Jiji la Dodoma kibiashara na kimaisha kwa ujumla

Jiji la Dodoma kibiashara na kimaisha kwa ujumla

Hakuna unafuu kama mji wa Kigoma, vyakula vyote bei juu tofauti na kigoma ndizi bei chini , unga bei chini, samaki mgeb uka bei chini , maharage bei chini, mafuta mawese bei chee, Dodoma kila kitu bei juu, hadi nyumba za kupanga, mfano wapemba wakija bungeni hupendelea kupanga vyumba vya maeeneo ya chinangali na chang`ombe
vyumba bei rahisi tena wanapanga wapemba wanne chumba kimoja cha shs 10000, DODOMA channel za biashara pia siyo super maana hakuna viwanda kwa hiyo biashara zote za jumla inabidi kuagiza bidhaa toka DSM MFANO CEMENT , MABATI na SUKARI.

Dodoma ni mji mkuu kwa sasa fursa pekee ni viwanja na nyumba za kupanga kuwa bei ju, pia unaweza ukapata bahati nyuma yako ikapangishwa na ofisi za serikali au shirika au NGO yoyote.

Dodoma na wagogo wake ni ngome ya CCM hivyo ni watu wa kuridhika tu hawawezi kudai haki au fursa mfano watu wa Mbeya hili nalo ni tatizo la Dodom ni watu wA heya chalumba.

Pia Dodoma iliathiriwa na watangulizi wake ambao walichelewa sana kujitambua, mfano Malacela mpaka anastaafu alikuwa hajitambui, pia akina askofu Chiwanga walikuwa ni wabinafusi tu wamechangia sana kuidumaza Dododma pamaja na kuwa makao makuu haiwezi kuchangamuka kama DSM

Kwa ujumla Dodoma haina fursa nyingi na kuwa kimbilio la watu wa makabila yote kama ilivyo DSM, zaidi ya kuwa makao makuu na makao ya Bunge hakuna jipya hivyo mleta mada ukija Dom jipinde kweli kupata fursa.

Kuna wagogo wachache tu waliifanya Dodoma ichangamke lakini bahati mbaya walitangulia mbele za haki nao ni Alexander Kanyamala na Andrea Masikini pia wako watu kama Lod SWAI wamejitahidi kuipaisha Dom kwa kiasi cao lakini hawakupata support ya wawekezaji wengine sababu kuu ikiwa ni ubnasi wa akina Job Lusinde, severin Supa, Pancrious Ndejembi na Chizomoche yake n,k

Ni hayo tu mleta mada kama mengine nimesahau utanikumbusha.
Umejaa chuki na ccm ndio maana unaponda sana Dodoma,,,,,



India habari za usiasa kisha weka mambo halisi sio chuki




By the way Dom iko poa sana kibiashara sema tu we una mahindi ya kusaga unataka ukauzie stendi ya daladala pale 7 7,,,, yaani kiufupi hujui ramani ya biashara,,.
 
Wengine ni wadau wazuri sana wa biashara wa jiji hili ila kiuhalisia Dodoma pagumu sana tena sana. Wafanyabiashara wao akina Kazimoto na Cityboys hawana mawazo ya kuangalia mbele wanajiona wamelishika jiji. Watunga sera akili zao zimegota hawana hata akili mpya. Huu mji unatakiwa uwe na viwanda vingi sana. Nenda sijui soko jipya limepewa jina la ajabu kweli hakuna kitu pale. Stendi haina vichochoe vya biashara kabisa. Jambo la kushangaza serikali ya CCM baada ya ule mradi mkubwa chinese Mall wapeleke Dodoma, wameamua kuujenga Dar pale stendi ya ubungo. Dodoma inahitaji viwanda kama 50 hivi ili kuleta uhai.
LM kazimoto au city boy s au Peter fashion hana idea mpya,,, kwanini usiweke ya kwako ili tuifate?


Sometym MTU anacoment kibabe wakati hana hata genge la nyanya,,,,..
 
Kwakuanza maisha jijini ni rahis sana sema tu usije kibabe,,,,, unapanga rent ya 200k unaanza na sofa Mara gari unajisahau kuwa umepanga bado,

Kifuatacho km utakuwa mfanya biashara utarudi kwenu siku inayofuata,,,,
Coz biashara nyingi ni za msimu,,,, wanaonufaika Dodoma ni wakulima hasa nafaka,,,,, kwasababu wengi wa wakazi hupenda kununua vya debe (mahindi, Michele, maharagwe n.k) kisha wanaweka ndani kwaajili ya kusota navyo mwezi mzima.
 
