Habari Watanzania, Heri ya miaka 58 ya uhuru!

Bila kupoteza muda ngoja tuongee namna ya kununua vitu kutoka nchini China hasa kupitia platform ya Alibaba (Made in China).

Kwanza kabisa Alibaba sio platform peke yake ya kuweza kununua vitu nchini China kuna platforms kama Global sources, Made-in-China, Banggood na kadhalika.

Najaribu kufikiria unafahamu kuingia kwenye mtandao wa alibaba na unaweza kutafuta bidhaa. Sasa nataka kukuonesha namna ya kuwa mbele ya wauzaji wa kichina kwenye platform ya alibaba na vitu vya kufanya kuepuka kupoteza muda na kuumia kichwa mbeleni.

1. Bidhaa (Product)
Hakikisha muuzaji wa kichina (supplier) anafahamu nini kabisa unataka kununua hapa inamaanisha (products specifications). Hakikisha unaeleza vizuri kwa ufanisi na kiundani unataka nini hasa kwenye bidhaa yako. Ushauri Chukua dakika 10-15 kuandaa maelezo ya bidhaa, vitu kama
- Size (Ukubwa)
- Material (Materio)
- Grade (kiwango cha ubora)
- Application (In use)
- Packaging (uhifadhi wake)
- Quantity (Uwingi)
- Shipping Terms (namna ya usafiri)
- Target Price (Bei uliyopanga) HII NI MUHIMU SANA

2. Fanya Kuhakiki (Evaluation)
Mara zote unapoongea na muuzaji wa kichina ( supplier ) jaribu kuhakikisha vitu vingi tu nje na mbali ya bei ambayo watu wengi wao wanaangalia sana hii na kukosea kuto kuangalia vitu vingine. Jaribu kufirikia kwa namna hii
- Je wanajibu message zako kiusahihi na kwa wakati ) Are they responsive?
- Je wanauliza maswali yanayoendana na nini unataka katika bidhaa yako au wanakupa tu maelezo ya bidhaa zao?
- Je wanapicha za bidhaa unazozitaka wewe?
- Je mnaweza fanya mawasiliano kwa kuwapigia calls, whatsapp call au skype?
- Je wao ni watengenezaji au wao ni kampuni ya kuuza na kununu ( Manufactures Vs Trading company) Hii tutaiongelea siku zijazo
- Je wanatoa maelezo kiuwazi au kuna vitu wanaficha kuuliza?
- Nchi zipi sana wanauza hiyo products zao? Hii ni kubwa sana kwasababu hii inaweza kuonesha ni UBORA gani ambao hawa wanatengeneza.


3. Mazungumzo zaidi ya Biashara (Negotiations)
Wachina wanamsemo unasema “一分钱一分货” “Yi fen qian Yi fen huo” maana yake "unapata unacholipia"
Hii inamaanisha sio kila wakati ufanye manunuzi ya bei ya chini chini sana, mara nyingi bei za chini na ubora wa bidhaa huendana sana.

Wakati unapokua unaongea na wauzaji wengi kwa wakati mmoja unapotaka biadhaa jaribu kuweka mahusiano ya muda murefu unapoengea nao na useme " unataka biashara ya muda mrefu sio biashara ya siku moja tu" kwahiyo ni vizuri kutengeneza urafiki nao ( Hii ni mtazamo wa biashara wa kichina)

Pointi ya kubeba, hata kama una haraka vipi at least ongea na wauzaji zaidi ya 3 kujua vizuri bei ya bidhaa unayoitaka.

Pia Jaribu kuulizia Bei za bidhaa zako zikiwa na uwingi tofauti, kwasababu katika ulimwengu wa wachina uwingi ndiyo kila kitu . Unaweza uliza bei ya piece 5,000 na Bei 50,000 ukakuta gap lililopo ni kubwa sana. Katika mazunguzo zaidi, usisahau kuongelea bidhaa kuwa nyingi.

4. Hakikisha Kimtandao (Online Research & Due Diligence)
Sio kila king'aacho ni almasi, Yes ni kweli sio kila muuzaji wa kichina ni wa kweli, hakikisha unapitia maelezo yake vizuri kuogopa kuibiwa na kudanganywa mtandaoni. Yes watu wanaibiwa kila siku na kila saa kwa wauzaji wapo kwenye mitandao ya kina alibaba. Kwa teknolojia ya photoshop na kuedit vitu, hata vijana wa chuo wanaweza weka profile zao kwenye alibaba na kuuza.

5. Uliza Sample (Sample)
Baada ya kuona huyu supplier ni mzuri na unaweza kumuamini kwa kiwango kikubwa, na bei nakila kitu kimekamilika, wakati mzuri wa kuomba Sample.

Hapa hatuongelei imani tu kwa kuamini kwa macho, omba SAMPLE utumiwe uone. Sample inaweza tumia siku 5-12 kufika kwa DHL, Fedex na wengine lakini ni vyema zaidi ya kuanza kutengeneza vitu vyenye uwingi mkubwa na vikawa tofauti na unachokihitaji.

6. Pokea Sample (Evaluate Sample)
Ihakikishe sample yako kama ipo sawa na kile unachokihitaji, kama unataka kubadirisha na kufanya design yako pia ni muda sahihi wa kufanya hivyo.

7. Purchase Order (P.O)
Unaponunu kitu chochote kwenye mtandao wa alibaba au platform ya China au hata kwa mikataba ya uso wa uso hakikisha unakua na Purchase order ambayo itakulinda kwa siku za usoni. HAKIKISHA Purchase order inakua na maelezo yote unayotaka kuanzia

8. Payments
Unapofanya malipo ya aina yoyote kwanza kabisa hakuna 100% inalipwa bila kupata kitu chochote upfront.
Hakuna standard inayosema lazima ulipe 30% advance payment na baadaye ulipe 70% hii ni imekua kama kawaida lakini kuna wauzaji ( supplier) wanataka 50% advance na 50% kabla hawajatuma kwa meli.

Unaweza kuongeza zaidi na mnaweza kubadirisha mawazo namna mnavyotaka iwe.

Usikubali kutuma kwa njia ya Western Union, mara nyingi 98% ni utapeli. Kwa order ya aina yoyote hakikisha unafanya Bank Transfer.

DIRTY TRICK: HAKIKISHA MPOKEAJI WA PESA NA JINA LA USAJILI WA KAMPUNI AU KIWANDA VINAFANANA. KAMA HAIFANANI HII NI BENDERA NYEKUNDU KABISA KUNA MCHEZO UNAWEZA FANYIKA WA UTAPELI ( KUA MAKINI)

9. Usafirishaji (Shipment)

Inashangaza kwamba watu wananuna kontena na kontena, lakini hawakagui mzigo kabla haujasafirishwa kutoka China kuja Tanzania. Nimesikia case sio moja ni zaidi ya tano watu wanaagiza A wanapokea Z ( wanapokea tofauti na wanachoagiza). Hakikisha unafanya ukaguzi kabla mizigo yako haijaondoka kuanza safari kuja Tanzania.

Kuna makampuni ya ukaguzi ambayo yanafanya hii, lakini mengine yanakua na deal na viwanda kuwaandikia report kua mzigo ni sawa japokua ni mzigo mbovu. (Kuwa makini)

Baada ya kufanya ukaguzi ndiyo unaweza kuruhusu mzigo kuondoka na kuja sehemu husika.

Kiufupi hii ni namna unaweza kufanya unaponunua bidhaa kutoka China.

Kama unataka wasiliana nami unaweza nitafuta kwa number +255627637767

Karibu Pia ofisini kwangu Mikocheni, Hekima Garden kwa maelezo zaidi.

Asante.
 
Habari zenu wana jukwaa, JF ni mahali ambapo wapo wachuzi na wazoefu wa mambo ya mbalimbali. Kifupi JF haijawahi shindwa kitu.

Sasa basi hivi karibuni niliingia katika mtandao wa Alibaba nikiwa na lengo la kutafuta camera.

Nilipata camera nilizokuwa nazihitaji kwa bei tofauti, sasa basi baadhi ya seller wameweka namba zao za WhatsApp nikawacheki baadhi yao na mmoja tumefikia makubaliano na anataka nimlipe kupitia Western Union na yeye mzigo wangu ataniagizia kupitia DHL.

Kiukweli ukilinganisha na bei ya kupata hiyo camera kwa Tanzania ni karibia mara tatu yake.

Wadau lakini mimi naingia hofu kufanya malipo kupitia huo utaratibu kwa sababu naona tutakuwa tumefanya biashara nje ya utaratibu wa Alibaba, hivyo nahisi sitakuwa na uhakika wa usalama wa pesa zangu ikitokea yule jamaa ni tapeli.

Naomba mwenye uzoefu wa kufanya malipo kupitia Western Union wanisaidie je, naweza kuwa na control yoyote juu ya hela zangu mpaka nitakapo pata mzigo wangu?

Au nikishalipa ndo imetoka hakuna namna yoyote naweza rudisha hela zangu nisipopata mzigo wangu?

Ahsante nawasilisha.
 
:D :D unawezapigwa au usipigwe

siri ya kulipa nje ya Alibaba ( Trade Assurance ), ni bond kati ya wewe na muuzaji

nakumbuka mara ya kwanza kuagiza Alibaba, buyer alitaka nimlipe kwa nje ( Bank deposit ), nikagoma, nikalipa kwa ndani ( Trade Assurance )

ila baada ya purchases kama nne ivi kwa mda tofauti tofauti ( kila purchase inakaribia 300 usd ) , nikaanza mlipa nje, na gharama ikashuka kwa asilimia 60%

hawapendi kulipwa kwa ndani kwasababu ya makato makubwa
 
:D :D unawezapigwa au usipigwe

siri ya kulipa nje ya Alibaba ( Trade Assurance ), ni bond kati ya wewe na muuzaji

nakumbuka mara ya kwanza kuagiza Alibaba, buyer alitaka nimlipe kwa nje ( Bank deposit ), nikagoma, nikalipa kwa ndani ( Trade Assurance )

ila baada ya purchases kama nne ivi kwa mda tofauti tofauti ( kila purchase inakaribia 300 usd ) , nikaanza mlipa nje, na gharama ikashuka kwa asilimia 60%

hawapendi kulipwa kwa ndani kwasababu ya makato makubwa
Kwa hapo no kubet
 
Unatumia njia gani ili kujilinda kwa dharura yoyote itakayotokea
:D :D unawezapigwa au usipigwe

siri ya kulipa nje ya Alibaba ( Trade Assurance ), ni bond kati ya wewe na muuzaji

nakumbuka mara ya kwanza kuagiza Alibaba, buyer alitaka nimlipe kwa nje ( Bank deposit ), nikagoma, nikalipa kwa ndani ( Trade Assurance )

ila baada ya purchases kama nne ivi kwa mda tofauti tofauti ( kila purchase inakaribia 300 usd ) , nikaanza mlipa nje, na gharama ikashuka kwa asilimia 60%

hawapendi kulipwa kwa ndani kwasababu ya makato makubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom