JK amteua Jaji Kiongozi mpya

Ok.. tukubaliane kuwa alikuwa Wakili wa kujitegemea miaka mitano iliyopita. Watu wakisoma majibu yangu mara zote nimetumia qualification kwa maana ya kwamba info zaidi zikipatikana itasahihishwa. Sasa watu wamefikia kuitana waongo.. kwa sababu tarehe ya uwakili wake haikuwekwa definite.

Jamani msome basi kilichoandikiwa! wengine tunatumia maneno vizuri sana tukitaka kumaanisha tunachotaka kusema tunakisema hivyo hivyo.

Nimesema kwenye taarifa ya kwanza "kama mwaka mmoja"

nilipomjibu Jmushi nikasema "exactly! as far as I know"..

wakosoaji na wanaopenda ligi zisizo na ulazima hawajui maana ya "kama" au "as far as I know"!
 
Kuna kazi tu anaenda kufanya huyo mchaguliwa ,inaonyesha Kikwete anajipanga kupambana na rungu la 2010.
__________________
Mwiba, sidhani kama Jaji Kiongozi ana role ya maana na kubwa kwenye uchaguzi wa rais. Siyo mwanachama wa chama cha siasa, hana fungu kubwa na kama inavyojulikana hali ya mahakama zetu ni hoi kabisa kila siku wanalia ufinyu wa bajeti. Mamlaka ya majai katika uamuzi wa kesi hayawezi kubadilishwa na Jaji kiongozi wala jaji mkuu wala rais, hajipangii kesi na wala hawezi kujipangia kesi kwa sababu anakuwa ni jaji wa kituo cha Dar es Salaam lakini kanda ya Dar es Salaam in jaji mfawidhi wake. Ni vigumu kidogo kwa mtu ambaye hayuko within the legal fraternity kuelewa vizuri kazi za jaji kiongozi na jina lenyewe linamfanya awe mkubwa sana, lakini ukweli ni kwamba mhimili wa mahakama unaongozwa na Jaji Mkuu na wala si jaji Kiongozi. Labda nieleze kidogo kwamba nafasi ya jaji kiongozi inatokea tu kwa sababu mahakama kuu ya Tanzania siyo 'union matter'. Yaani haina mamlaka ndani ya Zanzibar. Mahakama ya Rufani ndio mojawapo ya mambo ya Muungano kwahiyo jaji mkuu anakuwa ni jaji mkuu wa Tanzania ingawa na zanzibar kuna jaji mkuu lakini power kwenye mahakama ya rufani, kwahiyo Jaji kiongozi ni ya kiundeshaji wa mahakama kuu na usimamizi wa mahakama za chini. ndio maana hana hata tenure of office. Ukiangalia vizuri jaji Manento kakaa takriban miaka 3, wakati Massati kakaa mwaka mmoja tu kabla ya kupelekwa mahakama ya rufani, usishangae Jundu akapelekwa mahakama ya rufani ndani ya muda mfupi.
 
Tunakaa tunajadili UONGO uliotungwa na mtu badala ya kujikita kwa mambo muhimu ya Taifa letu. Sasa hapa mawazo yetu yote tulikuwa tunajua huyu jamaa ana mwaka kama mmoja tangu ateuliwe kuwa Jaji wa Mahakama Kuu, kumbe ni mawazo ya mtu anayotunga. Hii ni sawa na ile ya mhindi aliyeua naye kajiua, tunajadili mara jana kaonekana mahakamani. Nadhani Jujuman MUONGO umemjua, ukitaka nitamtaja.

wenzako huwa hawajiumu maneno, ukimuona mtu mwongo unamwita mwongo. Katika kufanya hivyo unaonesha kuwa mtu huyo alikuwa anajua ukweli wa kile anachosema na kwa makusudi ameamua kupotosha kwani uongo hauwezi kuwa uongo hadi ijulikane kuwa ukweli ulikuwa unajulikana.

Kutoa taarifa isiyo sahihi au ambayo si kamili si uongo, kutoa habari ambayo haina details zote au baadhi ya taarifa zake bado zinatafutwa siyo uongo. Uongo kifalsafa nyepesi ni kusema kitu cha kupotosha ilhali ukweli unajulikana.

