Kwa maelezo ya Baba Mwita na kuwepo kwa kipindupindu jijini DSM RC yuko sahihi kutumia jeshi JWTZ

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
8,226
5,948
RC, hana mamlaka ya kutoa AMRI kwa JWTZ. Kanuni za jeshi zinamtaka yeye (RC) kufanya maombi kwa fomu maalum kwa Waziri wa Ulinzi ili jeshi lije uraiani. Lakini, kuna masharti, kabla ya kupeleka ombi, ni lazima eneo husika liwe na FUJO (riot) au shughuli hatarishi ambapo jeshi hupelekwa KULINDA MALI & UHAI wa raia.

Vinginevyo, hakuna namna kisheria RC atapewa ruhusa kutumia jeshi. Suala la KUFAGIA si moja ya mazingira yaliyotajwa kisheria. Hili ni jambo la KISIASA zaidi.

--
AMRI KWA JWTZ KISHERIA:

Jeshi la Wananchi (JWTZ) limeanzishwa chini ya ib. 147 ya Katiba ya nchi. Jukumu kuu la JWTZ ni KULINDA KATIBA ya nchi. Katika kutekeleza majukumu yake, Jeshi linafuata mwongozo wa Sheria ya Ulinzi wa Taifa (The National Defence Act, 1966), pamoja na Kanuni zake (Defence Forces Regulations). Pia, jeshi letu linafuata miongozo ya sheria na kanuni za Kimataifa kama "Laws of Armed Conflicts au LOAC" & "Geneva Convention", kama ilivyo kwa majeshi mengine.

UTEKELEZAJI WA AMRI (ORDERS):

JWTZ hutekeleza maagizo ya watu wenye nguvu & mamlaka kisheria kutoa maagizo hayo. Rais wa JMT amepewa mamlaka hayo chini ya ib. 148(1) ya Katiba ya nchi KUAMURU majeshi yote yaliyoorodheshwa kikatiba. Pia, mwanajeshi hutakiwa kupokea amri halali (lawful order) toka kwa askari mwenye cheo kilicho juu yake. Amri hizi zinazotolewa kisheria hutofautiana na kuna MIPAKA ya kimamlaka kwa maofisa wa jeshi kutoa amri hizo.

AGIZO KWA JWTZ KUJIHUSISHA NA SHUGHULI ZA KIRAIA:

Ukiacha Sheria ya Ulinzi wa Taifa, JWTZ inaongozwa na KANUNI zinazojulikana kama "DEFENCE FORCES REGULATIONS au DFRs). Ambapo ni DFR 1, 2 & 3; moja ni ya masula UTAWALA, nyingine FEDHA na ya mwisho inahusu mahakama za Kijeshi (Court Marshall). Kanuni hizi zimeweka utaratibu wa namna mwanajeshi atatoka Kambini na kwenda kujihusisha na shughuli za kiraia.

RAIS WA NCHI:

Rais ana mamlaka ya kuamuru majeshi yote chini ya ib. 148(1) ya Katiba. Isipokuwa, sharti lililowekwa kikatiba, Rais anatakiwa afuate matakwa ya sheria iliyotungwa na Bunge katika kutoa AMRI husika. Vinginevyo, Katiba inatambua AMRI yoyote itakayotolewa kinyume na takwa la sheria ni BATILI.

MSIMAMO WA SHERIA NA AMRI YA MKUU WA MKOA KWA JWTZ.

Kwa mujibu wa vifungu 21 - 23 vya Sheria ya Ulinzi wa Taifa, mwanajeshi amepewa MAMLAKA YA KIPOLISI (kwa muda tu) na jeshi la wananchi linaweza tu kupewa amri ya kuingia URAIANI iwapo kuna FUJO (riot) na jukumu lake kubwa ni KULINDA UHAI & MALI za raia. Basi.

Rais, kupitia sheria hii, kama atataka kuleta jeshi uraiani (military mobilisation), atatakiwa kutoa TANGAZO kwenye gazeti la Serikali.

RC, hana mamlaka ya kutoa AMRI kwa JWTZ. Kanuni za jeshi zinamtaka yeye (RC) kufanya maombi kwa fomu maalum kwa Waziri wa Ulinzi ili jeshi lije uraiani. Lakini, kuna masharti, kabla ya kupeleka ombi, ni lazima eneo husika liwe na FUJO (riot) au shughuli hatarishi ambapo jeshi hupelekwa KULINDA MALI & UHAI wa raia. Vinginevyo, hakuna namna kisheria RC atapewa ruhusa kutumia jeshi. Suala la KUFAGIA si moja ya mazingira yaliyotajwa kisheria. Hili ni jambo la KISIASA zaidi.

RAIS KUKASIMU MAMLAKA KWA RC.

Rais anaweza kukasimu baadhi ya mamlaka yake kwa RC lakini si mamlaka ya AMIRI JESHI MKUU. Haya ni mamlaka ya rais pekee, na hayakasimiwi kwa mtu yeyote. Utaratibu wa Rais kukasimisha madaraka fulani kwa RC umeelezwa kwenye Sheria ya Tawala za Mikoa (The Regional Administration Act, CAP 97) chini ya kifungu 6(1), ambapo sharti ni kwamba Rais anapokasimisha madaraka kwa RC, anatakiwa afanye hivyo kwa njia ya MAANDISHI kwa mkono wake yeye (rais), kisha yawe kwenye "Public Seal". Madaraka ambayo rais anaweza kukasimu, ni yale yenye utaratibu uliyotajwa na sheria ya Bunge au Kanuni (Principle or Subsidiary Laws) - key phrase kwenya s6(1) ni "under any written laws"

Kwa mujibu wa Sheria ya Tafsiri za Sheria (The Interpretations of Laws Act, CAP 1), kifungu 4 kimetoa tafsiri ya "written law", ambapo Katiba sio mojawapo. Kutokana na hilo, na kwa kuzingatia s6(1) ya Sheria ya Tawala za Mikoa, mamlaka ya "AMIRI JESHI" ya rais wa nchi, hayakasimishwi kwa Mkuu wa Mkoa.

Hivyo basi, Mkuu wa Mkoa hana UHALALI wa kuagiza jeshi la wananchi kufanya jambo lolote.

ANGALIZO:

ikitokea jeshi limeingia barabarani, likapiga watu, basi kisheria RAIS ANAHUSIKA katika hilo.

HITIMISHO:

Niliombe JWTZ itoke hadharani itoe ufafanuzi kuhusu hii kauli ya RC wa DSM maana raia walio wengi, wana uelewa mdogo na wana HOFU kutokana na namna RC alivyowasilisha ujumbe huu.
 
RC, hana mamlaka ya kutoa AMRI kwa JWTZ. Kanuni za jeshi zinamtaka yeye (RC) kufanya maombi kwa fomu maalum kwa Waziri wa Ulinzi ili jeshi lije uraiani. Lakini, kuna masharti, kabla ya kupeleka ombi, ni lazima eneo husika liwe na FUJO (riot) au shughuli hatarishi ambapo jeshi hupelekwa KULINDA MALI & UHAI wa raia. Vinginevyo, hakuna namna kisheria RC atapewa ruhusa kutumia jeshi. Suala la KUFAGIA si moja ya mazingira yaliyotajwa kisheria. Hili ni jambo la KISIASA zaidi.
CHANZO

View: https://twitter.com/BabaMwita/status/1746523654630854689


Wanakutana kuteta jambo

 
Back
Top Bottom