Je, Hayati Magufuli alikabidhi nchi kwa jeshi?

ngaiwoye

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
1,749
2,437
Baada ya kumsikiliza mkuu wa majeshi mstaafu katika mahojiano yake na vyombo vya habari vya serikali, nimewaza jambo.

CDF Mabeyo anasema wakuu wa vyombo walijulishwa hali ya mkuu wa nchi, na walimhamishia Mzena ambapo waliweka restrictions za watu kumwona mgonjwa Ili apumzike na kupata MATIBABU.

Anasema hayati alipozidiwa aliomba mkuu wa majeshi atoe amri arudishwe nyumbani.. Hii kauli ni nzito sana sana kwamba hayati alitaka mkuu wa majeshi aamrishe arudishwe nyumbani akafie nyumbani (MAANA yake mkuu huyu ndie alikuwa na mamlaka wakati huo kuliko yeyote)

Anasema alipofariki wao wakuu wa vyombo ndio waliwajulisha viongozi kama PM, CS na BAADAE VP.. Tena wote hawakuwepo eneo la tukio...

Hatuoni mahala makamo wa Rais,mwanasheria mkuu, Wala judge mkuu Wala spika wakiwa na maamuzi yeyote. Kila kitu kilipangwa na jeshi.

Na baada ya misuguano ya zile siku mbili ambazo watu walisahau katiba kidogo, mkuu wa majeshi aliwakumbusha na ndipo tarehe 19 akaapishwa mh. Makamu wa Rais Ili awe Rais....

JE INAWEZEKANA RAIS MAGUFULI ALIACHIA NCHI KWA JESHI NA VYOMBO VYA USALAMA NA VYENYEWE KWA WELEDI MKUBWA VILIHAKIKISHA VIMEILINDA KATIBA NA KUISIMAMIA KAMA WALIVYOAPA NA KUHAKIKISHA MAKAMU WA RAIS ANAAPISHWA KIWA RAIS.

KAMA HIVI NDIVYO, BASI MKUU HUYU ATUNUKIWE TUZO YA AMANI NA HESHIMA KWA KUSIMAMIA KAYIBA YA NCHI NA KUILINDA
 
Rais amekufa sasa unategemea nchi iwe chini ya nani kwa wakati huo.? Au mlitaka mtangaziwe kwenye vyombo vya habari kuwa nchi ipo chini ya jeshi.? Ukweli utabaki kuwa nchi ilikuwa chini ya Mabeyo mpaka pale samia alivoapishwa.
Kwani katiba inasemaje Rais asipokuwa ofisini? Mfano wewe umechukua sick sheet ukaenda kutibiwa Mloganzila, ofisi yako huwa unamwachia nani? Au kwenu hamna delegation of authority?
 
Kwani katiba inasemaje Rais asipokuwa ofisini? Mfano wewe umechukua sick sheet ukaenda kutibiwa Mloganzila, ofisi yako huwa unamwachia nani? Au kwenu hamna delegation of authority?
Kwa kawaida makamu wa rais huapishwa ndani ya muda mfupi baada ya rais kufa, haya niambie nchi ilikuwa chini ya nani kwa zile siku mbili.?
Kumbuka jeshi halimtambui makamu wa rais.
 
Magufuli alipochukua sick sheet kwenda kutibiwa ofisi alimwachia nani? Jibu kwanza swali langu ambalo nimeuliza mwanzo kabla hujaleta lako
Mkuu usilete nadharia zako. Nchi bado ilikuwa chini yake mana kuumwa haimaanishi ameshindwa kuongoza nchi, kwan story za kuumwa zilianza lini.? Zungumzia akiwa amekufa au kama ni kuumwa bc iwe ni kuumwa ad kupelekea makamu wa rais kuapishwa huku rais akiwa hoi kitandani
 
Kwa mtazamo wangu, nchi ilikua chini ya M/Rais, ila afya ya JPM ilikua chini ya uangalizi wa Vyombo vya ulinzi na usalama. Na ni kwa sababu za kiusalama watu wengine walipigwa stop kwenda kumuangalia kwa sababu hawezi jua nani ana fanya kazi na nani.

Hata tetesi za kupelekwa kenya, huenda ni kweli, na sababu ikiwa ni kutokuamini mazingira ya nani.

Ikisema nchi ilikua chini ya jeshi, thats means serikali nzima ilikua inafuata amri ya CDF, kitu ambacho hakikua kweli. Wengi huku chini walikua hawajui hata kua kiongozi wao anaumwa.
 
Back
Top Bottom