Haya ndiyo maslahi ya nchi na haki za wananchi alizosimamia Hayati Rais John Pombe Magufuli

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
344
1,007
HAYA NDIYO MASLAHI YA NCHI NA HAKI ZA WANANCHI ALIZOSIMAMIA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI

Leo 15:15hrs 06/12/2021

Rais John Magufuli katika Awamu ya tano,kwa kutekeleza usimamizi wa maslahi ya nchi na haki za Wananchi ni kama aliingia vitani,tuliona maadui mbali katika sura ya "Kigogo" "Chahali" na wengineo, kuna baadhi ya maadui katika mitandao walisema JPM hafiki Uchaguzi wa 2020,kwa hakika Rais Magufuli alihitaji msaada na ushirikiano wa kila Mzalendo aliyekuwa na mapenzi mema kwa Mama Tanzania, hitaji la msaada katika vita hii kubwa kuliko Vita nyingine yeyote,

Vita ya kusimamia maslahi ya nchi na haki za Wananchi,ilikuwa ni vita mbaya sana na hasa tulipoona wadogo zetu wakienda Ulaya kumtukana Mama yetu Tanzania,ilisikitisha sana na hivi sasa wengine wanataka kurudi kwa huyu huyu Mama Tanzania waliyekuwa wakimtukana kila kukicha,sababu ni kwamba Rais John Pombe Magufuli aliamua kusimamia maslahi ya Nchi na haki za Wananchi wote wa Tanzania,sio kusimamia haki za matajiri tu na kuwaacha wanyonge,Niwapongeze na kuwatia moyo Wazalendo wote na Wanataifa wote popote walipo,daima wasichoke kuupiga vita ubepari, ubeberu na udhalimu wowote wa kuliibia Taifa Mama la Tanzania,Mungu mpumzishe kwa amani Rais John Pombe Magufuli, Mungu ibariki Tanzania.

-Niyaelezee kwa Ufupi, Mazuri ya CCM chini ya Rais John Magufuli.

-Serikali isiyoyumba.

Moja ya sifa ya uongozi ni kuwa na msimamo. Ni lazima kama kiongozi ujulikane dhahiri kuwa kipi kwako unataka kipi kwako hukitaki. Na uwe na uwezo kuamua na kusimamia maamuzi yako bila kuyumbishwa.

Serikali ya CCM ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli ilijipambanua kuwa na uwezo wa kuamua na kuyasimamia maamuzi yake, Yapo mambo ya kimaamuzi; mathalani kuhamia Dodoma (ambapo kama angefuata 'njia za makaratasi), ingechukua miaka 50 mingine kuweza kuhamia Dodoma) Mradi wa Umeme wa mto Rufiji ujulikanao kama stigglers gorge (ambao unahitaji msimamo thabiti ili kuusimamia,Rais Magufuli sasa amelala milele tunaona mradi huo unavyopigwa dana dana).

Vigogo kuweza kuguswa na mkono wa Serikali ni ishara ya uthabiti wa Serikali ya CCM ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli na kamwe si Serikali dhaifu. Kuwa na Serikali yenye msimamo na maamuzi ni suala la kupongezwa sana na ndio maana Wananchi walifurahishwa sana na Uongozi wa Rais John Pombe Magufuli.

-Kudhibiti Rushwa kubwa.

Ni suala la kujua kwamba hela ya Umma ni Sumu hadi Rais Magufuli analala milele nchi yetu hatukusikia upigwaji wa 'dili' kubwa zaidi ya propaganda kusema hela hii haipo imepelekwa kununua ndege,sijui 1.5T hizi zilikuwa ni propaganda na zilifafanuliwa na Naibu Waziri wa Fedha kuwa zilikuwa ni hati fungani zilizokuwa zinasubiriwa kuiva ambao Serikali ilizihesabu kama ni hela japo ilikuwa haupo mkononi,na CAG alikuja kuiulizia na kusema haipo mkononi,katika Awamu ya nne tuliona Epa, Richmond, Escrow ni kati ya rushwa kubwa zilizopoteza imani ya wananchi kwa serikali,ndiyo zinaathiri mahusiano ya kiuchumi ya serikali na mashirika ya kimataifa,lakini awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli ilijitahidi sana kupiga Vita rushwa kubwa na Ufisadi.

