Uraibu wa kubeti unavyowamaliza vijana

Mkulima na Mfugaji

JF-Expert Member
Jul 26, 2013
1,013
1,634
Huyu jamaa simjui wala hanijui ni moenzi wa makala zake ila makala iliyonigusa zaidi ni hii ya kuhusu kamari

URAIBU WA KUBETI UNAVYOWAMALIZA VIJANA.

Na Thadei Ole Mushi.

Kama hujawahi kushiriki mchezo wa bahati nasibu maarufu kama "KUBET" Basi utakuwa umewahi kuusikia.

Kubet kama wenyewe wanavyouita ni kitendo cha kufanya predictions ya matokeo ya mchezo fulani kabla haujachezwa.

Mchezo huo unaweza ukawa mpira wa miguu, nashindano ya magari, Riadha na kadhalika, japokuwa kwa hapa Tanzania wachezaji wengi wa Kamari hii hutabiri matokeo ya mpira wa miguu katika Ligi mbalimbali.

Kama tujuavyo Kubet ni kamari iliyohalalishwa na kamari ni Kitendo cha ku risk-Fedha au kitu cha thamani kwa kutegemea kushinda ili upate fedha zaidi. Kwa maana hiyo Kamari hii inakwenda na option mbili kubwa kupoteza au Kupata. Unachopoteza hapa ni fedha au kitu chako cha thamani ulichokitumia kuchezea kamari hiyo.

#Kwa sasa madhara ya moja kwa moja hayajaonekana juu ya mchezo huu ambao umejumuishwa kwenye michezo ya bahati nasibu nchini.

#Kwa siku za karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa sana la vituo vya uchezeshaji wa mchezo huu... na unachezwa na rika zote kwenye jamii.

#Pamoja na kwamba vitabu vya dini vinakataza kwa pande zote kwa wenzetu Waislam na Wakristo ila vijana wake wamekuwa ndio wachezaji wakuu wa mchezo huu. Cha ajabu hata viongozi wetu wa dini wanahalalosha uchezaji wa kamari kwa kuwa wala hawakemei.

MADHARA YAKE NI YAPI?

Madhara ya kubet ni mengi sana japokuwa makampuni yanayoendesha michezo hii wanajiinhizia fedha nyingi sana.

Kwa kuwa mchezo huu umekuwa ukichezwa sana na vijana ambao wengine wapo mashuleni na wengine ndio wazalishaji mali basi wamekuwa wakipoteza muda mwingi sana.

Ili uweze kuucheza mchezo huu vizuri itakulazimu kujifunza na kuelewa mambo mengi ya msingi katika mchezo husika. Mfano itakulazimu kuzielewa odds zinazotolewa za matokeo mbalimbali. Uwe up to date na takwimu zote kuhusiana na mechi husika kama vile, wachezaji majeruhi, walio katika fomu, waliosimamishwa, hali ya hewa, ubora wa wapinzani, wapi mechi zinachezwa na mambo mengi mengine ambayo yatakulazimu kushinda mitandaoni au kwenye vijiwe vya Soka ili kupata taarifa zote hizo muhimu.

Kama ni mwanafunzi huyu moja kwa moja ataathirika kitaaluma na kama ni mzalishaji mali ataathirika kiuchumi kutokana na upotevu mkubwa wa muda na uvivu.

#Athari nyingine ni kuongezeka kwa magonjwa yabPresha kwa wachezaji. Kwa sasa athari hii haijaonekana moja kwa moja ila huko tuendako hili litajitokeza.

Wachezaji wengi wa mchezo huu wamekuwa wakiishi maisha ya wasiwasi na Presha wakisubiri timu zao walizobet zishinde ili wapate fedha za chapchap. Kama mchezaji kamari hii atakuwa anafuatilia mchezo husika na timu aliytabiri kushinda haielekei kushinda basi huwa na wakati mgumu kiafya.

Pamoja na hayo mchezo huu kwa vijana unachochea ujambazi na wizi. Kama ilivyokuwa kwa vijana waliokuwa na Uraibu wabkutumia madawa ya Kulevya basi mchezo huu nao umeanza kuelekea kuwa na watu wenye uraibu.

Binafsi nimeshawahi kufuatwa na vijana zaidi ya sita wakikopa fedha za kwenda Kubet. Yaani kuliko aache bora akope what if ataikosa fedha hiyo? Basi ataanza udokozi na baadaye atakuwa mwizi kabisa.

Kwa Watu wazima wamekuwa wakitumia fedha za familia kwenye mchezo huu. Badala ya kupeleka mahitaji ya msingi nyumbani anaona ni bora atumie fedha hizo kujaribisha kama anaweza kuambulia chochote kitu.

#HUKO TUENDAKO

Tanzania ijiandae kuwa na vijana wengi walioathirika kiafya kutokana na mchezo huu.

Kwa hii kasi ya ueneaji kwa hapa nchini tuanze kufikiria kuanzisha taratibu za Rehabilitations. Kwa wenzetu wazungu wameshaanza kukumbwa na matatizo makubwa ya kubet na wameshaanzisha vituo vya kufanya rehabilitations.

#Kama hujaanza kucheza michezo hii usifikirie kucheza na viongozi wetu wa dini waseme waziwazi kuwa ni kinyume na taratibu za dini zetu.

#Serikali ione kwa jinsi gani inaweza kuwanasua vijana hawa kwenye huu uraibu na kuwaelekeza kwenye maswala ya Uzalishaji mali zaidi. Hawa kina Tarimba Abbas wanatumalizia nguvu Kazi huku wao wakineemeka.

#Na kwa sasa kila mtu anawaza kuanzisha mchezo wa bahatu nasibu nchini anajua tumeshapata uraibu wa kutosha hivyo ni rahisi kuamini tunaweza kupata fedha za chap chap.

#Wachina nao wamekuja na mashine zao za kutumbukiza mia mbili mia Mbili. Nendeni kwenye hivi vituo muone utitiri wa vijana amabo hawana kazi.

Ole Mushi

Baadhi ya aliyoyaandika yameshaanza kujitokeza
 
Dini imeshafeli katika hili,viongozi wengi wa dini ni wahuni kama wahuni wengine hawana ushawishi tena katika maisha ya vijana kwa sasa.
 
Back
Top Bottom