Jiji la Dodoma kibiashara na kimaisha kwa ujumla

Jiji la Dodoma kibiashara na kimaisha kwa ujumla

Itachukua muda kiasi kwa Dom kuwa eneo zuri kwa fursa maana bado mzunguko wa pesa bado haujaimarika maana population iliyopo fedha yake ni ya kipindi wafanyakazi mwisho wa mwezi, wanachuo mpk vyuo vifunguliwe, wabunge mpk kipindi cha bunge nk. Ili paendelee lzm wafanyabiashara wavutike waelekeze shughuli zao huko wanaweza kusaidia na wanawezaje kufanya hivyo mazingira yawe rafiki
 
R.i.P Maimu......
Kwanza inaonekana ulikua mtu mwenye wivu na husda tele, na kuwajua walio kutangulia kwenye biashara haimaanishi basi eti Dodoma nzima uliifahamu.
Na hata huyo Maimu marehemu, alifariki akiwa tayari amesha fikisika.
Naomba nisiwe msemaji wa majina ya walio tangulia kufanikiwa, lakini nivyema nikaweka wazi kwamba mafanikio ni Jambo jema, na ubaya wa watu kama wewe ni kutokukubali kwamba tayari ulifika sehem na ukakuta wapo walio fanikiwa kabla yako, (hata ukiwaita matajiri) bado sio mbaya kwasababu ukweli ni kwamba walikutangulia tayari mkuu.
Nilikua na husda???

Lini tena mkuu?? Usiniwekee maneno na Sidhani hata kama umenielewa
 
Mkuu, nilidhani ungeweza kuleta hoja za maana.....
Kumbe umekuja na mipasho (personal attacks).
Na usidhani eti kwakuwafahamu hao matajiri wa zamani wa Dodoma ndipo tutakuona unajua sana, zaidi naona kama unazungumzia mambo binafsi/hulka na maisha ya watu ambao wapo kila mahali duniani.
Acha kudandia treni ndugu yangu. Hizo komenti zilikua reply za mchangiaji alichosema

Kuna mengine mengi nimechangia mbona unaruka ruka kama mkizi??
 
Dodoma Ni mji unao kua kwa msukumo wa Siasa.Huo ndio ukweli.Na itaendekea kuwa hivo...watumishi wa Umma watakapo maliza kujenga nyumba zao ,mji utagota !
Na hàmna kosa walifanya Manispaa Kama kuwa uzia watu viwanja maporini ,wakifikiri ndio wanapanua mji...itachukua mudamrefu Sana!
Hata hivyo ktk kipindi Cha miaka 3 Kuna mabadiliko.makubwa Sana.
Kwa maoni yangu Dodoma ilitakiwa iwe jiji dogo la kisasa ,mfano mji wa Serikali ungejengwa eneo la Hazina kuelekea Vilima vya Ntyuka na Pale 88,then pale kstikakati pangejengwa Trade Centre ya nguvu !
Kuhusu Viwanda ,Serikali iweke msukumo wa nguvu ,la sivyo mtu hawezi kuleta kiwanda chake Dodoma!
 
Ukuaji wa miji huja automatic, ukiangalia historia ya kuanzia Paris, London, New York sijui hata Bagamoyo kibiashara mji unakua wenyewe na ikiisha unakufa pia. Huwezi kulazimisha kusisimua kisiasa wakati mtu anajua akiwekeza hela kias hicho hicho sehem nyingine atapata zaidi. Ndo uhalisia huo

Mbona kina Fresho na Jambo wamefungua viwanda shinyanga huko bila kusisimuliwa na mtu. Sio mwanza ambapo kuna shughuli tayari ila shinyanga inajikuta tu inahotaji uwekezaji wa namna hiyo

Kiwanda cha maji tu simpo hicho Asante cha Dodoma kimekuja kufunguliwa juzi juzi na bado kinasuasua

Makampuni yenyewe ya Dar niliyoyaona yamekimbilia Dodoma mengi ni ya Mikopo(Imarisha maisha, Lughano nk) na yale ya upimaji/uuzaji viwanja(kina Global Fortune, infinity nk) wote wanalenga wafanyakazi