-Kupunguza 'political tension'.

Kuna msemo kuwa fedha huwa haikai sehemu yenye kelele. Moja ya vikwazo vikubwa sana vya kiuwekezaji na uchumi afrika ni 'vuguvugu za siasa'. Kunapokuwa na sekeseke za kisiasa muda wote, uwekezaji na ufanyaji biashara unakuwa mgumu sana. Maandamano na mikutano ya kisiasa muda wote havina afya katika ukuzaji uchumi. Hivyo ni vyema maamuzi ya kiserikali juu ya kudhibiti 'shughuli za kila uchao' za kisiasa yamefanyika.

Mapungufu: ni dhahiri kuwa maamuzi hayo katika Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli kwa vigezo vyote hayakuzingatia sheria,ni wakati sasa wa kubadili sheria zetu (katiba Mpya)hasa za Vyama vya Siasa kuweza kukidhi mahitaji ya wakati ya Taifa na sio kupinga kila siku,Najua kilochofanyika ni administrative orders, lakini tukapata mabadiliko ya Sheria ya vyama vya Siasa ili iweze kudhibiti ujinga ujinga wa vyama vinavyotoka nje ya Maadili ya Mtanzania.

-Kuboreka ama kuimarika kwa matumizi ya fedha za umma.

Moja ya changamoto kubwa nchi za kiafrika, ni fedha za Umma kuishia katika 'mambo ya hovyo' na mifukoni mwa mtu mmoja mmoja, Ni vyema Mh Rais Magufuli alivyodhibiti safari 'zisizo na tija', vikao 'visivyo na tija' vya kiserikali, posho nyingi. Hili lilikuwa ni jambo jema na la kupongezwa sana.Na tumeona hatua hii ikileta tija katika kuziba upotevu wa fedha ya Serikali.

-Nidhamu katika Utumishi wa Umma.

Watumishi wa Umma wana wajibu wa kwanza wa kuwahudumia wananchi kikamilifu (haki). Katika kutimiza hili ni muhimu watumishi waheshimu muda wa kukaa katika vituo vya kazi. Ofisi nyingi za umma kwa sasa walau wanakaa ofisini, walau wanasikiliza na kuhudumia wananchi wakati.Sasa basi nidhamu hii ya utumishi isiwe kama ile nidhamu ya baba mkali mwenye nyumba. Kuna familia ambazo baba mwenye nyumba ni mkali sana na akiwepo nidhamu ya familia ni ya hali ya juu, asipokuwepo maisha ni shagharabaghara. Familia hizi hazidumu baba akisafiri au baba akifa. Hivyo tuna wajibu wa kuijenga nidhamu hii iwe sehemu yetu ya maisha "part and parcel " ili kuweza kufanya kazi kwa mafanikio yetu binafsi, kwa taifa na kwa maslahi Mapana ya kizazi kijacho.

-Ushauri kwa Mapungufu machache.

-Kukanywa na kufundwa kwa Wateule wa Mh Rais.

Moja ya doa kubwa katika awamu zote ni Watumishi wa Umma kutopita katika Vyuo vya Maadili ya Utumishi wa Umma hasa ma DC na RCs. Hawa wamekuwa na sura ya kufanya baadhi ya mambo yakionyesha dhahiri kutopikika katika vile vyuo vya Hombolo, Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Kivukoni ndio maana wanafanya baadhi ya mambo nje ya miiko ya kimaadili ya Utumishi wa Umma, wengi wamekuwa wanatukana wananchi, wanatusi watendaji wa Chama na Serikali.Najua Mh Waziri Mkuu Majaliwa ni mtu mwenye ubobezi wa utumishi wa umma, awakumbushe wateule away miiko na maadili yao. Semina za mara kwa mara zitawarudisha kwenye mstari.

-Kuimarika Utawala wa sheria.

