Jinsi wanigeria wanavyoingia USA kila siku

Jinsi wanigeria wanavyoingia USA kila siku

Mimi nimewaza nikitaka kuzamia USA kutokea Tz ...
Ningeenda kwanza Bahamas ambapo hakuna viza kuingia ...

Halafu kutokea Bahamas na Florida ni masaa Tu Kwa meli za abiria..
Ningetafuta hata kibarua kwenye hizo meli..
Ikifika Florida tu .. done
Meli gani inampa Ajira Mgeni asie na Karatasi zama hizi?
 
Wakuu habari za majukumu

Nimeona Kwa takribani majuma kazaa jukwaa letu limejaa nyuzi za kujilipua namimi nikasema ngoja nijaribu kuandika chochote kuhusu kuingia USA nilichojifunza Kwa Nigeria

Kwenye kitabu cha biblia kuna kisa kimoja cha watu wanaitwa "wakoma wanne" (2 wafalme 7:3-20),Kwa kifupi hawa watu kwenye nchi yao (samalia) kulikuwa na njaa kubwa sana ya kuua mtu, lakini kwenye nchi ya jirani (washamu) ambao ni maadui kulikua na vyakula tele,ila kila MTU aliogopa kwenda kuuwawa na maadui.
Hawa wakoma wanne wakasema kama tukibaki hapa tutakufa na njaa na kama tukienda Kwa washami jeshi lao litatuua,wakaamua ni bora wakafe Kwa washami Kwa jeshi kuliko kufa Kwa njaa.

Hii ndio njia kubwa wanayoitumia wanigeria kwenye kuomba Visa kuingia USA.
nchi zetu hizi za Africa ni failed state


Nimekuwa nikijaribu kufuatilia njia halali za kwenda USA nikataka kujifunza Kwa wa Nigeria wanavyofanya nikaingia kwenye platform yao inayofanana na JF hapa kwetu iitwayo nairaland.com kuna vitu vingi sana nimejifunza hasa kwenye uziwao uitwao
Re: General USA Student Visa Enquiries-part 16
Ukiingia hapo utakupa wanatoa tips namna walivyokosa Viza na namna walivyopata visa kuna pages nyingi sana karibia 170.hope mtu akimaliza hapo atakuwa amejifunza kitu na wengi wanaomba kwenda kusoma.

KWANINI USA
Nchi za wenzetu zilishaendelea sana na kipato Chao ni cha juu sana fikiria dereva wa uber/Trucks kulipwa $100/hr hakuna mfanyakazi wa kawaida anaweza kumfikia Tz hii.kwahio wanaenda kukusanaya pesa baada ya miaka 5 hadi 10 wanarudi na mitaji yao.

KUHUSU KAZI NA SSN
Watu wanaoenda USA hutofautiana kimalengo wengine kusoma kweli wengine kutafuta kazi.
Sasa iliupate kazi kihalali USA inabidi upate SSN (social security card No) ambayo inatolewa na SSA ( social security Administration) kupitia wizara ya mambo ya ndani na ulinzi (DHS).
Kwahio kama ulienda kimasomo unaweza kupata kazi Kwa mda wako ambao utakuwa upo huru.

ILA Kwa wewe ambaye ulienda Kwa njia nyingine halali ila huna uwezo wa kupata SSN itakubidi utumie njia zifuatazo ili ufanye kazi
1.utafute kazi maeneo ya mijini ndio kuna mchanganyiko wa watu si rahisi kufuatiliwa na immigration (usiende miji midogo yenye wazawa wengi)

2.utafute mtu akupe SSN yake uitumie kuanya kazi Kwa makubaliano.

3.jifunze vitu ambavyo haviihitaji uwe na SSN mfano driving (upate lesseni)

4.kama unataka kusoma na hukwenda kwa njia Viza ya kusom (F1) tafuta kunavyuo ambavyo hawafuatilii sana mambo ya makaratasi mfano michigan University (Hii sina hakika sana ila fuatilia)

4.ukipata kazi jitahidi sana kutunza mtaji ili urudi nyumbani kufanya kazi zako kwasababu ukitimuliwa hutaruhusiwa kuingia tena Kwa muda USA kwasababu utakuwa "stayed out" wenyewe wanaita.

