Dkt. Dugange: Viongozi Waelezeni Wananchi Mafanikio Sekta ya Afya

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
943
Viongozi wa sekta ya afya wametakiwa kuwaeleza wananchi mafanikio yanayopatikana katika sekta ya afya ili kufahamu namna serikali ilivyoboresha huduma za afya nchini.

Naibu waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Festo Dugange ametoa maagizo hayo alipokuwa akifungua kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa Mpango wa Afua za Takwimu za Bidhaa za Afya (IMPACT) jijini Dodoma .

Dkt. Dugange amesema kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mhe.Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya kwa kujenga vituo vya kutolea huduma za afya, ununuzi wa dawa na vifaa tiba pamoja na kuajiri wahudumu wa afya hivyo ni jukumu la kila kiongozi kuyasemea mafanikio hayo kwa wananchi.

Akizungumzia kuhusu vifaa tiba vilivyonunuliwa na serikali, Dkt. Dugange amewaagiza wahudumu wote kuvitunza vifaa hivyo ili viweze kudumu kwa muda mrefu.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu kutoka Ofis ya Rais Tamisemi anayeshughulikia Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe Dkt. Charles Mahera amewaagiza waganga wakuu wa mikoa kudhibiti wizi wa vifaa tiba na dawa unaotokea sehemu mbali mbali nchini.

“Tumekuwa tukipokea taarifa za wizi wa madawa na vifaa tiba,nendeni mkasimamie hilo hasa mikoa ya mipakani ambako dawa zinaibiwa sana. Jana tumeona hospitali ya Mkoa wa Njombe kuna seti za televisheni zimeibiwa. Msipodhibiti hilo mnahujumu juhudi zinazofanywa na serikali katika kuboresha huduma za afya nchini,” amesema.

GAEqcsqW8AA9Qhf.jpg

GAEqcsqW8AE2i9t.jpg
 
Nitawaeleza Kwa mifano, kuwa alivyopata Ajali siku Ile ....au basi!
 
Yaani msomi ila hana akili unaanzaje kuwaambia watu mafanikio badala wayaone wenyewe mbona mnalazimisha sisi wananchi tuone mnafanya kazi kubwa kumbe ungese tu. Leo msomi anasema kawaelezeni kana kwamba huduma zimeboreshwa tuko safi na uhalisia huko mahospitalini wajawazito wanakufa kwa makusudi ya wahudumu alafu viongozi waje kutueleza mafanikio. STUPID
 
Back
Top Bottom