Ukimuona fisadi usisite kumwita fisadi kama unauhakika kuwa vitendo vyake vinalingana na vile vya kifisadi. Ukimuona mwongo, na unajua kuwa ni mwongo (kwa sababu anajua ukweli lakini kauficha) basi usisite kumwita mwongo.
 
Sheria inasema jaji anateuliwa na Rais so, njia pekee ya kumuondoelea hii nguvu ni kubadili sheria. Hata hivyo suala la majaji karibu nchi zote duniani zinamuachia Rais au mkuu wa Nchi uwezo huo. Labda tuangalie kuwa jinsi gani akishamteua mtu basi mtu huyo athibitishwe na Bunge..
__________________
Mwacheni jamani,akimchagua mwanakijiji 2010, si ataubatilisha urais wake
najilinda jamani,,nani aupendi URAIS??mmh hata watoto natumain wanashiriki kwa hili maana wanajua impact yake kubwa!!!wanaweza sikia tu ""IKULU"" kwa JINA
 
Ni kweli kumwita mtu Muongo si matusi, lakini ni neno lenye makali na kamwe halipaswi kutumiwa na mtu muungwana kama wewe.

Si lazima mtu akisema kitu ambacho 'sio ukweli' basi ni 'uongo'. Uongo ni upotoshaji wa makusudi (mtu anakuwa maekusudia kupotosha) na tena ni tabia inyojirudia mara kwa mara. Kama mtu amesema kitu ambacho si kweli lakini wakati anakisema aliamini kwa dhati ni ukweli basi huyu hatupaswi kumwita muongo.

Tazama Kaka Mdogo alivyorekebisha kiungwana 'ukweli' kuhusu rufani za mahakama kuu (nimeona umekuwa wa mwanzo kumpa 'Thanks' kwenye hii post yake!)

Kama angelikuwa si muungwana angeweza tu kuwaita waliochangia mwanzo kwamba ni waongo!Lakini alichgua njia hii ya kiungwana kwa kusema/kutoa ukweli bila kumwita/kuwaita jina lolote wachangaiaji ambao hawakuwa na habari sahihi juu ya taratibu za rufani katika mahakama ya rufaa.

SMU, naomba sana usinifananishe na mtu humu, uungwana wa Kaka Mdogo hauwezi kuwa uungwana wa Mfumwa. Hivyo nakuomba sana jadiliana na Mfumwa kuhusu yaliyopo bila kusema nani kaandika nini kiungwana.

Mfano mimi nikisema kuwa Mfumwa ni Mhindi tena ni mara ya kwanza, wakati kila mtu anajua Mfumwa ni mbantu wa TZ, basi mimi ni muongo. Kuripoti kitu usichokijua, ama kuongezea tu ili kupindisha ukweli ni uongo, si lazima ujifanye unajua kila kitu.

Hakuna anayesema ukweli na hakuna anayesema uongo! Ukweli ni kuwa Jundu aliteuliwa kipindi cha Mkapa na si hiki cha Jakaya but ni mwishoni kabisa so it could be less than 5 years ago. Cha muhimu hapa ni kuwa ana muda mfupi katika ujaji. Nakumbuka kituo chake cha kwanza kilikuwa Moshi na alikuwa chini ya Jengafibili Mwaikugile ambaye sasa atakuwa chini yake.

Ok.. tukubaliane kuwa alikuwa Wakili wa kujitegemea miaka mitano iliyopita. Watu wakisoma majibu yangu mara zote nimetumia qualification kwa maana ya kwamba info zaidi zikipatikana itasahihishwa. Sasa watu wamefikia kuitana waongo.. kwa sababu tarehe ya uwakili wake haikuwekwa definite.

Jamani msome basi kilichoandikiwa! wengine tunatumia maneno vizuri sana tukitaka kumaanisha tunachotaka kusema tunakisema hivyo hivyo.

Nimesema kwenye taarifa ya kwanza "kama mwaka mmoja"

nilipomjibu Jmushi nikasema "exactly! as far as I know"..

wakosoaji na wanaopenda ligi zisizo na ulazima hawajui maana ya "kama" au "as far as I know"!.


Na waungwana wakikuambia ulisema uongo, mwerevu hujitokeza na kusema kweli nilipotosha. Jobo kajitokeza na kusema, kuwa hakuna aliyesema ukweli na wakati huohuo anasema hakuna aliyesema uongo. Nikamuelewa kuwa alighafirika, lakini kwa Jobo kweli data zake zilikuwa kiasi fulani ni tangible. Manake kaonesha huyu jamaa aliteuliwa wakati wa Mkapa. Lakini za Mwanakijiji, sina neno la kutumia nisijeambiwa narudia lilelile (muongo), manake anasema alikuwa wakili kama mwaka mmoja uliopita ndio akateuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Hili la Mwanakijiji ndio ulikuwa upotoshaji mkubwa kiasi watu tukaanza kujadili kitu ambacho si cha kweli, sasa jee kweli tukubali kuwa tunajadili mawazo ya watu wanaoandika kwa makusudi wasiyoyajua. Hapana hatuendi hivyo, ukipata habari bora useme ni tetesi, ama nasikia hata mwaka hajatimiza katika ujaji. Basi kama ingeandikwa kwa kuhisi nisingesema kuwa kuna kudanganyana.

Kwa niaba yangu, na kwa niaba ya Mke wangu ambaye anasoma posts zangu, NAPENDA KUCHUKUA FURSA HII KUWAOMBA SAMAHANI WAKUU MWANAKIJIJI NA JOBO kwa kusema kati yao kuna MUONGO. Lakini pia kwakuwa sipendi mambo ya kuzusha, kusema jambo lisilo kweli, kujipendekeza nk, nasema hivi WOTE WANAOITUMIA JF KAMA ENEO LAO LA KUZUSHA MAMBO HAWAFAI. Wajirekebishe ili tuweze jadili mambo yaliyo na ukweli, kama huna lakuandika bora kukaa kimya. Nilivyo sitasita kumuweka sawa mtu yoyote anayezungumza lisilo la kweli.

NB: Napata tatizo, niliandika ilipotuma imepote, sijui wengine mnapata hayo matatizo, halafu nikawa JF haipatikani kabisa.
 
wenzako huwa hawajiumu maneno, ukimuona mtu mwongo unamwita mwongo. Katika kufanya hivyo unaonesha kuwa mtu huyo alikuwa anajua ukweli wa kile anachosema na kwa makusudi ameamua kupotosha kwani uongo hauwezi kuwa uongo hadi ijulikane kuwa ukweli ulikuwa unajulikana.

Ukimuona fisadi usisite kumwita fisadi kama unauhakika kuwa vitendo vyake vinalingana na vile vya kifisadi. Ukimuona mwongo, na unajua kuwa ni mwongo (kwa sababu anajua ukweli lakini kauficha) basi usisite kumwita mwongo.

Usinipangie, mimi sio mtu wa kujiuma uma, nakupa pongezi panapostahili, na nakurekebisha unapokosea. Na hili ni kwa yoyote. Huwezi kama mwandishi kama bado unatafuta taarifa useme kuwa Jaji Jandu alikuwa wakili kama mwaka mmoja uliopita ndio akateuliwa kuwa Jaji. Si uwandishi huo eti, ungetwambia tu "Kikwete kamteua Jandu kuwa Jaji Kiongozi", halafu uombe anayemjua zaidi ama mwenye CV yake. Sasa ukishasema kama mwaka mmoja uliopita alikuwa wakili, ina maana unajua kitu fulani, sasa mwaka mmoja ni wakati wa Kikwete, tunaambiwa alichaguliwa wakati wa Mkapa. Huu sio uwandishi, ni upotoshaji ama kutokujiamini. Kwani ukisubiri upate habari kamili utakosa nini?.

[/QUOTE]Kutoa taarifa isiyo sahihi au ambayo si kamili si uongo, kutoa habari ambayo haina details zote au baadhi ya taarifa zake bado zinatafutwa siyo uongo. Uongo kifalsafa nyepesi ni kusema kitu cha kupotosha ilhali ukweli unajulikana.[/QUOTE]

Taarifa yako ilikuwa kamili, unajua usitake kucheza na lugha "kama" mwaka mmoja, ukisema kama mwaka mmoja yaweza kuwa miaka 2 kwa mtazamo wa juu na mwezi 1 mpaka miezi 11 kwa angalizo la chini. Haiwezekani kama mwaka 1 ikawa miaka 3. Hivyo taarifa yako ulitoa kama vile una uhakika. Kwa hiyo ulikuwa na "details" ukazificha ili tujadiliane kwanza ilhali ukiwa kando unaangalia?.
 
