JK amteua Jaji Kiongozi mpya

Ndio, inatokea sana hasa kwenye 'majeshi' (polisi, magereza, jwtz nk). Nadhani pia ni lazima tukumbuke issue ya performance kwenye nyadhifa uliyopo. Kama mtu ana poor performance sidhani kama ni busara kumopandisha cheo kwa sababu tu ni senior! Hili lipo hata kwenye sector binafsi - mtu wa chini anaweza kupanda vyeo kuwazidi hata wale waliokuwa senior kwake kama anaonesha good performance.

Hata hivyo lazima nikiri kwamba sina information kuhusu performance ya huyo JK mpya na wala wale ambao inaonekana 'wameachwa'.

that exactly the point.. kama una jaji ambaye hana perfomance nzuri au kazi yake haiendani na majukumu yake kuna taratibu za kumuondoa Jaji (impeach) (of course Rais hawezi kumfukuza jaji kazi). Lakini kumruka Jaji mzembe au asiyetimiza wajibu yake ndiyo yale waswahili wanasema "yale yale"..
 
Ndio, inatokea sana hasa kwenye 'majeshi' (polisi, magereza, jwtz nk). Nadhani pia ni lazima tukumbuke issue ya performance kwenye nyadhifa uliyopo. Kama mtu ana poor performance sidhani kama ni busara kumopandisha cheo kwa sababu tu ni senior! Hili lipo hata kwenye sector binafsi - mtu wa chini anaweza kupanda vyeo kuwazidi hata wale waliokuwa senior kwake kama anaonesha good performance.

Hata hivyo lazima nikiri kwamba sina information kuhusu performance ya huyo JK mpya na wala wale ambao inaonekana 'wameachwa'.

Mkuu, hapo inabidi kuwa mwangalifu. Kama kuna majaji wanaofikia 50 hivi na JK anamchukua mtu ambaye yuko below 20, unaweza kuelezeaje performance ya hao 1-20? Ni ujumbe gani anaowatumia hao ambao labda inaonekana kama wana poor performance? Nahisi kuna mwangwi mkubwa kwenye hili zaidi ya haya tunayoweza kuyaona kwa macho ya kawaida.
 
Vizuri kuhoji,lakini pia inatakiwa tuelewe mtu anayeteuliwa ujaji anatakiwa kuwa na sifa gani.
Jani lazima awe na degree ya kwanza ya sheria LLB na awe na uzoefu wa kutosha katika mambo ya kisheria(mahakama,uwakili na mambo yanayohusiana na hayo).
So jamaa naona anaqualify. Mwanakijj hajasema jamaa ana uzoefu wa miaka mingapi ya uwakili.Labda akisema hilo tunaweza kujadili vizuri.
Suala jingine, watu wanaostahili kuwa majaji ni wengi kwenye soko kuliko uwezo wa kuwaabsorb. Kama tunakumbuka Kikwete alisema atajitahidi kuwe na majaji wengi zaidi ili kesi ziamuliwe mapema kuliko kuwaacha watu waendelee kusota rumande muda mrefu.
Naomba kuwasilisha.
 
ina maana anamnyima haki yake au kile anachostahili kwa sababu ya umri wake? Kwanini basi asimuombe astaafu tu kuliko kumuacha aone jinsi anavyorukwa!?

Mzee,
Kwa Tanzania teuzi za Rais ingawa sio takwa la KIKATIBA mara nyingi linazingatia "busara" zake yeye mwenyewe. Mara nyingi naona wanazingatia DINI zetu kuu mbili. Na hili limezingatiwa zaidi kwenye awamu hii ya nne kuliko wakati mwingine wowote. Mkuu wa Majeshi (CDF) mkristo, msaidizi wake (CoS) mwislamu, Jaji Mkuu mkristo, Jaji Kiongozi mwislamu. Hata baraza la mawaziri limeangalia dini na mikoa!
Kwa kuwa hatuna chombo kingine kinachoangalia/thibitisha teuzi hizi, tutaendelea kuona miujiza kama hii ya Jaji Kiongozi muda mrefu ujao!
 
Wakuu yote mnayosema yanawezekana kuwa na ukweli ndani yake e.i utendaji wa kazi, umri wa kumstaafu e.t.c

Ila kitu kimoja mmekisahau, naona Rais JK alikuwa anataka kuweka "fresh ideas" kwenye system ya mahakama zetu ndio maana akaangalia nje ya system kwenye uteuzi wake.
 
ina maana anamnyima haki yake au kile anachostahili kwa sababu ya umri wake? Kwanini basi asimuombe astaafu tu kuliko kumuacha aone jinsi anavyorukwa!?

Mzee Mwanakijiji,
Nadhani unaelewa sana mambo haya kwamba ukirukwa maana yake ni nini? Kimsingi katika dunia iliyoendelea ukirukwa na kama unaona hukustahili kurukwa basi unajiondoa.
Anyway kwa issue hii ya majaji sidhani kwamba kwenye ajira zao kuna mahali panasema kuwa uteuzi ni lazima uende kwa seniority. Ladba mazoea ndiyo yanayotupelekea kufikiria hivyo. Kumbuka hata kiti cha urais nacho kilikuwa kinaonekana kana kwamba ni cha kupokezana kati ya Bara na Visiwani, lakini hakuna mahali palipoandikwa.
Vilevile seniority si kwamba inakupa uhakika wa kufanya kazi kama inavyotajiwa ukizingatia kuwa Jaji Kiongozi ana majukumu mengi ambayo si ya kawaida kama walivyozea majaji wa kawaida. Kwa maana hiyo basi uwezo wa kusimamia mahakama kuu unaweza kutofautiana toka jaji mmoja kwenda mwingine.
 
Mkuu, hapo inabidi kuwa mwangalifu. Kama kuna majaji wanaofikia 50 hivi na JK anamchukua mtu ambaye yuko below 20, unaweza kuelezeaje performance ya hao 1-20? Ni ujumbe gani anaowatumia hao ambao labda inaonekana kama wana poor performance? Nahisi kuna mwangwi mkubwa kwenye hili zaidi ya haya tunayoweza kuyaona kwa macho ya kawaida.

Kwa uelewa wangu katika teuzi ambazo Rais anafanya, mara nyingi hupelekewa majina kadhaa (say matano) ya watu wanao-qualify kwa nafasi husika. Majina haya mara nyingi huandaliwa na taasisi husika na kupelekwa kwa Rais kwa uteuzi wa mwisho. Kwa mfano, inawezekana kabisa Rais alipelekewa majina matano ya watu ambao wanaweza kuchukuwa nafasi ya Jaji Kiongozi pamoja na CV zao(including their performance).

Ninachotaka kusema hapa ni kwamba kwa kawaida Rais hawezi kukurupuka tu na kumteua mtu (kwa sababu yeye binafsi hawafahamu watu) ni lazima kuna mchakato/mchujo ambao unaanzia ngazi za chini kidogo. Nimeshuhudia utaratibu huu kwenye uteuzi wa Vice Chancellors wa vyuo vikuu vya umma ambapo Rais anafanya uteuzi wa mwisho lakini kutoka miongoni mwa orodha ya majina yaliyowasilishwa kwake na chuo husika.

Sasa kama kwa mfano 'the judiciary system' yenyewe wameombwa wapeleke majina matano na la huyo bwana likawemo, naamini ana sifa zinazokubalika kuwashinda hao walioachwa.

Hata hivyo nakubaliana na wewe kwamba Tanzania 'lolote' linawezekana. 'Mawingu' yametanda kila mahali!
 
Wanasiasa mnaingilia uhuru wa mahakama? tutaongea sana hapa bila jibu lakini bado jambo ambalo litatupa mwanga ni CV yake ipatikane hapa kwanza including dini, kabila, chama gani etc kwani tusifiche ukweli huo ndiko tunakoelekea!
 
MKJJ nilikuwa nina swali especially kwenye highlight nyekundu...Je ulimaanisha kuwa Jaji Faki Jandu alikuwa wakili hadi mwaka jana ndio akapewa ujaji mkuu na mwaka huu(sasa) akapewa ujaji kiongozi? Je ina maana chini ya mwaka mmoja amepanda ngazi zote mbili toka alipokuwa wakili wa kujitegemea? If thats the case nina mashaka na madhumuni ya teuzi hizi....Tangu huu mtiririko wa kina Hosea,DPP na Chenge bila kusahahu mkemia mkuu.
Samahani kama nimetoka nje ya mada ila kuhusu hilo la Jaji kiongozi lina utata hapo kwenye kasi ya kupandishwa vyeo.

Kwa mujibu wa sheria wakili wa kujitegemea anaweza kuwa jaji,lakini uangalifu unatakiwa katika kuteua jaji ni vema yule ambaye amepractice kama hakimu ( Resident Magistrate ) kwa muda mrefu akapewa uprioprity,wakili aliyedumu katika ujaji kwa mwaka mmoja tu kupewa uongozi katika majaji wa mahakama kuu nafikiri kuna agenda ya kisiasa hapa. Ni kweli kikwete ana haki ya kuangalia upepo wa kisiasa lakini kwa hili mmmm, kuna majaji wengi tu walianza kazi hiyo kabla ya huyo Jandu je walifikiriwa? jibu anajua mwenyewe.
 
Sheria inasema jaji anateuliwa na Rais so, njia pekee ya kumuondoelea hii nguvu ni kubadili sheria. Hata hivyo suala la majaji karibu nchi zote duniani zinamuachia Rais au mkuu wa Nchi uwezo huo. Labda tuangalie kuwa jinsi gani akishamteua mtu basi mtu huyo athibitishwe na Bunge..

Mkuu MM

Kuthibitishwa na bunge itakuwa ndio BUSARA HALI YA JUU kuthibiti uteuzi wa viongozi wanaoteuliwa Direct na Presidwaaa.

Thnx
 
Wanasiasa mnaingilia uhuru wa mahakama? tutaongea sana hapa bila jibu lakini bado jambo ambalo litatupa mwanga ni CV yake ipatikane hapa kwanza including dini, kabila, chama gani etc kwani tusifiche ukweli huo ndiko tunakoelekea!

kwa misingi na taratibu zilizowekwa na wajenzi wa taifa hili CV ya mheshimiwa jaji mkuu haina sababu yeyote ya kuonesha kabila, dini au chama chake. Ni ajabu kuona watu ambao ungetegemea wangekuwa wanatetea usawa bila kujali dini, kabila wala rangi wanakuwa wa kwanza kuhoji dini ya kiongozi mmoja aliyeteuliwa na rais, kisa jina lake lina muelekeo wa dini fulani ambayo wanadhani hawana haki ya kushika nafasi fulani fulani. Kwa bahati mbaya wengi wao wanaheshima kubwa hapa JF hivyo kuhofia kuchafua CV zao wanajenga hoja vivuli ili kupenyeza ajenda zao za udini. Sote tunafahamu fika hoja ya seniority katika uteuzi ilivyo dhaifu lakini wakulu hapa wameifanya kuwa ndio hoja ya msingi. Hata mbumbumbu mzungu wa reli angeweza kufahamu kuwa seniority ni moja ya vigezo tu na wala sio 'sole' kigezo.Ushauri wangu ni kwamba upepo unapoelekea tunapafahamu leteni tu hiyo hoja yenu ya dini tujadili wazi badala ya kuificha chini ya mwavuli wa uzoefu(ambao hamna ushahidi wa kutosha) na seniority(sina mengi juu ya hoja hii)
 
Aah, yaelekea hii ni recent development kwa nafasi ya JK kutengwa "maalum" kwa ajili ya majaji waislam,. Tukianzia na Amir Manento, akafuatiwa na Salum Massati na sasa Fakihi Jundu.Hii imeanza kujitokeza katika utawala wa awamu hii, ndiyo sababu wanapewa nafasi hiyo huku wakiwa hawana uoefu wa kutosha. Matokeo yake majaji waliopo ambao ni "senior" kuliko Jundu kamwe hawawezi kuheshimu maamuzi yake, naye pia anawagwaya.
KITONZEGU
 
Wanasiasa mnaingilia uhuru wa mahakama? tutaongea sana hapa bila jibu lakini bado jambo ambalo litatupa mwanga ni CV yake ipatikane hapa kwanza including dini, kabila, chama gani etc kwani tusifiche ukweli huo ndiko tunakoelekea!

Mimi siyo mwanasiasa na sina nia ya kuingilia uhuru wa Mahakama. Labda kitu cha kujiuliza ni Jaji Kiongozi ni nani katika Mahakama? JK ndiye kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Bara. Anatarajiwa kuwa the most senior in the rank of judges of the High Court.

Jaji Jundu ameteuliwa kushika wadhifa wa ujaji kama miaka mitano hivi iliyopita akitokea katika Uwakili wa Kujitegemea. Alikuwa na ofisi chovuchovu sana pale Dar na mara chache alikuwa akienda Arusha kufanya kazi katika ofisi za uwakili za Mwale Advocates mara baada ya Wakili JJ Mwale kufariki.

Jaji Jundu ni Mwislamu wa madhehebu ya ...........(siyo sunni) na hicho ndicho kimekuwa kigezo kikubwa cha uteuzi wake kwani Jaji Mkuu wa sasa ni Mkristo wa madhehebu ya Kianglikana (siyo wale wa Marekani).

Ni kweli kuwa seniority haikufuatwa katika uteuzi wake na hii si ajabu kwa teuzi za Kikwete kwani hata Mkurugenzi wa Mashitaka ni kijana na mfupi wa kimo!

Kihistoria, Jaji Kiongozi wa mwisho Mkristo alikuwa Jaji Samatta, miaka mingi iliyopita. Huyu alifuatiwa na Nassoro Mzavas, Jaji Hamis Msumi, Jaji Amir Manento na Jaji Salum Massati. Kwahiyo naomba wanaJF msishangae sana kuwa Jundu kateuliwa.

Sijui sana kuhusu uwezo wake kwani mimi siyo wakili wala sijawahi kuwa mdai, mshitakiwa, mdaiwa au mlalamikaji. Kuhusu uzoefu, msijali, Masati alikuwa Jaji kwa miaka 3 tu kabla ya kuteuliwa, manento miaka minne. wapo pia majaji wa mahakama kuu ambao wameteuliwa wakiwa na umri mdogo kwa sababu ya kutaka usawa wa kidini katika mahakama zetu!

Ninaomba mpunguze mashambulizi kwangu ...sijatoa opinion, just hard facts.
 
Mkuu MM

Kuthibitishwa na bunge itakuwa ndio BUSARA HALI YA JUU kuthibiti uteuzi wa viongozi wanaoteuliwa Direct na Presidwaaa.

Thnx

Itakuwa vile vile ni njia moja ya kupunguza madaraka ya Rais kama maoni ya wengi yanavyotaka. Nadhani madai ya katiba mpya yanabidi yafanywe kwa nguvu mpya .....hapo ndio tutapata nafasi ya kuweka mawazo yetu.
 
Hivi Jaji Josephat Makanja wa Mahakama Kuu mwenye uzoefu wa miaka 20 akiwa jaji alishastaafu?????!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Hivi Jaji Josephat Makanja wa Mahakama Kuu mwenye uzoefu wa miaka 20 akiwa jaji alishastaafu?????!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Bado! Nadhani ameongezewa miaka miwili baada ya kufika umri wa kustaafu
 
Ila kitu kimoja mmekisahau, naona Rais JK alikuwa anataka kuweka "fresh ideas" kwenye system ya mahakama zetu ndio maana akaangalia nje ya system kwenye uteuzi wake.

Yebo Yebo. Ni uhamuzi mzuri.

Na hilo alishalifanya kwa kumteua kuwa J kutoka wakili wa kujitegemea.

Sasa ndani ya kipindi kifupi tangu alipoingizwa kuja na 'fresh ideas' amerushwa kuwa JK kutoka miongoni mwa J1-J50! Miongoni mwao very seniour>

Kwa uelewa wangu katika teuzi ambazo Rais anafanya, mara nyingi hupelekewa majina kadhaa (say matano) ya watu wanao-qualify kwa nafasi husika. Majina haya mara nyingi huandaliwa na taasisi husika na kupelekwa kwa Rais kwa uteuzi wa mwisho. Kwa mfano, inawezekana kabisa Rais alipelekewa majina matano ya watu ambao wanaweza kuchukuwa nafasi ya Jaji Kiongozi pamoja na CV zao(including their performance).

Ninachotaka kusema hapa ni kwamba kwa kawaida Rais hawezi kukurupuka tu na kumteua mtu (kwa sababu yeye binafsi hawafahamu watu) ni lazima kuna mchakato/mchujo ambao unaanzia ngazi za chini kidogo. Nimeshuhudia utaratibu huu kwenye uteuzi wa Vice Chancellors wa vyuo vikuu vya umma ambapo Rais anafanya uteuzi wa mwisho lakini kutoka miongoni mwa orodha ya majina yaliyowasilishwa kwake na chuo husika.

Sasa kama kwa mfano 'the judiciary system' yenyewe wameombwa wapeleke majina matano na la huyo bwana likawemo, naamini ana sifa zinazokubalika kuwashinda hao walioachwa.

Hata hivyo nakubaliana na wewe kwamba Tanzania 'lolote' linawezekana. 'Mawingu' yametanda kila mahali!

Inawezekana uko sahihi. Pale TRA Kamishna wa Forodha alimaliza muda wake wa utumishi tangu mwezi juni 2008. Ilipofika November 2008 wakatangaza nafasi hiyo. Uasili ukafanywa lakini mpaka leo hakuna Kamishna wa Forodha pale TRA.
 
Rais Kikwete amemteua Jaji Fakihi Jandu kutoka Mahakama Kuu Iringa kuwa Jaji Kiongozi mpya kuchukua nafasi ya Jaji Salum Massati ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa.

Jaji Jandu alikuwa Wakili wa kujitegemea kama mwaka mmoja uliopita hadi alipoteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu na sasa kuwa Jaji kiongozi.

Jaji Jundu ameteuliwa kushika wadhifa wa ujaji kama miaka mitano hivi iliyopita akitokea katika Uwakili wa Kujitegemea. Alikuwa na ofisi chovuchovu sana pale Dar na mara chache alikuwa akienda Arusha kufanya kazi katika ofisi za uwakili za Mwale Advocates mara baada ya Wakili JJ Mwale kufariki.

Mwanakijiji anasema kama mwaka mmoja uliopita Jandu alikuwa wakili hadi alipoteuliwa kuwa Jaji. Jobo anasema Jandu aliteuliwa kushika wadhifa wa ujaji kama miaka mitano iliyopita. Sasa sijui hapa nani MUONGO.
 
Mimi nadhani hoja ya kuhoji dini ya JK mteuliwa ni pale mtoa hoja aliposhindwa kupata kigezo kilichotumika kumpa cheo hicho mtu ambaye inaonekana miaka miwili/mitatu iliyopita alikuwa hata haoti kuwa hata angekuwa judge! Labda dini ndio kilikuwa kigezo! Siungi mkono hoja za udini lakini kufikiri bila mipaka ni muhimu katika kupata majibu ya maswali magumu! Naamini angewateua kwa mfano issa shivji, harubu othman, palamagamba kabudi, na wengine wanaofanana nao (huu ni mfano tu sina maana ya maprofesa hawa - namaanisha tu watu wenye integrity kama yao) kuwa majaji hilo swali la dini lisingekuwepo! Ila unapomteua mtu asiyejulikana lazima watu wajiulize na ni haki kujiuliza bila mipaka! Tatizo la udini lipo TZ hata JK analisema kila siku, na hii ni sababu tosha ya kutokulikimbia kulijadili.

Wiki haijapita tangu amteue mataka kwenye task force muhimu sasa anakuja tena na uteuzi huu! Next time anaweza kuwa chenge au mkapa na cheo kikubwa - kama sheikh yahya alivyosema! Kweli taifa limepoteza mwelekeo.
 
Back
Top Bottom