Jenerali Ulimwengu na makala zake

Swali la kutafakari wakati tukimsubiri Mwanakijiji aki-condense hicho kitu. Je uongozi ni sifa anayozaliwa nayo mtu au ni sifa inayotokana na uzoefu wa maisha?
 
Swali la kutafakari wakati tukimsubiri Mwanakijiji aki-condense hicho kitu. Je uongozi ni wa kuzaliwa au kutengenezwa?

Nadhani muunganiko wa vyote viwili ndio huleta kiongozi bora. kwa kuzaliwa lazima awe na kipawa fulani na mvuto wa kuwa kiongozi, lakini pia inabidi kutengenezwa kwa kujibidisha kutafuta maarifa ili aweze kukabiliana na hali halisi ya mabadiliko ya mazingira na majukumu, na kuboresha hicho kipaji chake ili afanye vyema.
 
Ili tuendelee, hatuhitaji vitu vingi

Jenerali Ulimwengu
Oktoba 31, 2007


NAPENDA kupeleka salamu zangu za heri na furaha kwa wasomaji wa jarida hili jipya, na kuwatangazia kwamba, baada ya kimya cha muda mrefu kidogo, sasa narejea dimbani, ingawaje ni katika jarida jipya, nikiwa na shauku ya kuendeleza kile nilichokianza mnamo miaka ya 90 na kukiendeleza kwa takriban miaka dazeni kabla sijatua ili kupumua kidogo.

Shauku inayonituma kurejea inatokana na ukweli kwamba, kwa kuangalia na kutafakari hali ya nchi yetu, na hata nchi nyingine katika bara letu, kwa muda mrefu hakuna kikubwa kilichobadilika, na matatizo yetu ni yale yale, na katika medani fulani fulani, matatizo hayo yamezidi kukomaa bila kuonyesha dalili za wazi za utashi au uwezo wa kuyatatua.

Mwanajamii mwenye akili timamu, anapokuwa mkabala na matatizo tunayoyaona, atachagua moja kati ya mawili: ama atashika tama kwa kukata tamaa na kusema, ‘hayanihusu’, au ‘liwalo na liwe.’Miaka kadhaa iliyopita niliandika katika safu kama hii kuhusu msemo wa lugha ya Kihaya, ‘ka kitandugaho’, ambao maana yake (neno kwa neno) ni kusema, ‘neno hilo lisije likatoka kwangu’kama njia ya kujivua uwajibikaji juu ya suala lo lote linalojadiliwa kwa wakati huo. Huu ni mwelekeo wa kukata tamaa, na mara nyingi pia ni mwelekeo unaotokana na hofu ya kuonekana kama ‘mkorofi’, ‘mpinzani’, ‘mlalamishi,’ ‘mzushi’, na kadhalika.

Mwanajamii anayeijali jamii anamoishi na ambamo wanawe na wajukuu zake wataendelea kuishi kwa karne na karne baada ya yeye kutoweka duniani, hawezi kuwa na mtazamo kama huo. Atajua kwamba kila linalotokea katika mazingira yake linamhusu kwa njia moja au nyingine na kwamba, kwa vyo vyote vile, athari zake angalau zitakuja kuwapata wale watakaobaki nyuma yake. Kama anawapenda, atajali, na atadhihirisha kujali kwake kwa kuwawekea warithi wake mazingira mazuri yatakayowawezesha kuishi na kustawi katika amani na furaha.

Hakika ni mpuuzi tu ndiye anaweza kuwa na mtazamo wa kujijengea maisha mazuri, yaliyojaa kila aina ya raha na starehe bila kufikiria hali ya kesho na keshokutwa itakuwa vipi kwa kizazi chake wakati yeye amekwisha kuyoyoma. Aidha atakuwa ni mpuuzi, au mtu mwenye utindio wa ubongo, atakayewekeza katika mali za kuwaachia wanawe huku akisahau kuwekeza katika utangamano wa jamii watakamoishi.

Hivyo, basi, inatubidi sote, bila kuchoka, tuchange mawazo na nishati ya kifikra katika kuboresha mazingira yetu ya sasa na ya baadaye. Tufanye hivyo tukielewa fika kwamba sote tunahusika, na kwamba akina ‘Ka Kitandugaho’ hawana nafasi miongoni mwa wajenzi wa mustakabali wa jamii yetu, iwe ni ile ya Watanzania au ile ya Waafrika kwa ujumla.

