Jiji la Dodoma kibiashara na kimaisha kwa ujumla

Jiji la Dodoma kibiashara na kimaisha kwa ujumla

Eizyek

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2019
Posts
800
Reaction score
2,780
Wapendwa habari ya mchana naomba kujua kuhusu jiji la Dodoma kibiashara na kimaisha. Je mtu kama unataka kuanza maisha kuna unafuu?

20201007_133004.jpg
 
Hakuna unafuu kama mji wa Kigoma, vyakula vyote bei juu tofauti na Kigoma ndizi bei chini, unga bei chini, samaki mgebuka bei chini, maharage bei chini, mafuta mawese bei chee, Dodoma kila kitu bei juu, hadi nyumba za kupanga, mfano wapemba wakija bungeni hupendelea kupanga vyumba vya maeneo ya Chinangali na Chang`ombe.

Vyumba bei rahisi tena wanapanga wapemba wanne chumba kimoja cha shs 10000, DODOMA channel za biashara pia siyo super maana hakuna viwanda kwa hiyo biashara zote za jumla inabidi kuagiza bidhaa toka DSM MFANO CEMENT, MABATI na SUKARI.

Dodoma ni mji mkuu kwa sasa fursa pekee ni viwanja na nyumba za kupanga kuwa bei juu, pia unaweza ukapata bahati nyuma yako ikapangishwa na ofisi za serikali au shirika au NGO yoyote.

Dodoma na wagogo wake ni ngome ya CCM hivyo ni watu wa kuridhika tu hawawezi kudai haki au fursa mfano watu wa Mbeya hili nalo ni tatizo la Dodoma ni watu wa heya chalumba.

Pia Dodoma iliathiriwa na watangulizi wake ambao walichelewa sana kujitambua, mfano Malecela mpaka anastaafu alikuwa hajitambui, pia akina askofu Chiwanga walikuwa ni wabinafsi tu wamechangia sana kuidumaza Dododma pamoja na kuwa makao makuu haiwezi kuchangamka kama DSM.

Kwa ujumla Dodoma haina fursa nyingi na kuwa kimbilio la watu wa makabila yote kama ilivyo DSM, zaidi ya kuwa makao makuu na makao ya Bunge hakuna jipya hivyo mleta mada ukija Dom jipinde kweli kupata fursa.

Kuna wagogo wachache tu waliifanya Dodoma ichangamke lakini bahati mbaya walitangulia mbele za haki nao ni Alexander Kanyamala na Andrea Masikini pia wako watu kama Lod SWAI wamejitahidi kuipaisha Dom kwa kiasi chao lakini hawakupata support ya wawekezaji wengine sababu kuu ikiwa ni ubinafsi wa akina Job Lusinde, Severin Supa, Pancrious Ndejembi na Chizomoche yake n,k

Ni hayo tu mleta mada kama mengine nimesahau utanikumbusha.
 
Hakuna unafuu kama mji wa Kigoma, vyakula vyote bei juu tofauti na kigoma ndizi bei chini , unga bei chini, samaki mgeb uka bei chini , maharage bei chini, mafuta mawese bei chee, Dodoma kila kitu bei juu, hadi nyumba za kupanga, mfano wapemba wakija bungeni hupendelea kupanga vyumba vya maeeneo ya chinangali na chang`ombe....
Shukrani sana kwa ushauri mzuri
 
ukitaka kupambana na maisha magumu na ya kusaga meno kaishi dodoma au dar, kheri dar unaweza pambana kwenye biashara ila dodoma kama bunge hakuna na vyuo vikifungwa unaweza kulia na kusaga meno
Shukrani sana
 
Wapendwa habari ya mchana naomba kujua kuhusu jiji la Dodoma kibiashara na kimaisha je mtu kama unataka kuanza maisha kuna unafuu?

View attachment 1592982
10% ya wakazi wa jiji la Dodoma ni wanafunzi wa Udom, Mipango na CBE. Kama utaenda kufanya biashara inayowalenga hao watu utafanikiwa sana. Pia kundi jingine ni lile la maafisa wa serikali wana hela zao za ufisadi kidogo.

Biashara zinazolipa Usafiri (boda boda, bajaj, Daladala)
Vyakula
Bar, pub and restaurants

NB,ukienda kipindi vyuo vimefungwa, wabunge hawapo Dodoma ni sawa na Makambako.
 
Wengine ni wadau wazuri sana wa biashara wa jiji hili ila kiuhalisia Dodoma pagumu sana tena sana. Wafanyabiashara wao akina Kazimoto na Cityboys hawana mawazo ya kuangalia mbele wanajiona wamelishika jiji. Watunga sera akili zao zimegota hawana hata akili mpya. Huu mji unatakiwa uwe na viwanda vingi sana.

Nenda sijui soko jipya limepewa jina la ajabu kweli hakuna kitu pale. Stendi haina vichochoe vya biashara kabisa. Jambo la kushangaza serikali ya CCM baada ya ule mradi mkubwa chinese Mall wapeleke Dodoma, wameamua kuujenga Dar pale stendi ya Ubungo. Dodoma inahitaji viwanda kama 50 hivi ili kuleta uhai.
 
Back
Top Bottom