MVUMBUZI
JF-Expert Member
- Jan 8, 2011
- 5,182
- 2,304
Hofu ya JK kutokana na kipigo alichopata kwenye uchaguzi mkuu 2010 imemfanya ahamishe watoto wake wawili waliokuwa wanasoma shule maarufu ya St Patric hapa Arusha. Watoto hao sasa wamepelekwa kusoma nchini Malawi. JK kama mzazi alikuwa na mazoea ya kuja St. Patric mara kwa mara kuhudhuria sherehe mbalimbali mfano graduation. Ktk shule hii pia wanasoma watoto wa vigogo wengine wa serikali ya TZ wakiwemo watoto wa mafisadi. JK alisema eti Arusha ni mji wa vurugu hivyo usalama wa hao watoto wake utakuwa hatarini kama wataendelea kusoma hapo hasa baada ya Jimbo la Arusha mjini kutwaliwa na Mh. Godbless Lema. Huu ni uoga wa kijinga au tu ni mwendelezo wa maamuzi ya kukurupuka ya Mheshimiwa? Ukiona rais anaogopa sehemu fulani ya nchi yake ujue anataka kuchangia uasi ndani ya nchi yake kwani akili zake zinamwonyesha upinzani ni uadui. Na kwamba kuwa mpinzani basi wewe si raia wa TZ