Jinsi wanigeria wanavyoingia USA kila siku

Jinsi wanigeria wanavyoingia USA kila siku

Aisee kuna mataifa yana ushirikiano haswa..! ..

Hata hapa bongo wakati halotel/viettel inaanzishwa nakumbuka kipindi kile wale wa Vietnam wapo wengi ila wanapanga apartment moja wana share usafiri binafsi, kiufupi wapo vzirui kwenye kupunguza gharama ushirikaiano wao ulikuwa unawasaidia sana
Tena Wachina hata kama mshahara unaingia benk anautoa, hela ya mchina ana lala nayo ndani. Utaona wakipata immigration rides waki searchiwa Unamkuta mtu ana €20,000 ndani ya nyumba.
 
Tena Wachina hata kama mshahara unaingia benk anautoa, hela ya mchina ana lala nayo ndani. Utaona wakipata immigration rides waki searchiwa Unamkuta mtu ana €20,000 ndani ya nyumba.
Immigration wanazunguka mara kwa mara au mpaka wapate intel kuhusu jambo au watu fulani?
 
So mkuu hao wakenya waliotoka KE kuja TZ , ni kwasababu KE hakuna fursa? ...Au wamekuja kutafuta fursa?

Sasa kuna ubaya gani mTz akitaka kwenda nchi nyingine yyte kutafuta fursa, we unang'ang'ana wabikie tu hapa sababu za msingi huna!
Kenya kuna fursa gani? kama Mkenya anaweka kambi Bongo wewe mwenyeji unakimbilia wapi? na hapo uhitaji VIZA, WORK/RESIDENCE permit. Wabongo tuache kulia-lia. Ukiongeza jitihada kidogo bongo unatoboa
 
Immigration wanazunguka mara kwa mara au mpaka wapate intel kuhusu jambo au watu fulani?
Immigration mpaka wapate intel. Watu wanaotoka Asia (China, India, Phillipines, Vietnam na Indonesia) wanadakwa kama kuku Australia. Wengi huingia kwa kujidai watalii wakifika wanapiga kazi za ujenzi na restaurants. So ni rahis kuwadaka maana Immigration wanaibukia kazini wanakukuta huna hili wala lile.
 
Immigration wanazunguka mara kwa mara au mpaka wapate intel kuhusu jambo au watu fulani?
Immigration mpaka wapate intel. Watu wanaotoka Asia (China, India, Phillipines, Vietnam na Indonesia) wanadakwa kama kuku Australia. Wengi huingia kwa kujidai watalii wakifika wanapiga kazi za ujenzi na restaurants. So ni rahis kuwadaka maana Immigration wanaibukia kazini wanakukuta huna hili wala lile.
 
Kuna dada wa Kinigeria nilimfahamu kwa karibu. Alikua ananisuka nywele. Nilikuwa ninamfuata kwake, alikuwa na mtoto mmoja wa miaka mitatu yeye na mume wake waliishi chumba kimoja. Wote hawana vibali, wamepata vibali vya watu wanafanyia kazi na wanawalipa hao wenye vibali.

Aliniambia huyu mwanaume ndiye mpenzi wangu wa kwanza tangu tuko shuleni. Baada ya kumaliza Form Six mwanaume aliondoka. Amefika Ulaya alilipa mahari kwa familia ya mke na kumtumia ticket.

Tegemeo lao ni mtoto akifika miaka saba kuna sheria inamruhusu kuendelea kuishi hata kama wazazi hawana vibali wanapata vibali kutokana na mtoto midhali amezaliwa nchi hiyo.
Vizuri ila sie watanzania tunashida aswa kusaidiana kwenye ushauri tu...
 
Wakuu habari za majukumu

Nimeona Kwa takribani majuma kazaa jukwaa letu limejaa nyuzi za kujilipua na mimi nikasema ngoja nijaribu kuandika chochote kuhusu kuingia USA nilichojifunza Kwa Nigeria

Kwenye kitabu cha biblia kuna kisa kimoja cha watu wanaitwa "wakoma wanne" (2 wafalme 7:3-20), Kwa kifupi hawa watu kwenye nchi yao (samalia) kulikuwa na njaa kubwa sana ya kuua mtu, lakini kwenye nchi ya jirani (washamu) ambao ni maadui kulikuwa na vyakula tele ila kila MTU aliogopa kwenda kuuwawa na maadui.

Hawa wakoma wanne wakasema kama tukibaki hapa tutakufa na njaa na kama tukienda Kwa washami jeshi lao litatuua, wakaamua ni bora wakafe Kwa washami Kwa jeshi kuliko kufa Kwa njaa.