Mara kwa mara katika mfululizo wa makala hizi nitazungumzia masuala yanayolihusu bara la Afrika kwa ujumla, ingawa msisitizo mkubwa zaidi utakuwa kwa Tanzania. Hiyo ni kwa sababu ingawa ukingo tulikosimama uko Tanzania, lakini tunaweza kuona ng’ambo ya pili na kuitambua hali ya huko kama isiyokuwa tofauti sana na hapa tuliposimama, na kwamba kihistoria, kijografia, kiutamaduni na kimustakabali tunashabihiana, na kwamba, pamoja na vijitofauti kadhaa, katika zahama zetu hakuna wa kumcheka mwenziwe.

Ni kitambo tangu nianze kuzisanifu makala zitakazotoka katika mfululizo huu, na kwa hiyo zitakuwa na mtazamo mrefu kimsingi, ingawaje hapa na pale habari za leo na jana zimeongezwa ili kutoa ladha hai ya jinsi mambo yanavyoenenda wakati makala hizi zikichapishwa. Alimradi lengo langu ni kutengeneza jukwaa muafaka la kujadili masuala kadhaa ambayo, kwa mtazamo wangu, hayana budi kuwekwa bayana kama kweli tunayo dhamira ya kujikwamua kutokana na zahama kuu iliyotuandama sote Waafrika, zahama ya maendeleo duni; umasikini uliokithiri; unyonge wa watu wetu wanaozidi kuwa dhalili kila siku ipitayo kiasi kwamba sasa wanaelekea kukata tamaa kabisa; msigano unaozidi kujitokeza kati ya utajiri wa nchi na umasikini wa wananchi; ubovu wa mifumo ya kisiasa na kiutawala; nakisi ya uongozi na kutokujali kwa watawala; kushamiri kwa kila aina ya ufisadi miongoni mwa watawala hadi ngazi za juu kabisa; msambaratiko wa jumla wa utu wetu na mmomonyoko wa mshikamano wa kitaifa.

Kama nilivyosema hapo juu, tunaweza tukaamua kwamba hatuna tunaloweza kulifanya kutibu ndwele hizo nilizozitaja na nyingine nyingi tu ambazo zinatokana na hizo. Tukifanya hivyo, twafa!, na wanetu wafa, hata kabla hawajazaliwa. Kwani tutakuwa tunausabili mustakabali wa nchi yetu, na kwa ujumla bara letu, katika mikono ya hao hao waliotufikisha katika hali hii ya kutisha. Ama kwa hakika hivyo ndivyo wangependa mambo yawe, kwani iwapo sote tutakata tamaa tutakuwa tumewaachia uwanja wa kutamba pasi na pingamizi.

Wenye nguvu duniani wamezidi kujiimarisha kwa kila njia, na mtandao wa maslahi yao umetamalaki na kuigubika dunia nzima.

Wameshika hatamu zote kuu za kiuchumi; wametandaza watawala wanaowataka katika nchi nyingi duniani, watawala ambao watafanya lo lote wanaloamuriwa kufanya; wameimairisha nguvu zao za kijeshi, na majeshi yao yanatumika kuwaondoa watawala wasiokubaliana nao; wameshika hatamu za maamuzi ni nani apate “misaada” ya kiuchumi na nani asipate; wamewafanya hata wale watawala waliochaguliwa na watu wao kuwa kama vikaragosi tu, kwa jinsi wanavyowatumia. Sisi sote tu mateka.
Tu mateka, tumetekeka, tumekamatika, tumeshikika, tumedhibitika, tumepigika.

Nguvu hii ya ubeberu inahusiana moja kwa moja na udhaifu wetu kama wazalendo wa nchi hii na bara hili, kwa maana kwamba sisi ndio tuliouachia nafasi ya kutamba kiasi hicho, na ni sisi pia ambao tunaendelea kukenua huku tukigombea makombo yanayodondoka kutoka meza za mabwana zetu, wakati tungetakiwa kujua kwamba hicho wanachokula, na sisi tukaambulia makombo, ni chetu. Nguvu yao inatokana na ujuha wetu unaotufanya tuendelee kuamini kwamba hatuwezi kujikimu kwa mali zetu wenyewe bila kuzitoa kwa wakubwa hao na kisha tukasubiri watutupie sadaka. Nguvu yao inatokana na ulemavu wa akili tuliojivisha, wa kuamini kwamba hatuwezi lo lote bila wakubwa.