AHSANTENI SANA

Naruhusu kukoselewa vikali sana kwasababu haya ni Kwa mujibu wa uchunguzi wangu huenda wengine wanajibu tofauti

PIGA,IBA,UWA,NYONGA,NING'INIZA.-VYOVYOTE ITAKAVYOWEZEKANA.
OMBA/FANYA UFANYAVYO UINGIE MAREKANI NA GREEN CARD,-UNAKUWA ZAIDI YA 50% MBELE YA HATA ALIEINGIA MIAKA KUMI ILIYOPITA MAREKANI KIMASLAHI IWAPO HANA KARATASI.

UNAFANYAJE KUIPATA HIYO GREEN CARD.
1. Itahitaji uwe na Bahati, Cheza /Shiriki DV Lottery (Inachezwa wiki ya kwanza ya Mwezi wa 10 kila Mwaka)
2.Oa/Olewa na mwenye Ukazi wa kudumu au Raia wa Marekani.
3.Ndugu yako wa Damu Mwenye ukazi wa kudumu Marekani( Baba,Mama,Mtoto,Kaka,Dada kama unae anaeishi kihalali 'a-file' Petition/sponsorship kwaajili yako wewe kuhamia huko (Hii inawezachukua muda kiasi kutegemeana na uhusiano)

Nje ya hapo ni Mateso na kubangaiza kwa jasho na muda mrefu tofauti na njia hizo za hapo juu.

Nawasilisha.
 
Mimi nimewaza nikitaka kuzamia USA kutokea Tz ...
Ningeenda kwanza Bahamas ambapo hakuna viza kuingia ...

Halafu kutokea Bahamas na Florida ni masaa Tu Kwa meli za abiria..
Ningetafuta hata kibarua kwenye hizo meli..
Ikifika Florida tu .. done
Hakuna viza kwa wa Tz?
 
Tatizo ni wabongo wanaofika majuu kuwa wabinafsi kupigiana "assist" kusaidia wenzao wanaotaka kufika huko.....wabongo waliyoko USA na EUROPE wakifungua roho zao kama wanaijeria wengi watasafiri.

Mimi nina dada yangu wa damu kabisa mama mmoja baba mmoja, ananiambia niende kambini nikakae hata miaka 5 kutafuta nafasi za wakimbizi wanaopelekwa US na UROPA eti niteseke kama walivyoteseka wenyewe kufika CANADA....ingekuwa wanaijeria watu kibao ktk familia wangekua majuu.....lakini kwa kuwa wabongo wana asili ya kubaniana ndio hivyo.
 
Bongo kama huna aibu fursa kibao sana ndugu. Komaa na biashara za mazao kwa mfano unatoboa mapema asubuhi. Ni aibu kwenda kusafisha vyoo nchi za watu.
Kweli kabisa. Wala hana sababu ya kwenda mbali. Aanzie hapo hapo kwao yaani Kibaigwa kwenye solo la Kimataifa la Mahindi
 
Wacongo, Wakenya Wacomoro wanigeria upeana sana connection Sana nje ya nchi
 
Tatizo ni wabongo wanaofika majuu kuwa wabinafsi kupigiana "assist" kusaidia wenzao wanaotaka kufika huko.....wabongo waliyoko USA na EUROPE wakifungua roho zao kama wanaijeria wengi watasafiri.

Mimi nina dada yangu wa damu kabisa mama mmoja baba mmoja, ananiambia niende kambini nikakae hata miaka 5 kutafuta nafasi za wakimbizi wanaopelekwa US na UROPA eti niteseke kama walivyoteseka wenyewe kufika CANADA....ingekuwa wanaijeria watu kibao ktk familia wangekua majuu.....lakini kwa kuwa wabongo wana asili ya kubaniana ndio hivyo.

Anataka uendelee kumsujudia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom