John, stuka au utaachwa solemba pale Ubungo mataa!

daah mkuu heshima kwako yaani nataman john apitie huu uzi huu ni ukweli mtupu jamaa wanamuhujumu kwenye uongozi wake inabidi ang'oe pandikizi wote walio teuliwa na vasco la sivyo itakuwa balaa kwake john
 
Watoto wa mjini wanasema ukizubaa,utaingizwa kingi.

Napenda kukupa tahadhali ewe mkuu John, unatakiwa ushtuke mapema kwani mambo yanavyokwenda utalala doro!

Mkuu hujiulizi, inakuwaje watu wateuliwe kushika nyazifa kubwa siku tatu kabla ya kukabidhiwa rungu? Tena yule wa mwisho aliteuliwa kuwa katibu tawala pale lindi siku moja tu kabla hujaapishwa, mwingine ukapewa umwapishe kuwa mshauri wako wa mikataba yote utakayoingia, ikiwa ni masaa 18 tu toka upewe rungu, duh! Kwani hujui kule kusini kuna nini kinatakiwa?

Haya sasa, leo unatenguwa uteuzi halafu unafanya uteuzi kwa mtu huyohuyo kuwa mbunge, siku hiyohiyo mtu huyo anajitoa kutaka cheo kile na siku hiyohiyo anataka kingine hivi ni kweli haya maamuzi ya kiswahili umeyatoa wewe jembe letu John au umebambikiwa?

Haya juzi uneenda kuikagua ile mashine pale hosipitalini, ikatengenezwa, siku tatu tu imeharibika. Tena, imeharibika moyo wake. Kwakukufafanulia tu ni kuwa, ile mashine imeharibika kifaa kiitwacho (Redio frequence amplifier) ambacho ndio moyo wake, bila hicho hakuna hiyo mashine!! Kwa mujibu wa mtandao wa hiyo kampuni iliyopewa zabuni ya ya ukarabati kifaa hicho kinauzwa usd 97,000! Mil. 200 za madafu, upo mkuu?

Ukienda lesi tena unapigwa kivingine hujashtuka tu?
Mkuu John ngoja nikuache, usiposhtuka sasa, solemba pale ubungo mataa inakuhusu !

Asiyesikia la mkuu ....... mimi naona zile Biblia Takatifu na Quruan Tukufu wa nazo zitumia ilhali wakijua si sawa naona ndio laana inapoanzia.
 
Hata tanroad walikuwa hivohivo wakanyooka, polepole tutaelewana, nasie tukijua unafanyakazi muhimbili hatuji kwenye msiba wako wala hatuchangii harusi yako.

Utaenda tu na harusi utachangia
 
Masikini John kawekwa kama antenna nje ndani watu wanabadilisha channels kwa raha zao!

Rimoti ni mzee wa msoga na mzee wa malofa. Chini ya uu mfumo hakuna jipya uraisi ungekua ni taasisi isiyoingiliwa na wabinafsi wachache at least tungepga hatua. Sio ya uraisi tu ni taasisi zote nchi hii.
 
Mnyika ni mjanja sana ila asiposhtuka halmashauri inakuwa chini ya Ukawa lakini wanaongozwa na ccm! Shtuka John
 
Pombe tayari ameshaingizwa chaka.
Mistake kubwa ya kwanza ni kumrudisha mwanasheria mkuu wa serikali ambaye anapokea maagizo kutoka kwa mkwere.
Yani hii inadhihirisha CCM ni ile ile coz soon atamteua Wasira kuwa mbunge kupitia viti 9 vilivyobaki.
 
Pombe tayari ameshaingizwa chaka.
Mistake kubwa ya kwanza ni kumrudisha mwanasheria mkuu wa serikali ambaye anapokea maagizo kutoka kwa mkwere.
Yani hii inadhihirisha CCM ni ile ile coz soon atamteua Wasira kuwa mbunge kupitia viti 9 vilivyobaki.

Yaani akimteua huyo, itakuwa kaingia chaka ambalo hawezi kujinasua!
 
Naona mwezi wa nyumbu kurudi point A toka B umefika. Wanapeana faraja. Nyumbu wanaomba sana mamba asikatishe mtoni manake wao akianza kukimbia mmoja wote wanafuata...
..nyumbu bwana, Johny ana wiki tu. Mnaomuombea mabaya mtashidwa na kuaibika nyie.
 
Naona mwezi wa nyumbu kurudi point A toka B umefika. Wanapeana faraja. Nyumbu wanaomba sana mamba asikatishe mtoni manake wao akianza kukimbia mmoja wote wanafuata...
..nyumbu bwana, Johny ana wiki tu. Mnaomuombea mabaya mtashidwa na kuaibika nyie.

Eli79, Kumshtua ni kumtakia mema na sio mabaya!
 
Back
Top Bottom