Napenda nieleweke kwamba sina chuki dhidi ya watu kutoka nje ya bara hili; chuki yangu inaelekezwa dhidi ya utamaduni unaoendeleza dhana, inayosukumwa pia na watawala wetu, kwamba hakuna kinachowezekana bila Wazungu na wageni wengine, wakati tukijua, au tukitakiwa kujua, kwamba utajiri tulioukalia ni nyenzo kubwa ya kutufanya tukawa mabwana badala ya watwana. Tumekuwa kama tumbili waishio kando ya barabara zinazotumiwa na watalii, ambao hushinda kutwa barabarani wakisubiri watupiwe ndizi na watalii ilhali matunda wameyaacha porini, tele.

Upo mjadala usioisha nchini hapa kuhusu rasilimali zetu na jinsi ambavyo tunazitapanya na kuzigawa hovyo kana kwamba ni takataka zisizokuwa na thamani. Wapo wananchi wanaohoji jinsi mali hizo zinavyotolewa holela, lakini bado hawa ni wachache mno, na wamekuwa wakibezwa na wakubwa na kuambiwa kwamba ni wapuuzi wanaotaka sifa na umaarufu wa kisiasa tu. Maswali wanayouliza ni ya kimsingi, lakini badala ya kupewa majibu ya msingi wanapatilizwa kwa kutumia vigezo vya kiufundi tu.

Swali mojawapo baina ya mengine mengi ya kujiuliza ni: Hata kama hao wanaohoji wanatafuta sifa na umaarufu, ili wafanikiwe kuvipata hivyo, si lazima wawe wamezungumzia jambo ambalo litawagusa wananchi? Sifa na umaarufu tunaoutaja hauna budi kutokana na wananchi kuyapokea na kuyakubali hayo wanayoyasikia kwa kiwango fulani. Kama wananchi wataona kwamba hayo wanayoyasema hao wanaosema ni upuuzi mtupu, hizo sifa na huo umaarufu vitatoka wapi?

Aidha, nadhani ni kosa kujibu malalamiko yanayoelezwa kuhusu uporaji wa nchi yetu kwa kuning’iniza hirizi ya ‘amani na utulivu’. Raia wanaouliza maswali magumu kuhusu uporaji wa mali za nchi yao sio wanataka kuleta hali ya vurugu na kuvurugika kwa amani. Watakaoleta hali hiyo ni wale wanaoulizwa maswali na wakashindwa kuyajibu kwa ufasaha, au wakawakaripia na kuwafokea wale wanaouliza kile ambacho ni haki yao kukiuliza. Namkumbuka vyema mwanafalsafa aliyesema kwamba hakuna swali la kijinga, ni majibu tu yanaweza kuwa ya kijinga.

Ye yote anayefuatilia mijadala inayoendelea nchini, na ambayo sina shaka itaendelea kwa muda mrefu, hatakosa kutambua kwamba yapo matatizo makubwa yanayoikabili nchi hii.

Haiingii akilini, wala haiyumkiniki kwamba nusu karne baada ya Uhuru, watu wetu wanazidi kuwa masikini, tena masikini hohe hahe, wakati nchi yao imesheheni kila aina ya utajiri: ardhi nzuri, maji mengi katika mito na maziwa, mabonde yenye rutuba kwa ajili ya kilimo na ufugaji, misitu, mbuga za wanyama, na kadhalika. Zaidi ya yote, raia wasikivu (hadi leo) ambao wakielekezwa wanaelekezeka.

Tulifundishwa kwamba ili tuendelee tunahitaji vitu vinne: watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora. Watu ndio hao niliowaeleza hapo juu, na ardhi pia. Siasa safi na uongozi bora vinaingia pamoja, kwa maana kiongozi bora ni yule mwenye uwezo wa kubuni siasa safi na kujua namna bora ya kuitekeleza.

Hapa ndipo tatizo linapojitokeza. Kiongozi bora si yule anayetangaza siasa, hata kama ni safi, kisha akaiacha ijitekeleze, kwa sababu, dhahiri, haiwezi kujitekeleza. Na wala siasa safi haiwezi kutekelezwa na kiongozi mbovu. Aidha, kiongozi safi hawezi kutekeleza siasa mbovu. Ikijitokeza kwamba siasa safi inahubiriwa na kiongozi anayejulikana kuwa mbovu, au kiongozi bora anajaribu kutekeleza siasa inayojulikana kuwa mbovu, hapo ni dhahiri kuna mchezo wa kuigiza ambao hatima yake ni mashaka matupu.

