Ndiyo maana naita kujiuma uma.
Hapa unapointi, habari niliyoipokea mimi kutoka kwenye hiyo source ndiyo ilisema hivyo. Chanzo hicho bila ya shaka na chenyewe hakikuwa na uhakika wa muda wa ujaji lakini details nyingine hazikuwa sahihi kabisa kama zinavyoonekana na kusahihishwa.
Mwanakijiji, mimi sijiumiumi wewe, soma maelezo yangu vizuri. Hivi huwa kila kitu unachokipokea unakichukua kama kilivyo. Huwezi hata kuulizia kando. Mimi suala linabaki palepale kuwa UMEPOTOSHA, sitaki tumia lile neno ambalo Mkuu SMU kaniambia kuwa sijui sio la kistaarabu, nimemuomba neno la mtu anayedanganya hajajibu.
Rais Kikwete amemteua Jaji Fakihi Jandu kutoka Mahakama Kuu Iringa kuwa Jaji Kiongozi mpya kuchukua nafasi ya Jaji Salum Massati ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa.
Jaji Jandu alikuwa Wakili wa kujitegemea kama mwaka mmoja uliopita hadi alipoteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu na sasa kuwa Jaji kiongozi..
Hapa ndio kwenye tatizo, mtu makini huwezi ambiwa tu jambo na kulichukua bila hata kudodosa. Ungekuwa makini hata huyo jamaa aliyekupa hizi habari ungemuliza inakuwaje ateuliwe kuwa JK wakati ana muda mfupi kama wa mwaka mmoja tangu awe Jaji?. Majibu ya huyo jamaa yangekufanya nawe pamoja na yeye kutafakari, baada ya kutafakari mngeamua kutafuta habari zaidi. Lakini inaonekana ukipata tu habari unataka ujiweke wewe ndio "SOURCE" ya hiyo habari. Habari ni vizuri kuweka "source" yake, mfano unasema imetoka Majira, Michuzi nk. Sasa uliripoti kama wewe ni msemaji wa Ikulu (Rweyemamu) ama Katibu Mkuu Kiongozi (Luhanjo). Huo sio uwandishi. Ama umekuwa Mkurugenzi wa Idara ya habari Maelezo?.
Kinachokuponza ni kutaka kila kitu uonekane wewe ndio wa mwanzo, habari haziendi hivyo, ungekuwa uko Ikulu ningesema sawa. Kwa habari yako ungesema kutokana na jamaa aliyenifahamisha masaa machache yaliyopita, Kikwete kateua JK, na huyo JK mpya alikuwa Wakili wa kujitegemea kama mwaka mmoja uliopita hadi alipoteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu na sasa kuwa Jaji kiongozi. Hapa tungejua hii habari umeisikia ama umeipata kwa mtu.
Tatizo lingine hupendi kuambiwa ukweli, na waliokuzunguka wanakusifia tu hawakwambii ukweli (hadithi ya Mfalme aliye uchi, na wapambe wanamshangilia kapendeza). Sasa mimi siko hivyo, siwezi sifia kitu kina makosa.