JK amteua Jaji Kiongozi mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK amteua Jaji Kiongozi mpya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Feb 24, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Feb 24, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Rais Kikwete amemteua Jaji Fakihi Jandu kutoka Mahakama Kuu Iringa kuwa Jaji Kiongozi mpya kuchukua nafasi ya Jaji Salum Massati ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa.

  Jaji Jandu alikuwa Wakili wa kujitegemea kama mwaka mmoja uliopita hadi alipoteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu na sasa kuwa Jaji kiongozi.
   
 2. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #2
  Feb 24, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  Mwanakijiji kweli you are always present! Thanx
   
 3. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #3
  Feb 24, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Kwa nini JK ateue karibu kila mtu???

  hakuna vyombo vingine vya kuteua?
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Feb 24, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Sheria inasema jaji anateuliwa na Rais so, njia pekee ya kumuondoelea hii nguvu ni kubadili sheria. Hata hivyo suala la majaji karibu nchi zote duniani zinamuachia Rais au mkuu wa Nchi uwezo huo. Labda tuangalie kuwa jinsi gani akishamteua mtu basi mtu huyo athibitishwe na Bunge..
   
 5. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #5
  Feb 24, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,594
  Likes Received: 1,982
  Trophy Points: 280
  MKJJ nilikuwa nina swali especially kwenye highlight nyekundu...Je ulimaanisha kuwa Jaji Faki Jandu alikuwa wakili hadi mwaka jana ndio akapewa ujaji mkuu na mwaka huu(sasa) akapewa ujaji kiongozi? Je ina maana chini ya mwaka mmoja amepanda ngazi zote mbili toka alipokuwa wakili wa kujitegemea? If thats the case nina mashaka na madhumuni ya teuzi hizi....Tangu huu mtiririko wa kina Hosea,DPP na Chenge bila kusahahu mkemia mkuu.
  Samahani kama nimetoka nje ya mada ila kuhusu hilo la Jaji kiongozi lina utata hapo kwenye kasi ya kupandishwa vyeo.
   
 6. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #6
  Feb 24, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  hivi rank za majaji sikoje?...unajua kama afande anaanza na koplo,sgt koplo etc hadi kufika kwa rank ya brigedia....and stuff like that...so majaji ndiyo inakuwaje?
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Feb 24, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kuelewa vyeo hivi ni lazima uelewe mtiririko wa mahakama zetu ulivyo..

  a. Mahakama za Mwanzo
  b. Mahakama za Wilaya
  c. Mahakama Maalum (kama Mahakama ya Kazi, Biashara n.k)
  d. Mahakama Kuu (ziko kikanda hizi) na hapa pia kuna mtiririko wa Mahakama ya Kuu ya Zanzibar
  e. Mahakama ya Rufaa (ndiyo Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano ambapo kesi zote za rufaa iwe Zanzibar, Bara, au Majeshi zinatolewa uamuzi wa mwisho ambao hukumu yake haiwezi kukatiwa rufaa mahali pengine popote).

  sasa: Mahakama za Chini zinaongozwa na Mahakimu na wa juu kati yao anakuwa ni Hakimu Mkuu Mkazi (maarufu kati ya mahakama hizo za chini ni hiyo ya Kisutu ingawa mahakama za Hakimu mkazi zipo mikoani vile vile kwa kadiri ninavyojua).

  Mahakam Kuu ina majaji wengi na ndiyo chombo ambacho kinasimamia haki na watu wengi wanaujuzi nao katika maswala ya kawaida. Mkuu wa Majaji wa Mahakama Kuu ndiyo anaitwa Jaji Kiongozi, kutoka kwa Jaji kiongozi ndio utakutana sasa na namba za majaji mbalimbali kama tunavyozifahamu.

  Kikatiba Majaji wa Mahakama Kuu hawatakiwi kupungua 15!


  Majaji wa Mahakama ya Rufaa wako juu ya Majaji wengine kwa hiyo mtu akitoka Ujaji wa Mahakama Kuu (kama Jandu) na akipewa Mahakama ya Rufaa siyo uhamisho tu bali ni kupanda cheo.
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Feb 24, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Sijasema Ujaji Mkuu bali alitoka uwakili na kupelekwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
  exactly! as far as I know

  I would not dare to speculate the motives naamini JK anatimiza wajibu wake wa Kikatiba.
   
 9. DDT

  DDT Member

  #9
  Feb 24, 2009
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 43
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mzee Mwanakjj
  Unaweza kupata CV yake ukaitundika hapa?
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Feb 24, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  itakuwa ngumu kwa upande wangu.. unajua tu nzi huwa hatuingii kwa undani tunagusa juu juu tu halafu huto tunatimka!!
   