Kama ambavyo Nyerere alipofanya kosa la kunyang'anya watu mali zao bila kuwepo sheria ya suala hilo, na kisha kuweka sheria baadae. Basi tuimarishe sheria zetu na tufanye mabadiliko sawa sawa na hitaji la nyakati,Ziwekwe sheria za kusimamia maamuzi yaliyokwifanyika kwa matamko. Sheria ya Vyama Vya Siasa ibadilishwe Ili yafanywayo yawe kisheria. Na isiweko upendeleo kisiasa na kuwaumiza Wananchi bali Sheria zikusudie kuleta faida kwa Mwananchi na kwa Taifa.

-Kuimarisha mifumo ya kisheria.

Ili hatua zote za kimaendeleo zilizopigwa katika awamu ya 5, ili nidhamu 'hii ya uoga' ya utumishi iwe ni nidhamu ya kitaasisi, ikiwa sasa umepumzija milele bado bombardier,Airbus na Boeing ziwe bado zinaendelea,kupunguza tumbuatumbua za watendaji wabovu ambazo zinatujengea uhasama usio wa lazima, basi suluhu ni moja Kuongeza baadhi ya mambo kwenye katiba na kuimarisha mfumo wa Mahakama(Katiba Mpya) Mahakama yenye uhuru, Mahakama yenye watu weledi,inavyoanza kuonekana sasa,ifike wakati mwananchi akimshitaki DED kwa kumjibu hovyo ofisini, mahakama ikamtoza faini na kumdemote ama kumfukuza kutoka nafasi hiyo basi atakayefuata atatii sheria na kufuata miiko ya kimaadili ya Utumishi wa Umma. Yule RPC anayehukumu watu mbele ya hadhara akiburuzwa mahakamani, hakuna RPC mwingine atakayewageuza watuhumiwa kuwa ni watenda makosa,wale polisi waliokamatwa wakisindikiza dhahabu wakishtakiwa basi wengine hawatajaribu tena kufanya hivyo,yule mkaguzi anayeita bunge dhaifu akichukuliwa hatua basi kila mtumishi wa Umma itampasa kujua miiko ya kimaadili ya Utumishi wa Umma kusema tuhuma mahali husika na sio kwa mabeberu,kuchukukiwa hatua kutajenga nidhamu, Utaifa na Uzalendo kwa nchi yako ambayo ni kitu kizuri.

Ni jukumu letu kama wadau na Wazalendo kwa Taifa letu la Tanzania kwa hisia za uzalendo na uchungu wa maendeleo ya Taifa letu, Kwa namna yoyote iliyo sahihi kupongeza juhudi za Rais na Mwenyekiti wa CCM wa Awamu ya tano,Dr John Pombe Magufuli lakini pia kukosoa pale panapolazimika kwa lengo la kuleta tafsiri sahihi aliyoilenga Mwenyekiti wetu ilipoonekana kutokana na weledi wetu katika fani mbalimbali na kupitia vyanzo mbalimbali vya habari kwamba, utekelezaji wa mambo fulani hayakufanyika au yamekwenda kinyume na ‘mfumo’ wa kiutekelezaji, sheria,sera na ilani ya Chama chetu cha CCM.Mungu ibariki Tanzania, Pumzika kwa amani Rais wetu John Pombe Magufuli.

Rais Magufuli, aliliokoa Taifa toka kwenye Madawa ya Kulevya.

-Takwimu za waathirika wa madawa ya kulevya kwa mwaka zilionyesha 700,000 mwaka 2013 hii ilikuwa ni hasara kubwa kwa Taifa hasa takwimu za jeshi likionyesha lina askari vijana wapatao 30,000 na kuongeza au kupunguza kidogo (around 30,000).

Hii ni sawa na kusema ukichukua vijana waliathiriwa na madawa ya kulevya unapata ndani yake vijana ambao walipaswa kulitumikia jeshi la Tanzania (kwa idadi ya watu). Hili ni kundi ambalo kwa kiasi kikubwa halizalishi, halilipi kodi, ni tegemezi na wengi wao ni wahalifu ingawa uhalifu zaidi ni matokeo ya uathirika wao.Kupiga vita madawa ya kulevya kuliokoa kizazi hiki na jamii imeliona hilo na sasa hakuna waathirika hawa wa Madawa ya kulevya.