Hivyo, basi, hatuna budi kusaili mwenendo wa uongozi wetu na siasa unayoitekeleza katika kila fani ya maisha ya kitaifa. Hatuna budi kuachana na mtazamo lemavu wa kuwaona wale wanaohoji mienendo ya viongozi kama watovu wa uzalendo. Mzalendo wa kweli ni yule anayetambua kwamba viongozi tunaowachagua wanalo deni kwa waliowachagua, na deni hilo hawana budi kulilipa kwa kufanya yale waliyosema watayafanya.

Kinyume cha hilo ni kukubali siasa za uongo na ufisadi na imani kwamba kiongozi akisha kuchaguliwa anakuwa ni mungu-mtu asiyesailiwa. Hakuna kiongozi hata mmoja aliyelazimishwa kuwa kiongozi. Wote wamefanya kampeni, tena wengi wamefanya kampeni hizo kwa gharama kubwa, pamoja na kwenda kwa waganga, kuwapiga vikumbo washindani wao, kuwapigia magoti wapiga kura na kila aina ya vituko.

Ni kweli kwamba tunaishi chini ya utamaduni wenye makengeza. Haiingii akilini kwamba vikumbo vyote vinavyopigwa na waheshimiwa hawa vinapigwa ili tuwape fursa ya kututumikia. Uko uongo fulani tunaoukubali katika michakato ya uchaguzi, na uongo huo, ambamo sote tu washiriki, umetufikisha hapa tulipo leo na mikanganyiko tunaoishuhudia hivi sasa.

Eti mtu analipa fedha, anagawa khanga, anapika na kuwalisha watu, ananunua pombe ya halaiki… ili apate fursa ya kutumikia wananchi?! Kama nia yake kweli ni kutumikia wananchi, si aanze tu, bila kufanya kampeni na kupoteza fedha.
Katika nchi hii, na barani Afrika kwa ujumla, tumeshuhudia ukweli unaotisha kwamba siasa ndiyo sekta ya uchumi inayokuwa kwa kiasi kuliko kilimo, ufugaji, uvuvi, viwanda na biashara nyingine.

Kimsingi hili linatokana na ukweli kwamba katika siasa zetu mshiriki hahitaji ujuzi wala stadi ya aina yo yote, alimradi aweze kupiga domo na kutawanya fedha. Kama shughuli nyingine zote zimeshindikana, ama tija yake ni ndogo, ingia katika siasa, uone jinsi tija inavyopaa.

Ndani ya siasa, hasa kama umebahatika kupewa nafasi ya utendaji kama vile waziri, mkuu wa mkoa n.k., angalia jinsi unavyoibuka kuwa mfanyabiashara mkubwa, mkulima maarufu, mfugaji wa mfano nk., kwa sababu mambo yote hayo sasa yanatengenezwa na ile nafasi ya ‘uongozi’ uliyopewa na sasa unaiuza kwa maslahi yako binafsi. Lakini, kaa chonjo usije ukapoteza nafasi hiyo, la sivyo unarudia kule kule ulikokuwa kabla ya neema ya uongozi.

Kwa jinsi hii tumejenga kada kubwa mno ya ‘viongozi’ ambao hawana sifa yo yote ya uongozi bali ni matapeli na wababaishaji.

Kadri tunavyoendelea na mtindo huu ndivyo tunavyoshuhudia ongezeko kubwa la watu ambao tunawaachia nafasi ya ‘kutuongoza’ hata kama tusingediriki wakati wo wote kuwakabidhi jukumu la kuwaongoza mbuzi au kondoo wetu, kwa sababu tusingewaamini kufanya kazi hiyo.

Ni kwa vipi, basi, tumefika hapo, yaani kuweza kusabili majaliwa yetu kwa watu ambao tusingethubutu kuwakabidhi majaliwa ya mifugo yetu? Jibu la haraka lingekuwa kwamba hatujijali, hatujipendi.

Hii si kweli kwa sababu, kwa kuangalia tunavyoenenda, tunajipenda kupindukia, ili mapenzi yetu kwetu yamezama zaidi katika kujidekeza na kujiendekeza badala ya kujielekeza katika kujenga taifa endelevu lenye mustakabali unaotabirika.

Hali hii imetokana na ukosefu wa uongozi imara, unaoona mbali, na unaodiriki kuchukua maamuzi magumu bila kujali nani anaudhika, alimradi maamuzi hayo yanajenga mustakabali wetu. Hali hii ndiyo ninayokusudia kuijadili katika safu hii kwa kipindi hiki.
 