LM kazimoto au city boy s au Peter fashion hana idea mpya,,, kwanini usiweke ya kwako ili tuifate?


Sometym MTU anacoment kibabe wakati hana hata genge la nyanya,,,,..
Hahahahahaha mimi hao nawajua sana na nimekuja kufanyabiashara hapo. Wana mfumo wa ujima sana
 
Ukuaji wa miji huja automatic, ukiangalia historia ya kuanzia Paris, London, New York sijui hata Bagamoyo kibiashara mji unakua wenyewe na ikiisha unakufa pia. Huwezi kulazimisha kusisimua kisiasa wakati mtu anajua akiwekeza hela kias hicho hicho sehem nyingine atapata zaidi. Ndo uhalisia huo

Mbona kina Fresho na Jambo wamefungua viwanda shinyanga huko bila kusisimuliwa na mtu. Sio mwanza ambapo kuna shughuli tayari ila shinyanga inajikuta tu inahotaji uwekezaji wa namna hiyo

Kiwanda cha maji tu simpo hicho Asante cha Dodoma kimekuja kufunguliwa juzi juzi na bado kinasuasua

Makampuni yenyewe ya Dar niliyoyaona yamekimbilia Dodoma mengi ni ya Mikopo(Imarisha maisha, Lughano nk) na yale ya upimaji/uuzaji viwanja(kina Global Fortune, infinity nk) wote wanalenga wafanyakazi

Hao kina Feza Schools, Shoppers plaza sijui Nakiete wenyewe nao ni vibranch tegemeo hao wafanyakazi tu pia

Labda tuendelee kuangalia over time wananchi wote kwa pamoja watachangamka na kuchangamsha mji kwa ujumla ila kwa sasa nadhani bado kwakweli
Eti bado, we ulitaka kesho ukiamka asubuhi ukute Dodoma ipo kama Dar.
Watu wengine buana
Hivyo vikampuni ulivyovitaja awali vilikuepo?
Kama jibu ni la basi ndio kukua kwenyewe huko.
 
Eti bado, we ulitaka kesho ukiamka asubuhi ukute Dodoma ipo kama Dar.
Watu wengine buana
Hivyo vikampuni ulivyovitaja awali vilikuepo?
Kama jibu ni la basi ndio kukua kwenyewe huko.
Mada imekuzidi kimo
 
City Boys, Kazimoto kina Frank Mtei na Priscus Alex eti ndo mafogo wa Dodoma[emoji23][emoji23]
Bhanji
Shabiby
Marehem Maimu

Labda watu watoke dar aisee ndo watakuja kuichangamsha
R.i.P Maimu......
Kwanza inaonekana ulikua mtu mwenye wivu na husda tele, na kuwajua walio kutangulia kwenye biashara haimaanishi basi eti Dodoma nzima uliifahamu.
Na hata huyo Maimu marehemu, alifariki akiwa tayari amesha fikisika.
Naomba nisiwe msemaji wa majina ya walio tangulia kufanikiwa, lakini nivyema nikaweka wazi kwamba mafanikio ni Jambo jema, na ubaya wa watu kama wewe ni kutokukubali kwamba tayari ulifika sehem na ukakuta wapo walio fanikiwa kabla yako, (hata ukiwaita matajiri) bado sio mbaya kwasababu ukweli ni kwamba walikutangulia tayari mkuu.
 
Kutokana na uchumi mdogo hivyo soko la vitu vikubwa vikubwa hamna.
Mazingira na raw materials production ni ndogo huwezi kwenda kufanya biashara kubwa sehem ambayo hamna availability ya resources wala market.