Ok.. tukubaliane kuwa alikuwa Wakili wa kujitegemea miaka mitano iliyopita.

Jamani msome basi kilichoandikiwa! wengine tunatumia maneno vizuri sana tukitaka kumaanisha tunachotaka kusema tunakisema hivyo hivyo.

Nimesema kwenye taarifa ya kwanza "kama mwaka mmoja"

Sasa ukiendelea na obfuscations kama hizo utaanza kuonekana mwongo, na mimi nitakuja kukuita mwongo!

Umekubali kwamba alikuwa wakili miaka mitano iliyopita halafu unataka kuanza kuuma uma ulimi na kujitetea kwamba uliposema "kama mwaka mmoja" ilitosha ku qualify kujuimisha miaka mitano.

Toka lini "kama mwaka mmoja" ikawa sawa kukadiria kipindi cha miaka mitano na kusababisha mjadala mrefu kuhusu uzoefu?

Hii stori ya pili mfululizo umeleta hapa imepinda (pamoja na Jamiiforums kufungiwa Chuo Kikuu Dar). Sasa uko kwenye shimo la credibility, cha kwanza cha kufanya ukiwa kwenye shimbo ni kusimamisha kuchimba. Ukijitetea tetea ovyo ovyo ndo utaonekana mwongo.

Habari ulizoleta inaonekana si za kweli, umesema mwenyewe zinaweza kusahihiswa kwa hiyo usisema wanaokusahihisha wanaleta ligi.
 
Hii stori ya pili mfululizo umeleta hapa imepinda (pamoja na Jamiiforums kufungiwa Chuo Kikuu Dar). Sasa uko kwenye shimo la credibility, cha kwanza cha kufanya ukiwa kwenye shimbo ni kusimamisha kuchimba. Ukijitetea tetea ovyo ovyo ndo utaonekana mwongo.

Tatizo lako unachukulia JF kuwa kama Reuters au Associated Press...

Hii ni forum kwa taarifa yako. Kuna kila aina ya habari hapa. Ndio maana namsema kila siku kuna watu wanafanya JF kama sehemu takatifu ya maombezi....kuna wanaoiona JF kuwa kama shule....wengine wanaifanya JF kuwa chombo cha habari....wengine tuko hapa kuzuga tu na hatupandwi na jazba tunapokuja kubaini makosa ktk mada fulani au habari fulani.

Mwenzetu wewe uko kwenye Galaxy nyingine kabisa.
 
Lakini za Mwanakijiji, sina neno la kutumia nisijeambiwa narudia lilelile (muongo), manake anasema alikuwa wakili kama mwaka mmoja uliopita ndio akateuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.

sasa hapa muongo ni nani? sijasema hivyo!

Hili la Mwanakijiji ndio ulikuwa upotoshaji mkubwa kiasi watu tukaanza kujadili kitu ambacho si cha kweli,

Mimi sihusiki na watu wanavyojadili kitu ambacho sijasema. Watu wana akili timamu na wanaweza kujadili chochote wanachotaka kujadili.

Basi kama ingeandikwa kwa kuhisi nisingesema kuwa kuna kudanganyana.

Ungesoma kilichoandikwa usingelazimika kujikuta unasema kitu ambacho si kweli.
 
Usinipangie, mimi sio mtu wa kujiuma uma, nakupa pongezi panapostahili, na nakurekebisha unapokosea.

Ndiyo maana naita kujiuma uma.

Na hili ni kwa yoyote. Huwezi kama mwandishi kama bado unatafuta taarifa useme kuwa Jaji Jandu alikuwa wakili kama mwaka mmoja uliopita ndio akateuliwa kuwa Jaji.

Angalia nilichosema!

Si uwandishi huo eti, ungetwambia tu "Kikwete kamteua Jandu kuwa Jaji Kiongozi", halafu uombe anayemjua zaidi ama mwenye CV yake. Sasa ukishasema kama mwaka mmoja uliopita alikuwa wakili, ina maana unajua kitu fulani, sasa mwaka mmoja ni wakati wa Kikwete, tunaambiwa alichaguliwa wakati wa Mkapa. Huu sio uwandishi, ni upotoshaji ama kutokujiamini. Kwani ukisubiri upate habari kamili utakosa nini?.

Hapa unapointi, habari niliyoipokea mimi kutoka kwenye hiyo source ndiyo ilisema hivyo. Chanzo hicho bila ya shaka na chenyewe hakikuwa na uhakika wa muda wa ujaji lakini details nyingine hazikuwa sahihi kabisa kama zinavyoonekana na kusahihishwa.




Taarifa yako ilikuwa kamili, unajua usitake kucheza na lugha "kama" mwaka mmoja, ukisema kama mwaka mmoja yaweza kuwa miaka 2 kwa mtazamo wa juu na mwezi 1 mpaka miezi 11 kwa angalizo la chini. Haiwezekani kama mwaka 1 ikawa miaka 3.

Hiyo ndiyo maana kwa sababu ningekuwa na uhakika nisingetumia neno "kama".

Hivyo taarifa yako ulitoa kama vile una uhakika. Kwa hiyo ulikuwa na "details" ukazificha ili tujadiliane kwanza ilhali ukiwa kando unaangalia?.

Hakukuwa na details nyingine zaidi ya hizo. Sasa kuficha kati ya mwaka mmoja au vinginevyo inasaidia nini.
 
..orodha ya Majaji wa Mahakama Kuu. hii siyo the most recent. it could be about two years old. source yangu ni Tanganyika Law Society.

Mh. Jaji Amiri Ramadhani Manento.... Jaji Kiongozi

2 J.1 Mh. Jaji Joseph E.C. Masanche... Mfawidhi, Dodoma

3 J.2 Mh. Jaji Lawrence B. Mchome... Mfawidhi Iringa

4 J.3 Mh. Jaji Josephat Mabondya Mackanja... Mfawidhi, Mwanza

5 J.4 Mh. Jaji Ernest K. Mwipopo... Mfawidhi Kazi DSM

6 J.5 Mh. Jaji Anthony Crisant Mrema... Mahakama Kuu Mbeya

7 J.6 Mh. Jaji Dr. Steven James Bwana... Mfawidhi Arusha

8 J.7 Mh. Jaji Donasian Marwa Mwita... Mfawidhi, Tabora

9 J.8 Mh. Jaji Bernard Michael Luanda... Mfawidhi, Biashara DSM

10 J.9 Mh. Jaji Mary Harriet Chibibi Stella Longway... Mfawidhi Ardhi DSM

11 J.10 Mh. Jaji Juxton Isaac Mlay... Mahakama Kuu DSM

12 J.11 Mh. Jaji Simon B. Lukelelwa... Mfawidhi, Mbeya

13 J.12 Mh. Jaji William Stephen Mandia... Mahakama Kuu DSM

14 J.13 Mh. Jaji Semistocles Simon Kaijage... Mfawidhi, DSM

15 J.14 Mh. Jaji Emilian Matata Ezekiel Mushi... Mkuu wa Chuo, LJA

16 J.15 Mh. Jaji Katherine Kimathi Oriyo... Mahakama Kuu DSM

17 J.16 Mh. Jaji Bethuel Mpakani Kasefu MmiIla... Mfawidhi Sumbawanga

18 J.17 Mh. Jaji Njengafibili M. Mwaikugile... Mahakama Kuu DSM

19 J.18 Mh. Jaji Salome S. Kaganda... Mfawidhi, Songea

20 J.19 Mh. Jaji Projest A. Rugazia... Mahakama ya Ardhi

21 J.20 Mh. Jaji Raziabegum H. Sheikh... Mahakama Kuu Arusha

22 J.21 Mh. Jaji Salum A.L. Massati... Mahakama ya Biashara

23 J.22 Mh. Jaji Augustine F. Shangwa... Mahakama Kuu DSM

24 J.23 Mh. Jaji Thomas Bashite Mihayo... Mahakama Kuu DSM

25 J.24 Mh. Jaji Fakihi Abdallah Rhino Jundu... Mfawidhi, Moshi

26 J.25 Mh. Jaji Mariam Simbo Shangali... Mfawidhi Mtwara

27 J.26 Mh. Jaji Regina M. Rweyemamu... Mahakama kuu Mwanza

28 J.27 Mh. Jaji Mussa Kipenka... Mfawidhi Bukoba

29 J.28 Mh. Jaji Richard E.A. Mziray... Mahakama Ardhi DSM

30 J.29 Mh. Jaji Sauda Mjasiri... Mahakama Biashara

31 J.30 Mh. Jaji Mohamed Chande Othman... Mahakama DSM

32 J.31 Mh. Jaji Augustine Gherabast Mwarija... Mahakama Kuu DSM

33 J.32 Mh. Jaji Augustine Alex Mtana Shayo... Mahakama Kuu Tanga

34 J.33 Mh. Jaji Sekieti Suleiman Said Kihiyo... Mahakama Kuu Tabora

35 J.34 Mh. Jaji Geofrey Paul Shaidi... Mahakama Kuu DSM

36 J. 35 Mh. Jaji Robert Vincent Makaramba... Mahakama Kuu DSM

37 J. 36 Mh. Jaji Gad John Kimweri Mjemmas... Mahakama Kuu Mtwara

38 J. 37 Mh. Jaji Frederick Mwita Werema... Mahakama Kuu Iringa

39 J. 38 Mh. Jaji Laurence Mbasha Kuhirwa Uzia... Mahakama Kuu Songea

40 J. 39 Mh. Jaji Agathon Alois Nchimbi... Mahakama Kuu Sumbawanga

41 J. 40 Mh. Jaji Noel Peter Zaudin Chocha... Mahakama Kuu Arusha

42 J. 41 Mh. Jaji Alice Flora Chinguwile... Mahakama Kuu Tabora

43 J. 42 Mh. Jaji Aisheli Nelson Marko Sumari... Mahakama Kuu Mwanza

44 J. 43 Mh. Jaji Aisha Charles Nyerere... Mahakama Kuu DSM

45 J. 44 Mh. Jaji Stella Esther Augustine Mugasha... Mahakama Kuu Moshi

46 J. 45 Mh. Jaji Imani Daud Aboud... Mahakama Kuu DSM

47 J. 46 Mh. Jaji Kakusulo Mwakipombe Mbutolwe Sambo... Mahakama Kuu DSM

48 J. 47 Mh. Jaji Shabani Ally Lila... Mahakama Kuu Dodoma

49 J. 48 Mh. Jaji Amiri Rajabu Mruma... Mahakama Kuu DSM

50 J.49 Mh. Jaji Aloyisius Kibuuka Mujulizi... Mahakama Kuu Tabora

51 J.50 Mh. Jaji Mwanaisha Athuman Kwariko... Mahakama Kuu Dodoma

52 J.51 Mh. Jaji Vicent Kituio Damian Lyimo... Mahakama Kuu Bukoba


..Majaji wa Mahakama ya Rufaa.

1 Mh. Jaji Mh. Jaji Augustino S.L. Ramadhani Jaji Mkuu

2 JR.1 Mh. Jaji Damian Z. Lubuva

5 JR.2 Mh. Jaji John A. Mroso

6 JR.3 Mh. Jaji Eusebia Nicholaus Munuo

7 JR.4 Mh. Jaji Harold Reginald Nsekela

8 JR.5 Mh. Jaji January Henry Msoffe

9 JR.6 Mh. Jaji Simon N. Kaji

10 JR.7 Mh. Jaji Edward Mukandara Kakwezi Rutakangwa

11 JR.8 Mh. Jaji Engera Arnold Kileo

12 JR.9 Mh. Jaji Nathalia Philip Kimaro

13 JR.10 Mh. Jaji Laurean Butulaniza Kelegeya

14 JR.11 Mh. Jaji Mbarouk Salim Mbarouk

..kuna mchangiaji anaweza kutueleza kwanini Majaji wa Mahakama ya Rufaa wameorodheshwa kama # 1,2,5,6..14? kwanini hakuna # 3 na 4?
 
Last edited:
sasa kwa kumsaidia rais itabidi teuzi nyeti kama........jaji mkuu, mkuu wa majeshi,mkuu wa polisi ,mkuu wa usalama,mkurugenzi wa takukuru,magereza,jkt,na viongozi waandamizi wengine wakiwamo majemedari mbali mbali na wakurugenzi wa makampuni nyeti ya umma ..wanapoteuliwa wawe wanaenda bungeni for QUESTIONING....kama wanavyofanya senate au uingereza ...kabla ya uteuzi kurudishwa kwa rais kwa uidhinishwaji ....au kwa kufikiriwa upya..!
 
Sasa ukiendelea na obfuscations kama hizo utaanza kuonekana mwongo, na mimi nitakuja kukuita mwongo!

sasa wewe ukiniita mimi mwongo, na wewe nitakuita nani? UONGO ni kwa makusudi kuficha ukweli. Well, kati ya mimi na wewe rekodi zetu ziko wazi.

Umekubali kwamba alikuwa wakili miaka mitano iliyopita halafu unataka kuanza kuuma uma ulimi na kujitetea kwamba uliposema "kama mwaka mmoja" ilitosha ku qualify kujuimisha miaka mitano.

Maana yake ya "kama" siyo kujumuisha miaka mitano. Ni kuwa sikuwa na uhakika wa muda aliokuwa Wakili huko nyuma. Sasa ningekuwa na uhakika wa asilimia 100 (kwa kiwango chochote cha miaka) nisingetumia neno "kama".

Toka lini "kama mwaka mmoja" ikawa sawa kukadiria kipindi cha miaka mitano na kusababisha mjadala mrefu kuhusu uzoefu?

Nimeshajibu hapo juu, chanzo kilichotoa taarifa hiyo kwangu ndicho kilichokisikia muda huo. Details za nani ameteuliwa, kutoka wapi na kwenda cheo gani zilikuwa sahihi, kwamba aliyeteuliwa alikuwa ni Wakili kabla ilikuwa sahihi, tatizo lilikuwa kwenye muda siyo mimi wala chanzo kilikuwa na uhakika. Now, if that is a big deal so be it!

Hii stori ya pili mfululizo umeleta hapa imepinda (pamoja na Jamiiforums kufungiwa Chuo Kikuu Dar).

As usual.. you don't read what actually was written! Ungekuwa unasoma wala usngekuwa unapata shida hizi.

Sasa uko kwenye shimo la credibility, cha kwanza cha kufanya ukiwa kwenye shimbo ni kusimamisha kuchimba. Ukijitetea tetea ovyo ovyo ndo utaonekana mwongo.

Hilo shimo nimeingia mara nyingi sana na miongoni mwa vitu ambavyo siogopi kuingia. Uzuri wake ni kuwa masterfully and incredibly I know how to get myself out of it in the amazement of my perpertual and sworn critics.. it is what make the man. So, don't try too hard kwa sababu when it comes to credibility, you have no standing.

Habari ulizoleta inaonekana si za kweli, umesema mwenyewe zinaweza kusahihiswa kwa hiyo usisema wanaokusahihisha wanaleta ligi.


once again, you don't get it. Habari nilizoleta zina ukweli!

a. Jaji Fakihi ameteuliiwa kuwa Jaji Kiongozi - it is not true according to you
b. Jaji Fakihi ametokea Iringa akiwa Mahakama Kuu - It is not true according to you
c. Jaji Fakihi alikuwa wakili wa kujitegemea - not true
d. Imemchukua muda mfupi tangu kuwa Jaji wa Mahakama Kuu hadi kuwa Jaji Kiongozi - Not true

then if that is the case, truth has lost its meaning! Ninachokubali na kitu ambacho mtu yeyote anaweza kukiona ni kuwa sehemu ya habari niliyoleta haikuwa sahihi. Kitu kutokuwa sahihi haina maana ni uongo. I need to teach philosophy, for real!
 
Mheshimiwa Kuhani, tuliza boli ama sivyo utafungwa magoli mengi na Mwana Kijiji ameyaeleza aliyokufunga. Under normal procedure Jaji Fakih amepungua viwango vya uteuzi. Kwa heshima yake hatutaki tulete mengi hapa kukuhakikishia wewe usiyeamini, unayeacha ujumbe na kumshambulia mjumbe.
 
nafikiri ile ni typo error kwenye serial number lakini namba za ujaji ziko sawa zenyewe zimeandikwa JR1, JR2 etc
 
nina tatizo la mtandao, samahani post zinajirudia, sio kusudio langu na sioni nitaziondoaje.
 
..Majaji wa Mahakama ya Rufaa.