Nadhani muunganiko wa vyote viwili ndio huleta kiongozi bora. kwa kuzaliwa lazima awe na kipawa fulani na mvuto wa kuwa kiongozi, lakini pia inabidi kutengenezwa kwa kujibidisha kutafuta maarifa ili aweze kukabiliana na hali halisi ya mabadiliko ya mazingira na majukumu, na kuboresha hicho kipaji chake ili afanye vyema.

Je ni vitu hivyo viwili tu au kuna zaidi? Kwa mfano, can someone choose to become a leader? Can leadership skills be learned?
 
Kiongozi mzuri ni yule mwenye vision na akili ya kutatua matatizo ,sio mla rushwa na lazima awe mpenda haki kwa wote.
 
Swali la kutafakari wakati tukimsubiri Mwanakijiji aki-condense hicho kitu. Je uongozi ni sifa anayozaliwa nayo mtu au ni sifa inayotokana na uzoefu wa maisha?


Nyani.. right there... you are brushing on the "thing" (this sound nasty). Ila hauko mbali sana na fikra zangu.. wacha niendelee kuibia..
 
Nadhani muunganiko wa vyote viwili ndio huleta kiongozi bora. kwa kuzaliwa lazima awe na kipawa fulani na mvuto wa kuwa kiongozi, lakini pia inabidi kutengenezwa kwa kujibidisha kutafuta maarifa ili aweze kukabiliana na hali halisi ya mabadiliko ya mazingira na majukumu, na kuboresha hicho kipaji chake ili afanye vyema.



Ukishakuwa na sifa hizo hapo juu then unaweza kuwa kiongozi wa kitu chochote, iwe siasa, uzalishaji, timu ya michezo,a u hata vitani....


Je ni vitu hivyo viwili tu au kuna zaidi? Kwa mfano, can someone choose to become a leader? Can leadership skills be learned?

So, jibu lako hapa Nyani; mimi naona ni Yes. PRACTICALITY of Leadership skills can be learned; but you have to be born or grow up in the enviroment that qualify you as above (Rwabugiri post).
 
Kwa bahati mbaya, kiswahili kina upungufu kiasi kwa maneno ya utawala. Hivi, uongozi ni lipi kati ya haya - Leaders, Administrators, Managers, Commanders, Directors.
Je, nchi inahitaji yupi kwenye huo uongozi bora.
 
Swali la kutafakari wakati tukimsubiri Mwanakijiji aki-condense hicho kitu. Je uongozi ni sifa anayozaliwa nayo mtu au ni sifa inayotokana na uzoefu wa maisha?


Ukiona mtu baada ya kuwa na uzoefu fulani wa maisha akatokea kubadilika na kuwa kiongozi mzuri basi ujue huyo alikuwa kiongozi mzuri tokea alivyozaliwa, isipokuwa kipaji hicho hakikuonekana mapema kwa sababu alikosa kitu au uzoefu fulani wa kutekenya hicho kipaji chake cha uongozi, na yeye mwenyewe kuwa na ujasiri wa kusimamia na kukiendeleza kipaji chake.
 
Kwa bahati mbaya, kiswahili kina upungufu kiasi kwa maneno ya utawala. Hivi, uongozi ni lipi kati ya haya - Leaders, Administrators, Managers, Commanders, Directors.

Je, nchi inahitaji yupi kwenye huo uongozi bora.


Kwa maoni yangu; Leader ndiye anayetakiwa. Hayo majina mengine ni ya vyeo kama tulivyozoea kwenye jamii zetu.

Swali lako la pili nathani ndilo hasa Jenerali Ulimwengu amelielezea kwa kirefu.
 
Je ni vitu hivyo viwili tu au kuna zaidi? Kwa mfano, can someone choose to become a leader? Can leadership skills be learned?


Good leaders are born and made. Some people can never make good leaders whatever good environment they maybe given if they were never born leaders. Atalazimisha tu na ndio hao wanatuingiza kwenye matatizo.

Tatizo ninaloliona mimi ni pale ambapo jamii inashindwa kugundua viongozi wazuri na kuwachagua hao. Kimsingi, viongozi siku zote katika jamii ni wachache sana. Ni jukumu la jamii kuhakikisha kuwa siku zote wanachagua viongozi kutoka miongoni mwa wale wachache. Shida yetu ni kwamba mara nyingi kwa sababu ya ghiliba nk tumechagua viongozi kutoka miongoni mwa watu ambao hawana attributes za uongozi na kuwaacha wale ambao wanazo. Hapo ndipo tunapokuwa tumeliwa!
 
