DAR si LAMU
JF-Expert Member
- Mar 31, 2007
- 2,928
- 544
Gamaba la nyoka,
Zingatia ni nini zaweza kuwa athari za kauli ya Jenerali kwamba vyama havina misingi ya kifalsafa. hapa si suala la kutanguliza maslahi ya vyama. Kauli kama hiyo aliyoiandika inatosha kabisa kudhohofisha jitihada zote za wanamageuzi nchini. Jiulize kauli ya Mwalimu aliposema wapinzani hawana sera iliudhohofisha kiasi gani mfumo wa mageuzi nchini. Aliitoa kauli hiyo wakati akimnadi 'Mr. Clean'
Au fikiria kauli kama za akina Jaji Warioba aliyepata kusema, tuna chama kimoja na wapiga kelele 17
Vijineno kama hivi vinavuruga sana harakati za kuwang'oa mafisadi, mara utasikia wengine wanasema, wapinzani hawana jipya, na kisha watu wanawaamini kwa sababu ya umaarufu wao.
Maslahi ya taifa hayawezi kulindwa au kutetewa kwa kutoa kebehi za kudhalilisha vyama vinavyotetea maslahi hayo hayo.
Aondoe kauli yake hiyo, hayo mengine aliyoyaandika ni ugonjwa ulioko kwenye chama ambacho yeye ni mwanachama. kama ana nia ya dhati ya kuutibu aje kambi ya mageuzi tushirikiane badala ya kuvunja watu moyo.
..upinzani kama ni dhoofu ni dhoofu tu.
..ukweli unaposemwa watu wajifunze na kukubali kuonyeshwa mapungufu.