Vijana ni nguvu kazi ya taifa, ndio nguzo ya taifa. Nguzo hii ikiliwa na mchwa taifa linaanguka.

Kwa hiyo kila mtanzania ameshukuru awamu ya tano kwa kufutilia mbali Madawa ya Kulevya, Shukrani Mh Rais Magufuli alipigana vita ya kufa kupona dhidi ya madawa ya kulevya na umeokoa afya za vijana wetu.

Angalizo: Kila mtu anaweza kuwa mwathirika wa madawa ya kulevya.

-Rais Magufuli aliupiga Vita Ujangili.

-Kilo moja ya meno ya Tembo ilipata kuwa na thamani ya Tsh. 200,000.Ripoti zaidi kuhusu ujangili zilikuwa hazileti furaha kwa wazalendo ambao tulitegea maliasili zetu zilinufaishe Taifa kwa faida ya kizazi kijacho.

Miaka ya nyuma Al Jazeera walipata kuiita Tanzania 'Point of extinction'. Kwa maana eneo la kuondoa uhai asilia Duniani, au eneo la maangamizi, wakiakisi hali ya ujangili katika Tanzania inayoonesha kuwa Tembo walipungua kutoka 109,051 mwaka 2009 na kufikia 43,330 mwaka 2014.

Tembo 85181 waliouawa kwa kipindi cha miaka 5 ni Sawa na tembo 17,016 kila mwaka. Maana yake kwa tembo 43,330 waliobaki ukigawa kwa 17,016 basi kwa miaka chini ya mitatu mfano 2015 hadi 2018 tembo wangekuwa wamekwisha kama hali isingebadilika. Hiyo ni kwa Tembo tu. Ahsante Mh Rais Magufuli kwa kuupiga Vita Ujangili na sasa tembo bado wapo na wamezaliana mara dufu kwa takwimu wameongezeka 100,000 sawa na kuzaliwa kwa tembo 20,000 kwa miaka 5.

-Rais Magufuli aliupiga Vita Ufisadi
Escrow, Epa, Richmond, Meremeta, Mabilioni ya Uswisi,na madudu mengine kibao yalitosha kuonyesha kwa nini Wananchi walitaka Mabadiliko mwaka 2015,Mh Rais Magufuli alijenga imani kwa wananchi kwa kushughulika na mafisadi kama ulivyoahidi.Hivi Leo wezi wa Escrow wapo Mahabusu kama alivyoahidi japo wengine wametoka lakini tuliona uthubutu ukitenda kazi katika Awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli, Ahsante Mh Rais Magufuli kwa kuwa Mzalendo kwa Taifa lako.

-Rais Magufuli aliifanya Upya mikataba ya Madini, Mafuta na Gesi.

Tulishuhudia ugeni mkubwa nchini petu mara baada ya ugunduzi wa Mafuta na Gesi. Lakini hata sasa watanzania wana wasiwasi kuhusu mikataba ya siri iliyofanywa awamu ya nne na wageni wake Rais Obama wa Marekani na Xi Ji Ping wa China.

Tumeonewa sana kwenye Madini hili alilitamka sana Rais Magufuli,Wamiliki wa migodi hii sio tu ni watu Matajiri bali pia ni watu wenye ushawishi mkubwa kwenye Serikali za mataifa yalipoasisiwa makampuni hayo. Mh Rais Magufuli alituokoa na dhuluma hii kwa kuzuia Makinikia ambayo bado yalikuwa na dhahabu ndani yake,Ndege zilikuwa zinatua mgodini barrick pale kahama, sasa tungejuaje kama tunaibiwa ama la, kwa hakika umezuia kukombwa kwa rasilimali zetu kwa ridhaa yetu wenyewe. Kwa hakika umelitendea haki Taifa la Tanzania kwa faida ya kizazi kijacho.Ahsante Mh Rais John Magufuli.

-Rais Magufuli alibadili vifungu vya Katiba ili viendane na Hali ya sasa.

Ahsante Mh Rais Magufuli kwa kuwa huru na kuacha kufuata mihemko ya siasa za vyama kwenye mambo ya msingi na kubadili baadhi ya vifungu vilivyopitwa na wakati na kuweka vifungu vinavyokwenda na hali ya sasa kwa maslahi Mapana ya Taifa.

Nimalizie kwa kusema, Mh Rais Magufuli kwa kutekeleza mambo hayo hapo juu ni kama aliingia vitani. Rais Magufuli ulihitaji msaada wa kila Mzalendo mwenye mapenzi mema, ila Mungu aliwahi kukuchukua pengine aliona hatukupi msaada uliostahili.

-Wananchi wa Tanzania walifurahishwa sana na style ya utendaji kazi wa Rais John Pombe Magufuli.

Baada ya Uchaguzi wa 2015 Watanzania baada ya kuona Kiongozi Mpya Rais John Pombe Magufuli akichukua hatua madhubuti dhidi ya Utendaji mbovu, Wizi wa Mali ya Umma, Ufisadi, Kutowajibika ipasavyo kwa Watumishi wa Umma kulinda na kupigania mali ya Umma,Kwa hakika asilimia kubwa ya Wananchi wa Tanzania walifurahishwa sana na Utendaji wa Kiongozi Mpya na hatua stahiki zilizokuwa zinazochukuliwa,

Maisha yaliendelea, matukio mengi yalitokea yakiwa na sura za kufurahisha, kustaajabisha, kushangaza, mengine yalizua hisia tofauti tofauti hasa kwa Wale vyeti feki, Mafisadi, Watendaji ambao hawakuwajibika ipasavyo, Matukio haya yakichagizwa na mabadiliko makubwa ya hali ya kiuchumi ambapo fedha nyingi ilielekezwa katika miradi mikubwa ya kitaifa kama Ufufuaji wa Mashirika ya Umma kama TTCL, ATCL, Ujenzi wa miundo mbinu Barabara za juu na kuanza kujengwa Bwawa la Umeme ikiwa ni Mradi mkubwa wa kuzalisha Umeme katika Mto Rufiji, ujulikanao kama "Stigglers Gorge ".

Kuelekea 2020 na Muonekano Mpya wa CCM kama Chama tendaji na Chama Cha Kizalendo chenye muonekano wa kuwasaidia wanyonge na waliokata tamaa,kurudisha heshima kwa Wakulima na Wafanyakazi.CCM kufanya mabadiliko mara kwa mara na hii inakifanya kila wakati kuibuka Chama kipya.CCM imejifanyia tathmini kubwa na kufanya mabadiliko kila uchao.

Baada ya miaka kumi ya Rais Magufuli angekuha kiongozi mwingine wa CCM ambaye angerekebisha makosa ya CCM yanayojitokeza wakati ikiendelea na mabadiliko ya kimfumo na kujenga taasisi imara, mfano kuondoa Ufisadi, CCM kurudi kwa Watu na kukiondoa mikononi mwa matajiri wachache waliokishika,kila mtu atashabikia CCM na CCM itaendelea kutawala daima na milele.

Hii ilikuwa ni style ya mabadiliko kama yale tuliyowahi kuyaona katika awamu ya nne chini ya Rais Kikwete,Mabadiliko ya kujivua gamba, kuangalia upepo uendapo!! na kubadilika.

Siasa ni kama biashara kila mmoja ana mbinu zake za kupata wateja na uuzaji, Chadema mbinu yao ni ya kujitoa mhanga kuichafua Serikali na Tanzania kwa ujumla, wanakalia bomu wanadhani likilipuka wao watapona,

Tuliona utendaji wa kuacha alama katika awamu ya tano, tuliona uwajibikaji uliotukuka na kwa hakika Mabadiliko ya kimaendeleo yaligusa kila mmoja wetu, kama uoni basi utashika utagundua Kweli kuna mabadiliko, kama hushiki basi utakanyaga na utagundua mabadiliko makubwa ya kimaendeleo, ukitoka kibaha kuja Mbezi hadi Kimara utaona kazi kubwa inayofanyika ya ujenzi wa Barabara ya Morogoro, utajua kweli Serikali ya Rais Magufuli inafanya kazi.

Awamu ya tano ilivyoingia Madarakani tuliona utendaji huu,

-Ujenzi wa Hostel za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (udsm).

-Ujenzi wa Hostel za Askari Magereza.

