kuanzia tarehe 1/7/2013
Kabwe Z. Zitto, Mb
Kigoma Kaskazini
Dodoma, 13 Mei 2013
Siasa za kishamba za kuwindana zitamaliza uhai kiduchu wa upinzani. Mnadhani mnamchafua zitto kumbe ndio mzidi punguza uhai wenu.
Kama kapotea iweje muendelee kumsakama? CHADEMA hata aibu hawana. Mwenzao anaugulwa na mama yake mzazi, wao kazi ya kumsakama
Mtawalinda sana wezi ila wakiingia kwenye 18 lazima wapopolewe..Hii inadhihirisha jinsi gani upinzani unavyofight ili upate madaraka na kulifirisisha kabisa taifa.