Jenerali Ulimwengu ameweka vyama vyote kwenye kapu ikiwemo vya upinzani kuwa havina falsafa wala itakadi:

http://www.raiamwema.co.tz/08/04/23/4.php

Hebu mlio karibu na Raia Mwema mumwambia asome hapa:


http://www.chadema.net/maoni/kijue.php

ili wiki ijayo aendelee kujadili kama CHADEMA nao hawana falsafa wala itikadi?

Asha

Nakubaliana na Ulimwengu juu ya hili kwamba vyama vyetu vyote haina itikadi
ambayo viko tayari kuitangaza na kuitekeleza.

Walichoandika na wanachoongelea ni vitu tofauti kabisa.

Inasikitisha kuona kwamba pamoja na CCM kuwa chini mno na kufilisika kiitikadi lakini vyama vingine vinashindwa kutumia nafasi hii kujijienga na kutangaza itikadi zao.
 
Asha Abdala,
Alichosema Jenerali ndio ukweli wenyewe. Hata kama Chadema mtakuwa na maandishi lakini sio lazima yawe itikadi, yatabaki kuwa maandishi tu. CCM kama Chadema wana maandishi, lakini je wanaishi katika hayo maandishi? kwa upande wa Chadema ni hali kadhalika, labda ungetushawishi vinginevyo, kutuonyesha Chadema inaishi katika hiyo itikadi kwa maneno na vitendo na inaweza kujipambanua kutoka kwenye vyama vingine ya upinzani hali kadhalika CCM.

Nyongeza: kama Jenerali akiamua kuanzisha chama ya wajamaa wa kujitegemea basi naamini nitakuwa wa kwanza kukata kadi ya chama hicho. Ubepari wa Kitanzania ni Unyama, Ukatili, ujambazi, wizi, rushwa na matakataka yote.
 
Haitoshi kwa Jenerali kubainisha kwamba vyama havina falsafa wala itikadi bila kwenda hatua moja mbele na kubainisha falsafa gani anafikiri ndio stahiki. labda kwa kuwa kasema makala yake inaendelea, mwanzisha thread usisite kutubandika mwendelezo huenda akaitaja falsafa yake.

By the way, hivi mwajua ya kuwa neno demokrasia ni sawasawa na maneno nguvu ya umma ( demos cratos a.k.a peoples' power) sasa wana chadema( chama cha peoples' power and development) ni nini tofauti yenu na wademocrat wa marekani? Nauliza tu

Aidha nimwombe Jenerali, asome humu jamboforums mawazo ya wabongo wenzake kuhusu falsafa na itikadi, mbona zimo labda aseme na zenyewe hazifai.
 
Tatizo sio falsafa au itikadi...issue hapa ni nadharia na matendo juu ya falsafa au itikadi inayozungumzwa.
 
Hata CCM wana itikadi lakini je wanatekeleza? Unaweza kuandika itikadi yako lakini kama unaitumia tu kama njia ya kudanganyia wananchi na huitekelezi kwa matendo, ni kupoteza muda bure.

Vyama vijitahidi kuja na itikidi ambazo kweli wanaziamini na wanaweza kutekeleza na sio mambo kibao wakati wanatekeleza vitu tofauti kabisa.
 
Nakubaliana na Ulimwengu juu ya hili kwamba vyama vyetu vyote haina itikadi
ambayo viko tayari kuitangaza na kuitekeleza.

Walichoandika na wanachoongelea ni vitu tofauti kabisa.

Inasikitisha kuona kwamba pamoja na CCM kuwa chini mno na kufilisika kiitikadi lakini vyama vingine vinashindwa kutumia nafasi hii kujijienga na kutangaza itikadi zao.

Mbona wanachoongea na wanachotenda ni sawa sawa! Soma hapa wakiwa wanazungumza na wananchi:
http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/3/26/habari22.php

Halafu kwani anachokifanya Dr Slaa si kupinga ufisadi kwa "nguvu ya umma"? Au Zitto Kabwe alipokuwa akisema rasilimali za Watanzania zitumike kwa manufaa ya watanzania si alikuwa akisimamia falsafa na itikadi ya CHADEMA?

Asha
 
Back
Top Bottom