1 Mh. Jaji Mh. Jaji Augustino S.L. Ramadhani Jaji Mkuu

2 JR.1 Mh. Jaji Damian Z. Lubuva

5 JR.2 Mh. Jaji John A. Mroso

6 JR.3 Mh. Jaji Eusebia Nicholaus Munuo

7 JR.4 Mh. Jaji Harold Reginald Nsekela

8 JR.5 Mh. Jaji January Henry Msoffe

9 JR.6 Mh. Jaji Simon N. Kaji

10 JR.7 Mh. Jaji Edward Mukandara Kakwezi Rutakangwa

11 JR.8 Mh. Jaji Engera Arnold Kileo

12 JR.9 Mh. Jaji Nathalia Philip Kimaro

13 JR.10 Mh. Jaji Laurean Butulaniza Kelegeya

14 JR.11 Mh. Jaji Mbarouk Salim Mbarouk

..kuna mchangiaji anaweza kutueleza kwanini Majaji wa Mahakama ya Rufaa wameorodheshwa kama # 1,2,5,6..14? kwanini hakuna # 3 na 4?[/QUOTE]

kwa mujibu wa sheria si inatakiwa wawe 15? au pungufu inakubaliwa ila wasizidi 15? mana hawa wako 12 ukimuhesabu na jaji mkuu
 
Jaji Kajji sasa ni marehemu. Jaji Massati anayeonekana katika orodha ya majaji wa mahakama kuu, ameishateuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa. Nadhani kuna nafasi ziko wazi au kuna majaji wanaonekana kwenye orodha ya mahakama kuu lakini wameishateuliwa kuingia rufaa.
 
MawazoMatatu, baija bolobi,

..naamini Tanganyika Law Society waliandaa orodha hiyo mara baada ya uteuzi wa Augustino Ramadhani kuwa Chief Justice.

..baada ya uteuzi huo Raisi aliwapandisha ngazi kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufaa Jaji Chande, Jaji Masati, na mwingine simkumbuki.

..nadhani kwa sasa hivi idadi ya Majaji wa Mahakama ya Rufaa imetimia.

NB:

..tangu orodha hiyo itoke, Jaji Masati amepandishwa kuwa Jaji Kiongozi, na baadaye Jaji wa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania.
 
Mheshimiwa Kuhani, tuliza boli ama sivyo utafungwa magoli mengi na Mwana Kijiji ameyaeleza aliyokufunga. Under normal procedure Jaji Fakih amepungua viwango vya uteuzi. Kwa heshima yake hatutaki tulete mengi hapa kukuhakikishia wewe usiyeamini, unayeacha ujumbe na kumshambulia mjumbe.

Mimi nisiyeamini? Huyo unaemtetea unajua alichosema mwishoni lakini au unatishwa tu na profile?

Posted by Mzee Mwanakijiji:
Ninachokubali na kitu ambacho mtu yeyote anaweza kukiona ni kuwa sehemu ya habari niliyoleta haikuwa sahihi.``

Kwa hiyo wewe Baija Bolobi hata hujui unachokiongelea, ngoja niku bypass. Turudi kwa chanzo cha habari chenyewe, Mwanakijiji.

Waungwana, wengi mmeonyesha maturity and humility kwa kusema kwamba mtu akikosea haina maana ni mwongo, sawa kabisa, lakini wakuu, sikieni: Ndugu yetu Mwanakijiji anasema kwamba, akisema "kama mwaka mmoja" hiyo ni disclaimer inayotosha kujuimisha miaka mitano!

You get that? Kwa lugha ya hisabati, arithmetics, huu ni uwiano wa moja kwa tano. Kwamba siku ikitokea Fulani bin Fulani ana uzoefu wa kazi wa miaka 10, tuseme, Mwanakijiji anaweza kutuletea taarifa akisema "Fulan bin Fulani amekuwa kiongozi kama miaka miwili" halafu baadae ukweli ukijulikana ataanza kuhalalisha hilo potofu kwa kigezo kwamba aliweka neno "kama." Moja kwa tano ni sawa na mbili kwa kumi, na moja inawiana na tano! Na, neno "kama" ukishaliweka basi uko huru kusema chochote kile!

Waungwana, huyo mtu anaefikiri hivyo hawezi kuonekana kama anafanya makusudi?
 
Back
Top Bottom