Hii ndio njia kubwa wanayoitumia wanigeria kwenye kuomba Visa kuingia USA.
Nchi zetu hizi za Africa ni failed state



Nimekuwa nikijaribu kufuatilia njia halali za kwenda USA nikataka kujifunza Kwa wa Nigeria wanavyofanya nikaingia kwenye platform yao inayofanana na JF hapa kwetu iitwayo nairaland.com kuna vitu vingi sana nimejifunza hasa kwenye uzi wao uitwao
Re: General USA Student Visa Enquiries-part 16

Ukiingia hapo utakupa wanatoa tips namna walivyokosa Viza na namna walivyopata visa kuna pages nyingi sana karibia 170. Hope mtu akimaliza hapo atakuwa amejifunza kitu na wengi wanaomba kwenda kusoma.

KWANINI USA
Nchi za wenzetu zilishaendelea sana na kipato Chao ni cha juu sana fikiria dereva wa uber/Trucks kulipwa $100/hr hakuna mfanyakazi wa kawaida anaweza kumfikia Tz hii. Kwahio wanaenda kukusanya pesa baada ya miaka 5 hadi 10 wanarudi na mitaji yao.

KUHUSU KAZI NA SSN
Watu wanaoenda USA hutofautiana kimalengo wengine kusoma kweli wengine kutafuta kazi.
Sasa iliupate kazi kihalali USA inabidi upate SSN (social security card No) ambayo inatolewa na SSA ( social security Administration) kupitia wizara ya mambo ya ndani na ulinzi (DHS).
Kwahio kama ulienda kimasomo unaweza kupata kazi Kwa mda wako ambao utakuwa upo huru.

ILA Kwa wewe ambaye ulienda Kwa njia nyingine halali ila huna uwezo wa kupata SSN itakubidi utumie njia zifuatazo ili ufanye kazi
1.utafute kazi maeneo ya mijini ndio kuna mchanganyiko wa watu si rahisi kufuatiliwa na immigration (usiende miji midogo yenye wazawa wengi)

2.utafute mtu akupe SSN yake uitumie kuanya kazi Kwa makubaliano.

3.jifunze vitu ambavyo haviihitaji uwe na SSN mfano driving (upate lesseni)

4.kama unataka kusoma na hukwenda kwa njia Viza ya kusom (F1) tafuta kunavyuo ambavyo hawafuatilii sana mambo ya makaratasi mfano michigan University (Hii sina hakika sana ila fuatilia)

4.ukipata kazi jitahidi sana kutunza mtaji ili urudi nyumbani kufanya kazi zako kwasababu ukitimuliwa hutaruhusiwa kuingia tena Kwa muda USA kwasababu utakuwa "stayed out" wenyewe wanaita.

AHSANTENI SANA

Naruhusu kukoselewa vikali sana kwasababu haya ni Kwa mujibu wa uchunguzi wangu huenda wengine wanajibu tofauti

Yaaani ulivyoandika hapo ni wazi kwamba umepotea sana, mambo hayako hvyo unavyofikiria wewe.

Dereva wa uber halipwi per hr.
Huwez kupata drive license bila ssn kifupi huwez kujigunza gari kama huna learner permit na kuipata hii lazima huwe na ssn.

Labda unachoweza kufanya ni kudrive kwenye licence ya mtu mwingine ila omba wasikamate.

Marekani hakuna mtu wa kukuhukiza unatoka wapi mtaani, maybe una makosa, ila mtaani hapana.


Njia raisi ya kufanya ukiwa marekani naisi ni kufanya kaz kwa ndugu au kweny ssc ya mtu mwingine, maybe inaewekani alafu sio kwenye kampuni kubwa
 
Tunashukulu Kwa ushauri Mkuu.kama nilivyoeleza wengine hawana haja ya uraia wanataka wakachukue mtaji waje wawekeze.

Hivi Mkuu unajua kua tz kupata mtaji ni ishu ngumu sana tofauti na USA kama mtu yuko determined hachagui kazi mtaji anaupata anarudi kupiga mishe zake

Nakuelewa Mkuu,

Lakini;Kwanza, sijashauri wala kuhimiza watu wakabadilishe Uraia.
Pili, Mtaji hauchukuliwi, -Unatafutwa. Huendi tuu kufanya Kazi, utahitaji ulipwe stahiki zako kulingana na Kazi yako, ama sivyo?

Tatu, Hoja yangu ya msingi imejikita kwenye kuingia huko Marekani, ili kuweza kutafuta huo Mtaji wako unaousema lakini bila ya usumbufu kutoka kwa Mamlaka za ndani au kunyonywa na unaowafanyia Kazi na Kulipwa Malipo halali yanayoendana na aina na muda unaopaswa wewe kufanya Kazi zako.

Wapo wanaonyonywa miaka na miaka, wanakomaa tu kutokana na shida.
Lakini kingine, Ukiwa na Makaratasi unao uwezo wa kwenda kuchukua huo Mtaji wako na kurudi lakini utakuwa na jeuri ya kwenda tena siku za baadae/mbeleni bila usumbufu wa kuhitajika kuomba Viza.

Nikumegee tu Kazi ya aina moja na sehemu/Ofisi moja upo uwezekano wa kuwa na malipo tofauti kati ya alie na Ruhusa ya kufanya Kazi /Vibali na yule asie navyo na sababu kubwa ni kuwa hata ukibinywa maslahi utaenda kumlalamikia nani?
 
Swadakta! Kuna msichana nimekutana nae, akaniambia amekaa kambini huko Zambia kwa miaka 12. Sio mchezo. Safari za Ughaibuni kutafuta maisha zinahitaji moyo haswa. Aliondoka akiwa na watoto wawili wenye umri wa miaka 3 na 5. Wameingia Denmark, watoto wameishakuwa teenagers.
Wamevulia shida nyingi sana kwenye makambi ya Wakimbizi, lakini mwisho wao umekuwa mwema. Shida zote zimekwisha, na FUTURE yao ipo guaranteed.
Ndio inavyokuwa wanavumilia ila wakifanikiwa kuondoka afrika wanasahau shida zote.
Anko wangu alivyotoka kigoma kwenda zimbabwe yeye na mke watoto 2 na shemeji yake wa kike ...ndugu zake waliona kama anapoteza muda tu....wakawa wanamshauri arudi lakini alikataa akawa anaenda afrika kusini kupiga vibarua...maisha yalikuwa magumu sana huko kambini hadi akawa hana simu ya kuwasiliana na ndugu.....baada ya miaka 10 ndio akaingia USA na alikuwa ana miaka 50 kipindi anaondoka nyumbani kgm kafika kwa Biden ana 60yrs,watoto ndio watafaidi maisha kwani bado wadogo.Ndugu sasa hivi wanamuheshimu kwa sababu anasaidia.
 
Tatizo ni wabongo wanaofika majuu kuwa wabinafsi kupigiana "assist" kusaidia wenzao wanaotaka kufika huko.....wabongo waliyoko USA na EUROPE wakifungua roho zao kama wanaijeria wengi watasafiri.

Mimi nina dada yangu wa damu kabisa mama mmoja baba mmoja, ananiambia niende kambini nikakae hata miaka 5 kutafuta nafasi za wakimbizi wanaopelekwa US na UROPA eti niteseke kama walivyoteseka wenyewe kufika CANADA....ingekuwa wanaijeria watu kibao ktk familia wangekua majuu.....lakini kwa kuwa wabongo wana asili ya kubaniana ndio hivyo.
Dada yako hana roho mbaya, ukiingia Ulaya na stori ya ukimbizi ni rahisi kupata vibali vya kufanya kazi au hata kusoma.
 
Immigration mpaka wapate intel. Watu wanaotoka Asia (China, India, Phillipines, Vietnam na Indonesia) wanadakwa kama kuku Australia. Wengi huingia kwa kujidai watalii wakifika wanapiga kazi za ujenzi na restaurants. So ni rahis kuwadaka maana Immigration wanaibukia kazini wanakukuta huna hili wala lile.
Aisee... sasa ukiwa kama mwafrika unaishi na niggaz wa kule usa.. si itakuwa ngumu kugundulika mpaka mtu akuchomee??
 
Mimi ndo mara ya kwanza kusikia ila sishangah sana.

Numeishi state tano hiyo kitu sijawah kutana nayo kabisa
Haiwezi kukukuta umekaa tu. Wewe unafikiri wanaoendesha magari wote wana papers? La hasha. Unaweza kuwa na driver's license halali kabisa kutoka DMV bila kuwa na papers
 
Mimi ndo mara ya kwanza kusikia ila sishangah sana.

Numeishi state tano hiyo kitu sijawah kutana nayo kabisa
Kuna States zaidi ya tano unaweza kupata driving licence bila papers ikiwemo New Jersey na new York.
Waliona ajali nyingi zilitokea kwasababu watu hawajifunzi mafunzo ya udereva
Screenshot_20210509-223344.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom