SoC01 Jinsi ya kuboresha Sekta ya Afya ili kuongeza pato la nchi

Stories of Change - 2021 Competition

Divine_lady

Member
Jul 19, 2021
22
13
Tanzania ni nchi ambayo pato lake bado lipo katika ukuaji japokuwa tupo katika uchumi wa kati ila tunasafari ndefu ya kufika pato la juu.

Hili tutaweza kulifikia endapo nchi na wananchi wake tukawekeza nguvu kasi ambayo itazaa matunda mazuri kwa miaka ijayo.

Leo ninawazo zuri ambalo kwa namna ya kipekee naona litasaidia kuboresha sekta ya afya ususani katika kutengeneza mashine ambacho itawasaidia wagonjwa waliopooza (kuparalaizi) upande mmoja wa mwili pia, kwa wagonjwa ambao walipata ajali na kuathiri uwezo wao wa kutembea(vilema) na kushindwa kuongea (mfano: ulimi kukatika, taya kuathirika nk).

Hii mashine (haina jina) itawekwa kwenye mkono wa mgonjwa ambao unafanya kazi vizuri halafu itakuwa inatuma meseji kwa mtoa huduma (mfano; nesi, daktari, mke, mume, mama nk. inategemea huyo mgonjwa yupo mazigira gani aidha nyumbani au hospitali). Halafu huyo mtoa huduma atakuja kumsaidia mgonjwa kwa kumpa huduma aliyohitaji.

Lengo la hii mashine ni kufanikisha mawasiliano kati ya mgonjwa na mtoa huduma. Hii mashine itaprogramiwa meseji nne ( Mfano; Nahitaji chakula na maji, Nahitaji kwenda chooni, Najisikia vibaya nk) zitakuwa kwenye lugha mama ya mgonjwa na mtoa huduma (mfano: Kiswahili, Kingeleza, Kifaransa nk) ambapo mgonjwa atakuwa anazungusha mkono aidha kulia, kushoto , juu au chini katika nyuzi 90 na 45 tu.

Kwa hiyo kila nyuzi inameseji zake ambazo zitaonekana katika display ya kifaa na kutumwa kwenye simu ya mtoa huduma. Meseji zitakuwa zinatumwa kwa kifaa kinachoitwa GSM ( Global System for Mobile Communication) ambacho kitawekewa laini ya simu (mfano: Vodacom, Tigo, Halotel kwa Tanzania) ambayo mtandao wake unatumika katika nchi husika.

Halafu kila meseji moja itakayo tumwa mashine itatoa alamu lengo kuhamasisha kuja kutoa msaada kwa mgonjwa. Hiyo mashine itatumia aidha betri, umeme au solar. Hiyo mashine itakuwa katika muonekano kama mashine ya kupima pressure ya mwili.

Faida ya hiyo mashine;

1) Teknologia yake ni rahisi kwasababu vifaa vyake havina gharama sanaa ukilinganisha na mashine zinazotumia vifaa ghali.

2) Husaidia mawasiliano kuwa bora kati ya mgonjwa na mtoa huduma wake. Mwanzoni mgonjwa akiwa na njaa anashindwa kuongea anaumia ndani kwa ndani hadi akija kupewa chakula muda unakuwa ni mrefu, pia suala la haja unakuta mgonjwa anahitaji huduma ya choo anashindwa kusema kwahiyo anamalizia haja zake pale pale kitandani, mgonjwa anajisikia vibaya (mfano; kutapika ) anashindwa kusema anajitapikia tu. Kwahiyo hiyo mashine itarahisisha mawasiliano na kutatua hitaji la mgonjwa.

3) Ongezeko la pato la nchi. Kwakuwa machine itatengenezwa ndani ya Tanzania (Made in Tanzania) tutapata wateja wengi kutoka nchi tofauti tofauti ķwahiyo tutashika soko la dunia endapo tutatengeneza hizo machine nzuri na zenye ubora makini.

4) Uboreshaji wa sekta ya afya.
Kwakuwa swala ni kutatua changamoto ya hawa wagonjwa, elimu kubwa itatolewa kwa madaktari na manesi ili kuweza kutumia hizo mashine vizuri na pia kuweza kutafuta mawazo mapya ya kutengeneza mashine za aina zingine ambazo zitasaidia wagonjwa wa aina nyingine.

5) Mashine hiyo itatumiwa katika mfumo tofauti tofauti wa umeme. (Mfano; betri, solar, system chaji) kwahiyo hata mgonjwa awe kijijini au mji kifaa kitatumika tu.

Tamati;
Serikali yetu ikiwekeza nguvu katika hili wazo litaweza kufikisha Tanzania yetu mbali sana kwani itaweza kujulikana na mataifa mengi hapo itainua sekta ya Utalii kwa kuwa baadhi ya watalii watatamani kuja kutalii nchini mwetu.

Pia, sekta ya elimu itakuwa kwani watu wengi watatamani kujifunza uhandisi wa vifaa tiba ( Biomedical Equipment Engineering).
 
Back
Top Bottom