Kwa Dodoma biashara ni
Vyakula
Nguo
Usafiri (sio usafirishaji wa mizigo)
Bakery
Nyumba/apartment
Bar,pubs na restaurant (sio hotel na lodge)
Barbershop na Cameramen
Mkuu ebu usiwe mpotoshaji, kwasasa Dodoma inajengwa biashara nyingi zikiwemo Mashule, Vituo vya mafuta, nyumba za ibada, Mall's, supermarket's, Viwanda, Shops nakadhalika.
By the way, nikiitazama Dodoma ya miaka tatu nyuma na Dodoma ya leo, ni vitu mbili tofauti.
Kwakifupi Dodoma ni jiji linalokua kwa kasi sana.
Hata itakapo kamilika bandari kavu na ring roads zikikamilika pamoja na SGR, hakika Dodoma haitokua kama leo mnavyo isimulia.
Alafu, mbadiliko sio kitu cha siku moja, maana hata hiyo Mwanza/Dar ilichukua muda kidogo hadi ikafikia hivyo ilivyo leo
 
Dodoma sahivi viwanja ni ghali kidogo na watu wamejenga sana sasa hivi pembezon mwa mji hivo kama unayo cash ni muda wa kuchumbia maeneo badae faida ipo kubwa mno.
Wachache watakuelewa mkuu, zaidi naona wengi wanaponda tu kwasababu wanaichukia sisiem na mwenye kiti wake
 
Hahahaa hamna kitu huyo Dodoma sema ukishatika kidogo tu unakaa meza moja na watu wakubwa basi na vibastola vyao vya kutushia watu wanaanza kujidai “Kipofu mwenye miwani nyeusi”

Kama ni hivyo mbona hakumsaidia ndugu yake nani yule Mselia sijui aliyejiua shambani Msalato baada ya kukutwa na magumashi enzi viroba vinafungiwa

Kuna siku nimekaa na mtu ananiambia hadi Mmanga eti afisa hahahaaa

Mmanga huyu huyu wa Korie sijui Scania na Martin Luther??

Dodoma pagumu sana pale mpaka kushikilia mfereji wa pesa sio kama mikoa mingine
Mkuu, nilidhani ungeweza kuleta hoja za maana.....
Kumbe umekuja na mipasho (personal attacks).
Na usidhani eti kwakuwafahamu hao matajiri wa zamani wa Dodoma ndipo tutakuona unajua sana, zaidi naona kama unazungumzia mambo binafsi/hulka na maisha ya watu ambao wapo kila mahali duniani.
 
Boss elimu yako na vyeti vyako weka kabatini. Mimi naongea kwenye viatu vya mwekezaji sio mwanasiasa au mchumi wa makaratasi. Kwanini niwekeze Dodoma ambako soko lake halifiki hata 10% ya Dar? Kwanini nisiwekeze Dar ambako nina uhakika wa soko kubwa Tanzania nzima?
Kakuuliza kuhusu uchumi lakini yaelekea haujui uchumi wenyewe, gdp ya tz 70% ni dar ilhali dar ni 10% ya watz wote, ukiweka kiwanda dom wakati soko kuu ni dar utaongeza gharama za usafirishaji wa bidha pengine na malighafi
 
Wengi wao ni wapuuzi kwa michango yao ya kijinga,Dom ni manispaa tangu enzi za miaka ya 80 na Hadi sasa ni jiji Kuna huduma na biashara zote zinasapoti maisha vizuri kabisa.
Kwa sasa mji unakua kwa Kasi Sana sasa umewahi ona wapi kwenye watu kukawa hakuna pesa?
Dom inakua bana, sikuiona kwa miaka mitatu, juzi nimepita mji umekua mno, ukiungana toka kule stand mpaka singida road kule.. Aisee itakua balaa, naambiwa dom mbuzi hawatoshi
 
Dodoma sio pa kuishi yaani[emoji51]
 
Basi sawa mawazo yako ndio haya. Hapa mawazo ni kuchangamsha jiji kiuchumi ili liweze kuisaidia Dar.
Uchumi unataka kiwanda kijengwe pale penye uhitaji, pale penye biashara, pale penye watu.

Wazo zima la kuhamishia mji mkuu kwenda Dodoma ni la kisiasa zaidi ya kiuchumi.

Ndiyo maana serikali imeweka nguvu sana kuchangamsha mji miaka yote, lakini mji hausitawi.

Ni kama unakwenda kulima jangwani kwa kutumia nguvu sana, unapeleka maji sana, lakini hali ya hewa ya asili ya eneo hilo hairuhusu kilimo. Unalazimisha tu.

Kwa nchi ambayo ina fedha chache za kigeni, na zina kazi nyingi, zoezi zima la kuhamisha mji mkuu lilikuwa "biashara kichaa".

Na mpaka leo bado ni biashara kichaa.

Ila wabongo tunapenda sana hizi white elephant pdojects za biashara kichaa.
 
Back
Top Bottom