 11. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #11
  Feb 24, 2009
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Ni kweli kabisa kama ulivyosema, labda kwa kuelimishana kidogo hasa hapo nilipoweka mkazo mwekundu. Kesi kwenye mahakama ya rufaa husikilizwa na majaji watatu, na hukumu ikitolewa kama hujaridhika na hukumu hiyo, bado unaweza kukata rufaa kwenye mahakama hiyo hiyo ya rufaa, na rufaa yenyewe itakuwa ni kuiomba mahama ya rufaa "as a full bench of the high court". Hapa ina maana majaji wote wa mahakama ya rufaa kwa idadi yao wakae wote na kusikiliza rufaa na kuitolea maamuzi. Baada ya hapo, no more rufaa. Japokuwa rufaa za namna hii ni nadra sana kutokea, imeshawahi kutokea mara chache sana, na kunakuwa na technicalities nyingi sana hadi ikubalike kwa majaji wote wa mahakama ya rufaa kukaa. Pia mahakama ya rufaa inaweza kukaa kupitia hukumu yake yenyewe, na hapa inabidi 'full bench" ikae ili kupitia (to revise its own ruling), hukumu ya mahakama ya rufaa iliyotolewa na majaji watatu.
   
 12. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #12
  Feb 24, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Huyu jamaa ni dini gani vile....!! Maana teuzi za Muungwana bwana hufanyikia Jamatini ...
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Feb 25, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Umeangalia masharti ya mtu anayeweza kuwa Jaji?
   
 14. D

  Dotori JF-Expert Member

  #14
  Feb 25, 2009
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 547
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Duh! Nilikuwa sijauangalia uteuzi huu kiudini.Kazi ipo!
  Lakini jambo la msingi la kuangalia hapa ni pamoja na haya:
  1. Je, uteuzi wa majaji wa mahakama kuu na rufaa, umesaidiaje kuboresha huduma za mahakama nchini?
  2. Vile vile tuangalie upande mwingine wa shilingi. Je, inawezekana Raisi akawa anateua majaji "marafiki" ili watoe hukumu "nafuu" kwa "washtakiwa marafiki"?
   
 15. t

  tk JF-Expert Member

  #15
  Feb 25, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 270
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hapa JK amefanya la maana kwani mlundikano wa kesi katika mahakama zetu utapungua tu kama watateuliwa majaji wa kutosha. Naona msisistizo huu wa uteuzi wa majaji katika mahakama kuu na mahakama ya rufaa ungewekwa pia katika mahakama za mwanzo na za wilaya. Kucheleweshwa kwa kesi za watu kwa kweli ni uonezi wa aina fulani kwani "Justice delayed is Justice denied"
   
 16. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #16
  Feb 25, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Ingekuwa poa kama Bunge lingewaidhinisha hawa majaji au kamati ingine independent na Executive na Judiciary! Yaani waweze kuwa scrutenised kabla hawajaapishwa!

  Uganda kumbe mawaziri wakishateuliwa huwekwa kiti moto na Kamati ya Bunge- Tz utamaduni huu haupo!

  Leo Waziri mpya wa uchumi aliyeteuliwa juzi na M7 amepigwa chini na kamati ya Bunge - eti ana mental problem
  Monitor Online | News | MPs block Mbeiza appointment
   
 17. A

  August JF-Expert Member

  #17
  Feb 25, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,511
  Likes Received: 724
  Trophy Points: 280
  Mimi naona tuangalie taratibu zetu zina faa au hazi fai badala ya kuangalia Dini/kabila nk. na kama hazotoshelezi nini kifanyike ili tuondokane na hiyo taratibu, kumsema kikwete itakuwa ni kumuonea maana mifumo hiyo hiyo imetumiwa na wengine kupandikiza mashemeji, kaka, dada etc etc Hapa juzi juzi tuliona la Dr Patrer Msolla na Tume ya Technology or something like that.
   
 18. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #18
  Feb 25, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hii taarifa ina makosa, angalia hayo maandishi mekundu hapo juu. Jaji jandu aliteuliwa kuwa kuwa Jaji wa mahakama kuu zaidi ya miaka miwili (naweza kusahihishwa)
   
 19. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #19
  Feb 25, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  If you keep on thinking like this for sure uwezo wako wa kufikiri utaendelea kupungua siku hadi siku, think big!
   
 20. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #20
  Feb 25, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mkuu nimekugusa nini? why are you taking it personal?
   
Loading...