Hao kina Feza Schools, Shoppers plaza sijui Nakiete wenyewe nao ni vibranch tegemeo hao wafanyakazi tu pia

Labda tuendelee kuangalia over time wananchi wote kwa pamoja watachangamka na kuchangamsha mji kwa ujumla ila kwa sasa nadhani bado kwakweli
Dodoma inategemea ma staff wa serikali na wabunge ambao ndio wana hela. Mzunguko hauwezi kuwa mkubwa sababu watu wa kule ni wavivu kinoma.
 
Kuna opportunities nyingi sana Dodoma kuliko Dar. Yaani kuna upungufu mkubwa sana wa huduma hapo Dodoma kiasi kuwa ukiwekeza kwenye huduma hizo utapanda sana. Usitake kufanya biashara za ki-Dar es-Salaam ndizo ukapeleka dodoma; utakwama sana. Wewe nenda pale katumie kama wiki mbili uangalie mapungufu yaliyopo ndipo uchukue opportunities uanzishe a biashara tofauti sana na zile za Dar es Salaama zikiendena na mapungufu yaliyoko Dodoma; utashangaa mafanikio utakayopta.
 
Dodoma hapafai, nilichoka siku nimeopoa dada poa usiku wa manane Mbuge wangu nae anampigia huyo huyo dada poa!! Kumuuliza kulikoni akasema hata hii simu yake imenunuliwa na mbuge wangu
 
Shukrani sana kwa ushauri mzuri
Hakuna unafuu kama mji wa Kigoma, vyakula vyote bei juu tofauti na Kigoma ndizi bei chini, unga bei chini, samaki mgebuka bei chini, maharage bei chini, mafuta mawese bei chee, Dodoma kila kitu bei juu, hadi nyumba za kupanga, mfano wapemba wakija bungeni hupendelea kupanga vyumba vya maeneo ya Chinangali na Chang`ombe.

Vyumba bei rahisi tena wanapanga wapemba wanne chumba kimoja cha shs 10000, DODOMA channel za biashara pia siyo super maana hakuna viwanda kwa hiyo biashara zote za jumla inabidi kuagiza bidhaa toka DSM MFANO CEMENT, MABATI na SUKARI.

Dodoma ni mji mkuu kwa sasa fursa pekee ni viwanja na nyumba za kupanga kuwa bei juu, pia unaweza ukapata bahati nyuma yako ikapangishwa na ofisi za serikali au shirika au NGO yoyote.

Dodoma na wagogo wake ni ngome ya CCM hivyo ni watu wa kuridhika tu hawawezi kudai haki au fursa mfano watu wa Mbeya hili nalo ni tatizo la Dodoma ni watu wa heya chalumba.

Pia Dodoma iliathiriwa na watangulizi wake ambao walichelewa sana kujitambua, mfano Malecela mpaka anastaafu alikuwa hajitambui, pia akina askofu Chiwanga walikuwa ni wabinafsi tu wamechangia sana kuidumaza Dododma pamoja na kuwa makao makuu haiwezi kuchangamka kama DSM.

Kwa ujumla Dodoma haina fursa nyingi na kuwa kimbilio la watu wa makabila yote kama ilivyo DSM, zaidi ya kuwa makao makuu na makao ya Bunge hakuna jipya hivyo mleta mada ukija Dom jipinde kweli kupata fursa.

Kuna wagogo wachache tu waliifanya Dodoma ichangamke lakini bahati mbaya walitangulia mbele za haki nao ni Alexander Kanyamala na Andrea Masikini pia wako watu kama Lod SWAI wamejitahidi kuipaisha Dom kwa kiasi chao lakini hawakupata support ya wawekezaji wengine sababu kuu ikiwa ni ubinafsi wa akina Job Lusinde, Severin Supa, Pancrious Ndejembi na Chizomoche yake n,k

Ni hayo tu mleta mada kama mengine nimesahau utanikumbusha.
DODOMA kuna fursa nyingi sana hasa kwenye kilimo cha umwagiliaji na kilimo cha zabibu
Tukianza na umwagiliaji dodoma kwa sasa inakua kwa kasi na mahitaji yanaongezeka hivo kilimo cha umwagiliaji ni deal kwa dodoma na nakupa mfano moja mimi nipo fika apaa mwaka jana nkapata eneo CHIKOPELO na nalima vitungu na nyanya na mambo yanaenda safii
Sasa nmepata shamba la zabibu kijiji cha Nkome na nmechimba mitaro teari
 
Pia dodoma maeneo ya bahi kuna chumvi uki wekeza unapiga hela unaeza ukaingia ubia na kiwanda cha chumvi ukawa unawapelekea ama ukafungua kiwanda kidogo kama una hela
 
Dom inakua bana, sikuiona kwa miaka mitatu, juzi nimepita mji umekua mno, ukiungana toka kule stand mpaka singida road kule.. Aisee itakua balaa, naambiwa dom mbuzi hawatoshi
True hapo serikali imeongeza chachu ya ukuaji lakini even before ilikuwa inakua vizuri tu maana ni mjo uko junction.
Zamani ilikuwa ukiwasikiliza wapita njia wanavyosimulia Dom au Singida au Tabora unaweza sema labda huko ni Kuna nuka njaa na umaskini na watu Wana dhiki kuu kumbe ni wapuuzi tu saizi ukifika hiyo miji imekua Sana.Mfano Leo hii Manispaa ya Singida huwezi linganisha na Moshi,Shinyanga,Songea na Imeizidi hata Iringa kwa ukubwa tofauti yake na Iringa ni kwamba Kairinga kana tumagorofa turefu twingi twingi
 
Itachukua muda kiasi kwa Dom kuwa eneo zuri kwa fursa maana bado mzunguko wa pesa bado haujaimarika maana population iliyopo fedha yake ni ya kipindi wafanyakazi mwisho wa mwezi, wanachuo mpk vyuo vifunguliwe, wabunge mpk kipindi cha bunge nk. Ili paendelee lzm wafanyabiashara wavutike waelekeze shughuli zao huko wanaweza kusaidia na wanawezaje kufanya hivyo mazingira yawe rafiki
Huo mzunguko unaulinganisha na miji ipi kwa mfano? Dom iko Bora zaidi kushinda miji mingi ya Tzn nje ya Dar labda na Mwanza Ila kwingine nako Kuna pesa za msimu kutegemeana na shughuli.Mikoa ya kilimo ina msimu,mikoa ya utalii ina msimu Sasa si Bora hapo Dom wafanyakazi ni wengi pesa ipo mda mwingi?
 
Mkuu ebu usiwe mpotoshaji, kwasasa Dodoma inajengwa biashara nyingi zikiwemo Mashule, Vituo vya mafuta, nyumba za ibada, Mall's, supermarket's, Viwanda, Shops nakadhalika.
By the way, nikiitazama Dodoma ya miaka tatu nyuma na Dodoma ya leo, ni vitu mbili tofauti.
Kwakifupi Dodoma ni jiji linalokua kwa kasi sana.
Hata itakapo kamilika bandari kavu na ring roads zikikamilika pamoja na SGR, hakika Dodoma haitokua kama leo mnavyo isimulia.
Alafu, mbadiliko sio kitu cha siku moja, maana hata hiyo Mwanza/Dar ilichukua muda kidogo hadi ikafikia hivyo ilivyo leo

Dodoma imebadilika na kukua sanaa kwa mtu aliyeifahamu toka zamani ila kwa mtu aliyetoka Dar leo na kuhamishiwa Dom ataona kama ni masikhara.

Ubaya wa Dom inakuzwa na siasa yaani ukiangalia investments kubwa ni za serikali na si watu binafsi. Tena kheri baada ya watumishi kuhamia nadhani mji utakuwa una uhai maana zamani vyuo na bunge vikifungwa mji unazima

Uzuri wa Dodoma itaendelea kuwa middle class city. Toka nimeifahamu Dom ni ya watu middle class na wapo westernized kiasi ukilinganisha na majiji makubwa kama mwanza hivyo biashara kama malls, private schools kubwa, vyakula, Vinywaji na recreational centres lazma zipeform vizuri zaidi.

Pia mji wa Dodoma unakuzwa kutoka kwenye centre ya siku zote hivyo naamini utakua vizuri tofauti na miji mingine
 
Soma title vizuri mzee imeandkwa "Jiji la Dodoma na MAISHA KIUJUMLA" unaelewa maana ya maisha kiujumla? au unasoma title nusu nusu
Mkuu shida ni kwamba sababu uliyotoa ni yakitoto sana ukilinganisha na mjadala, maji ya chumvi ni natural factor so unataka wakazi wa Dodoma wayabadilishe[emoji23][emoji23][emoji23],

Afu kitu kingine changia mada ukiwa na fact kwamba Dodoma mara ya mwisho umekuja lini, sio umepita njia tu unachangia mada

Dodoma ya sasa sio kama ya zaman mkuu
 
Kwanini mtu aweke kiwanda Dodoma na si Dar ambako kuna 80% ya soko lake?!
Means kiwanda kinazalisha kwa ajili ya Dar tu,
[emoji23][emoji23][emoji23]Labda kama kiwanda cha mikate na maandaz.

unamaanisha hamn export mikoa mingine,
Iyo 80% unayosema soko ni Dar tu kumbuk pia kuna whole seller wanawez chukua iyo bidhaa kiwandani na wakauza kwa suppliers wadogo wa mikoani as asilimia kubwa ya watu wanatoka mikoani kuja Dar kufunga mzigo

Na kuiangalia kwa mfano mikoa ya magharibi na nyanda za juu kusini ni rahis kufika Dodoma kuliko Dar na hiyo itapunguza Cost

Point yako itakua na maana kama tu icho kiwanda Labd kinatengenez nn sijui ambacho target ni Dar pekee na sio sehemu nyingine
 
Hahaaa ivi kila mwekezaji akija na fikra izo nchi hii viwanda vitakua dar tu
Pwani kuna viwanda vingi tu tujiulize watu wake hali zao zakimaisha vipi? Haijalishi uwingi wa viwanda na sababu kubwa ni kuwa mishahara ni midogo sana ya kumfanya mfanyakazi kuweza kumudu kutumia pesa anapata ya kujikimu tu ya siku kama vibarua tu. Siku dry port wakifungua Dodoma na SGR kukamilika itakuwa sehemu ya kuchukulia mizigo mikoa mingi sababu Dodoma ni karibu na mikoa mingi fursa zipo na zitakuja taratibu na zaidi Airport mpya wakimaliza kujenga itafungua fursa nyingi tu. Wafanyakazi wa serikali kwa standard yetu Tz tunawachukulia ndio middle class wanakopesheka kirahisi. Ukiona sehemu yoyote wahindi wanaanza kuongezeka basi ujuwe fursa zinaanza kufunguka... wanajuwa kunusa...
 
Means kiwanda kinazalisha kwa ajili ya Dar tu,
[emoji23][emoji23][emoji23]Labda kama kiwanda cha mikate na maandaz.

unamaanisha hamn export mikoa mingine,
Iyo 80% unayosema soko ni Dar tu kumbuk pia kuna whole seller wanawez chukua iyo bidhaa kiwandani na wakauza kwa suppliers wadogo wa mikoani as asilimia kubwa ya watu wanatoka mikoani kuja Dar kufunga mzigo

Na kuiangalia kwa mfano mikoa ya magharibi na nyanda za juu kusini ni rahis kufika Dodoma kuliko Dar na hiyo itapunguza Cost

Point yako itakua na maana kama tu icho kiwanda Labd kinatengenez nn sijui ambacho target ni Dar pekee na sio sehemu nyingine
Sawa.
 
Back
Top Bottom