Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 21,496
- 37,789
Zamani Nilikuwa najiuliza Kwa nini miswada ya sheria mbalimbali inapopelekwa Kwa hati ya dharura Wabunge wa upinzani wanapinga Sana huku wale wa CCM wakiunga mkono Kwa nguvu zote na kufikia kuwaita wale wa upinzani hawana Uzalendo.
Naukumbuka vema Muswada wa sheria ya ulinzi wa raslimali za Taifa wa mwaka 2017. John Mnyika akiwa Mbunge wa Kibamba alisimama na kuomba Mwongozo Kwa Spika (Yob Yustino Ndugai) akitaka serikali iondoe udharura wa Muswada huo ili kuwapa nafasi wadau wa sheria na uwekezaji Muda wa kutosha kupitia na kujadili Muswada huo Kwa maslahi mapana ya Taifa siku zijazo.
Jenista Mhagama (Sera, uratibu na Bunge) alimshukia kama Mwewe huku Kibajaji, Mlinga na Msukuma wakiwa wimawima kuomba watoe nyongeza ya Mwongozo Hadi pale Spika aliposema aliyeombwa Mwongozo ni yeye Ila amemruhusu Mhagama Kwa vile ni Chief Whip.
Lakini matokeo ya Tabia ya kuendekeza udharura tumeanza kuyaona kwenye kesi ya juzi tulipopigwa Billion 75 tena Kwa kuomba tumalize nje ya Mahakama.
Nimejiuliza sababu ya Wabunge wa CCM kushangilia miswada inayopelekwa Kwa hati ya dharura nikagundua sababu kubwa ni kwamba inawarahisishia kutolaumiwa. Hawana Muda wa kusoma na kuchambua miswada pale inapoletwa Kwa njia ya kawaida. Kwa hiyo hati ya dharura inawapa kirahisi sababu ya kujitetea.
Niliwahi kuambiwa na rafiki yangu kwamba mwaka 2019 Mbunge mmoja wa Iringa aliombwa elfu 30 na Mtoto wa dada yake ili akalipe faini baada ya pikipiki yake kukamatwa na traffic, yeye akasema faini ya pikipiki ni elfu 5 tu Huyo traffic anataka kumpiga hela.
Akaahidi kumpigia RPC Iringa kulalamika lakini majibu aliyopata ni kwamba, "Mheshimiwa nyie ndo mmepitisha faini hii Bungeni". Kilichofuata ni aibu kwake.