Jinsi gani tatizo la Uraibu wa Kamari limeharibu maisha yako upande wa kijamii, kiimani na kiuchumi?

Tipstipstor

JF-Expert Member
Nov 29, 2021
1,531
3,331
Tatizo la uraibu (addiction) wa kamari linaendelea kukua siku baada ya siku kwa vijana wengi wa Kiafrika hususani Tanzania. Makampuni ya kamari yanakimbilia sana katika mataifa ya kiafrika ambako umaskini umetamalaki kuja kuwekeza huku wakilenda soko lao kubwa kuwa ni vijana.Vijana ambao wana ndoto ya kupambana na kuondokana na umasikini.

Hali hii imekuwa kinyume kwani wengi wa vijana hao wameendelea kupoteza pesa kila kukicha kitendo kinachowapelekea kupata msongo wa mawazo,kutokujiamini, wasiwasi na pia kupoteza dira kiuchumi.

Vijana wengi wamekuwa wakificha tatizo hili katika familia zao au kwa marafiki zao yaani ni kama vile waraibu wa madawa ya kulevya wasivyotaka kujulikana kuwa wana matatizo ya ulevi wa madawa ya kulevya.

Karibu katika uzi huu ueleze matatizo unayokumbana nayo katika Kamari (betting) na pia waliofanikiwa kuacha tatizo hili waeleze njia walizotumia kufanikiwa kuacha.

Asanteni na karibuni.
 
Kama huna hela usikope kwa matumaini utashinda uilipe, huna hela ya akiba usilaze watoto njaa kisa ulikwangua pesa ya chakula ukitegemea ushindi mnono. Bet what you can afford to lose
 
Kama huna hela usikope kwa matumaini utashinda uilipe,huna hela ya akiba usilaze watoto njaa kisa ulikwangua pesa ya chakula ukitegemea ushindi mnono. Bet what you can afford to lose
Kwahiyo unabeti ili kujifurahisha tu...? Kwa ninavyojua hata binadamu awe tajiri vipi bado hayupo kupoteza hata shilingi moja aliyoitolea jasho kizembe
 
Wapi nimesema nabet? Mkuu umeanzisha uzi wacha wadau wachangie badala ya kulisha maneno unayoyataka mwenyewe
Kwahiyo unabeti ili kujifurahisha tu...? Kwa ninavyojua hata binadamu awe tajiri vipi bado hayupo kupoteza hata shilingi moja aliyoitolea jasho kizembe
 
Back
Top Bottom