Kuhani,
..kwani Julie Manning alipotoka kuwa AG moja kwa moja aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu?
..binafsi sifahamu Mama Manning alikuwa akifanya shughuli gani baada ya kuondoka wizara ya sheria, mpaka Raisi Mwinyi alipomteua kuwa mjumbe wa Tume ya Uchaguzi.
..vilevile sifahamu ni sababu zipi zilizopelekea Mama Manning akaondolewa toka kuwa Waziri wa Sheria na Mwanansheria Mkuu wa Serikali, na nafasi yake kuchukuliwa na Joseph Sinde Warioba.
..hivi kutoka kuwa AG na kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu siyo DEMOTION? vipi kuhusu AG[lubuva] kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa? au DPP[shaidi] kuwa Jaji wa Mahakama Kuu?
NB:
..kama madai ya Jaji Munuo ni kweli, kwamba yeye ndiye mwanamke wa kwanza kuteuliwa Jaji wa Mahakama Kuu, basi inawezekana Mama Julie Manning alikuwa mtaani kwa kipindi fulani kabla naye hajateuliwa kuwa Jaji.
Kuwa jaji wa mahakama kuu kutoka AG ni promotion, na mara nyingi AGs huwa wanateuliwa kuwa majaji na ndicho kitakachotokea kwa Johnson Mwanyika (kama JK akiamua kumwondoa). Lubuva pia alikuwa AG kabla ya kuteuliwa kuwa jaji wa mahakama kuu na baadaye mahakama ya rufaa. Kumbuka uteuzi wa majaji hapo mwanzoni kabla ya sheria haijabadilishwa, ilikuwa kwamba, Rais akimteua jaji hawezi kumfukuza kazi. Kufukuzwa kazi ilikuwa mpaka jopo la majaji kutoka jumuia ya madola wafanye uchunguzi kuhusiana na makosa anayotuhumiwa kwayo, na tume ya jopo hilo ndo lipendekeze kwa rais hatua za kuchukua kama ni kufukuzwa au vinginevyo.
Sheria hii ilifanyiwa mabadiliko miaka ya mwishoni mwa utawala wa Mzee Mkapa. Na kwa sasa rais ana uwezo wa kumfuta kazi jaji yeyote anayemteua.