-Ununuzi wa Ndege 6 (Nyingine 2 ziko mbioni kuja).

-Ujenzi wa Flyover Tazara na Ubungo,

-Upanuzi wa Airport Mwanza,Bukoba,Mbeya,Songea,Dodoma na Musoma.

-Upanuzi barabara ya Moroco Dsm,Mwanza na Arusha.

-Upanuzi wa Kisasa Airport Dar ,terminal 3.

-Kusimamia misingi ya kimaadili ya Utumishi wa Umma, Kukomesha Rushwa
Kurejesha nidhamu Makazini.

-Ujenzi wa reli kwa ajili ya treni ya Umeme (Standard Gauge)

-Ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba.

-Ujenzi wa kota za Magomeni.

-Ununuzi na Ujenzi wa Rada Mpya ya kuongozea ndege katika anga lote la Tanzania.

-Elimu bure na Mafunzo ya kujitegemea katika Veta na Jkt kwa wahitimu wa Elimu ya Sekondari.

-Kukomesha Watumishi Wenye Feki hivyo kuokoa Mabilioni ya Fedha.

-Barabara ya kuunganisha Wilaya za Kibondo kigoma Kaliua huko Tabora.

-Miradi Mikubwa ya Maji,Ujenzi wa Matenki makubwa Dar es Salaam na mradi mkubwa wa Maji toka Ziwa Victoria kuja Tabora hadi Dodoma.

-Uwezeshaji Ujenzi Bomba la Mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Jijini Tanga,Tanzania.

-Usimamizi wa Mazao Mfano Korosho,Pamba,Katani,Alizeti,kahawa,Chai,Maharage,Kilimo cha Mpunga na kutafuta masoko nje ya Nchi kwa ajili ya kupata fedha za kigeni kuinua uchumi wetu.

-Kuboresha Sekta ya Utalii kwa kununua ndege kurahisisha usafiri wa Watalii toka Mabara yote kuja Tanzania.

-Usimamizi wa Mapato ya Mali asili zetu,mfano Madini ya Dhahabu, Tanzanite na Almasi.

-Ukusanyaji Mapato baada ya kuziba nianya ya ufisadi na wizi wa mapato na mali ya Umma.

-Kujenga Utaifa na Uzalendo.

-Ujenzi wa Bwawa la Umeme katika Mto Rufiji "Stigglers Gorge".

Kwa hakika katika awamu ya 5,Serikali ya CCM iliyoongozwa na Rais Magufuli iliifanya CCM kuwa Mpya katika utendaji wa kasi na wa uhakika pasipo porojo wala propaganda, Mwenye macho anaona hata sasa utendaji katika sekta mbali mbali kuijenga Tanzania Mpya ambayo itakwenda kuwa Baba la Uchumi barani Africa,

Nimalizie kwa kuwapa usiha makapi yaliyokataliwa na JPM ambayo yanapambana kuivuruga CCM na kuivuruga legacy ya JPM kwa kutumia,hawatafanikiwa wala kueleweka kwa Wananchi,Kuanzia handling ya mpango wa kumchafua JPM,mfumuko wa bei usioeleweka! Matatizo ya maji na umeme! yote yanaibomoa CCM kuliko kuijenga,makapi hawatoweza kumbomoa JPM wakaeleweka na umma kwa sasa, wadeal na issue zao hesabu 2025.makapi yote yaliyompinga JPM na kumtukana mtukana ndio hao sasa wameanza kuweka mikataba yao na kufurahia uwekezaji wenyewe wanasema wanalainisha vyuma vilivyokaza enzi ya Magufuli hawa makapi wataishia kuumbuka tu mbele ya Wananchi na kushindwa vibaya Uchaguzi wa 2025.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;-
-Assessment on the effects of micro-financing on Poverty Reduction.
 

Dr Mabuga 30

JF-Expert Member
May 8, 2021
320
329
WaPo Wapuuzi watakuja kusema et unatafuta uteuzi , wakati umeongea kitu ambacho ni Cha Ukweli kwa ajili ya masilahi mapana ya kitaifa, Ahsante Sana
 
4 Reactions
Reply
Top Bottom