1. Bei unazoziona sio sahihi, ongea na seller kuhusu bei husika.
2. Postal shipping wanaitumia kwa sample tu, full mzigo wanataka express.
3. Make sure mnanegotiate na kulipana ndani ya Alibaba system (Trade assurance)
 
Ahsante mkuu kwani na mimi nilikia nataka ku place order ila nilipata matatizo kidogo kwa namana ya kufanya trusted shipping ila umenifungua akili kwani nilijua forwarding companies ni za magari tuu na bidhaa zingine kubwa
 
Heloo JF.Hakika huko Customs department+TRA kwenye airport zetu kuna shida nyinginyingi, na si mara ya kwanza kusikia complaints kutoka kwa wadau pengine wazoefu watupe tricks.
Package imechukua 4 days kutoka China kufika TZ ila sasa ndio hivo, bongo bahati mbaya madudu lazima yawepo.
Mzigo umefika 15 July Nilijaza c34 form na kutuma documents zote kama invoice, TIN certificate, LOA by 17 July, na kufikia 22 July nikapewa assessment form na payment note yenye gharama za VAT+, TBS, Custom processing fee pamoja na issue nyingine according to TRA, payment receipts nilituma siku hiyogiyo. sasa mara leo naambiwa invoice yako imekataliwa mara nin, najiuliza hilo kadirio la kodi lilifanyikaje kwa kutumia invoice ambayo ni invalid/incomplete ?.
.Leo niliwapandia hewani wame acknowledge makosa yao, I hope this week nitapokea mzigo wangu.
 
mm hua natumia Aliexpress ni nzuri saana na ni bonge ya market af iko very simple na wanakata pesa direct kwenye account yako ys master Card
 
Waweza kunisaidia namna ya kufanya malipo ya kodi Tanzania kwa mzigo ulioingia kutoka nje mkuu? Naona kuagiza mzigo kutoka nje hakuna shida, shida ukishafika hapa Tz namna ya kuupata, wanaohusika wanakuwa ni wa ghali sana kukuhudumia. Nisaidie hapo tu.
 
Kampuni ya usafirishaji wakikupigia simu au wewe utaona kwenye tracking kuwa Mzigo umefika Julius Nyerere International Airport (Incase of Air Shipment) kinachofuata ni Customs Clearance, Unahitaji kuwa na TIN Certificate, Commercial Invoice ya bidhaa uliyo nunua ili TRA waweze kukupa kadirio la Taxes/Duties.
kama hutaki kutumia wakala wa clearence mchek members mwenzetu humu anaitwa Mwl RCT atakupa mwongozo maana mimi nilifanyiwa clearance na Sunfresh LTD sababu nipo mbali sana na Dar kwahiyo kama ningesafiri gharama zingekuwa kubwa zaidi.
 
Basi Mwl RCT popote ulipo naomba unisaidie kwa hili, haiwezekani kufanya clearance mwenyewe online or otherwise hadi ufike Dar es salaam?
 
Basi Mwl RCT popote ulipo naomba unisaidie kwa hili, haiwezekani kufanya clearance mwenyewe online or otherwise hadi ufike Dar es salaam?
Kwangu hawa clearance agents nawaona kama some kinds if vishoka. Ambapo mtu unapewa ugumu wa kupata mzigo wako kama hutaki kutumia hao jamaa.
 
Usaidizi kwa mfano nimenunua labda kama kitabu kimoja au computer moja nayo inahitajika kuilipia kodi na kuufuata hyo computer hadi J.k Airport
 
Kaka
Mkubwa,nimejaribu kujiunga na paypal lkn nimekwama pale sehemu ya kujaza adress line 1 na adress line 2. Hizo adress line ndo zp?
 
Nauza Betri za Energizer zinazotumika kwenye Radio, Rimoti za TV, magetin na kwenye magari, pia kwenye tochi, vipimo vya Maabara, vipimo vya uzito na kadhalika


Tupo Calico complex, Tazara Dar
Bei ni poa kabisa
Nipigie 0784112347
0769017151
Unaletewa Popote ulipo
 
"Parcel Status Arrived in destination country; awaiting customs clearance"
- Je ni kampuni kani imesafirisha bidhaa yako?
- Fanya mawasiliano nao, Kuna taarifa wanahitaji, ili taratibu zingine zifuate.
 
- Je ni kampuni kani imesafirisha bidhaa yako?
- Fanya mawasiliano nao, Kuna taarifa wanahitaji, ili taratibu zingine zifuate.
kwenye track nimetumiwa tracking Number
kwenye shipment wameandika
Logistics company:
AliExpress Standard Shipping

Niende nikaulize posta au?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…